Aisha Asema Neno Kuhusu Watoto Walioshinda Tuzo za SZIFF

Mwanadada mkongwe katika ukuaji wa sanaa hasa ya filamu nchini,  AISHA kutoka kundi la siku nyingi la maigizo la MAMBO HAYO, amefunguka na kutia neno katika tuzo za filamu Tanzania zilizotolewa wikiendi iliyopita zikiwa zimeandaliwa na AZAM TV.

Aisha anasema kuwa pamoja na kwamba wanalengo la kukuza vipaji lakini wamekosea sana kuwapa TUZO hizo watoto wadogo ambao ni wasanii wachanga na hata vipaji vyao bado havionekani kama vinaweza kushindwanisha na wasanii kama Wema sepetu , Gabo na hata Monalisa kama walivyofanya.

Aisha kutoka mambo hayo aliandika kwa kusema ”

Nimetoka kuangalia sinema zetu! Nilibahatika kuiona kidogo Filamu ya kesho! Msema kweli mpenzi wa Mungu watoto walioshinda kwenye uigizaji bado kabisa! Wanajikanyaga mno! Bado hawajakomaa kabisaa!! Kwenye uchezaji!! Hata mai zumo ni bora Mara Mia! Kuwapa ushindi dhidi ya wema, Monalisa, gabo , johari, phd na wengine ? sijui ni vigezo vipi wametumia! Kama ni kura tu ni kura zipi zilizopigwa kuwazidi wakongwe waliokuwa wanapigiwa usiku na mchana? Je hawa watoto wapo nyuma ya Nani? Nani kafanya hili deal litiki? Mimi ile naiita Aibu ya mwaka! Ni Aibu kubwa sana sana kwenye tunzo za sinema zetu! Yaani uigizaji ule ndio uwafanye wewe bora? Wenzetu wa Kenya, Uganda, nigeria wakibahatika kuiona filam ya kesho na kuwaona wale watoto wanavyoigiza eti ndio waigizaji bora si Aibu hii jamani? Hiki ni kichekesho kilichopitiliza kwa kweli! (hayo ni mawazo yangu tu mhenga Mimi)nimeudhika mpaka nimetoa povu Leo!”

Wasanii wengi wamelalamika sana kuhusu Tuzo hizo wa sababu wasanii waliopata tuzo hizo hawakutegemewa wala kujulikana katika tasnia ya filamu nchini na hata kazi yao haijajulikana sana kama ilivyokuwa ikitegemewa .

Filamu za Bongo Movies Mbovu :-Dr Cheni

Mchezaji wa filamu wa bongo movies wa muda mrefu, dr cheni amefunguka na kusema kuwa kwamwe hawezi kujutia kauli yake ya kuwa wasanii wa bongo movieshawazalishi muvi nzuri kwa sasa kama zamani.akiongea na Clouds media mapema leo Dr cheni anasema kuwa kamwe hawezi kujutia kusema kauli hiyo kwa sababu ina ukweli ndani yake.

Dr Cheni aliwahi kusikika akisema kauli hiyo na baada ya hapo wasanii waliibuka na kusema kuwa amewavunja sana moyo, lakini cha ajabu ni kwamba hata baada ya kuulizwa leo Dr cheni anasema kuwa hajutii kusema hivyo zaidi ya kuwataka wasanii kujifunza kutokana  na kauili yake.

Dr cheni kwa kuendelea kusiisistiza kauli ya kuwa hatokaa aangalie filamu za bongo , amewataka pia mashabiki kuacha kuziangalia mpaka pale watakapotengeneza zenye ubora.

.Anasema ‘mtitu alitakiwa alifanyie kazi hilomkwa sababu inawezekana ni kweli kuwa filamu za sasa hazina bora, angenihakikishia kuwa kuna filamu yake ina ubora wa kiasi gani na ndipo aweze kupinga kwa hoja,  hatuna haja ya kutengeneza fialmu mbovu na nina waambia mashabiki wasiangalie filamu za bongo movies  mbovu.”

