Mange Kimambi Amtolea Povu Zito Wema Baada Ya Kutangaza Kurudi CCM

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni Mange Kimambi amemtolea povu zito muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kutangaza kuwa anahama Chadema na kurudi kwenye chama chake cha zamani CCM.

Habari zilianza kusambaa tangu mwanzoni mwa wiki hii kuwa Wema anampango wa kurudi CCM. Leo kupitia ukirasa wake wa Instagram Wema ameujulisha uma wa watanzania kuwa ameamua kuondoka Chadema na kurudi chama chake cha zamani CCM Wema alifunguka kama ifuatavyo:

Siwezi kuendelea kuishi kwenye nyumba inayonikosesha amani, Peace of mind is everything for me natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi Nyumbani there is no place like home….feels good to be back”.

Baada ya kutoa tangazo hilo la kuamua kurudi CCM Mange hakupoteza muda kutoa maoni yake juu ya kitendo alichofanya Wema, kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange alimwagia Wema povu hili:

Not sure what to say i only blame her for not being strong enough Nyerere alikaa jela for 27 years she could have taken 2 or 3 years ya hiyo kesi yake Kimara nzima imebomolewa nyumba na wanaishi sembuse yeye mwenye kubwa. Na lipshone zako walizozipiga marufuku so what?  Ungekomaa na msimamo wako serikali ingechoka kukuandama Wema your weak very weak! Hujawaangusha Watanzania tu umejiangusha wewe mwenyewe, your fans na Watu wote who cared for you”.

 

Wema Adai Anatamani Kufa, Aamua Kujiondoa Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu amerudi tena midomoni mwa watu baada ya kumwaga povu na kutangaza kuachana na mitandao ya kijamii.

Tetesi za Wema kuhama zimetawala mitandao ya kijamii kwa wiki nzima sasa tangu rafiki yake Steve Nyerere adai Wema atarudi tu CCM ingawa mwenyewe amekataa kuwa habari hizo ni za uongo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchana huu Wema amefunguka na kudai kuwa watu wanamsema sana hivyo amefikia uamuzi wa kuachana na mitandao ya kijamii kwa muda:

Ipo siku ntakufa hakuna mtu anayeishi milele sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndiio itakuwa ‘Maskini ya Mungu Dada wa watu alikuwa hivi na vile Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi’ Kuna muda mwingine huwa natamani Subhana Wata’ allah anichukue tu… Ya duniya ni Mengi sana…Kuna muda mwingine nakufuru Mwenyezi Mungu nakutamani nisinge-exist …Ila acha niendelee kumtegemea yeye kila jambo linatokea kwa sababu hili nalo litapita…I think I need time of social media…kwa mara nyingine tena…siwezi jamani….”.

Wema hajaweka wazi sababu gani illiyompelekea mpaka kuandika maneno hayo mazito au ni nani aliyemkasirisha kiasi hicho mpaka kufikia hatua ya kutamani angekuwa amekufa.

Mange: Muda Wowote Wema Sepetu Atatangaza Amerudi CCM

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni Mange Kimambi amefunguka na kudai kuwa muigizaji Wema Sepetu na Mama yake mzazi wamerudi CCM.

Wema alihama chama hicho mapema mwaka huu baada ya kukamatwa kwa kutuhumiwa kuuza na kutumia madawa ya kulevya. Baada ya kuachiwa huru Wema aliita vyombo vya habari na kutangaza nia yake ya dhati kabisa ya kuhamia Chadema.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Wema anampango wa kurudi CCM ingawa alikataa lakini leo asubuhi Mange kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kuwa Wema amerudi CCM:

