Rose Ndauka :-Mc pilipili Alikuwa mtu wa Masihara

Mwanadada msanii wa bongo movies, Rose Ndauka amefunguka na kusema kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na mchekeshaji Mc pilipili kama ambavyo imekuwa ikizushwa katika vyombo vya habari, Rose anasema kuwa mara zote alikuwa akichukulia kama swala la utani.

Mc Pilipili baada ya kumvisha pete mchumba wake mpya, watu walisema kuwa Rose ndauka anakuwa moja kati ya wasichana wanaumia sana na swala hilo kwa sababu aliwahi kutoka nae kimapenzi Mc Pilipili.

Mc pilipili nilikuwa nafaya nae kazi Times Fm na alikuwa kila mara ni mtu wa masihara tu  sijawahi kumcukulia kuwa serious kabisa, kwaio sijawahi kuhisi kitu kama ananipenda wala kama alikuwa akinitaka kimapenzi.

Akiongea kuhusu swala la kwenda kutambulishwa kwao Dodoma, Rose anasema kuwa ndio aliwahi kwenda Dodoma lakini ilikuwa ni kikazi tu na wala sio vingine kwa sababu waliweza kwenda Dodoma na kufanya kazi na kila mtu alifikia katika hotle yao na walikutana tu ukumbini.

Mc Pilipili Ampigia Magoti Rose Ndauka

Mc Pilipili ampigia magoti Rose Ndauka kumuomba radhi hadharani baada ya actress huyo maarufu kuwa mkali kwa kumburuza kwa wanasheria kumtaka amlipe million 150 za Kitanzania kwa kumchafua mbele ya umma kuwa ameshatembea nae kimapenzi huku akijua sio kweli anadanganya jamii

Katika barua iliyoandikwa tarehe 9 January 2019 na wanasheria kutoka kampuni ya KIKA Attorneys ya jijini Dar es salaam inamtaka Mc Pilipili kumuomba radhi Muigizaji huyo kwenye media hizo hizo alizotumia kumchafua mteja wao ambapo Rose anakiri taswira yake mbele ya jamii kuchafuka kwa matamshi ya Pilipili. Asipoomba radhi hatua zaidi zitachukuliwa kulipa fidia ya million 150 kumchafua muigizaji huyo

Barua hiyo ya wanasheria wanaomuwakilisha Rose inasema asilimia 70% ya kazi zake za Sanaa na biashara nyingine anazofanya hutegemea reputation ya Jina lake alilojijengea kwa miaka takribani kumi sasa hivyo ameanza kuathirika ikiwemo kukosa deals kadhaa kwa kuchafuliwa huko. .

iSku chache zilizopita baadhi ya watu walikuwa wakimdhihaki na kumkejeli mitandaoni Rose kufuatia mc Pilipili kumchumbia mwanamke mmoja wakidhani rose ni zilipendwa wa mc Pilipili kumbe si kweli. Juzi Kwa Mara ya pili Rose aliandika kumtaka Mc Pilipili aseme ukweli asiendelee kuchafuka lakini hakufanya hivyo kitu ambacho kinaashiria Rose kwa Mara ya Tatu kuamua kufuatia proffesional route zaidi kwa wanasheria badala ya kumbembeleza Mc Pilipili

Katika nyakati tofauti kuanzia 2016 MC Pilipili kwenye interviews na media mbalimbali alikuwa akijitapa kutembea kimapenzi na baadhi ya wasanii maarufu wa kike akiwemo Rose Ndauka ambapo mwaka 2016 Rose alikanusha kutembea na Pilipili lakini mchekeshaji huyo aliendelea kusema ametembea na actress huyo aliyejipatia umaarufu sababu ya kazi zake za Sanaa

Leo MC Pilipili amepost kumuomba radhi Rose lakini akiwa amezuia comments section watu wasitoe maoni Yao

Rose Ndauka Kuangalia Fursa Nyingine Mbali na Filamu

Muigizaji wa filamu za Bongo Movie Rose Ndauka amefunguka na Kuvunja ukimya baada ya kutosikika na kutoonekana akifanya kazi yoyote ya kisanaa kwa muda mrefu.

Rose amefunguka na kuweka wazi kuwa ameamua kuweka sanaa kando kwa sasa na kuelekeza nguvu zake Kwenye shughuli nyingine kutokana na majukumu yake kuongezeka.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Amani, Rose alisema kuwa mtoto wake sasa hivi anakua na anahitaji mahitaji muhimu kama elimu bora na vitu vingine vingi hivyo lazima aangalie upande mwingine wa kufanya kitu mbali na filamu ila maisha yazidi kusonga mbele.