Wasanii Wamekimbilia kulima Matikiti na Kuuza Chakula :-JB

kama ambavyo wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu kudumaa kwa bongo movies , na kusema kuwa wasanii wengi wamejikuta wakiingia katika biashara zao nyingine na ndivyo msanii mkubwa wa bongo movies JB amethibitisha hilo .

JB anasema kuwa wasanii wengi kwa sasa hivi wamekuwa wakikimbilia kufanya biashara na shughuli nyingi za kilimo  na uuzaji wa chakula na kuachana na maswala ya chakula.

Kwa kuangalia hilo, wasanii wengi kama shiloleh an wengine wengi wamekuwa wakitangaza kuwa wamekuwa wakikaka kimya muda mrefu ili kufanya shughuli zao nyingine nyingi hasa za kilimo ambapo ndipo walipogundua kuwa kunalipa.

 

Tausi , Uwoya Waionja Polisi kwa Masaa Mbeya.

Mwanadada Irene uwoya na Tausi Mndegeleko wamejikuta wakiingia katika wakati mgumu baada ya wasanii hao kusemekana kuwa walizidisha muda wa tamasha ambalo lilikuwa likiendlea mkoani huko kama mwanadada Irene ambae alikuwa akipost sana kuwa kwa wikiend hii alikuwa Mbeya.

Hata hivyo taarifa za wali zilizokuja  ni kwamba wasanii hao walikamatwa na  baada ya muda walifanya mazungumzo na mamlaka husikia kutokana na kosa hilo la kuzidisha muda na kisha kuachiwa huru huku tamasha tayari likiamuriwa kufungwa kutokana na muda.

Kufuatia mamla husika kuamua kufuatilia sana maswala la ukiukaji wa sheria watu wengi wataonekana kuumia lakini ni kutokana na kutokubali kwao kufuata sheria.

Ester Kiama Aamua Kurudi Kijijini Kukimbilia Kilimo.

Mwanadada Ester Kiama kutoka bongo movies ameamua kuukacha umaarufu na usista duuh na kuamua kurudi kijijini na kujikita katika kilimo ambacho ameamini kuwa kinaweza kumtoa kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.

Ester anasema kuwa uamuzi huo ameuamua baada ya kuona kuwa anaweza kukaa mjini sana na kupotexa muda wakati kijijini kuna shughuli nyingi za ukulima zinaweza kumuingizia kipato.

Ester anasema kuwa amekuwa akijaribu kufanya vitu vingi lakini anaona kabisa kuwa kila anachofanya hakimfanyi kutimiza maelngo yake hivyo kwa sasa ameona kuwa ni bora kuangukia huko kwenye kilimo tu.

kipinidi tulichonacho sasa hivi sio cha kuangalia nini cha kufanya kabisa,ni bora kujiingiza kwenye kitu chochote ambacho unaona kuwa inaweza kukiingizia kipato na kujikwamua kiamisha maana maisha ya sasa ni magumu mnoo.:-Alisema hayo alipokuwa akionea na GPL.

 

Harusi ya Mafufu Kuonyeshwa Live Agosti hii.

Harusi ya moja ya waigizaji nguli wa filamu nchini, Jimmy Mafufu inategemewa kuonyeshwa live mwezi huu wa agosti 25 , ikiwa ni ndoa yake ya pili kufungwa na mwanamke huyo baada ya kuachana na mke wake  wa kwanza.

Akiongea na kujibu kwa nini ameamua harusi hiyo kuonyeshwa live katika channeli ya WASAFI  TV, jimmy amesema amefanya hivyo ili kuonyesha kuwa wazi na kwamba yuko tayari kwa maswali yote kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu ndoa zake zote mbili hata ile ya kwanza iliyovunjika.

unajua nilipotaka kuoa niliongea na mungu kwa njia ya sala kwaio, na hata sasa siku yangi itakuwa ikionekana hatua kwa hatua kupitia televisheni, na niko tayari kuulizwa kitu chochote kinachohusu ndoa yangu mpya na hata ile ya zamani.

Lucy Komba Ammwagia Mapovu Irene Paul.

