Tuzo Haziendi kwa Jina Wala Historia Yako :-Nikki wa Pili

Msanii wa bongo fleva nchini Nikki wa Pili nae ameamua kufunguka na kuzngumzia swala la tuzo linalozungumziwa na kila mtu katika mitandao ya kijamii.

Tuzo za sinema zetu ambazo zilitolewa wikied iliyopita na kuwaa cha watu midomo wazi hasa baaada ya kupatiwa tuzo hizo watoto wadogo ambao ndio wameingia  katika tasnia muda sio mrefu.

Watoto hao ambao walishindwanishwa na wasaniii wengine wakubwa na wenye vipaji vya muda mrefu , walichukua tuzo hizo na kuwaacha wasanii wakubwa wakitokwa na mapovu ya kukataa kulinganishwa na watoto wadogo.

Hata hivyo baada ya tuzo hizo, wasanii waliongea kila mtu la kwake na kusema kuwa watoto hao walitakiwa kuwekwa katika kategoria ya kwao na sio kama za wasanii wakongwe,

Akiongelea kwa mtazamo wake, mwanamuziki huyo alisema kuwa hakuna tuzo zinazotolewa kwa sababu ya jina au ukubwa wa umri wa mtu bali ni tathmini ya kazi uliyoifanya kwa muda fulani.

Anasema “tuzo haziedi kwa jina wala historia yako, ukubwa au kwa yale uliokwisha fanya….tuzo hupima kile umefanya kwa mwaka husika.”

Nikki wa pili Awaingiza Wasanii Wenzake Darasani

Msanii Nikki wa pili amefunguka na kuongelea swala la wasanii wengi kuongezeka nchini huku wakiwa na majina makubwa na umaarufu kuliko hata kipato wanachoingiza kutokana na majina yao na uatajiri wao haulingani na  vile wanavyoongelewa.

Nikki  anasema kuwa wasanii wengi wanahitaji elimu ya masoko ili kuongeza wasanii wenye majina na vipato pia kwa sababu wasanii wengi wamekuwa wakifurahia kupata majina na kusahau kuwa majina hayo yanahitaji nkuendana na  utajiri wao.

Nikki wa pli anasema “Kuibali sanaa kuwa kipato ni hata ngumu sana, iwe uchoraji au uchongaji au kitu chochote, wasanii wengi wanabaki na snaa zao kama hobi tu  na sio kitu cha kupatia kipato.somo la marketing pia linahitajika sana kwa wasanii  branding na huduma kwa wateja pia kwa wasanii ni muhimu pia.

Maneno ya Nikki yanakuja kutokana na ukweli kuwa wasanii wamekuwa wengi na wnegi wamekuwa na majina lakini pesa wanayipata kutokana na sanaa hiyo haiendani na majina yao na hii uthihirika zaidi pale ambapo wasanii wanapopata matatizo kama magonjwa na kujikuta wakiomba misaada sana.

Nikkki Atoa Ushauri kwa Linex

Msanii wa hip-hop nchini  Nikki  wa Pili amefunguka na kutoa usahuri kwa wasanii wote ambao wanatamani kufaya kazi kubwa na makampuni makubwa nchini kuwa hata kama wanakuwa wanachaguliwa na makampuni kufanya kazi hizo haimaanishi kuwa wao ni bora zaidi kuliko wengi swala la muhimu ni kuboresha kazi zao hili waweze kufanya izuri.

Huku akimtaja msanii Linex sunday mjeda,, nikki wa pili anasema kuwa kwa sasa watu wengi wa makampuni hawapendi sana kupata hasara kwa kufanya kazi na msanii ambae hajitumi , hivyo wanatakiwa kufanya kazizenye ubora na kupambana kazi kuwa bora kwa sababu hata makampuni pia hayataki hasara.

Nikki amekuwa moja ya wasanii walio wazi sana inapokuja maswala ya kazi, pesa na ushauri kwa wasanii na vijana pia hivyo  muda wote amekuwa akisema na makundi hayo ili kuwasaidia katika mafanikio.

Nikki Atoa Sababu ya Kumchagua na Kumvisha Pete Mpenzi Wake

Mwanamuziki Nikki wa pili ambae wikiendi iliyopita aliamua kuvunja ukimya na  kumvisha pete mwanamke aliyekuwa nae katika mahusiano kwa muda mrefu  na hata kuanza harakati za kufunga ndoa.

Akiongea na EATV, Nikki anatoa sababu kubwa za kumfanya kuamua kumuamini mpenzi wake huyo na kuamua kumvisha pete huku sababu kubwa akisema kuwa ni mwanamke mwenye mapenzi ya kweli na anaamini kuwa anampenda.

kwanza ananipenda, icho cha kwanzalakini cha pili tunaweza kuelewana tukiwa katika huzuni, furaha na hata maumivu pia.yeye anaweza kuelewa kuwa hapa nikki yuko hivi kwa sababu ya hivi lakini pia anauwezo wa kuelewa kuwa Nikki  ana mabaya yake mengi na mazuri pia, kitu ninachiweza kupungukiwa anaweza kujaza.