Breaking News Wema Sepetu na mama yake wanarudi CCM very soon…Mimi nilijua tu nilipomuona Wema kaenda Rwanda kakacha tarehe ya mahakamani bilauoga nilijua tu kuna mkono wa CCM, kuna mtu Mkubwa CCM aliniletea taarifa kuwa nyumba ya mama Wema inabomolewa wasiporudi CCM wamepewa muda wa kufikiria, na notice ya kubomolewa nyumba wameshapewa. That’s their family house, ila kaniambia mama Wema kashakubali kurudi sahivi anam-convince Wema, kaniambia Wema keshakubali kurudi lakini anaona aibu ni jinsi gani atai-face jamii…yaani unaambiwa mama Wema alivyoambiwa nyumba yake inabomolewa fasta akakubali kurudi CCM. Na kesi kaambiwa akirudi CCM itakwisha vizuri ila akikataa kurudi kila siku atapelekwa mahakamani mpaka arudi na asiporudi anaweza kufungwa”.

Pia Mange aliendelea  kufunguka na kudai kuwa Ana uhakika asilimia 100 kuwa Wema atarudi CCM:

Kilichobaki ni Wema kutangaza tu kwaiyo Watanzanua kaeni sawa muda wowote Wema na Mama yake wanatangaza kurudi CCM na wakisharudi CCM Magufuli habomoi nyumba zao na wakirudi wameambiwa lazima wamsifie na waseme wameona Chadema haifai na yeye ndio anafaa”.

 

 

Msambwanda Wa Wema Wazua Gumzo Mtandaoni (picha)

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu maarufu kama ‘Tanzania Sweetheart’ amezua gumzo mtandaoni / Instagram baada ya kuweka picha zake zilizochora umbo lake.

Msambwanda wa Wema umezua gumzo mtandaoni baada ya kuweka picha zilizomuonyesha akiwa amevaa mavazi ya kumchora umbo lake. Wasanii mbali mbali wa Bongo fleva wakali kama Diamond na Aslay wamemuimba Wema na shepu yake hiyo matata.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Wema akiwa nchini Rwanda alihudhuria sherehe inayojulikana kama Instagram party ambapo alipiga picha mbali mbali ambapo picha hizo ndizo zilizozua gumzo huku kila mtu akifunguka lake juu ya msambwanda wake wa haja.

Hizi ni baadhi tu ya picha za Wema Sepetu zilizozua gumzo mtandaoni:

 

 

 

 

.

Wema Atoa Siri Ya Kupungua Kwa Mwili Wake.

Watu wamekuwa wakishangaa na wengine wakisema vibaya pale wanapoona mtu fulani amekonda kwa ghafa, alianza Gigy Money ambae watu walisema sana kuhusu kukonda kwake na baadae Gigy Money alikuja kusema kuwa alikuwa akifanya diet na kunywa dawa za kupunguza uzito.

Hivi karibuni baadhi ya mashabiki wa msanii Wema Sepetu walianza kuongea katika mitandao kuhusu kupungua kwa mwili wa mpenzi wao wema sepetu na kuwa ameanza kukonda na kuisha kabisa huku kila mmoja akitoa sababu zake tofauti huku zingine zikienda katika upande wa afya yake.

Akiongea na gazeti la ijumaa wema sepetu amewajibu mashabiki wake na kusema kuwa sio kweli kuhusu watu wanavyosema vibaya kuhusu afya yake bali ameamua kupunguza mwili wake kwa sababu amona kuwa unaongezeka kila kukicha bila kuwa na staa ya kuvaa baadhi ya nguo.

Unajua nilikuwa nikiangalia kila nguo ninayovaa inanibana.wakati mwingine unakuta nguo ni kubwa kabisa lakini hainotoshi kabisa.nikaona nina kila sababu ya kupunguza mwili wangu  ambao sio hata mzuri hata kwa afya-Alisema Wema sepetu.

Muonekano wa Wema Sepetu wa sasa

Hivi karibuni Wema Sepetu alikuwa nchini  Rwanda ambapo alikwenda katika instagram party ambapo alikutana na mashabiki na watu wake wanaomfuatra katika mtandao wa instagram.

 

Wema Sepetu Ajitapa Kuirudisha Bongo Movie Kwenye Ramani Kama Enzi za Kanumba

Muigizaji wa Bongo movie, Wema Sepetu amefunguka na kudai kuwa yeye ndio muigizaji wa Bongo movie aliyeirudishia heshima tasnia ya Bongo movie iliyopotea tangu kifo cha Kanumba.

