Umaarufu Haunipi Ninachokitaka :-Bright

Mwanamuziki Bright amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya sanaa na muziki amefunguka na kusema kuwa sababu kubwa ya yeye kukosa gari hadi sasa ni kwa sababu amekuwa maarufu lakini hana kile anachokitafuta kwa muda wote.

Bright anasema kuwa umaarufu alioupata sio sawa na kile anachokipata kimslahi kitu ambacho kina vunja sana moyo wa kujituma na kufanya kazi.

Bright wa sasa sio wa mika ya nyuma, lakini pia umaarufu nilionao hauendani kabisa na kile nilichonacho, bado sijapata pesa kubwa hivyo  ya  ya kwamba ninaweza kununua hata gari.

Hata hivyo mwanamuziki huyo amegoma kabisa kuzungumzia uongozi wake wake wa Fundikila ingawa habari chini ya kaeti zinasema wawili hao kwa sasa hawaelewani.

Bright Amkana Mtoto wa Nyoshi

Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini,Bright amefunguka na kukanusha kuwa na mahusiano na mtoto wa mwanamuziki wa dansi Nyoshi El Sadaat na kusema kuwa mwanadada huyo ni rafiki yake tu na wala sio vinginevyo.

Akiongea na PB ya EATV , bright amesema hayo alikuwa amekwenda kwa ajili ya ktambulisha ngoma yake mpya ya kingasti na kusema kuwa taarifa hizo amekuwa akizisikia lakini hakuna ukweli wowote kuhusu hilo.

sina mahusiano na mtoto wa nyoshi yule ni rafiki yangu tu.nimefahamiana nae baada ya kuambiwa kuwa amechora tatoo ya jina langu katika bega lake,kipindi hicho nilikuwa zangu Ifakara.

Lakini pia anasema kuwa hata swala lililouwa likizushwa na msichana huyo kuwa na mimba halikuwa na ukweli  wowte kwa sababu wao ni marafiki tu.

Bright:Sijawahi Kujiingiza Katika Mapenzi,Sijui Kuumizwa

Msanii wa  muziki anaefanya vizuri kwa sasa katika anga hizo Bright ambae sasa hivi ana kibao chake kipya cha Sina, ameiambia Clouds 360 kuwa hajawahi kujiingiza katika mapenzi wala hajui chochote kuhusu mapenzi kwaio hana chochote anachojua kuhusu kuumizwa na mapenzi.

Bright alipoulizwa kwanini muda mwingi amekuwa akiimba nyimbo zinazouhsu mapenzi , amesema kuwa kwa upande wake nyimbo anazokuwa anaimba ni kazi ya sanaa lakini haihusiani kabisa na maisha yake halisi ya muziki.

sijawahi kabisa kujiingiza na maswala ya mapenzi,kwaio sijui chochote kuhusu kuumizwa na mapenzi mimi ninafanya tu kazi ya sanaa kuimba nyimbo za mapenzi.kupenda hiyo ipo kama binadamu ni kawaida mtu anapedna lakini bado sijajiingiza katika mapenzi na siku nikiwa katika mahusiano kabisa mtajua tu kuwa nina mahusiano.

kuhusu zile picha za beach nikiwa na mdada zilikuwa ni picha za video, tulikuwa location

Mwanamuziki huyo akiendelea na mahojiano hayo alisema kuwa kufanukiwa kwake kimuziki kunatokana na ndhamu yake ambayo inatokana namalezi aliyoyapata kutoka kwao.pia bright anasema kuwa katika kazi zake zote hakuna hata nyimbo moja ambayo amewahi kuandikiwa ingawa hakitokea mtu akamwandikia hawezi kuacha kuimba.

tangu nmeanza muziki sijawahi kuandikiwa mashairi,nyimbo zangu zote nimekuwa ninaziandika mwenyewe ila ikitokea mtu ananiandikia na nikaupenda wimbo nitafanya kazi.

Kwa kuongezea pia bright ansema kuwa kwa sasa anjiusisha na kilimo cha mpunga na mahindi huko mkoani Morogoro ambako ndipo alipokulia na kusoma huko huko.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.