Nikki Wa Pili Amvisha Pete Ya Uchumba Mpenzi Wake

Msanii wa muziki wa hip hop nchini kutoka katika kundi la Weusi Nikki wa pili amemvalisha pete ya uchumba Mpenzi Wake wa siku nyingi anayejulikana kwa jina la Joan.

Bongo 5 wanaripoti kuwa Tukio  hilo lilitokea siku ya Jumamosi mkoani Arusha nyumbani kwa msanii huyo ambapo rasmi aliaga ukapera.

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na wasanii wenzake Kama vile Kama yake Joh Makini, Dogo Janja, Lord Eyes na Juma Jux.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikki wa pili alimuweka Mpenzi Wake huyo na kumsindikiza kwa maneno matamu na kuandika:

Queen, malkia, mwenye moyo wangu…….nuru ya uzuri wako imulike njia ya maisha yetu…..Nakupendaaaa sanaaaaaaaaa #sikuyetu ahadi ya kwanza nimetimiza”.

Nikki wa Pili Awazindua Watanzania kuhusu maktaba mpya ya UDSM

Msanii kutoka katika kundi la Weusi Nikki wa Pili alipata nafasi ya kuzungumzia uzinduzi mpya wa maktaba mpya ya kitaifa iliyojengwa chuo kikuu cha udsm ambapo ilifungukiwa November 27 na Mh rais.

akiandika  kama moja ya watu wanatajwa kuaminika asana kwa mawazo yao kwa vijana , Nikki ukiachana na kuwa msanii lakini pia amekuwa moja ya watu wanaohamasisha sana juu ya maisha na kutia bidii katika kile wanachokifanya na kukiamini.

katika ukurasa wake wa Twitter Nikki wa Pili aliandika “maktaba ya kuchukua wasomaji 2100 ina maana ni fursa kila siku kwa vijana 2100 kujivunia maarifa, itumieni sana itumieni vizuri ili kujenga maarifa vizuri kupanga mawazo na pia kutafuta ukweli wa kile unachoweza kujielezea , hili ni pori adhimu katika maisha, maktaba ni  uhai wa jamii.”

Nikki wa pili anasema kuwa vijana wanatakiwa kujifunza kuitumia maktaba hiyo kwa kujijengea kutafuta habari na maarifa mbalimbali  ili kuwa na wigo mpana wa mawazo.

Nikki Wa Pili Aandika Barua Ya Kumlilia Ruge

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Nickson Simon maarufu kama ‘Nikki wa pili’ amefunguka na kuweka wazi barua aliyomuandikia Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba.

Siku chache zilizopita familia ya Clouds Media iliweka wazi kuwa Ruge yupo hoi hospitalini kutokana na maradhi ambayo yamekuwa yakimuandama kwa kipindi kirefu sasa.

Msanii Nikki wa Pili amefunguka mengi kuhusu Ruge na hata kutaja mambo mengine mengi ambayo amemfanyia ambayo mpaka leo yameweza kumpa mafanikio makubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikki wa Pili aliandika maneno haya:

Muda wa kipindi kirefu sana katika maisha yangu ya shule nilikuwa naamini mim ni mtu wa kukaa nyuma, nisiye na uwezo wa kuzungumza mbele za watu, sikuwa nanyoosha mkono darasani hata kama najua jibu, nilio soma nao chuo wanajua nilivyo kuwa natoroka presentations.

Muda wa kipindi kirefu sana katika maisha yangu ya shule nilikuwa naamini mim ni mtu wa kukaa nyuma, nisiye na uwezo wa kuzungumza mbele za watu, sikuwa nanyoosha mkono darasani hata kama najua jibu, nilio soma nao chuo wanajua nilivyo kuwa natoroka presentations.

Akaniambia wewe ni public speaker mzuri, akaanza kunipa nafasi ya kuzungumza mbele za watu nilikuwa naona na kosea lakini kila niliposhuka alikuwa anaiambia umefanya vizuri sana ongeza hichi na hichi.

Leo nimekuwa naalikwa vyuoni, kwenye makongamano, semina,taasisi, kampeni mpaka makanisani, kama mzungumzaji au mtoa mada, na hata mitandaoni huwa naandika mawazo yangu bila woga, ingekuwaje nisingekutana na Ruge Mutahaba.

Mungu akupe wepesi urudi katika uzima wako, RG (genius)”.

Inaripotiwa Ruge yupo nchini Afrika Kusini akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya figo ambayo yanamsumbua kwa miezi kadhaa sasa.

 

Mawazo ya Afande Sele Yalipangwa Katika Ufahamu Mdogo :-Nikki wa pili

Msanii kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kusema kuwa mawazo ya msanii Afande Sele ambae aliwahi kusema kuwa wasanii wa kundil la weuzi wamekuwa wakipata tuzo za muziki wa KILI kila mara kuwa walikuwa wakipewa tuzo hizo kwa kuangaliwa kabila lao na wala sio kitu kingine.