Marehemu Steven Kanumba alikuwa mmoja wa wasanii wa Bongo movie aliyepata jina na hadhi kwa kuwa msanii aliyejaribu au kuthubutu kuipeleka sanaa ya Bongo movie mbali zaidi. Kanumba alithubutu kuifikisha Bongo movie nje ya Tanzania kwani alicheza filamu na wasanii mbali mbali kutoka nchi mbali mbali kama vile Nigeria.

Tangu kifo cha Kanumba miaka mitano iliyopita sanaa ya Bongo movie imeshuka kwa kiasi kikubwa viwango vya filamu hizo zimeshuka na kupelekea kupoteza soko lake kwani wanunuzi wa kazi hizi hawaoni ubora hivyo wameacha kuzinunua wala kufatilia.

Wema Sepetu alisafiri wiki hii iliyoisha kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya kazi zake kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio Wema alifunguka yafuatayo kuhusiana na  tasnia ya Bongo movie:

Zamani Bongo movie ilikuwa inafanya vizuri sana enzi za marehemu Steven Kanumba, alivyofariki ikawa kama na yenyewe ikafa. Tumekuwa tukiomboleza kifo chake na kifo chake kimetusababishia mazingira mabaya sisi kama waigizaji kwa sababu tuko kwenye fani moja. Wengi wetu tumejikuta watu wanaona kama Bongo movie kama haina mashiko”.

Pia Wema alifunguka kuhusu jitihada alizofanya kuirudishia heshima sanaa ya Bongo movie:

Kwa Bahati nzuri mimi nimeweza kuirudisha  bongo movie pale ilipokuwa wakati Kanumba yupo hai baada ya kutoa filamu yangu mpya ya Heaven sent. Bongo movie kiukweli ilikuwa imelala mpaka nilipozindua App yangu na kuiweka na halo ndo watu walipopata muhemko”.

Mama Mzazi Wa Wema Akutana Na Cha Moto Mahakamani

Ikiwa leo ni tarehe ya kusikilizwa kwa kesi ya Wema Sepetu ambayo bado ilikuwa kwenye muendelezo , na huku Wema Sepetu akionekana  katika mitandao ya kijamii akiwa nje ya nchi alipokwenda kwa ajili ya special appearance katika instagram party nchini humu, mama mzazi wa Wema Sepetu alikwenda mahakama kwa ajili ya kutoa hudhuru ya mwanadada huyo.

Katika kesi iyo wakili wa serikalai  Augustino  Michael aliitaja kesi iyo mbele ya hakimu  Simba na kusema kuwa ndio ilipaswa kushughulikiwa kwa muda huo lakini kitu cha  ajabu mama mzazi wa Wema Sepetu alinyoosha mkono na kuomba kupatiwa nafasi kuwa alikuwa ana jambo anataka kulisema.

Baada ya kunyoosha , hakimu alimpa nafasi mama huyo na mama huyo alisema kuwa Wema Sepetu amepata hudhuru na kushindwa kuhudhuria katika kesi hiyo huku akisema kuwa alikuwa amepata msiba wa kufiwa na shangazi yake.

Mheshimiwa Wema amepatwa na hudhuru ya kufiwa na shangazi yake kwaio amekwenda kushghulikia swala  la mazishi, ndio maana ameshindwa kuhudhuria  mahakamani hapa leo, na mimi mama yake nimekuja kumuwakilisha.

Hakimu anaeshughulikia kesi hiyo alipomaliza kusikiliza hudhuru hiyo alimuuliza mama huyo kama Wema amepata msiba na kushindwa  kufika  mahakamani imekuwaje yeye mama yake ameweza kupata muda wa kufika hapo.

Hakimu alimuonya mama yake Wema na kumwambia kuwa siku nyingine hapaswi kufanyia mchezo swala kama hilo la kutokufika mahakamani hapo. Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 14 December mwaka huu.