Mwanadada Lucy Komba amemtolea povu msanii mwenzake irene paul kutokana na ukweli kwamba amekuwa akishindwa kumapa yeye credit na shukrani kwa kuwa yeye ndi ealimsaidia kutoka katika movie na wala sio wakina ray au kanumba ambao mara nyingi amekuwa akiwataja katika media.

Lucy Komba anasema kuwa  yeye ndie aliemfundisha irene kuigiza na kumpa nafasi katika katika movie ya cleopatra na fedheha ambapo ndipo kipaji chake kilianza kuonekana akiwa chini ya uangalizi wake yeye,.

Katika post yake lucy komba aliandika cleopatra  na NANI KAMA MAMA ni movie mbili zenye stori tofauti , utunzi wake ulikuwa wa kipekee kabisa na hakuna aliyeweza huu utunzi.na ni msanii mmoja tu aliyeweza kucheza party zote mbili katika nafasi tofauti tofauti.lakini pia hiyo ndip picha ya kwanza ya angelina jolie asietaka kujishusha.

Hata baada ya kuandika hayo waandishi waliamua kumtafuta Lucy ili kuelezea kwa undani maneno hayo na ndipo aliposema kuwa Irene  paul anasumbuliwa na kutokujielewa na kuvimbiwa ustaa wa bongo, na kushindwa kukumbuka kuwa yeye ndie alimuibua katika sanaa.

Lucy anasema amewatoa wasanii kama Jackline Wolper,Yusup mlela, Mzee chilo na hata Irene uwoya.

Wasanii wa Tanzania na China Kufanya Kazi Pamoja

Wasanii wa China kupitia wizara ya utamaduni na utalii imeamua kutoa fursa kwa wasanii wao wa china na pia kutoka tanzania kubadilishana ujuzi wa sanaa wa kufanya kazi pamoja na  kuandaa washa ya siku mbili  iliyoandaliwa na wizara hiyo.

Mkurugenzi wa kituo cha utamaduni wa china Gao Wei  amesema kuwa wanategemea kupitia warsha hiyo wasanii hao watajifunza na kuzalisha kazi zao nyingi na zenye ubora sana  kutokana na kujifunza mambo mablimbali y anchi hizi mbili tofauti.

Ofisa mkuu wa wizara ya habari tanzania pia amefunguka na kusema kuwa kukutana na wasaniii hawa sio tu kutaongeza kkazi za sanaa lakini pia kutaongeza  thamani ya kazi za sanaa.

Bidhaa inapokuwa nzuri basi inaweza kuuzwa sehmu yoyote,kwaio tumieno warsha hiii kujifunza mambo mengi msiyoyajua  kutoka kwa wenzetu wachina  ili kukuza sekta  ya sanaa ya mikono.

Makala Aelezea Uhusiano Wake na Odama.

Mtayarishaji wa filamu nchini Tanzania Makala amefunguka na kuelezea mahusiano yake na mwanamaigizo na mtayarishaji mwenzake  Jenipher  Kyaka almaarufu kama Odama  kuwa wanamahusiano ya kikazi zaidi kwa sababu wote wanafanya kazi za sana na kwamba wote walikuwa zao kubwa kutoka kwa musa banzi amabe aliwatoa wasanii wengi chipukizi miaka ya nyuma.

Makala anasema kuwa watu wengi wa bongo wamekuwa na tabia ya kuzusha mambo bila kuwa na uhakiaka na kile wanachokiongea na yeye hana kitu chochote kinachoendelea kati yao.

Unajua kuwa wabongo wamekuwa wakizungumza mambo mengi sana, na hawajui mimi na odama tumetoa  wapi, na wameanza kusambaza ujumbe kuwa nina mahusinao nae ya kimapenzi, taarifa hizo sio za kweli na hawana hata uhakika nazo na laiti wangejua mimi na Odama tuko aje wasingeongea kabisa, maana Odama ni kama nimezaliwa nae tumbo moja na ninajiskia vibaya sana.