Nikki wa pili anasema kuwa swala hilo yeye hakubaliani nalo hata kidogo lakini pia anaamini kuwa afande sele alikuwa akisema hivyo huku akiwa na ufahamu mdogo wa kile anachokiongea.

Ingawa Nikki hataki kuonekana kama anajibizana na Afande Sele kwa kile alichokisema lakini bado anasisitiza kuwa kama ni kweli watuaji wa tuzo hizo wangekuwa kweli wanaangalia makabila  kama alivyosema Afande kuhusu kabila la wachaga basi alimia 90% ya tuzo zingekuwa zinaenda uko lakini haikuwa hivyo.

Nikki anasema kuwa afande sele arudi akajipange kusema upya kuhusu hilo kwa sababu anaamini kuwa hata kama alikaa muda mrefu kuchunguza na kuchambua swala hilo alilifanyia utafiti kwa uelewa mdogo.

 

Nikki Wa Pili Amwaga Povu Zito Kwa Wasanii Wakaa Uchi

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Nikki Wa Pili amewaji juu na kuwatolea povu zito mastaa ambao wameandamwa na skendo ya kuweka picha na video chafu zenye maudhui yasiyo ya kimaadili  kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nikki wa Pili amewachana watu hasa wasanii wanaotafuta kiki kupitia vitu visivyo na maana.

https://www.instagram.com/p/BpYt1DMjQna/?utm_source=ig_web_copy_link

Amber Rutty, Wema Sepetu na Gigy Money ni baadhi tu ya mastaa ambao hivi sasa wanatengeneza headlines kwa vitendo vyao vya kuachia picha chafu kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi yao wameshachukuliwa hatua za kisheria.

Nikki wa Pili Amkosoa Mwl Nyerere

Kila mwaka inapofika October 14 ,tanzania inakuwa inaadhimisha kifo cha baba wa taifa mwl julius kambarage Nyerere, kiongozi aliekuwa muhasiis wa Taifa letu na aliyetukomboa kutoka katika mikono ya wakoloni.Mwl alifanya mengi mazuri na makubwa yakutufanya tumkumbuke kila siku lakini imekuwa vizuri zaidi kutenga siku yake maarumu ili kumuenzi .

moja ya wasaii na wanafalsa nchini, nikki wa pili ambae amekuwa moja ya chachu kubwa kwa vijana kutokana na kuongea bayana bila kuogopa kitu pale anapoona jamii inakosea bila kuwa na mfungamanowa upande wowote ameibuka na kunagalia baadhi ya mambo ambayo yeye anaona kuwa yalikuwa ni makosa kwa uongozi wa mwalimu.

Nikki  ameandika yafuatayo kama makosa ya baba wa taifa

  • mwalimu alirithi serikali ya ukoloni  na  hakuibadili sana..sifa ya seriali ya kikoloni ni  ya serilai ya ukoloni ni ukandamizaji wa wananchi na wananchi hawana sauti…hata sera ya vijiji na ujamaa ilitekelezwa kwa mabavu.
  • chama kilichoshika hatamu hakikutenganisha chama na serikali…chama kikawa na nguvu mbele ya serikali
  • katiba ya rais ya kifalme na wala isyoshirkisha wananchi wakati wa kuiandika.
  • kufungiwa kwa jarida la wanafunzi la cheche..lililokuwa likihoji juu ya utekelezaji wa sera ya ujamaa ilikuwa ni uminyaji wa demekrasia na sauti za wananchi kuhusu maendelea ya jamii zao.
  • kudhoofisha ushurika na kuingiza siasa ndani yake.HAPPY  NYERERE DAY…NYERERE MY NUMBER ONE.

Nikki Wa Pili- Sitafuti Kiki Ni Ndoto Yangu Kugombea Uraisi

Msanii wa muziki wa hip hop nchini kutokea katika kundi la Weusi, Nickson Samson maarufu kama Nikki wa Pili amefungukia mipango yake ya Kugombea uraisi mwaka 2025.

Wiki iliyopita Nikki wa Pili alitrend Kwenye mitandao ya kijamii kwa taarifa ya kwamba ana mipango ya kugombea uraisi na hata kuna mashabiki walimtuhumu kwa kutafuta kiki Kupitia ishu hiyo.

Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Vibes, Nikki wa Pili alianika kwamba siyo kiki bali ni kweli ana mpango wa kuwania Urais wa Tanzania.

Watu wanaweza kufikiri kwamba ninatafuta kiki, lakini ukweli ni kwamba ni ndoto yangu siku moja kuwa Rais wa Tanzania. Kwa sasa ninasogeza umri, baada ya mwaka 2025, nitafahamu ni chama gani kitanipa tiketi.

Kuhusu nafasi hii ‘CV’ yangu inajieleza na namna ambavyo watu wananiamini, nitaendelea kufanya mambo ya kujenga uaminifu zaidi ili baadaye niwatumikie Watanzania”.

Siku za nyuma mbunge wa Kigoma Mh. Zitto Kabwe alishawahi kumtaka Nikki Wa Pili ajiunge na ACT Wazalendo Kupitia ukurasa wa Twitter jambo ambalo Nikki alikataa na kusema yeye sio mwanasiasa.