Wema anakabiriwa na kesi ya kukutwa na kutumia madawa ya kulevya.

Hata hivyo taarifa za kutokufika mahakamani kwa Wema zimekuwa hazina ukweli wowote kwa sababu msanii huyo amekuwa akionekana akipost katika ukurasa wake wa Instagram kuwa yupo nchi ya jirani kwa ajili ya kukutana na mashabiki wake na watu wa nchi hiyo ambao wanatumia mtandao wa instagram.

Huu Ndio Ushauri Wa Wema Sepetu Kwa Wanawake Kuhusu Wanaume

Muigizaji maarufu wa Bongo movie Wema Sepetu amewapa wanawake wenzake ushauri juu ya wanaume na mahusiano kwa ujumla.

Wema akiwa mmoja Kati ya watu maarufu Tanzania anaweza akawa anatazamwa na watu wengi kama role model kutokana na ushawishi aliokuwa nao kwa watu.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Snapchat, Wema kaamua kuandika ujumbe maalumu ambao amewapa ushauri wanawake au wasichana katika suala zima la mahusiano ya kimapenzi ambapo Wema amewapa wanawake njia za kujua endapo mwanaume ameyachoka mapenzi na anataka kusepa.

Wema amefunguka yafuatayo:

To my ladies mwanaume akikuchoka utamjua tu….Ni visababu vya kijinga ndio vinamfanya afanye big deal….when your man starts acting up funny for no reason mpe  space yake….Usimnag sana He wants space give him a football pitch…Don’t kiss azz!”.

Wema amewapa ukweli wanawake kuwa mwanaume akikuchoka kwenye mahusiano utamjua tu vitu vidogo vinakuwa vikubwa atatafuta tu kisababu kidogo ilimradi tu akununie na kama mwanamke umetambua hilo mwache mpe nafasi ya kufanya mambo yake usijipendekeze wala usimshobokee kiivooo.

 

Wema Sepetu Apokelewa Nchini Rwanda Kama Malkia, Hii Ndio Sababu Iliyompeleka

Muigizaji maarufu wa filamu za Bongo movie, Wema Sepetu amepokelewa kama malkia nchini Rwanda siku ya Jumatano ambapo ilikiwa ni mara yake ya kwanza kufika nchinni humo ambapo ameenda kwa ajili ya kuhudhuria tamasha.

Wema amewasili nchini Rwanda na kupata mapokezi makubwa na kuonyesha ni jinsi gani anapendwa nchini humo, pia sio tu ameenda nchini humo kwa ajili ya kwenda kutalii bali ameenda kikazi kuhudhuria tamasha la KFM Instagram party.

Wema ameenda Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la KFM Instagram party, tamasha lililoandaliwa na kituo cha KFM lenye lengo la kuwakutanisha wqtumiaji wote wa mtandao huo siku ya tarehe 24 Novemba katika ukumbi wa Chillax lounge, Nyarutarama nchini Kigali, Rwanda.

Kwenye mahijiano aliyoyafanya na kituo cha redio cha KFM huko Rwanda Wema amefunguka haya kuhusiana na tamasha hilo:

Ndio mara yangu ya kwanza nafika Rwanda na ninaweza nikasema vile vitu nilikuwa nasikia kuhusu Rwanda ama kweli nimeviona, nimekuja kwenye tamasha la Instagram party ni kitu kizuri kwa sababu mimi nimekuwa ni queen wa social media na sio nimejipa mwenyewe icho cheo bali ni watu, naamini siku hiyo itakuwa muda muafaka wa watu kukutana na Mimi na kupiga picha na kupiga stories mbili tatu ili watu waweze kupata taswira kamili kuhusu mimi kipenzi cha wengi kutoka Tanzania”.

 

.

Wema Aingia Katika Majibizano Ya Kisiasa Na Steve Nyerere

Msanii wa filamu Tanzania Wema Sepetu amejikuta akijibizana na msanii mwenzie Steven Nyerere katika mtandao wa instagram baada ya msanii huyo kuandika maneneo ambayo kwa namna  moja ama nyingine yanaonekana kumlenga mwanadada huyo.

