Mtu Kufuatilia Mambo ya Wengine Utakuwa na Kasoro Kubwa Sana.:-Chin Bees

Msanii wa bongo fleva Chin Bees ametoa yake ya moyoni kuhusu tabia ya baadhi ya wabongo  kukaa na kuwa wanafatilia mambo ya watu bila kuwa na uhakika nayo na kuanza kuyatangaza hadharani.

Chin bees anasema kuwa hiyo nikasoro kubwa sana kwa sababu kwa hali ya kawaida mtu mwenye maisha ya kawaida huwezi kukaa na kufatilia mambo ya watu na wakati huohuo unakuta hata  yale ya kwako yanakuwa bado hayajakaa sawa lakini unakuwa  unakosoa ya wenzako.

kama mtu unakuwa kazi yako kufatilia maisha ya wenzako basi wewe unakuwa na kasoro kubwa sana, huwezi kukaa unaongelea mambo ya mtu miwngine wakati wewe mwenyewe ya kwako yanakuwa hayajakaa sawa.

Chin bees anasema kuwa watu wenye tabia hizo waache na kuanza kujifunza kujali yale yanayowahusu tu.

Chin Bees Adai Anachukizwa na Wasanii Wapenda Kiki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na miondoko yake ya kuchana Musa Ramadhani maarufu kama Chin Bees amekiri kuwa anachukizwa sana na wasanii wanaopenda kiki.

Chin Bees ameongelea suala la kiki kumkera kwa sababu kwa sasa kuna baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wazuri katika kiki kuliko kazi zao yaani skendo zinateka kabisa kazi zao.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Chin Bees amesema anashangaa kuona wasanii wenzake wakifanya kiki mitandaoni wakati muziki ni biashara ambayo inahitaji ubunifu tu ili uweze kufanya vizuri na mashabiki wafurahie muziki wako.

 Mimi nachukizwa kwa kweli, wasanii wapo kwenye biashara kwa hiyo ni bora ukafanya kazi kwa ubunifu kuliko kufikiri kiki ndio itakayokufanya ukauza nyimbo zako, unaweza ukatengeneza kiki na bado usifanye biashara ukawa umejishushia heshima tu“.

Wasanii wengi wanapenda kutengeneza skendo fulani ambayo itawafanya wapate kuongelewa sana Kwenye mitandao ya kijamii kabla hawajaachia kazi zao ili waweze kupata airtime kubwa pale wanapotoa kazi zao.

 

Chin Bees Afunguka Kuhusu Tuhuma Za Kuvujisha Picha Yake Ya Utupu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Chin Bees amefunguka na kuongelea skendo iliyompata mwanzoni mwa wiki hii baada ya picha yake ya utupu kuvuja na kusambaa mtandaoni.

Wiki iliyopita picha ya utupu ilisambaa kwenye mtandao wa kijamii iliyomuonyesha Chin Bees akiwa kifua wazi bila nguo yoyote lakini pia alikuwa amemkumbatia msichana mrembo ambaye pia alikuwa mtupu. Picha hiyo iliwaonyesha wapenzi hao katika mkao wa kimahaba.

Baada ya picha hiyo kusambaa kitendo kilichotafsiriwa vibaya na mashabiki ambao moja kwa moja walidhani au ilisemekana kuwa picha hiyo imevujishwa na Chin Bees mwenyewe ili apate kiki.

 

Chin Bees amefunguka na kudai kuwa picha hiyo akiwa na mwanamke wote wakiwa watupu haijasambazwa na bali ilisambaa kwa mbaya baada ya kupoteza simu yake hata hivyo amesema yule mrembo ambaye yuko naye kwenye picha anakaa nje ya nchi kwa sasa na sio Mpenzi wake tena .

Kwenye mahojiano na Enews Chin Bees amefunguka yafuatayo:

Kilichotokea ni kwamba nilipoteza simu muda mrefu tu lakini nimekuja kushangaa hii kitu imetokea sahivi ila Simu yangu ilikuwa haina password lakini Mimi ni mtoto wa kiume kwaiyo vitu kama vile mimi huwa nafanya lakini sio kufanya public lakini mimi huwa sio mtu wa kutafuta kiki kusema ukweli hata mimi nilopoona ile picha nilikuwa shocked ila kilichotokea kimetokea hakuna cha kufanya ila nawaomba radhi mashabiki wangu”.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.