Nikki Wa Pili Atangaza Ndoto Yake ya kuwa Raisi, Wasanii Wamsapoti.

Akiwa kama moja ya wasanii wanaojitahidi sana kutoa maneno yenye kuhamasisha katika jamii,nikki wa pili kwa mara ya kwanza ameweka wazi kuwa ndoto yake kubwa  ni kuwa rais, ingawa msanii huyo kwa sasa hajaweka wazi kuwa yeye ni mfuasi wa chama gani lakini amekuwa akihamasiha sana vijana kupitia mitandao ya kijamii.

katika ukurasa wake wa  twitter, Niki wa Pili aliandika”Ndoto yangu ni kuja kuwa Rais

Hata baada ya kuweka tweet hiyo , baadhi ya wasanii walionekana kumsapoti msanii huyo kwa kumpongeza kwa kuwa na ndoto hiyo huku wakimtaka asikate tamaa,mmoja kati ya wasanii hao ni Dogo Janja ambae aliandika

ndoto yako ipalilie tu ndugu yangu, anayeona haliwezekani hilo ni tatizo lake sio kwako, husda ni tunu ya Taifa, isikusumbue fanya mambo yako #Nikiwapiliforthepresidency

 

 

Kiki Sio Mafanikio kwa Msanii:- Nikki wa Pili

Msanii wa bongo fleva Nikki wa Pili amefunguka na kusema kuwa katika maisha ya msanii kiki sio kitu cha lazima sana mpaka kufanikisha maswala ya muziki wake kwa sababu kuna vitu vingi ambavyo anatakiwa kuvifanya katika kazi hiyo.

Niki amemjibu Master J amabe ni msanii wa muziki wa siku nyingi  aliyesema kuwa muziki  na soko la sanaa la sasa hivi ni lazima kufanya kiki ndio uweze kuuza muziki wako na sio kama zamani enzi zao.

Niki anasema kuwa vitu vngi vinafanya msanii kufanikisha muziki wake ikiwa pamoja na kufanya video nzuri, uhusiano mzuri na wasanii wenzake na pia kuwa karibu na mdia zitakazosaidia kusambaza muziki wake.

sio kweli kwamba muziki ndi unafanikisha maisha ya msanii mbona kuna wasanii wengi tu wanafanikiwa kwa bila kuwa na kiki wala picha za utupu, kwa mfano sisi weuzi tumefanikiwa sana bila kuwa na kiki.

Nikki wa Pili Atupa Dongo kwa Babu Tale, ni Baada ya Kwenda South kwa Zari

Msanii wa Hip-Hop nchini, Nikki wa Pili amemtupia dongo Babu Tale baada ya babu tale kwenda afrika ya kusini na kurudi huku akitangaza kuwa lengo lake ku ilikuwa ni kwenda kumbebeleza zari ambae ni zazi mwenzie na diamond ili kurudiana na diamond.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, Nikki wa Pili alisema kuwa kazi ya babu tale kutumwa haijaanza leo ameanza kutumwa tangu akiwa kijana enzi hizo anatumwa na kaka yake ku-burn CD  na sasa hivi anatumwa na Diamond kubembeleza ndoa.

babu tale alikuwa akitumwa empty CDs na majani  pale bongo records ili ku-burn CD s za wasanii wa kaka yake,siku hizi natumwa akabembeleze ndoa SAUZI…. kweli swala la uadilifu katika utumishi  linaendelea.

Napenda Wanawake Natural, Hamtomuona Mke Wangu na Make-up

Rapa wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Weusi, Nikki wa pili amefunguka na kuweka wazi kuwa anapendelea kuwa na mwanamke ambaye hajirembi ‘natural’ hivyo msitegemee kumuona mke wake na make-up.

Niki wa pili amekuwa akimposti sana mpenzi wake Kwenye ukuras wake wa Instagram ambapo msichana huyo huoneka akiwa natural sana habari mawigi, anabana tu nywele zake lakini pia hapaki make up sana.

Wiki iliyopita Dogo Janja alimchana Niki na kumwambia mwanamke make up natural aiachie misitu comment ambayo ili trend sana lakini sasa Niki wa pili an Afunguka kuhusu kauli yake ya kupenda mwanamke ambaye hapaki make up.

Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv Nikki wa pili alifunguka na kuweka wazi mke wake hatokaa apake make up:

Hakuna kitu kizuri kama mwanamke ambaye yupo asilia natural kwani sisi binadamu ni wazuri kwa sababu ni asili  na mara nyingi ukibadilisha asili unakuwa unaiharibu na mimi naamini uzuri wa msichana upo kwenye asili yake hivyo msitegeemee kumuona amepaka make up labda lipstick kidogo”.

Niki wa pili amekuwa Kwenye Mahusiano na mrembo huyo ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa kipindi kirefu kidogo.

