Mashabiki Zangu Hawapendi Nitumie Mkorogo :-Upendo Nkone

Msanii wa injili wa siku nyingi, Upendo Nkone amefunguka na kusema kuwa alichogundua ni kwamba mashabiki zake hawapendi kabisa yeye hatumie mkorogo kwa sababu kila anapojaribu wamekuwa wakimshambulia sana katika mitandao ya kijamii.

Msanii huyo anasema kuwa mara ya kwanza aliwhi kujaribu kufanya hivyo lakini mashabiki zake walimjia juu sana na kuanza kumtukana na hata kumwambia kuwa hapendezi akifanya hivyo, na kwa sababu ameuwa aiwasikiliza mashabiki zake basi na yeye aliona bora aache kufanya hivyo.

Kuna wakati nilianza kutumia mkorogo,mashabiki wakaanza kunijia juu nikaona uwa hawapedni basi na mimi nikaacha.

Tuliwahi Kununiana na Mume Wangu Karibia Mwezi :-Upendo Nkone

Msanii wa nyimbo za injili Upendo Nkone amejaribu ku-share experience ya maisha yake ya ndoa na mashabiki wake kutokana na mawazo ambayo watu waengi wamkuwa nayo kuhusu watumishi wa mungu katika kupambana na matatizo yao.

Upendo Nkone anasema kuwa hata yeye katika maisha yake ya ndoa amekuwa na  changamoto mbalimbali kama wanazopitia watu wengi  huku akisema kuwa kuna muda hata yeye na mume wake huwa wanagombana.

Japokuwa mume wangu ni mchungaji lakini kuna muda huwa tunagombana na huwa tunalianzisha ,tunafunga na milanngo, tuliwahi kununiana ndani karibia mwezi.kwa mfano unakuwa kuna siku ninakuwa sijapika na huo ndio ugomvi wetu mkubwa na yeye,apike mdada wa kazi alafu unakuta chakula hakijakaa sawa hapo ndo utamjua mbena ni nani.-Anasema Upendo Nkone.

Staa wa nyimbo za Injili Upendo Nkone atuma ujumbe maalum kwa Rais John Magufuli

Mwimbaji Upendo Nkone ametuma ujumbe maalum kwa rais Magufuli akimwambia kwamba yuko tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge.

Nkone ata hivyo amesema hataki kujiunga na siasa kwa ubunge wa kugombea jimboni ila kama mbunge mteuliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Akiongea kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Upendo alisema kuwa yuko tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge iwapo Magufuli atamteua.

Upendo Nkone

“Sina mpango wa kuwa mwanasiasa, kwahiyo hata ubunge wa kugombea siwezi, lakini kama Rais wangu Magufuli akilala akiota kwamba anipe ubunge viti maalum, kwakweli napokea…. Mh. Magufuli nimeambiwa nigombee ubunge, basi unikumbuke baba,” alisema Upendo Nkone.

Nkone alisisitiza kuwa Rais Magufuli anapaswa kumteua kwasababu kuwa yeye mchakato wa kupata ubunge wa kugombea ni mgumu na una mambo mengi ikiwa ni pamoja na gharama, jambo ambalo haliwezi.