Sallam SK Adokeza Ujio Wa Kolabo Ya Diamond na Rihanna

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Sallam SK amedokeza uwezekano wa Kolabo kati ya Diamond na staa wa RnB kutoka Marekani,  Rihanna.

Kwenye mahojiano na Kituo kimoja cha habari, Sallam SK alijibu maswali katika kipengele cha YES/NO au NDIO/HAPANA kwenye …swali la endapo kuna collaboration kati ya Diamond na Rihanna, Meneja alijibu YES.

Siku za nyuma kumsema wahi kuwa na tetesi kuwa Diamond ana mpango wa kufanya kolabo na Rihanna ingawa uongozi wa Diamond haujaongelea kiundani zaidi kuhusu kolabo hiyo.

Diamond tayari ameshafanya Kolabo na wasanii wakubwa Marekani kama vile Neyo katika wimbo wake wa ‘Marry me’ na Rick Ross wimbo wa ‘Waka waka’.

WCB Watoa Tamko La Rich Mavoko Kwenda Kujisajili BASATA Kwa Mara Ya Pili

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameamua kujitoa rasmi katika Label yake iliyokuwa ikimsimamia ya WCB kwa ajili ya mgogoro wa mkataba aliopewa.

Baada ya kutoka WCB, Mavoko alionekana akienda kushtaki katika Baraza la Sanaa Tanzania ambapo pia alidaiwa kwenda BASATA kwa ajili ya kujisajili upya pamoja na kwamba alishasajiliwa chini ya WCB.

WCB wameibuka na kudai taarifa za Msanii huyo kwenda kujisajili BASATA sio sawa kwani tayari ameshasajiliwa chini ya Label hiyo mapema mwaka huu.

Kwenye mahojiano na GPL, Meneja kutokea WCB, Sallam SK amesema hayo alipokuwa akieleza ushirikiano uliyipo kati ya WCB na Baraza hilo kwa sasa.

Suala la kusema hatushirikiani na BASATA hilo litakuwa si la kweli na sisi tunashirikiana nao sana kuna vitu vinatokea bahati mbaya. Lakini ukiangalia wasanii wetu wote wamesajiliwa BASATA na hamna yeyote ambaye hajawahi kujisajili. Hata juzi kati hapa ilisemekana kuwa Rich Mavoko ndio alienda BASATA akajisajili, hapana!, kashasajili kupitia WCB, actually mwezi wa saba mwaka huu”.

 

Diamond ni Mtu Mwenye Damu ya Kipekee:-Ricardo Momo

Meneja wa msani Harmonizie kutoka katika kundi la wasafi anaejulikana kama Ricadro momo amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsema na kumfikiria diamond vibaya bila kujua undani wake, kwa upande wake anasema kuwa wao wanaoishi na Diamond wanajua ukweli wa diamond ni mtu wa aina gani.

Momo anasema kuwa anaweza kumuelezea Diamond kama mtu wa kipekee sana mwenye kuogopa sana Mungu  na anaamini kuwa Diamond ataiona Pepo.

Diamond ni mtu mwenye damu ya kipekee sana, ana imani sanaa,sijui kama mwenyezi mungu ataweza kumnyima pepo kweli sijui.

Akiongelea kuhusu post yoyote anayoweka katika ukurasa wake wa instagram , Ricardo momo anasema kuwa anapoweka kitu katika ukurasa wake hamlengi mtu yoyote zaidi ya wale wanaomfollow tu.

kwa upande wangu huwa siandiki kitu kwa ajili ya kumu-atack mtu kwaio hata kama nimepost sijamwambia mavoko.linakuwa linamuhusu mtu yoyote anayenifollow mimi katika instagram.

WCB Wadai Mamilioni Waliyowekeza Kwa Mavoko Hayajarudi Hata Robo

Msemaji wa Label ya WCB ambaye pia ni mmoja wa meneja wa Diamond Platnumz, Sallam Sk amemfungukia sakata hilo na kudai pesa ambazo Label hiyo zimewekeza kwa Rich Mavoko hazijrudi.