 

Ukiwa na Mchepuko Hakikisha Mchepuko Wako Mzuri Kuliko Demu Wako- Nikki wa Pili

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap kutoka katika kundi la Weusi, Nikki wa pili ameibuka na kutoa ushauri kwa wanaume wenzake wanaopendelea michepuko.

Nikki wa pili alizua sintofahamu baada ya ujumbe wake alioutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram kutafsiriwa vibaya ambapo aliandika:

chiti na demu mkali mpaka demu Wako akikufumania naye badala ya kumpiga mangumi anamuomba kupiga naye picha, na kumuuliza anatumia mafuta gani, amewezaje kuwa na ngozi nzuri hivyoo na namna alivyotunza shepu na kutokuwa na tumbo kabisa, so akiondoka haondoki na machozi anaondoka na notes alafu akukubali kuwa wewe mbaya yaani yeye mwenyewe kabahatisha kuwa na wewe”.

 

Nikki wa Pili Awatolea Uvivu BASATA.

Ikiwa bado sakata la kufungiwa kwa wasanii likiwa bado linashika kasi katika mitandao ya kijamii huku wengi wao wakingngunika kwa jinsi msanii wa bongo hip -hop ,Roma Katoliki alivyopewa adhabu kubwa ilhali muda wake wa kufanya marekebisho ya nyimbo hiyo yakiwa bado haujaisha msanii ,mwenzake Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi ameilalamikia BASATA kuhusu hatua kali wanazochukua wa wasanii huku akiwakumbusha mambo ya nyuma yaliyopita hasa kipindi cha siasa jinsi kulivyokuwa kumetapakaa kwa nyimbo za matusi lakini zilikuwa hazifanywi kitu chochote..

Niki wa Pili ambae amekuwa msemaji mzuri katika kitandao ya kijamii kuhusu maswala mbalimbali yanayotokea katika jamii anasema kuwa imekuwa  basata wamekuwa wakifumbia macho baadhi ya vitu na kuibuka na baadhi ya vitu kitu kinachowafanya watu waone kama vile hawatendi haki.

Akihoji kuhusu maamuzi ya BASATA , Niki  wa Pili amehoji kwanini kipindi cha kampeni kulikuwa na nyimbo nyingi za siasa zilizokuwa na matusi mengi lakini hazikuwa zikifungiwa lakini wameanza kuwakamta wasanii wenzao.

tukizungumzia nyimbo za matusi bwana zilizotoka wakati wa kampeni , bwana we matuzi ya nguoni,tena takitukana watu wazima  na heshima zao,hapa walezi wetu wakikaa kimya bBASATA kama walezi  wetu msisahau kuwa kuyalinda maadili yetu kiuchumi , kama mlezi  halafu watoto wako wanakuwa wanaishia kufa , inamaanisha hawakulelewa vizuri kiuchumi pia-Aliandika Niki wa  Pili akitaka BASATA kwaangalia pia wasani wake katika swala la kiuchumi.

Maneno ya Nikki wa Pili Kuhusu Upendo na Mahusiano.

Msanii wa bongo fleva kutoka kundi la Weusi nchini , Nikki wa Pili ambae amekuwa ni moja ya wasemaji wazuri sana hata kuwasemea vijana kuhusu maisha wanayoishi na kutoa manen mengi ya hamasa na kujenga kwa vijana , siasa na hata katika maswala ya uchumi amefunguka na kuweka wazi kuhusu kile anachokifikiria kuhusu upendo na mahusiano.

Nikki ambae mara yingi katika nyimbo zake amekuwa akitoa maneno yanayoumiza moyo hasa kwa vijana kama unaishi yale maisha aliyoimba katika nyimbo zake , amekuwa ni moja ya wasanii aanependa kutoa ukweli kuhusu wasichanaau vijana wanaojiingiza katika mahusiano bila kujua dhumuni la mahusiano hayo au ambao wapo kimaslahi zaidi.

upendo ni msaada , kusaidiana katika uchokoraa wenu na tabia zenu, ulemavu wa matendo yenu  na uyatima wa mioyo yenu.

upendo ni uvumilivu kupeana muda wa kutambuana na kurekebisha makosa,muda wa kukua na muda wa kujifunza.

upendo ni msamaha, kujisamehe mwenyewe kwanza ili usiwe na sumu ndani yako na kumrekebisha mwenzako.

upendo ni ndoto na maono.kuota maisha ya mwenzakoalivyozaliwa,kukua na kujua kwanini yuko vile alivyo.upendo sio kumpenda kama unavyojipenda kwa sababu hata wewe uanamambo yako mengi usiyo yapenda, so ukimpenda kama unavyjipenda yale usiyoyapenda kwako pia hutayaenda kwake…upendo ni ahadi ya kuendelea kuwa mkarimu hata kwa mambo yanayokuwa ndimu.

Nikki wa Pili yuko katika mahusino ya kimapenz na mwanadada mmoja ambae amekuwa akiweka picha zake katika ukurasa wake wa instagram kwa muda mrefu.