Makala anasema kuwa pamoja na yote lakini Odama kwake ni moja ya watu waliochangia sana mafanikio yake makubwa aliyonayo sasa kwahio anaomba watu wanapokuwa wanataka kuongea waongee kitu kinachoeleweka na chenye uhakika.

Mtoto wa Steve Nyerere Afananishwa na Single Mtambalike.

Ikiwa leo ni siku ya kuzaliwa na mtoto wa Steve  aliyezaa na Matilda Weru Sengo  kumezuka mapya atika kurasa mbalimbali za udaku baada ya mtoto huyo kufananishwa na msanii mwingine kutoka Bongo movies Single Mtambalike maarufu kama Richie.

Picha za mtoto huyo zilizosambaa sana katika mitandao ya kijamii huku wengi wakuthibitisha maneno mengi yaliyokuwa yakisemwa na wawili hao kuwa wanakanusha , hatimaye sasa ukweli umegundulika kuwa wawili hao walikuwa wapenzi lakini bado kitendawili kimeshindwa kutatuliwa baada ya watu wa udaku kuanza kumfananisha mtoto huyo na msanii mwenzao wa filamu nchini.

Steve Nyerere na Weru sengo wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu na lakiniwawili hao wamekuwa wakisema kuwa hawapo pamoja lakini kwa sasa wameamua kuthibitisha kwa kuonyesha kuwa wana mtoto  na ametimiza umri wa mwaka mmoja sasa.

Dotnata Akumbwa na Msiba Mzito.

Mwanamama mkongwe wa filamu za Kibongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’, amepata pigo baada ya kufiwa na mama yake mzazi, Ildegalda Alphonce aliyefariki dunia juzi, Jumatatu, asubuhi katika Hospitali ya Boch, Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akizungumza na Za Motomoto News, Dotnata alisema kuwa, kifo cha mama yake kimeacha pengo kubwa katika familia kwani kama mzazi, alikuwa na umuhimu mkubwa kwao, lakini ndiyo mapenzi ya Mungu hawawezi kuyapinga.

Kufiwa na mama siyo jambo dogo, ni kubwa mno, mama yetu ametuachia pengo kubwa na tutamkumbuka sana kwa mengi, ameugua kansa (hakupenda kutaja ya nini) kwa muda mrefu na ameteseka sana kwa kweli ndipo Mungu akaamua kumpumzisha. Tunaumia sana, lakini inabidi tukubaliane na kilichotokea maana kila nafsi lazima itaonja mauti. Tulimpenda mama yetu, lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema Dotnata huku akilia kwa uchungu.

Mwili wa mama wa Dotnata ulitarajiwa kusafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera, lakini mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni walikuwa hawajapanga siku ya kuusafirisha na msiba upo nyumbani kwa dada yake Dotnata, Segerea, Dar. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amen!

Tiko Aogopa Kutapeliwa , Aajiri Mwanasheria Wake.

Mwanadada Tiko Hassan kutoka bongo movies amefunguka na kusema kuwa tangu Mh waziri Harrison Mwakyembe alipokuwa akiwapigia kelele wasanii kuhusu kuangalia sana wanapofanya mikataba na makampuni mbalimbali kuwa makini ili wasitapeliwe na yeye amepata akili sasa ya kutafuta mwana sheria wake ili kuogopa kutapeliwa.

Tiko anasema kuwa kwa sasa kila kazi anayotakiwa kuifanya ni lazima amshirikishe mwanasheria wake ili kuepuka kuzurumiana na kuwa kutapeliwa na watu kama unavyofanyika kwa wasanii wengine wanaofanya kazi isiyokuwa na faida.

Unajua watu wamekuwa wakitumia nafasi ya njaa zetu kutudidmiza na kutusainisha mkataba ya ajabu hivyo tumeshtuka baada ya waziri wetu kulizungumzia hilo bungeni, nna kuchukua tahadhari mapema hivyo kwa sasa nina mwanasheria wangu kabisa  na meneja ambao wananisaidia katika kila kitu kwaio sio rahisi kuingizwa mkenge.-Alisema Tiko alipokuwa akiongea na Global Publishers

Tiko anasisitiza pia wasanii wengine kuwa makini na swala la kufanya mikataba kwa makubalino yasiyofuata sheria husika.

