Nay wa Mitego azindua msanii wake wa kwanza kwenye label yake mpya

Free Nation 966, label mpya ambayo Nay wa Mitego alizindua imefahamisha msanii wa kwanza.

Ni rapa anayejulikana kama B Gway atakaye fuatwa na mwimbaji hivi karibuni.

“Leo label yangu ya ‘Free Nation 966’ imemtambulisha kijana wake wa kwanza ‘B Gway’,” alisema Nay. “Ni msanii mkali sana, sikutaka kumchukua msanii ambaye anatanisumbua, tena wimbo wake wa kwanza ‘Sijachukua’ amenishirikisha,”

Aliongeza, “Kwahiyo ningependa kuwaambia mashabiki wasubirie mambo mazuri kutoka ‘Free Nation 966’. Pia siku chache zijazo tutamtangaza msanii mwingine wa kuimba,” Nay wa Mitego alieleza Bongo 5.

 

Nay wa Mitego amjibu Skyner Ally baada ya kudai ameshindwa kuwa baba bora kwa mtoto wake

Mwanamuziki wa Tanzania Nay wa Mitego hivi karibuni aliiabishwa na muigizaji wa filamu Bongo, Skyner Ally baada ya kumchana kwa kumwambia kuwa hajakuwa akimtunza mtoto wao kama anavyostahili.

Skyner na Nay wakona mtoto wa kike pamoja lakini muigizaji huyo wa filamu amedai kuwa Nay hajakuwa akimsaidia mwanae. Hii ilikuja baada ya Nay alipoweka picha ya mtoto wao mtandaoni wa Instagram huku akimsifu kwa uzuri wake.

Hata hivyo Skyner hakupendelea kwani Nay hajakuwa akihusika na mambo ya mwanae kwa muda mrefu sasa. Kilicho muuma zaidi ni kwamba Nay alikuwa anawadanganya mashabiki wake kuwa anawatunza wanawe vyema ilhali alikuwa ameshindwa kuwa baba bora kwa mtoto wa Skyner ambaye alizaa na yeye.

Inaonekana kuwa Nay aliweza kuiona post ya Skyner na kupitia mtandao wake wa Instagram, Nay aliandika kusema…

“Si kwa kichambo kile jamaniiiiii huh??! Jamani inatosha basiii Povuuu. Nitapeleka Matumiziiiii???. Nawapenda sana awa Watoto Wanguu?. Wasiopeleka Matumizi ya Watoto?? #Wapo,”

Haya basi, wacha tutazame watakacho kifanya hawa wawili sasa.

Skyner amchanwa na Nay baada ya kuposti picha ya binti yao

Skyner aliyekuwa mpenzi wa msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego, hivi karibuni aliamuaibisha baada ya kuweka picha ya binti yao mitandaoni huku akijisifu kwa uzuri wa mwanae.

Hata hivyo Nay wa Mitego hakukipata alichotarajia kutoka kwa Skyner ambaye alimchana kupitia Instagram huku akifunguka kuwa Nay hajakuwa baba kwa manae kwa miaka ilhali anawadanganya watu mitandaoni.

Ujumbe na Nay wa Mitego ulisema,

Skyner ambaye alikasirishwa na ujumbe huu aliandika ujumbe akimshangaa Nay ambaye anasemekana kuwa hataki kutoa huduma kwaajili ya mtoto. Aliandika kusema,

“Thats face you make when you see your ‘daddy jina’ anakufanyia promotions na kudanganya Watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi unayovaa hajui thamani yake maskini. Nimevumilia sana it’s 5 Years now nimejiskia kutapika na nimetapikaa. Am done Mungu wa mbinguni nakuomba unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki….. uzima wa afya nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake”

Aliendelea kwa kusema…

“Endelea na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki…Please unapost picha za mtoto wangu za nini…shobo dundo zanini? Sitaki shobo na mwanangu koma kama ulivyo komaaa…Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done”

Aliendelea kwa kuonyesha binti yake alivyokuwa muhimu katika maisha yake alivyoandika kusema…

“Hakuna anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba’ko hana analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy Birthday My Happiness,” alisema Skyner.

Hata hivyo rapa huyo bado hajazungumza chochote kuhusu sakata hilo, Bongo5 bado inafanya jitihada za mtafuta.

“Nay nataka round 3 tu za boxing kwenye stage”Muigizaji Yusuph Mlela aomba kupigana na Nay wa Mitego

Nay wa Mitego  alitumia ukurasa wake wa Instagram kukosoa baadhi ya  wasanii wa Bongomovie huku akiwataka wafanye kazi bora pia.

Nay alidai kuwa wasanii wa Bongomovies wanapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya kwa lengo la kutaka wafanyabiashara wanaouza filamu za nje ya nchi wafungiwe kwani hawafuati  taratibu ambazo wasanii wa bongomovie wanazifata wakati wa usambazaji wa kazi zao.

Muigizaji Yusuph Mlela alikerwa na maneno aliyosema Ney na kuamua kumjibu kwa hasira –alimtukana na pia kuomba apigane naye ngumi.

Yusuph Mlela na Nay wa Mitego

“Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizajiwanamuziki wakubwa….acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi… sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano.

“Nay wa Mitego acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe siyo msanii…halafu huwezi kufananisha filamu na muziki….. Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu….. This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana tabia za kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale” Yusuph Mlela alisema.

 

Nay Wa Mitego: Mwambieni Diamond pia awe mpole kwasasa alee watoto

Nay Wa Mitego amezua hisia tofauti baada ya kumpasha Rich Mavoko ujumbe ambao alitaka uwafikie wasanii wote wa Wasafi Diamond akiwepo.

Rich Mavoka aliandika kwa ukurasa wake wa Instagram kutambulisha wimbo wake mpya ambayo bado haujaachiliwa kwenye redio na runinga.

“Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ? #Showme” Rich Mavoko aliandika.

Nay Wa Mitego alimjibu haraka, alimwambia asubiri mbaka mwakani 2018 ndo watoe nyimbo (wasanii wa Wasafi.) Alimwambia apitishe ujumbe kwa Diamond ambaye alimtaka alee watoto kwanza.

Nay Wa Mitego na Diamond

“”NAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI. MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWASASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA✊?. Wimbo wetu wa TAIFA ni #Wapo LINK ON MY BIO☝”,”Nay Wa Mitego aliandika.

Ujumbe wa Nay Wa Mitego hata hivyo ni utani tu, Diamond ni rafiki wake mkubwa ambaye alishirikiana naye kutoa ngoma kali sana ‘Muziki Gani’.  Si mara ya kwanza wawili hao kutupiana vijembe kupitia mitandao.

Video ya WAPO itatokea rasmi siku hii kulingana na Nay wa Mitego

Nay wa Mitego ambaye amekuwa zungumzio kubwa Tanzania hivi karibuni baada ya wimbo wake mpya Wapo leo alitoa rasmi siku ambayo video ya wimbo huo itatokea.

Na alitoa ujumbe kwenye instgram yake.

hivi ndivo alivysema:

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.