Nikki Wa Pili Amewatolea Uvivu Watu Wanaotoa Msaada na Kamera Nyuma

Mwanamuziki wa hip hop ya Bongo fleva kutoka katika kundi la Weusi Nikki wa pili amewatolea povu kali watu wanaodai ni wasamaria wema ambao wanaenda kutoa misaada lakini wanabebea makamera ya kuwarekodi.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kwenda kwenye maeneo mbali mbali ambamo inajulikana wanaishi watu fulani wenye maisha magumu inaweza ikawa kituo cha watoto yatima ama hata vituo vya kuishi wazee na kutoa chochote alicho nacho lakini pia ni desturi kwa watu wengi kuita waandishi wa habari.

Wasanii wengi kwenye jamii yetu hawaoni shida kuanika mambo mema waliyofanya katika jamii ni jambo zuri ndiyo lakini sio lazima ujionyeshee kweli umetoa kama kweli ulitoa kwa moyo mmoja hutahitaji kila mtu ajue ingawa huo ni mtazamo wangu tu binafsi.

Lakini inaelekea Nikki wa pili ana mtazamo kama wangu ambapo amewapa makavu watu wote ambao hawaridhiki na kutoa msaada tu lakini watataka waanike kila kona ili waonekane na kila mtu kwaiyo inakuwa ngumu kumtambua yupi ana nia gani ya kweli au yupi ana nia ya uongo:

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka yafuatayo:

Ukitoka na marafiki au familia au wafanyakazi wenzako mkaenda kutoa msaada kwa wenye uhitaji mkifanya nyie na wao mnakuwa mmefanya kazi ya Mungu , maana alisema ukitoa sadaka na mkono wa kushoto mkono wa kulia usijue, lakini ukienda kutoa msaada umembatana na makamera kuandaa mapicha na mavideo kusambaza mtandaoni na kwingineko utakuwa umeenda kufanya kazi ya shetani…..kuwatumia watu wenye shida kujenga jina au brand au kutafuta ushawishi au kifaa cha kufanyia propaganda…saidia kama habari zitasambaa acha zisambae zenyewe ni maoni yangu lakini naweza nisiwe sawa pia”.

 

Nikki wa Pili Amjibu Mh.Nasarri Kuhusu Mh. Sugu

Msanii wa muziki nchini Nikki wa Pili amemjibu Mh Joshua Nassari baada ya kuwatuhumu wasanii kwa kukaa kwao kimya baada ya Mh.Sugu kukamatwa na kuweka polisi kwa zaidi ya siku kumi sasa wao wakiwa wamekaa kimya ilhali mbunge huyo alikuwa mstari wa mbele kuwatetea wasanii katika kupata maslahi yao.

Mh. Nasari anawataka wasanii wakumbuke kuwa Sugu ndie msanii wa kwanza kupigania haki zao kwa uda mrefu na kukataa kufanya kazi za muziki  bila kulipwa na haki hiyo.

wasanii wa bongo fleva mmesahau kabisa harakati za sugu kupigania muziki wenu kusimama.sugu yupo selo siku ya kumi sasa wasanii mmepiha kimya,courtin hamtokei,jela hamji kumuona , mmeamua kumtumikia kafiri.mmesahau kuwa alianzisha harakati za kugoma kuimba bure.

Katika kumjib Mh. Nassari nikki wa pili amemwambia kuwa wasanii wanaogopa kupaza sauti ya kutetea jambo kwa sababu hakuna umoja kati yao na hata wanapotaka kusimama kutetea jambo fulani mtu anaweza kujikuta peke yake.

Wasanii hawna umoja na chama chao hakina nguvu kwaio hata kinapotokea kitu  wasanii wakatakiwa kulitolea sauti hakuna platform   ya kulishikilia jambo hilo  na kujikuta kila msanii huyo yuko peke yake  na kupaza sauti peke yae wasanii wengi wanaogopa hilo.-Aliandika Nikkki wa Pili.

Mheshimiwa joseph mbilinyi jina la usanii sugu aliwekwa jela siku kama 10 zilizopita kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi kwa wananchi juu ya serikali iliyopo madarakani.

 

Nikki wa Pili Azungumza na Baraza la Sanaa.

Msanii wa muziki Tanzania Nikki wa Pili amefunguka na kuhoji juu ya vitendo wanavyovifanya baraza la sanaa vya kuwafungua wasanii kama ni vya halali bila kuzingatia mambo mengi na kujikuta wakijikita katika mavazi tu ilhali swala la maadili linakuwa linapande nyingi na sio swala la mavazi tu.

Nikki wa Pili alizungumza hayo alipokuwa naongea na mtangazaji wa EATV na kusema kuwa baraza linatakiwa kuangalia swala la maadili kwa upana sana na sio katika mavazi tu kwa sababu hata kwa upande mwingine ukiangalia utakuta kuwa hata wao kama baraza wanakuwa hawatimizi majukumu yao wa wasanii.

Nikki amesema kuwa Baraza wanakosea wanapokuwa wanawafungia wasanii tena hasa wa kike kwa sabau ya maadili ili hali wanapaswa kuangalia vitu vini kabla ya kutoa uamuzi huo,lakini pia yapo mambo mengi baraza wanatakiwa kuyanyoosha na kuyyaweka katika mstari kabla hawajaanza ku-judge kuhusu mavazi na maadili yao.