Wiki iliyopita msanii Rich Mavoko ambaye alikuwa chini ya Label hiyo kwa muda kidogo alitinga BASATA na kwenda kuwashitaki kwa mkataba wao wa kinyonyaji.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Sallam Sk ameweka wazi kuwa mpaka hivi sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB kimkataba zaidi.

Lakini pia ameweka wazi Kuwa mpaka sasa pesa ambayo wamewekeza kwa muimbaji huyo katika project zilizotoka haijarudi hata robo.

Mpaka sasa sielewi malalamiko ya Mavoko ni yapi kwa sababu ukisema sisi tunamnyonya mtu hicho kitu hakiwezekani alafu isitoshe Pesa ambayo tumewekeza kwa Rich Mavoko haijarudi hata robo”.

 

Diamond Atinga BASATA Kwa Ajili Ya Kesi Ya Mavoko

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi amefika katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya madai ya aliyekuwa msanii wake Rich Mavoko.

Rich Mavoko alimburuza Diamond na Label nzima ya WCB mbele ya BASATA kwa madai ya mkataba wa kinyonyaji waliompa wakati amesainiwa chini ya Label ya WCB.

Diamond aliongozana na Mameneja wake wawili, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Sallam Sharraf katika ofisi hizo mapema leo ili kuitikia wito.

Kwenye mahojiano na Global Publishers mmoja wa meneja wa Diamond, Sallam, amesema waliitwa na Basata na sasa wapo katika mazungumzo ya kutatua jambo hilo na kufikia mwafaka.

Sallam amesema ni vyema watu wakasubiria yatakayoamuliwa huko, ambapo wanaamini Basata itauambia umma nini kilichoafikiwa badala ya wao  kuwa wasemaji.

 

Mbosso Awakingia Kifua WCB Adai Sio Wanyonyaji Kama Madai Ya Mavoko

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Maromboso amefunguka na kuwakingia kifua WCB dhidi ya tuhuma za unyonyaji walizotupiwa na msanii Rich Mavoko.

Wiki iliyopita RIch Mavoko aliwaburuza WCB katika Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) na kuwatuhumu kwa unyonyaji kutoka na mkataba waliompa.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari Mbosso amefunguka na kudai yeye binafsi hajaona unyonyaji wowote WCB  hasa kwa upande wa mkataba wake Tena anaamini wamempa zaidi anachostahili.

Kiukweli kwa upande wangu tangu naingia WCB mpaka leo sijafikisha pesa ambayo wao wali invest kwangu kwaiyo nikiambiwa nanyonywa binafsi nitapinga kwa sababu mimi ndio naona nawanyonya kwa sababu mpaka leo hela waliyowekeza kwangu haijarusi na kuna wasanii wapo WCB mpaka leo pia hawajarudiasha hata nusu ya pesa kwaiyo ukiniambia WCB wananyonya wasanii nakuwa sikuamini labda uje na vigezo”.

 

Rich Mavoko Afunguka Baada Ya Kuwaburuza WCB BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko amefunguka kwa mara ya kwanza na kuongelea sakata lake na uongozi wake wa zamani WCB.

Siku ya jana taarifa zilisambaa kuwa Rich Mavoko amepeleka kesi yake mbele ya Baraza la Sanaa (BASATA) baada ya Tetesi za wiki kadhaa kuwa ameamua kujitoa WCB.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rich Mavoko amesema kuwa anashukuru kukutana na BASATA na kupata elimu ya kutosha huku akiwamwagia sifa kuwa hao ndio maana halisi ya walezi wa sanaa yetu nchini Tanzania.

https://www.instagram.com/p/BmRCQzVAj05/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=133n0dixilgpb

Siku ya jana Rich Mavoko alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ambapo amepeleka mkataba wake na WCB ambapo ameomba uangaliwe upya na kudai ni wa unyonyaji.

Wasanii kadhaa na wafanyakazi wanaojitoa WCB wamekuwa wakilalamikia suala la mikataba mibovu kutoka katika kampuni hiyo na wengine kudai walikuwa hawalipwi.

Mpaka sasa uongozi wa WCB hawajajibu tuhuma hizo na madai hayo ya Rich Mavoko.