Unajua Naveen anakua, sasa nikisema nikalie kazi moja ni ngumu sana, sasa hivi nimefungua House Beuty kwa ajili ya kupamba wanawake na masuala mazima ya urembo, kazi hii inaniongezea kipato na huku nikiendelea mdogomdogo na filamu”.

 

Joh Makini Haoni Tatizo Wasanii wa Kiume Kuvaa Vikuku.

Msanii kutoka katika kundi la weusi mwenye kipaji kikubwa cha kuchana katika kundi hilo amefunguka na kusema kuwa kwake yeye huwa haoni shida pale anaopoona wanaume wanataka kuvaa vikuku kama uamuzi wao wameamua kufanya hivyo.

Joh Makini anasema kuwa wanaume kuvaa vikuu ni fasheni kama fasheni zinginekwaio hakuna swala la ajabu katika swala kama hilo kwa wanaume.joh makini anasema hivyo kwa sababu anamini kuwa wasanii ni watu wanaoenda na fasheni na kila siku style huwa zinabvadilika katika fasheni.

sijui kesho itakuwaje lakini mimi niachoamini ni style kamastyle zingine, kwa sababu kama mimi ninaamua kufuga rast na pia kuna watu wanataka kuvaa vikuu,kutoboa poa au masikio kwa sababu ni aina ya maisha anayoamua kuchagua mtu.

Maneno haya , yanakuja baada ya msanii mkubwa tanzania diamond platinumz kuonekana amevaa cheni katika mguu wake na kusababisha mashabiki kumshambulia sana.

Rose Ndauka Afungukia Mapenzi Yake na Dj Ommy

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Rose Ndauka ameibuka na kufungukia taarifa za kuwa Kwenye Penzi Zito sana na Mtangazaji na Dj maarufu Dj Ommy Crazy.

Tetesi za Rose Ndauka kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Dj Ommy zilianza baada ya picha za wawili zilizoqaonyesha wakiwa pamoja kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Amani, Rose alisema hamna chochote kinachoendelea kati yake na DJ Ommy zaidi ya kuwa marafiki wanaosapotiana katika kazi hivyo kwenda kwake kwenye bethidei yake hivi karibuni kulikozua maneno lilikuwa ni jambo la kawaida tu na si vinginevyo;

Sina mahusiano na huyo mtu, mimi nilienda kwenye bethidei yake kama rafiki yangu tu na hakuna kingine. Nashindwa kuelewa hivi vitu vinatoka wapi? Wanataka mtu asimsapoti rafiki wa kawaida?“.

Tetesi hizi zinakuja kwani kwa muda mrefu Rose amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano na mwanaume ambaye ni mdau Kwenye mambo ya siasa lakini amekataa kumtaja mtu huyo.

Maisha ya Mitandao Yanatesa Wengi:-Rose Ndauka.

Mwanadada kutoka bong movies Rose Ndauka amefunguka na kusemakuwa maisha wanayoishi watu katika mitandao yanawapa matesi sana kutokana na ukweli kuwa wengi wao hawaishi yale maisha yao ya kiuhalisia na kuishia kuiga vitu ambavyo kwa namna moja ama nyingine sivyo walivyo.

Akitoa maoni yake kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii Rose Ndauka anasema ‘ maisha ya mitandao yanatesa wengi na wengine kusahau kabisa uhalisia watu na kupotea  na kujiona kuwa wao ndio wanahaki ya kila kitu.jamani tuwe makini na hii sehemu inayotukutanisha wengi , nadhani hata walioweka walikuwa na  nia nzuri”

Maneno ya Rose ndauka yanaweka ukweli uliopo bayana kabisa kwa maisha ya sasa ya mitandaoni ambapo watu wamekuwa wakijitahidi kuishi maisha yasiyo yao ilimradi tu kuwafurahisha au kuwaonyesha wengine wana uwezo wa kufanya kitu flani.

Rose Ndauka Adaiwa Kutapeli Pesa

Muigizaji wa Bongo movie Rose Ndauka amepatwa na skendo nzito ya utapeli ambapo amedaiwa kumtapeli mfanyakazi wake kiasi cha shilingi laki na nusu.

Kipindi cha Shilawadu cha Clouds Fm wanaripoti kuwa mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Stumai amemtuhumu Rose kwa kumdhulumu kiasi hicho cha pesa baada ya kumpa huduma.