Maneno ya nikki yanakuja baada ya Baraza la Sanaa kuwafungia baadhi ya wasanii wa kike kwa madai kuwa wasanii hao wamekuwa wakitoa video na kuchapisha picha za uchi katika mitandao na kutoa ahadi kuwa yeyeto atakae toa wimbo usiokuwa na maadili ya kitanzania basi wimbo huo na kazi zake zitafungiwa.

Wasanii waliofungiwa hivi karibuni kutokana na utovu wa nidhamu katika kazi za muziki ni pamoja na Gigy money na Pretty kindy huku wengine wakiambiwa kuripoti katika ofisi za baraza lakini pia wimbo wa Rostam wa Kibaa100 pia umfungiwa mpaka utakapofanyiwa marekebisho katika baadhi ya vipengele.

Hivi Ndivyo Zitto Kabwe Alivyomkaribisha Nikki Wa Pili Kujiunga na ACT Wazalendo

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe hajaona hiyana kumkaribisha Mwanamuziki wa Bongo fleva Nikki Wa Pili kujiunga na chama hicho.

Nikki Wa Pili ni mmoja kati ya wasanii wasomi nchini anayemiliki degree kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, tofauti na wasanii wengine wengi Nikki Wa Pili ni msanii anayependa kutoa maneno ya kizalendo ambayo yanalenga kujenga nchi yetu.

Zitto Kabwe baada ya kuvutiwa na upeo mkubwa wa Nikki Wa Pili alimuandikia ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter huku akimsihi kujiunga na ACT Wazalendo.

Njoo ACT Wazalendo ujenge chama cha kijamaa acha mambo yako”.

Baada ya Tweet hiyo ya Zitto Kabwe kumuomba Nikki Wa Pili ajiunge na chama chake ili akajenge ujamaa, Nikki alimjibu kuwa chama cha kijamaa kinajengwa na watu wanyonge bali yeye kama mtu Vyombo vya habari sio wa kuaminika kwani hachelewi kuwauza.

Chama cha Kijamaa hujengwa na Vugu vugu la wanyonge wenyewe, ni muwe tu na mkakati wa kuwaunganisha ki-ideoligia umoja zao hizo za boda boda, machinga, wakulima, sisi watu wa media hatukawii kuwauza sokoni kama nyanya”.

Wasanii wengi wa Bongo movie na hata Bongo fleva wamekuwa wakijiingiza katika vyama mbali mbali vya siasa lakini mpaka sasa Nikki Wa pili hajaweka wazi kuwa yeye ni mfuasi wa chama gani.

 

Mambo Atayoyafanya Nikki Wa Pili Akiwa Raisi

Mwanamuziki  Nikki wa pili kutoka katika  kundi la Weusi, ambalo linaundwa na wasanii watatu Joh Makini, G-Nako na Nikki wa Pili ,amefunguka na kuendelea kuonyesha nia yake ya kutaka kuingia kwenye siasa kwa spidi ya ajabu,Nikki wa Pili ambae anafanya vizuri wa kibao chake cha kihasara na quality time ambazo zinafanya vizuri zaidi katika vituo mbalimbali vya habari.

Nikki wa pili ametaja baadhi ya mambo muhimu atakayoyafanya endapo atakuwa raisi.Mwanamuziki huyo ambae alishawahi kusema kuwa anampango wa kuingia kwenye siasa anaendelea kuthibtisha nia yake hiyo kupitia maneno yake.Katika vitu alivyoviorodhesha ni pamoja na :

1.Kikao kikubwa cha serikali yangu itakuwa sio baraza la mawaziri bali  mkutano mkuu wa kijiji au mtaa(kitaa kitaongea)

2.Kipimo kikubwa cha maendeleo itakuwa ni kupanda au kushuka kwa maisha ya watu sio vipimo vya kukua kwa uchumi au makusanyo ya fedha.

3.Mfumo wa elimu utajikita katika kupima learning na sio ufeli au kufaulu

4.Vyama vyenye nguvu vitakavyokuwa vikifanya mikutano na kuhoji serikali sio vyama vya siasa  bali vyama vya wakulima, wafanyakazi ,walimu, machinga , bodaboda madaktari na kadhalika.

5.Serikali itakuwa mdau mkubwa  uchumi na mukewezaji  atakuwa ni mkulima,mfugaji, mchimbaji mdogo,wavuvi wadogo na wafanyabiashara wadogo.

6,Ardhi, maji ,elimu ,afya, havitakuwa bidhaa bali hifadhi za jamii

7.Maisha bila maadili hayana maana , kila mtoto ni lazima afundishwe kuwa na  maadili , uaminifu,heshima,ujamii,upendo, bidii, na kujiamini.

8,Mahusiano na mataifa ya afrika  hayatakuwa na neno wahamiaji haramu , mwafrika hawezi kuwa haramu maana Afrika ni nyumbani kwake.