Rich Mavoko Ashinda Kesi Dhidi Ya WCB BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameripotiwa kushinda kesi dhidi ya Label yake ya zamani WCB na kufanikiwa kuvunja mkataba na kutoka.

Rich Mavoko ambaye alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kwa vibao vyake vikali  alisainiwa na kujiunga na WCB siku za nyuma kidogo na kutoa nyimbo kadhaa zilizomrudisha Kwenye chati.

Lakini mapema mwaka huu kulikuwa na tetesi nyingi Baada ya Rich MAvoko kutoonekana Kwenye shughuli mbali mbali za WCB na hata kutoonekana kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Rich Mavoko pamoja na uongozi wake WCB wamekuwa kimya juu ya Tetesi za Rich Mavoko kuondoka WCB Mpaka sasa ambapo kuna taarifa kuwa Mavoko kajitoa rasmi.

Kituo cha Televisheni cha TV E  wanaripoti kuwa siku ya leo Mavoko amefanikiwa kushinda kesi dhidi ya WCB rasmi na inasemekana amejitoa Kwenye Label hiyo Lakini pia mkataba alikuwa nao umevunjwa.

Mpaka hivi sasa Rich Mavoko hajatoa tamko lolote kuhusu  nini kinachoendelea Mpaka sasa Uongozi wa WCB haujatoa tamko juu ya tuhuma hizo.

WCB Watoa Zawadi ya Gari kwa Wasanii Hawa.

wasanii wawili kutoka wcb, mbosso na lavalva siku ya 8-8 wamekabidhiwa zawadi ya gari na uongozi wa wcb ikiwa kama ishara ya kazi nzuri wanayoifanya katika lebel hiyo.Hii sio mara ya kwanza kwa uongozi wa wcnb kuwa wakitoa magari kwa wasanii wao hasa pale inapoonekana kuwa na juhudi katika kazi zao za muziki na katika kuitangaza lebel hiyo .

Hata baada ya kupewa zawdi hizo za magari,wasanii hawa waili walioneka akuwa na furaha na hata kusikika lavalava akisema ‘ eeeh bwana  kama unavyoona , mambo yamefana.tukutane sheli ,mwabie na mwenzio , mr mbosso waambie wasikie kuwa aiefanya kazi na asile.”

Wasanii hawa waili wamepewa magari aina ya Toyota Harrier , huku moja ikiwa nyeusi na moja ikiwa ni rangi ya maziwa.

Jux na Vanessa Wamewapa Changamoto Diamond na Wasafi Festival

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux na Mpenzi wake Vanessa Mdee wamewapa changamoto kubwa Diamond na timu nzima ya WCB.

Jux na Vanessa ambao wamemaliza tour yao ya ‘In Love and Money’ ambayo imesemwa kufanya vizuri sana kuliko ilivyotegemewa wameonekana kuwapa changamoto WCB ambao nao wametangaza kuja na Tour yao ya Wasafi Festival.

Babu Tale ambaye ni Meneja wa Diamond na mratibu wa Wasafi Festival ameiambia Bongo 5, kwamba mafanikio makubwa na tamasha hilo ni changamoto kwa tamasha la Wasafi Festival ambayo litaanza kutimua vumbi miezi michache ijayo.

Hii ni ishara ya muziki unakuwa, nchi zilizoendelea kila mwisho wa wiki unajua kuna show kubwa, kwahiyo hii ni ishara nzuri ukiangalia Vanessa amejaza viwanja kibao. Mimi nikiwa kama kiongozi au mratibu wa Wasafi Festival inanipa changamoto naanza mkoa gani? sisi tunafanya show zaidi ya mikoa 12 na tunapiga na Dar es salaam inakuwa histori“.

Kutokana na mafanikio makubwa ya Tour ya Vanessa na Jux wasanii hao wametangaza kwenda nchini Rwanda, Burundi na Congo.

Diamond Ataja Siku Wasafi Fm Itaanza Kurusha Matangazo Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amefunguka na kutaja tarehe ambayo Wasafi Fm, itaanza kurusha matangazo yake rasmi.