Katika ukurasa wake wa Instagram Steven Nyerere aliandika maneno ya pongezi kumpongeza mwanasheria alberto msando kwa  maamuzi yake ya kuamua kuamia katika chama cha CCM hapo jana na kukabithiwa uanachama wa chama hicho mheshimiwa raisi,hata hivyo akiwa kama mmoja wa wanachama wa CCM, Steve Nyerere alimpongeza Albert Msando  lakini pia alisema kuwa kuna msanii mmoja wa kike alikuwa amehama chama hicho anapswa kuiga mfano wake na kurudi kundini .

Ambapo kwa uhalisia wa hivi karibuni , wema sepetu ni moja ya wasanii wa kike walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi lakini walibadilisha uelekeo na kuamia kuhama chama hicho na kuamia Chadema.

Hata hivyo baada ya posti hiyo Wema Sepetu alionekana kuguswa na maneno hayo na kuamua kumjibu Steve Nyerere katika uwanja wa komenti na kumwambia kuwa ana imani kabisa kuwa anaeongelewa katika post hiyo sio yeye na kama ni yeye basi hana mpango wowote wa kurudi CCM tena.

HAHAHAA  SASA UTAKUWA MZALENDO WA KWELI ,MSANDO NAESHIMU MAAMUZI YAKO MAANA NI MAAMUZI SAHIHI , KWAKO PAMOJA NA FAMILY YAKO,RAFIKIZAKO,NASI TUPO PAMOJA NAWE,SOON NA YULEEEEEE RAFIKI YETU,DADA YETU MSANII MWENZETU NAYE YUPO NJIANI KUDUDI NYUMBANI ,COMING BACK TIVU,WELCOME MSANDO.

Ambapo baada ya hapo Wema Sepetu alijibu chini yake,

i hope hauniongelei mimi…maana mawazo hayo sina.

Ikumbukwe kuwa Wema Sepetu na mama yake mzazi walitangaza kujiunga na Chadema mwaka huu na kusema kuwa wamechoshwa na siasa za chama tawala.

Diamond: Wema ni Mshkaji Wangu Nawajua Mabwana Zake Wote

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz anaweza akawa ni mmoja kati ya msanii ambaye anaongelewa sana iwe kwa mziki wake au hata maisha yake binafsi lakini watu wengi wanavutiwa na Diamond kutokana na maisha yake binafsi hasa mahusiano yake.

Pamoja na kuwa ni kipindi kirefu kimepita tangu Diamond ameachana na aliyekuwa mpenzi wake muigizaji Wema Sepetu na sasa yupo na Zarinah Hassan lakini cha ajabu ni kuwa bado Diamond anahusishwa sana Wema tofauti na wasanii wa kike wengine waliowahi kuwa na uhusiano na Diamond kama vile Penny, Jokate, Wolper na wengineo.

Ingawa watu wengi wamezidi kueneza habari mbali mbali kuwa Diamond na Wema bado wanaonana hadi kufikia hatua ya kuonekana wote nyumbani kwa Diamond.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Dizzim Online siku za nyuma Diamond amefunguka na kueleza kwa nini bado anahusishwa sana na Wema na uhusiano wao ulivyo kwa sasa;

Wema alikuwa mpenzi wangu tukagombana tukawa maadui wakubwa sana japokuwa tulikuwa tunaficha lakini tulikuwa tuna uadui mkubwa ndani yake yaani ilikuwa mtu alikikaribiana na Wema tu simzimii maisha kama ni WCB nakufukuza kazi nikiona unajihusisha na Wema baadae bifu likaisha sahivi tumekuwa washkaji tunashirikiana katika mambo mbali mbali kama kuna kitu kinahitajika namsaidia na yeye hufanya hivyo hivyo lakini Wema nimoja kati ya wanawake ambao nilipata wakati mgumu sana kuachana naye coz niivyoachana ilikuwa hata kukutana naye sitaki Simu yake akipiga nakata yani ilikuwa ni vita mtindo mmoja”.

