Mshindi wa BSS Kuzawadia Milion 50

Kiongozi wa mashindano ya muziki ya BSS Tanzania Madam Ritha ametangaza kuwa zawadi kubwa atakayopewa mshindi ni shilingi milioni 50 za kitanzania ingawa pesa hizo hatopewa zote kwa mara moja.

Madam Ritha anasema kuwa wameamua kutoa pesa hizo kwa  awamu kwa sababu  kumekuwa na washindi ambao hawanufaiki na pesa hizo hasa wanapokabidhiwa zote kwa mara moja.

Akifafanua kwa undani zaidi, Madam Ritha anasema kuwa Mshindi atakuwa akipewa pesa hizo kila mwezi shilingi mil 1.2 lakini milion 5 za mwanzo atakabidhiwa kwa mara moja siku ya tukio.

Hata hivyo pia msanii huyo aatanza kufanya kazi chini ya Switch Rekodi ambao wameweza kuwakabidhi kwao na tayari walishasaini mkataba tayari.

 

 

Madam Ritha Atoa Top 6 Yake ya Washindi wa BBS.

Jaji mkuu wa shindano la BSS nchini , Madam Ritha amefunguka na kutoa list ya wasanii wake  6 kutoka katikamashindao  yaBSS kwa miaka iliyopita mabao mpaka sasa wanafanya vizuri na amekuwa akijivunia sana kila napoona mafanikio yao.

Madam Ritha nasema kuwa sio kwamba wasanii wengine hawafanyi vizuri lakini wapo wanafanya vitu vingine kulingana na muda na hali ilyo sasa na siasa nyingi zilizopo katika muziki wa bongo.

wasanii aliowataja Madam Ritha ni pamoja na Walter Chilambo,Peter Msechu, Kala Jeremiaah na Haji Hamadhani” wapo wasanii kama Walter Chilambo ambae yupo katika gospel na kama wewe sio mtu wa gospel utamjuaje,wapo wengine katika mabendi kama haji ramadhani ni mtu muhimu sana katika bend ya Twanga Pepeta,Peter Msechu na Kala Jeremiah je. lakini pia kuwa wengine ni ma-tv presenter wakubwa tu ,kuna Frida Amani ambae pia wimbo wake unafanya vizuri tu kwa sasa, Angel Mary kato pia .

Madam Ritha pia anasema kuwa wasanii hawa wamekuwa wakifanya vizuri lakini tu inategemea mtu anayetaka kuwasikia anataka kuwasikia kwa style gani na ndio maana wanaishia kusema hawapo katika game.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.