 

Mkude Simba Amjibu Steve Nyerere Kuhusu Tuzo za SZIFF

Muigizaji  maarafu kwa upande wa vichekesho Mkude Simba amejibu maneno ya Steve Nyerere ambaye alihoji kwanini wakongwe kama Ray, Irene Uwoya, Johari na wengine wengi hawakuwepo kwenye tuzo za movie za (SZIFF) zilizofanyika Mlimani City

Mkude amemjibu Steve na kumwambia kuwa sikutambua kusudio lake lakini ilikuwa sio lazima kila mwigizaji kuwepo kwenye tuzo hizo

Ambao movie tunazimiliki hatujauza haki zetu kwa muhindi ndio tuliweza kushiriki katika tuzo zile, lakini haimaamishi kwa wachekeshaji wote wawepo,” Mkude Simba aliiambia Bongo5

Thea Atoa Pongezi Zake kwa Makonda , Ni Baada ya Kampeni ya Kusaidia Wanawake

Msanii wa bongo movies Ndumbaye Misayo maarufu kama Thea ameandika ujumbe mrefu kwa ajili ya kumpongeza Mh Paul Makonda baada ya kuanzisha kampeni ya kusaidia wanawake ambao wametelekezwa na wanaume zao na kuwaachia watoto kulea peke yao.

Thea aliandika hivi kuhusu kampeni hiyo ya Mh Paul:

kwanza nimpogeze mheshimiwa paul makonda kwa kujitolea na kulikumbuka kundi hili la wanawake waliojitokezwa, kwakweli tatioz hili ni kubwa sana  n kumuachia Mh Makonda peke yake haitwezekana kwa sababu tatizo sio kwa dar peke yake bali ni Tanzania nzima.

niombe wadau wa maendeleo ya wanawake tanznia kutafuta suluhu ambayo ni endelevu kwa tatizo hili.upo ukatili unaotokea kama ajali lakini ukatili huu mwingi kwa wanawak na wasichana utokana na umaskini.

wanawake hawa waliojitokeza leo inamaanisha kuwa hawajaweza kumudu hata yake mahitaji ya msingi nitoe wito kwa wanawake na wadau wengine kumuunga mkono Mh Paul Makonda ili kuweza pia kuwakwamua wanawake hawa kiuchumi.

Tuwasaidie wanawake hawa kuwa na uchumi imara kwa sababu sio wanaume wote wanakataa kutoa matunzo kwa makusudi, wengine wamekuwa wakiyumba.

Hata hivyo kutokana na kampeni hiikila mtu amekuwa na muonekano tofauti kwa sababu wapo wanaosapoti na pia wapo wanaosema zoezi haliwezi kumaliza tatizo.

Bongo Movies Tunapesa Msituchukulie Poa:-JB

Msanii mkongwe wa bongo movies Jacob Steven amefunguka na kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakiwadharau sana wasanii wa maigizo na filamu kuwa hawana ela na ndio wanaoongoza kwa kuwa na njaa kwa sababu kazi zao zimekuwa hazifanyi vizuri na wamekuwa wakikosa masoko ya kazi zao.

Akiongea alipokuwa na wasaniii wenzake katika kampeni iliyozinguliwa jana na wasanii wengine wakiwepo huku kampeni hiyo ikiwa na lengo la kutafuta vipaji  na kuhamasisha vijana kujikita kufanya kazi hasa ya sanaa kwa sababu inalipa kuliko kukaa vijiweni na kujibweteka, anasema kuwa  kazi ya sanaa ina ela na hata wasanii wa bongo movie wana ela kwaio watu wasichukulie poa kazi hiyo.

Wasanii wa bongo movies wameamua kufanya kampeni hiyo ili kukuza kazi za sanaa za filamu kwa sababu kwa muda mrefu sasa kumekuwa na maneno kuwa  bongo movie imekufa j=na hata wasanii wake ni maskini.