Mwaka jana mwishoni Diamond Platnumz ambaye sio msanii tu bali Mfanyabiashara pia alitangaza kuwa anaingia Kwenye ulimwengu wa Media kwa kufungua radio station na television station ambazo ni Wasafi Tv na Radio.

Diamond Platnumz amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ni lini kituo chake cha radio cha Wasafi FM kitaanza kurusha matangazo kama ilivyo kwa kituo chake cha Runinga cha Wasafi TV.

Kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha Mayotte la 1ère cha kisiwani Mayotte ambapo yupo anafanya shoo Diamond alifunguka:

Nimefungua Tv inaitwa Wasafi TV na inafanya vizuri sana na tupo katika mikakati ya kuhakikisha inapatikana bara zima la Afrika na ulimwenguni kote. Lakini pia mwezi wa kwanza au mwishoni mwa mwaka huu tunafungua pia Wasafi FM itakuwa hewani”.

Wasafi Tv imekuwa hewani kwa kama Miezi miwili hivi na tayari imepata mafanikio makubwa sana ingawa haijaanza hata kurusha vipindi Rasmi na hata matangazo ya wadhamini lakini kwa maangalizo ya awali inaonekana Wasafi Tv inapita katika njia sahihi.

Almas Mzambele Afunguka na Kudai Babu Tale Ataiua WCB

Almas Mzambele ambaye alikuwa mfanyakazi wa WCB kwa miaka mingi kabla hajaonekana amefunguka na kudai mtu pekee ambaye ataiua WCB ni Meneja Babu Tale.

Almasi Mzambele alikuwa mtu ambaye alikuwa anashughulikia mambo ya mitandao ya kijamii WCB amefunguka kwa mara ya kwanza tangu ameondoka kwenye Label hiyo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Almas amefunguka mazito juu ya uongozi wa kampuni hiyo ambao ndio amedai una matatizo zaidi na unaweza kuua Label hiyo.

Tatizo pale lipo  kwenye uongozi wa WCB ambapo mwenye matatizo zaidi ni Babu Tale anayejiita meneja namba moja yaani anavuruga watu mpaka wanaacha kazi sio mchezo.

Babu Tale ndio mtu anayepelekea kuiua WCB kuna vitu vingi anakuwa anavifanya nyuma ya pazia ambavyo kama watu wangevifahamu sidhani kama wangetamani kumuona yeye anaendelea kuwa na Diamond kwa sababu naamini huko mbeleni sidhani kama tutaendelea kumuona Diamond huyu tunayemuona sasahivi”.

Lakini pia Almas aliendelea kutaja maovu ya Babu Tale:

Yaani kifupi tu Babu Tale ni mbinafsi na ni mmwinyi anapenda yeye ndio aonekane msemaji wa mwisho k a sababu ndio ametangulia kufahamiana na Diamond kwaiyo mkitofautiana mtazamo tu basi yeye anaanza kuleta visa vyake”.

Rayvanny Asitisha Ushindani Wa Kimavazi na Wasanii Wenzake

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka. WCB Rayvanny anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Chombo’ ameibuka na kutangaza Kumaliza ushindani wake wa kimavazi na wasanii wenzake huku akitaoa yeye ndio mshindi.

Sakata hili lilianza baada ya Dogo Janja kumtaja Rayvanny kama mmoja wa wasanii ambao haelewi anavaaga nini kwani hajui kujipangilia na kupendeza kitendo kilichomkera Rayvanny.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Rayvanny amesema kuwa anaamini ushindani upande wa mavazi anabaki kuwa yeye ni mwenye ujuzi na yuko katika viwango vya kuvaa vitu vya gharama zaidi hivyo hahitaji tena kushindana.

Akizungumzia hatua ya kutotaka tena kujihusisha na ushindani wa mavazi, Rayvanny aliongeza kuwa kwa sasa ana mambo mengi ya maana ya kufanya ikiwemo kujikuza zaidi kimuziki na kuandaa maisha mazuri ya mwanae JayDan kwa sasa na siku za Usoni.

Rayvanny ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chombo’ ambapo ametangaza ujio wa video siku yoyote kuanzia hivi sasa.