Nikki anasema kuwa maswali ataulizwa kipindi cha kampeni kikifika lakini anampango wa kuwa mgombea binafsi.

Nikki akiwa kama moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa na impact kubwa kwa jamii, atakapojiingiza katika siasa atakuwa amevumbua na kusaidia vijana wengine wengi wanaompenda na kumuamini pia.

Ukiachana na kazi za muziki anazofanya Nikki na wenzake lakini pia msanii huyu amekuwa akitumiwa na mashirika katika mikutano mbalimbali ya uhamasishaji wa vijana katika jamii.

 

Nikki Wa Pili Azungumzia Bifu La Dogo Janja Na Young Dee

Wakiwa bado wanavuma sana katika vichwa vya habari sehemu mbalimbali wasanii  wawili wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) msanii Dogo Janja kutoka Arusha na Young Dee kutoka wa Dar Es Salaam kutokana na bifu linaloendelea kati yao katika mitandao na vyombo vya habari , msanii mkongwe na mwenye mafanikio  kutoka kundi la Weusi ameamua kulizungumzia  bifu ilo ambalo linaonekana ni tatizo .

Nikki amekuwa ni mmoja wa wasanii ambao amekuwa akishauri na kusaidia watu wengi katika tasnia ya muziki na nje ya muziki pia, ukiachana na kipaji cha muziki alichonacho Nikki  akiaminika sana katika jamii kutokana na ushawishii wake mkubwa kwa vijana wenzake katika swala zima la maendeleo

Akiongean na  eNews ya EATV, Nikki wa Pili anaona kuwa bifu ilo linaendelea na linaweza kufika pabaya ilhali wasanii hao wameanza kuingia katika  maisha yao binafsi badala ya kuwa na ushindani wa kikazi “mimi naona kama kuna tatizo hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi,kwaiyo ningefurahi kuona wanashindana  kumuziki zaidi.” alisema Nikki wa Pili

Kwa kuongezea pia Nikki aliwashauri kuwa wao kama wasanii maneno mengi wanayoyasema huwa yanabaki kuishi katika jamii na ni vigumu kuyapoteza kwa mara moja hivyo kwa kila jambo wanalofanya au kuongea ni lazima wachagulie lile lililo sahihi ” maana unapokuwa maarufu ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika kirahisi kwa hiyo  ni vizuri zaidi kama watachagua maneno ya kutumia kila mara” aliongezea Nikki wa Pili

Dogo Janja na Young Dee waliingia katika bifu zito baada ya Young Dee kukataa kufananishwa na msanii mwenzie Dogo Janja, huku akitoa sababu kuwa yeye ni mkubwa kimuziki kuliko msanii mwenzie huyo, lakini haikuwa rahisi kwa Dogo Janja kukubaliana na kauli ya mwenzie hivyo aliamua kumjibu, katika majibu yake Dogo Janja alimwita Young Dee ‘mteja’ na kwamba hata yeye hawezi kulinganishwa kimuziki  na mtu anaekula unga, kitu kilichofanya wawili hao kundelea kuzozana.

Nikki Wa Pili: Ipo siku nataka kugombea uraisi

Mwanamuziki na Rapa maarufu Tanzania kutoka kundi la Weusi anayejulikana kama Nikki wa pili amekiri kuwa moja kati ya ndoto yake kubwa maishani ni kuja kugombea uraisi ili kusaidia nchi yake ya Tanzania kutokana na matatizo ambayo wananchi wanayo na wimbi kubwa la umaskini unaolikabili taifa hili.

Kukiwa na wimbi kubwa la wasanii wa muziki wa Bongo fleva kujiingiza katika fani ya siasa ambayo hayo yameonekana kwa wasanii wakubwa kwenye tasnia hii ikiwemo Mheshimiwa Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya mjini ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara ya habari vijana utamaduni na michezo maarufu kwa jina la sanaa kama “Sugu” ambaye aliachana na muziki na kuamua kuingia kwenye siasa. Pia mfano mwingine ni Proffesor Jay ambaye alikuwa ni rapa maarufu sana kwa nyimbo zake naye pia aliamua kuukacha muziki na kuamua kuingia katika siasa ambaye sasa ni Mbunge wa Mikumi lakini pia wasanii wengi wamejaribu kuingia katika siasa kama Wema Sepetu lakini hawakufanikiwa.

Katika mahojiano aliyoyafanya Nikki wa pili hivi karibuni alisema kuwa ni vizuri kwa wasaanii hawa kuingia katika siasa kama wabunge ili kusaidia jamii zao na Watanzania kwa ujumla lakini yeye kwa ubinafsi wake ameona kuwa hatogombania ubunge bali anataka moja kwa moja anataka akagombanie uraisi wa nchi ili apate nafasi kubwa zaidi kutatua matatizo ya wananchi. Mwanamuziki huyo alisisitiza:

“Ipo siku nataka nataka kugombea uraisi kwasababu nitakuwa na nafasi kubwa ya kutatua matatizo ya Watanzania kuliko kuwa mbunge”.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.