Lakini pia Diamond ameendelea kufunguka kuhusiana na uhusiano wake na Wema kwa sasa;

Nashukuru Mwenyezi Mungu ameweka mkono wake na sasa tumekuwa washkaji nimeshakutana naye sehemu tofauti tofauti akiwa na bwana ake na unajua sahivi mabwana zake wote anaokuwa nao nawajua yaani nikikaa sahivi najua Wema analiwa na huyu lakini pia yuko na mwanaume huyu kwa sababu naweza nikaongea naye anaweza akawa na stress za mwanaume wake basi ananiambia anaweza akawa analia basi mi nampa ushauri namwambia Fanya hivi na hivi kwaiyo ni mtu ambaye naheshimiana naye kwaiyo watu wasije wakahisi kuna michezo inayofanyika chini kuwa tunalalana hapana kwa kweli tumekuwa washkaji tu”.

Dkt. Louis Shika ‘900 Itapendeza’ Amefunguka Kuvutiwa na Wema Sepetu

Dr. Louis Shika anayejulikana kama bilionea wa nyumba za Lugumi au 900 itapendeza amefunguka kuwa moja Kati ya mastaa wa kike wanaomvutia nchini ni muigizaji maarufu wa Bongo movie Wema Sepetu.

Dr. Louis Shika alipata umaarufu nchini wiki chache zilizopita pale alipoenda kwnye mnada ambapo kulikuwa kunauzwa nyumba tatu za kifahari zenye thamani za mabilioni. Baada ya kushinda minada yote mitatu na kufanikiwa kununua nyumba hizo Dr. Shika alitakiwa kulipia asilimia 25 ya pesa zote kwa nyumba zote tatu lakini hapa kizazaa ndipo kilipozuka kwani ilijulikana kuwa Dr. Shika hakuweza kulipia pesa hizo kwani aliposachiwa mfukoni hakuwa na hata senti.

Baada ya sakata hilo kutokea Dr. Shika alipelekwa polisi alipokaa kwa siku kadhaa mpaka pale alipoachiwa huru, kuanzia hapo mzee huyo amepata umaarufu wa ghafla kwani kila sehemu atakayoenda waandishi Wa habari wanamfata na kumpiga picha kitendo kinachomfanya kuwa kivutio cha watu wengi.

Dr. Shika au maarufu kama bilionea wa nyumba za Lugumi amefunguka na kudai kuwa ‘Tanzanian sweetheart’ Wema Sepetu ni moja kati ya mastaa anaowakubali sana nchini panini pia amekiri kuwa mastaa wengine anaowakubali na kuvutiwa nao ni pamoja na mwanamuziki Ray C na mchekeshaji Ebitoke.

Martin Kadinda Kafunguka Kuhusu Lipstic Za Wema Kupigwa stop

Mwanamitindo Martin Kadinda ambaye ni meneja na rafiki wa karibu wa muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ameongelea suala la lipstic zinazojulikana kama ‘Kiss by Wema’ za mwanadada huyo kupigwa stop mapema wiki.

Mapema mwanzoni mwa wiki hii habari zilienea kuwa serikali  kupitia mamlaka ya dawa na chakula (TFDA) pamoja na Shirika la viwango nchini (TBS) limezifungukia bidhaa za Wema kwa kile walichodai kuwa rangi hizo za midomo hazina viwango vyovyote na pia hazina ubora kwa matumizi ya binadamu.

Baada ya taarifa hizo kuenea kwa kasi ya ajabu mtandaoni Martin amefunguka na kudai kuwa yeye kama meneja wa Wema hana taarifa hizo. Kwenye mahojiano aliyoyafanya na TVE  Martin amefunguka kuwa wao walikuwa na vibali vyote kutoka TFDA na TBS kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaaa hizo kwa hiyo haelewi taarifa hizo zinatokea wapi:

Hatuna taarifa kwa sababu vibali vyote vipo na tunavyo na bidhaa hizo za lipstic zimeshaenda sokoni na zilishaisha, kwa hiyo sisi kama sisi hatuna tena bidhaa hizo zipo sokoni, kama ni mtu aliamka akaamua kuandika hayo na kutangaza ninachoweza kusema ni all the best kwake sisi mzigo ulishakwisha Wema alitengeneza products za kwanza na sasa anakuja na products nyingine”.