 

Namzia Sana Gabo Kuliko Wasanii Wote:Norah

Msanii mkongwe wa maigizo na filamu nchini mwanadada Norah amefunguka na kusema kuwa katika wasanii wa kiume anaowakubali sana bongo movies basi Gabo ndio anaongoza wasanii wote.

Pamoja na kwamba kunwa wasaniiwengi wazuri na wakubwa wanaofanya vizuri lakini kwa upande wake anaaanza na gabo kwa sababua amekuwa mpiganaji na anaejiuma asana katika kazi za sanaa na amekuwa makini siku zote akiwa kazini.

Norah ameyasema hayo alipokuwa akiongea na kupiga stori juu ya sanaa na mwandishi wa GPL, norah akusita kumtaja Gabo kama msanii wake wa kwanza kumpedna kwa sababu ya umakini wake.

wapo wasanii wengi wa kiume ninao wakubali lakini Gabo anaongoza list ya wasanii wote wa kiume kwakweli, namzimia sana Gabo.wengine ninaowakubali ni pamoja na JB, Frank mwigongi,chiki mchoma na Dude.

 

Tin White Awaponda JB na Wema Sepetu.

Mchekeshaji maarufu bongo Tin White ameibuka na kumchana wema sepetu pamoja na JB  kwamba sio wasaniiwa ukweli ila washukuru mungu kwa kufika hapo walipo sasa kutokana mitandao ya kijamii mbayo imekuwa ikiwakuzia majina yao.

Tin White ameongea hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha eNews,baada ya kuwepo kwa wimbi la wasaini wengi kwa sasa ambao wamekuwa wakiingia katika sanaa bila kupitia vyuo vinavyohusiana na sanaa hivyo wamekuwa wakiharibu tasnia hii ya sanaa.

Unajua kuna kipaji yaani hiyo ni reality kabisa lakini pia kuna muongezo wakina kanumba walikuwa wanafanya kwa  vipaji  vyao vyenyewe tu lakini hawa wakina wema sepetu  walikuja tu kujaribu hao sasa ndo wa kuongezea .

mimi naongea ukweli kabisa  kutokana na mitandao ndo maana wakina Wema Sepetu wameweza kuitika  lakini hana reality yoyote ile.Hata huyo JB hakwa na historia ya kuwa msanii  alikuwa anauza mahindi ila yeye alilazimishwa na Single Mtambalike ili awe msanii siongei kwa ubaya ila naongea jambo la ukweli kabisa.

 

 

Mwanakheri na Niva Ndani ya Bifu Zito.

Wasanii wa bongo movies Niva pamoja na Mwanakheri wanasemekana wapo kwenye bifu zito ambalo limesababishwa na msanii mwenzao Riyama Ally.Baada ya kuchunguza kwa muda mrefu ilikuja kubainika kuwa wasanii hao wawili wapo katika bifu zito kwa  zaidi ya miaka miwili.

Sababu kubwa ya wawili  hao kuwa na bifu ni baada ya niva kumkataza mwanakheri kuwa anamtukana Riyama Ally kwa sababu yeye ndio aliemtambulisha katika tasnia ya maigizo.

Kampuni ya GPL  waliamua kumtafuta Niva ili aweze kuthibitisha swala hilo ambapo alikiri kuwa ni kweli yeye na Mwanakheri hawapo katika mahusiano mazuri na hii yote ilitokana na yeye kumkanya msanii huyo kuacha kumtukana mwenzake kwa kuwa ndie aliemtambulisha katika game.

Hata hivyo baada ya kumtafuta mwanakheri kumuuliza swala hilo alikana na kusema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu yeye kumtukana Riyama na hata huyo Niva hawaingei kwa sababu sio rafiki yake.

Sijawahi kumtukana riyamma,na huyo niva hajawahi kunirekebisha kwa kitu chochote  ila sipo nae kribu kwa sababu sio rafiki yangu.

