Kaka wa Godzilla Atuma Salamu kwa Bella

Kaka wa marehemu Godzilla, msanii wa hip-hop nchini ambae amefariki wiki chache zilizopita, amefunguka na kumuomba mwanadada ambae amekuwa akijitangaza kuwa amekuwa na mahusiano Godzilla kuacha mara moja kufanya hivyo.

Bella ambae alitangaza kuwa na mahusiano na Godzilla masaa machache baada ya kifo cha msanii huyo na kuzua gumzo kubwa katika mitandao ya kijamii , amekanywa na kaka wa marehemu kuwa mdogo wake hakuwahi kuna skendo kipindi cha uhai wake hivyo asimtafutie akiwa ameshakufa.

Anasema “mdogo wangu hakuwahi kuwa na skendo kipindi cha uhai wake, namuomba huyo dada anaetaka kupata kiki kupitia marehemu aache mara moja na hatuache familia maana anatuumiza sana katika kipindi hiki kigumu.

Familia Yafungukia Kifo Cha Godzilla na Ratiba Ya Mazishi

Familia ya aliyekuwa Msanii wa hip hop nchini Godzilla wamefunguka na kuweka wazi ratiba ya mazishi mara Baada ya kufariki siku ya jana.

Baba mdogo wa mwanamuziki huyo  amesema ndugu yake aliteswa na kitu kilichokwama tumboni kwa zaidi ya siku tatu na kumfanya atapike mfululizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Joyce amesema mwanamuziki huyo Golden Mbunda alikuwa akitapika kwa siku tatu mfululizo.

Jumapili (Februari 10, 2019) alilala muda mrefu, haikuwa kawaida. Baadaye akaomba barafu tulivyompa akaanza kutapika ndipo tulipompeleka hospitali na kugundulika ana malaria, sukari imepanda sana na presha imeshuka.

Pia marehemu alisema kuna kitu kiling’ang’ania tumboni kama vile kinataka kutoka ila kinagoma, alijaribu kukitoa kwa kujitapisha lakini hakikutoka“.

Makamu wa Raisi Ampa Heshima Hii Marehemu Godzilla

Makamu wa Raisi wa jamhuri ya muingano wa Tanzania Mama Samia Suluhu amemkumbuka Msanii Wa Hip Hop Godzilla ambaye alifariki ghafla siku ya jana.

Siku ya jana Mama Samia kabla hajaanza kuhutubia kwenye kongamano la dawa za kulevya aliwaomba watu kusimama kwa dakika moja kumuombea Godzilla.

Nimepata taarifa kuwa usiku wa kuamkia leo tumepata msiba wa msanii mmoja ambaye naye ni Ndugu Golden Jacob Mbunda kwa umaarufu anajulikana kama Godzilla. Sasa naomba wote tusimame kwa dakika moja tumpe heshima yake na kila mmoja aombe kwa kitabu anachokiamini”.

 

Miss bella Aamua Kuweka ukweli wa mahusiano yake na Godzila

Mwanadada anaejulikana kwa jina la Bella ambae alikuwa akifanya kazi katika studio ya Godzila na pia akiwa kama msanii anayesimamiwa na marehemu amefunguka na kuelezea kuwa yeye ndie aliekuwa msichana wake wa mwisho kabla ya mauti kumfika msanii huyo usiku wa jana.

Mwanandada huyo ambae ndio alikuwa akitumiwa na watu katika kutoa habari za marehemu na hata hatua zake za mwisho kabla ya kufariki amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwa vyomba vya habari alkini kumbe amekuwa na maumivu ya kuficha mahusiano hayo hivyo ameamua kuweka wazi kupitia ukurasa wake wa instagram

katika ukurasa wake,mwanadada huyo alisema

Hata Kama Nikifa Leo, Jina Langu Litabaki -Godzilla

Inaweza kuwa kama  roho ya mauti kumtembelea mtu, kwa nama moja ama nyingine anaweza sijue au akajua lakini akashidwa kusema kwa watu kile anachokuwa akijisikia kwa muda hu.Je hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Godzilla siku chache zilizopita kabla ya mauti yake, hakuna anaejua.