Tangu skendo hii itokee ya kufungiwa bidhaa zake watu mbali mbali wamekuwa wakiongea na kudai kuwa kuna mtu anayemfanyia Wema mchezo mchafu ambao unahusishwa na mambo ya kisiasa.

Wema Aamua Kukaa Kimya Kuhusu Bidhaa Zake Kufungiwa Na TFDA

Sio kawaida ya mwanadada Wema Sepetu kukaa kimya kwa muda mrefu kwa mashabiki wake hasa linapotokea jambo lolote kumuhusu yeye, lakini kwa sasa Wema amekuwa kimya sana kuhusu sakata lake la bidhaa zake kufungiwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA.Ikiwa ni kwa muda kidogo ulipita  tangu kuzagaa kwa tetesi hizo ambazo zilikuwa hazina uthibitisho wowote huku mwanadada huyo  akiamua kukaa kimya ndipo moja wa watu wake wa karibu kuamua kumuongelea na kukanushakuwa sio kweli kwamba bidhaa hizo zimefungiwa bali wapo katika kufata taratibu za kuingiza mizigo bandarini.

Wiki iliyopita ya November 11, TFDA ilithibitisha kuifungia bidhaa hiyo ya  lipstick inayojulikana  kama Kiss by Wema Sepetu   na kusema kuwa haikuwa na kiwango cha matumizi kwa wateja.Hata hivyo jambo la kushangaza ni kwamba hakuna tamko lolote lililotolewa na Wema Sepetu mwenyewe katika page zake wala katika vyombo vya habari  kitu ambacho so kawaida kwa mrembo huyo ambae alikuwa na tabia ya kufunguka inapotokea jambo lolote kumhusu, zaidi sana ameonekana kufanyia promo application yake inayopatikana katika Playstore.

Miaka mitatu iliyopita Wema Sepetu alizindua bidhaa hiyo ambayo ikiingia sokoni na kupendwa na watu wengi na kufanya vizuri kila kona ya Tanzania, lakini ishu ilikuja baada ya mzigo wa kwanza kuisha ndipo walipoamua kuagiza mzigo mpya ambao umezuia na mamlaka ya chakula na dawa kuingizwa sokoni.

Akiwa kama mfanyabishara na mpendwa na watu wengi, Wema Sepetu amekuwa akisubiriwa na mashabiki na wateja wake ili aweze kuliongelea swala hilo kwa undani ingawa yeye mwenyewe anaonekana ku-mute, hii inawezekana labda kwa sababu swala hilo liko katika mikono ya mamlaka husika, lakini mashabiki hawapaswi kufa moyo .

Wema sepetu kwa sasa amerudi kwa kasi katika kutangaza application yake akiwa kama mwanamke wa kwanza afrika kuwa na aplication yake katika playstore inayozungumzia maisha yake.

Harmorapa: Naamini Kuna Siku Wema Sepetu Atakuwa Mpenzi Wangu

Mwanamuziki na rapa anayeongoza kwa kupenda kiki ‘Harmorapa’ amerudi tena kwenye vichwa vya habari na kufunguka kuwa ana imani kuwa ipo siku atakuja kumuoa muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu.

Siku za nyuma kidogo Harmorapa hakusita kuweka hisia zake hadharani na kusema kuwa anampenda Wema Sepetu na ndoto yake kubwa maishani ni kumuoa na awe mke wake, kitu ambacho kilimpa sana harmorapa lakini Wema aliibuka na kumkataza Harmotapa kutumia jina lake ndipo pale Harmonize alipogeuza kibao na kuanza kumponda Wema kwa kumuita Bibi.