 

Bongo Movies Wanaounda Kundi La Uzalendo Wamkataa Steve Nyerere

Wasanii wa bongo movies ambao wanaunda kiundi la Uzalendo Kwanza wameamua kujiweka pembeni  na kuacha kukitumikia kikundi hicho na kweka pembeni kabisa   harakati hizo kwa madai kuwa hawamuelewi kabisa mwenyekiti wao wa kikundi hicho Bwana Steve Nyerere ambae amekuwa akijinufaisha mwenyewe na kuacha dhana ya uzalendo kwanza.

Wasanii hao wakiongozwa na viongozi wengine kama Davina,Dude na Thea wamesema kuwa hawamuelewi mwenyekiti wao kwa sababu kila kukicha anafanya vitu kwa kutumia kundi hilo kujinufaisha yeye mwenyewe bila kujali kuwa kundi limeundwa na watu wengi na lina malengo mengi.

Viongozi hao walisema kuwa wameamua kujiweka pembeni ili kuepusha ugomvi usiokuwa na tija kwa sababu kipindi wanaanza hawakuwa na lengo baya zaidi ya kuleta uzalendo, na wanasema kuwa pamoja na kwamba wameamua kujiengua lakini bado haki zao ziko palepale kwa sababu wao pia ni waanzilishi wa kundi hilo.

Kundi la Uzalendo Kwanza lilianzishwa miaka miwili nyuma kipindi cha kampeni za uchaguzi ikiwa na lengo la kuhamasisha uzalendo kwanza kwa wananchi na kuacha maslahi ya mtu moja moja katika kuchagua viongozi wa nchi.

Steve Nyerere  amekuwa akikumbwa na kashfa nyingi za kisiasa ambapo hivi karibuni alionekana hata kumkosoa kiongozi mmoja wapo mkubwa wa chama kilichopo madarakani baada ya msanii Wema Sepetu kutangaza kurudi CCM, hata hivyo kundi la uzalendo kwanza linaweza kuwa limemkataa mwenyekiti huyo kwa madai ya kile kuwa kipindi Wema anaondoka CCM kwenda CHADEMA  alileta maneno maneno  ya kugombana na wanakikundi hicho na kusema kuwa walikuwa wakifanya kampeni bila kulipwa ambapo wasanii wa kundi hilo walimjia juu ,ambapo aliingia ktika ugomvi na msanii mwenzie Batuli  , lakini kitu cha kushangaza ni kwamba hata baada ya msanii huyo kuamua kurudi bado Steve Nyerere  aliweza kumpokea .

 

Wafahamu Wasanii Wenye Mvuto Zaidi Bongo Movies

Hawa ni wasanii wa kike bongo movies ambao wamekuwa katika rekodi ya wasichana wenye mvuto zaidi.

ELIZABETH LULU MICHAEL

Ameanza kazi ya sanaa akiwa bado na umrri mdogo sana na mpaka sasa anafanya vizuri sana, Amepitia misukosuko mingi ambayo imemfanya kuwa imara zaidi katika maisha yake.Lulu uonekana maridadi na mwenye mvuto kila iitwapo leo.kwa malkia wa bongo movie yeye anaweza kuwa ni namba moja.

YOBNESH YUSUPH(batuli)

ni mwanamama mwenye mtoto mmoja wa kiume, lakini mvuto na urembo wake ambavyo anazidi kuutunza huwezi kuzania kuwa ni mzazi.

IRENE UWOYA

Tangu kuwa miss Tanzania mpaka sasa, irene amekuwa moja ya wasichana wanaongoza kuwa na muonekano mzuri, mwili wake haubadiliki na mavazi yake umfanya kuwa maridadi na mwenye mvuto zaidi.

WEMA SEPETU.

Wema Sepetu, mwanadada anaependwa karibia na Tanzania nzima, ni msanii wa kike anaeongoza kuwa na followers wengi  tanzania. Wema hachuji kwa uzuri na hakuna nguo atakavyovaa ikaacha kumpendeza .

WELU MATILDA SENGO

Malkia wa bongo movie alikuja kwa kasi katika tasnia, pia anafanya vizuri akiwa katika kazi yake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.