Gigy Money Na Amber Lulu Watoa Povu Juu Ya Mahali Wanapoishi

Baada kusemwa kwa muda mrefu kuhusu kukaa katika mitaa ambayo hayaendani na umaarufu wao, wasanii wawili wa kike ambao hawaishiwi drama katika mitandao ya kijamii kila siku na wamekuwa marafiki kwa muda mrefu Amber Lulu na Gigy Money wameamua kuwatolea uvivu wasanii na mashabiki ambao wamekuwa wakiwasema kuwa mahali wanapokaa hapalingani na hadhi yao kimuziki.

Maneno haya yanakuja baada ya kusambaa kwa video ilikuwa ikimuonyesha Gigy Money akigombana na mama mwenye nyumba ana mjumbe wa nyumba kumi huko mtaani kwao na huku mahali hapo pakionekana ni uswazi sana na mazingira hayo hayalinganai na maisha ya msanii tena hasa Gigy Money ambae  muda wote amekuwa akijitamba kuwa yeye ni moja ya wasnii wa kike wenye ela sana.

Baada ya kusambaa kwa tetesi hizo , Gigy Money akiwa na rafiki yake Amber Lulu waliposti  video katika ukurasa wa instragrama na kuongea kuwa watu wanaowasema kuwa wanaishi katika mazingira  yasiyoendana na wao wanasema tu lakini ukweli utababki kuwa kila mtu anaishi kulingana na  hali yake ana wengien wamekuwa wakiwasema hivyo wakati wao wenyewe wamekuwa wakisaidiwa kukaa mjini na kuwa wengine wansahau kuwa  wakati wanakuja mjini walipokelewa na hao hao wanaowasema.

 Watu wangu wa instagram kuna ujumbe nataka niwape najua tunapendana lakini Ifike sehemu tuambiane ukweli unafikiri kwako kukiwa na mazingira mazuri utaza kutoka nyumbani kwako na kwend akutembea sehemu zigine nzuri,bora kwako pawe pabaya ili uweze kutoka na kuwa unatembea tembea,pangeni vijumba vibovu ili mpate muamko wa kutembea.kwanz mnasema tuna nyumba mbovu hizo nyumba mbovu nyie wengine mnazo, mnatoka vijijini tunawapokea kwenye nyumba hizohizo mbovu. kwanza wengine kazi kushindwa mahotelini na kwa mashosti kila siku kutembea na vifuko vya rambo.

nyumba mbaya mmetulipia kodi, wengine  mnatoka vijijini na vifuko vya rambo lakini leo mnatuambia nyumba mbaya, tena mko**

Gigy Money alikumbwa na skendo hiyo ya kugombana na mjumbe wa mtaa anaokaa na baada ya kuambiwa akaombe msamaha alikata.

Gigy Money Amshauri Young Dee Kubaki Na Amber Lulu

Msanii wa kike ambae kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha ‘nampa papa’, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, mwisho ni mwa wiki iliyopita alijikuta akitoa povu zito kwa msanii mwenzie wa kiume anaejulikana kama Young dee kutokana na muenendo mbaya alionao katika mahusiano.kwa mujibu wa Gigy Money, Young Dee ni shemeji yake kutoka kwa Amber Lulu ambae pia ni msanii wa Bongo fleva lakini pia aliyekuwa na anaendelea kuwa moja ya ma-video queen wanaofanya   vizuri katika videos za wasanii mbalimbali wakubwa  nchini.

Gigy Money  alisikika akisema kuwa katika wanawake wote aliokuwa nao Young Dee ni msichana mmoja tu Amber Lulu ndie mwenye mapenzi ya kweli kwake sio hao wengine wanamchukulia kama kikatuni .Maneno hayo yalianza baada ya wasnii hao wote watuatu walipokutana nje ya jengo la EATV, wakitoka katika mahojiano ya kipindi cha Friday Nite Live ambapo , Amber Lulu aliona baadhi ya alama za kucha na vidole katika shigo ya Young Dee na kuanza kumshangaa na kumtuhumu kuwa itakuwa alikuwa katika ugomvi na mwanamke mwingine,

Kutokana na tukio ilo Gigy Money alipewa nafasi ya kuongea na kusema kuwa “Young Dee apunguze mitandao ya wanawake, maana inamchanganya wakati ukimwangalia umri wake ni mdogo sana,atulie tu na Amber Lulu maana katika wanawake wake wote mia  Amber Lulu ana mapenzi ya kweli kwake,wengine wote wanafata jina tu ilo la bongo bahati mbaya ,wanamuona kama kinyani wanamtakataka” alifunguka  Gigy Money ambae aliweka wazi pia kuwa kumbe wawili hao walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi.

Amber Lulu na Young Dee walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda kidogo uliopoita huku wakikataa kuwa katika mahusiano hayo, ilifikia hatua mpaka Amber Lulu aliamua kuchora tattooo ya jina la  Young Dee mkononi lakini walipogombana Amber Lulu aliamua kufuta tattoo iyo, hivi karibuni pia kuna picha zilisambaa za amber lulu na Young Dee , picha ambazo ziliwafanya wawili hao kupelekana polisi .

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.