Msanii wa bongo fleva khadija shabani taya, maarufu kama keisha ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM (NEC) siku ya mei 28 mwaka huu.Taarifa hizo zimetolewa na katibu mwenezi wa chama hicho bwana hamfrey polepole siku hiyo baada ya kutoka katika kikao cha kamati kuu ambapo ndipo uteuzi huo ulipofanyika.
Keisha ambae ni msanii wa siku nyingi aliingia katika siasa na kugombea ubunge UVCCM mkoani Dodoma na kushinda katika kura za maoni lakini alishindwa kuendelea mbele katika uchaguzi mwaka huo.
Hongera kwake kutokana na jitihada nyingi alizowahi kuzionyesha katika siasa na nia yake kubwa ya kuthubutu.