 

Babu Tale Aanika Ukweli Kuhusu Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Meneja wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Babu Tale amefungukia kwa mara ya kwanza tetesi zinazoendelea kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rich Mavoko katimuliwa.

Tetesi hizi zilianza wiki chache zilizopita baada ya Mavoko kutoonekana Kwenye tangazo jipya la Trailer ya Wasafi reality show lililowaonyesha wasanii wote wa WCB na familia ya Diamond.

Kwenye mahojiano  na Ijumaa kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa Marekani, Babu Tale alisema kwamba tetesi hizo siyo za kweli na Mavoko bado yupo WCB ila kipindi ambacho walikuwa wanachukua video ya Reality Show aliyoiposti Diamond ambayo ndiyo iliyozua maneno mwanamuziki huyo hakuwepo alikuwa kwao Mahenge, Morogoro kwenye msiba kwani alifiwa na dada yake.

Wakati tunarekodi hiyo video ya Reality Show, Mavoko alikuwa Mahenge kwao, alifiwa na dada yake kwa hiyo alikuwa kwenye msiba, lakini hizi siku zote yupo bize anashuti wimbo wake mpya na zamu inayokuja ni yake kuachia wimbo kwani sisi huwa tunaachiana muda wa kutoa nyimbo kwa hiyo sioni haja ya kuongopa kwamba hayupo WCB, kwa sababu hata asipokuwepo lazima itajulikana tu”.

Baada ya habari kuanza kusambaa Mavoko alimtafuta ili kuthibitisha taarifa hizo lakini alikataa kabisa kuongea na kutaka uongozi wake utoe majibu ya maswali hayo.

Mwarabu Fighter Athibitisha Bado Yupo WCB Hajafukuzwa Kazi

Bodyguard wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter ameibuka na kuweka wazi kuwa taarifa zilizosambaa kuwa amefukuzwa kazi sio za kweli.

Wiki chache zilizopita kuna taarifa zilisambaa kuwa Mwarabu Fighter amefukuzwa kazi na kudaiwa kuwa aliambiwa na Diamond akae nyumbani mpaka pale atakapopata taarifa.

Kwenye Interview na Global Publishers, Mwarabu amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa bado yupo WCB na anaendelea kufanya kazi na Diamond kama kawaida, kutokumuona naye ni kwa sababu ya taratibu za kiofisi ambazo hawezi kuziweka wazi ila siku yoyote tutamuona naye.

Taarifa za Mwarabu kufukuzwa ziliaminika kwa sababu aliokuwa anaonekana yuko Tanzania Wakati Diamond yupo na timu yake nchini Marekani kwa ajili ya Tour yake ya ‘A Boy from Tandale’.

 

Rayvanny Afungukia Suala la Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Rayvanny amefunguka kuhusu Tetesi za Msanii mwenzake Rich Mavoko kutimuliwa kutoka katika label hiyo.

Tetesi za Mavoko kutimuliwa WCB zilianza kusambaa mwezi uliopita baada ya kutoonekana Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na WCB ambao ulijumuisha wasanii wote wa label Lakini pia Mavoko hajaonekana Kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Rayvanny amesema hawezi kuliongelea sana suala hilo kwa sababu sio msemaji lakini amesema Rich Mavoko bado yupo na huwa wanawasiliana naye mara kwa mara:

Ujue sisi tunachekiwa kwenye group, leo kuna tukio hili na hili, so ukiona huyo kakosa ni masuala ya uongozi sana labda angekuwepo Diamond au Babu Tale angeweza kuongea sana lakini Mavoko yupo Wasafi kila siku.

Anakuja, anajiunga kwenye vitu lakini yeye kutokuja siku ile sijui sababu, kama kuna vitu vinavyoendelea ni yeye na uongozi. Mimi siwezi kuongea sana kwa sababu Mavoko ni mwanangu tunaongea tunachati, tunarekodi ngoma zetu“.

Lakini Hata hiyo Babu Tale alieleza kuwa siku hiyo Rich Mavoko alikuwa aki-shoot video ya wimbo wake mpya na kushindwa kuhudhuria.