Siku mbili zilizopita Harmorapa aliibuka tena na kuonyesha hisia zake kuwa hata kama muda umepita Lakini bado hisia zake juu ya Wema ziko pale pale. Harmorapa amedai kuwa naye anaamini ipo Siku atatimiza ndoto yake ya kumuoa Wema kama Dogo Janja alivyobahatika kumuoa Uwoya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmorapa alifunguka mazito juu ya kipenzi chake Wema:

Dah Naamini sana katika ndoto, kuwa ipo siku ndoto unayoota kuwa kuja kweli sina la kuongeza zaidu ya kumpa hongera Dogo Janja kwa kutimiza ndoto yake ya kumuoa Irene Uwoya naamini ushupavu wake na kumemfanya kutokuvunjika moyo ndio kumemfanya leo hii akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake…Nami sivunji imani naamini ipo Siku Wema Sepetu atakuwa wangu ugumu alioupata Janjaro umenipa matumaini kikubwa ni kutulia na ndoto yangu  na kulenga ipo siku itatimia…one day you will be mine Wema Sepetu”.

Baada ya Dogo Janja kufanikiwa kumuoa Uwoya ameonekana nimfano wa kuigwa kwa vijana mbali mbali huku akiwapa somo la uvumilivu na kuamini kuwa ipo Siku yatatimia, Wema Sepetu hajamjibu bado Harmorapa lakini inajulikana kabisa Wema atakuwa hajafurahishwa na kitendo hicho.

 

Wema Sepetu Aonyesha Hisia Zake Kwa Lazaro Nyalandu


[one_third] Contents [/one_third]Ikiwa ni muda mchache tu umepita tangu mbunge wa Singida Kaskazini kujiuzulu na kuitema ccm, msanii wa filamu nchini Madame Wema Sepetu amefunguka na kuonyesha  hisia zake za furaha kuhusu tukio alilofanya mbunge huyo na kusema kuwa anatamani kuwa kama Nyalandu, lakini pia ameonyesha shukranii zake kwamwenyezi munu na furaha kwa hali nzuri anayoendelea nayo Tundu Lissu

Katika ukurasa wake wa instagram msanii Wema Sepetu  alipost picha ya tundu lissu akiwa hospitali na kuonyesha pia  furaha yake kwa jinsi mbunge wa Singida mashariki Mh. Tundu Lissu anavyoendelea vizuri kwa sasa.

Ni jambo jema kuona shujaa wetu anaendelea vyema,Mungu ni mwema siku zote,lakini pia nikiwa mkubwa nataka kuwa kama Lazaro Nyalandu.Aliandika Wema Sepetu.

Wema Sepetu ni mmoja wa  wasanii wenye ushawishi mkubwa sana Tanzania kupitia mtandao wake wa instaram, hivyo Wema sepetu amekuwa akitumia fursa hiyo ya kupendwa na watu kufanya kampeni zilizowahamasisha watu  na mashabiki wake  kwa ujumla ili kuweza kumchangia mbunge huyo ela za matibabu ili aweze kujikimu na familia yake  kwa kipindi chote ambacho anapokuwa  yupo hospitali.

Wema Sepetu  ni mmoja wa makada na wanachama wa chadema, hivyo kitendo cka kuwa naonyesha ushirikiano katika chama hicho ni moja ya fadhila kwa viongozi wake,kitendo ambacho alikianza muda mrefu cha kuwaomba mashabiki wake na watu wenye kutaka kumchania waendelee kumchania mbune huyo ili aweze kutibiwa na kupona.

Hata hivyo Lazaro Nyalandu ambae amejiuzulu , ameomba nafasi ya kuinia katika chama cha chadema kama kuna nafasi , hii inadhihirisha kuwa yupo tayari kuamia katika chama hicho.Lakini pia ikumbukwe kuwa Mh.Lazaro Nyalandu pia alishawahi kutaka kufanya ufadhili wa matibabu wa Mh. Tundu Lissu ingwa ilishindikana.