Msanii Godzilla ambae amekutwa na umauti usiku wa kuamkia February 13, anasemwa kuongea maneno fulani katika ukurasa wake wa tiwtter akisema kuwa hata kama atakufa leo basi jina lake na litabaki daima.

Ni kweli kuwa jina lake haliwezi kusahaulika kutokana na harakati nyingi za kumuziki alizowahi kuzifanya  msanii huyo , lakini maneno haya yanaumiza zaidi kila mtu hasa kwa kusema kama ingewezekana tungeweza kuzia hilo.

Godzilla aliandika “Even if i die today, my name gonna be here….jokes on you

TANZIA”- Rapa Godzilla Afariki Dunia

Rapa bora na maarufu nchini Godzilla ameripotwa kufariki usikuwa kuamkia leo ghafla alipokuwa nyumbani kwao salasala huku bado sababu ya kifo icho ikiwa bado haijajulikana mpaka asubui hii,

Mwili wa Marehemu ulipelekwa kuifadhiwa katika hospitali ya lugalo jijini dar kwa ajili ya kusubiri tarartibu za mazishi pindi familia na wanandugu watakapo kubaliana.

Rapa godzilla anaacha pengo kubwa sana katika muziki wa rap na muziki kwa ujumla Tanzania kutokana na ufanyaji wake kazi na changamoto aliyokuwa akileta kwa wasanii wenzakke,Godzilla aliweza kufanya kazi na wenzake kwa kujituma na kwa upendo akiamini kuwa hiyo ndio njia ya kukuza muziki nchii.

Godzillah Afungukia Tetesi Za Kuwa Chapombe

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Golden Jacob Mbunda ‘King zilla’ auGodzillaau ‘Zilla’ ameibuka na kukana tetesi ambazo zimekuwa zikidai kuwa amepotea kwenye gemu kisa kunywa pombe.

Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa Zilla amepotea kwenye gemu na mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa juu yake. Pombe imekuwa ikitajwa kuwa ni chanzo cha yeye kupotea.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Godzilla alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikana mara moja na kuweka wazi kuwa hayo ni maneno tu ya wanadamu:

Huwezi kumzuia mtu mwenye mdomo kuongea kwa hiyo ndiyo hulka ambayo tunayo especially Watanzania. Kwa watu ambao wanamjua Zilla, ni mtu ambaye anapenda sana kuishi maisha ya kawaida, nakaa kitaa, napiga stori mbili-tatu na washkaji kwa sababu ndiyo wanasapoti kazi zangu, siwezi kuwavimbia, lazima nitafute muda wa kuongea nao na kupata mawazo kutoka kwao. Kuhusu pombe, kila mtu na starehe yake, wengine tukipata mbili-tatu zinatupa vibe la kutoa vitu vizuri, lakini sinywi kupitiliza kama wanavyosema”.

Lakini Godzilla alifungukia ukimya Wake kwenye gemu kwa muda mrefu na kudai yupo kimya akijiandaa kwa ajili ya kazi mpya:

Nipo kimya kwa muda kwa sababu naandaa albam yangu mpya ambayo bado mpaka sasa sijapanga lini nitaitoa inayokwenda kwa jina la 55555. Imebeba nyimbo nyingi nzuri, watu watainjoi muziki mzuri kwa sababu wanajuaga ninachokifanya ninapokuwa nimetulia.

 

 

 

 

Godzilla Athibitisha Kutokuwepo na Bifu Kati Yake na Bilnass.

Kwa muda mrefu kuliwahi kuwa na tetesi kuwa wasanii wawili Billnass na Godzilla  wamekuwa na bifu na hiyo ni kutokana na kwambaBilnass amekuwa akifuata nyayo za Godzilla na kuiga sana muziki wake.

Hata hivyo baada ya kusambaa sana kwa tetesi hizo Billnass aliwahi kukanusha hilo lakii hivi karibuni pia mwanamuziki huyo aliamua kusema kuwa ana album mpya inakuja na katika album hiyo kutakuwa na kolabo yake na Billnass.

Kwenye album yangu mpya inayoitwa 5555  kuna ngoma yangu moja niko na billnsa na wala sina tatizo nae na ndio maana tumefanya kzi pamoja.:- aliongea Godzilla alipokuwa akiongea na Lilommy wa Times Fm.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.