Kwenye Interview na kituo hicho mwanadada huyo anafunguka kuwa aliajiriwa Kwenye moja ya saluni za Rose Ndauka lakini baada ya kufanya kazi kwa miezi mitatu alikataa kumlipa na kudai hajaona faida hivyo avumilie atakuja kumsaidia kuwa supastaa.

Baada ya povu hilo Soudy Brown alimtafuta Ndauka ambaye alimwaga povu zito kwani hakufurahishwa na taarifa na kumtolea maneno haya:

Kama kesi inahusu wafanyakazi nenda Kwenye wizara ya Ajira na wafanyakazi sio Shilawadu, Soudy wewe ni mshkaji wangu Sitaki kupizana Kelele na wewe nina stress nyingine za maisha za Familia lakini stress nyingine za kujiunga za kipumbavu kama hizo sitaki kuziongelea kabisa”.

Mwishowe Rose amemtaka dada huyo aende mahakamani akashtaki au anaweza akaenda alipokuwa anafanya kazi Mwanzoni.

“Hii sio Tanzania Niliyoizoea, Tupaze Sauti”- Rose Ndauka

Muigizqji wa Bongo movie Rose Ndauka ni moja kati ya wasanii walioguswa na tukio la kinyama alilofanyiwa mwanafunzi Aqwilina Aqwline siku chache zilizopita na polisi.

Aqwilina ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo cha Usafirishaji (NIT) alifariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi kituo cha mabasi cha Mkwajuni Kinondoni ambapo polisi hao walikuwa wanawatawanya wafuasi wa Chadema Kitiona hapo na Aqwilina alikuwa anapanda basi kwa ajili ya kwenda kupeleka barua yake ya masomo Bagamoyo.

Rose Ndauka amefungukia suala hilo la kusikitisha na kueleza machungu yake kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika:

Enough is enough umefika muda sasa wa kuadress hili tatizo kama lilivyo without sugar coating it kwa namna yoyote! Recently kumekuwa na utumiaji mkubwa wa nguvu kusimamisha/ kuzuia / uhuru wa mawazo.Haya yamesababisha vifo ukosefu wa amani na furaha kwa Watanzania walio wengi kitu ambacho sio sawa, Amani ya Tanzania yangu na Watanzania wenzangu imekuwa mashakani na kama Amani inaanzia moyoni basi wengi wamekuwa waoga kusema hawana hiyo peace of mind. Huyu mwanafunzi ambaye hakuwa na uhusiano wowote wa tukio la jana kakumbwa na was umauti kwa kosa la polisi. Just one bullet stole a dream worth millions. Mungu akulaze pema mdogo wangu but this should be the beginning of the end of this brutality tupaze sauti kukemea suala hilo this is not the Tanzania am used to”.

 

Rose Ndauka Awatolea Uvivu Watoa Mimba

Wadada wengi wa mjini wamekuwa na dhana kwamba kubeba mimba na kulea mtoto ni moja  ya hatua ya kuzeeka au kuharibu mwili, hivyo wengi ukataa kubeba mimba na hata wakibahatika kubeba mimba basi wengi uzitoa  ili kuepukana na majukumu ya uzazi.Ingawa katika tasnia ya bongo movies na bongo fleva tunaona sasa wasanii wa kike wanaoendelea kuzaa na kuwa wazazi inaongezeka lakini bado wapo baadhi yao wameendelea kuwa na tabia ya kutoa mimba  wanazopata.

Rose Ndauka ni moja ya wasanii wa kike ambao pia ni walezi, yeye ni mama wa mtoto mmoja wa kike na amekuwa mama bora kwa mtoto wake.Akiongea kwa undani kuhusu watu wanaotoka mimba Rose Ndauka anasema kuwa mtoto ni faraja sana kwa mama na hata wazazi wote wawili pia kuwa na mtoto ni oja ya faraja pale unapokuwa katika waati mgumu kwaio wasanii wajifunze kuwa kuzaa sio bahati mbaya.

Rose Ndauka anasema kuwa wadada wengi wamekuwa wakitoa mimba bila kujua kuwa watoto ni baraka kwa familia pia ni faraja pale mtu unapopata changamoto.

Nawashangaa wasichana wengi wakipata mimba wanaanza kuwaz kutoa nila kujua kuwa mtoto ni faraja kubwa sana katika familia,I wishi wangekuwa wanajua  furaha na faraja ya mwanamke yoyote ile ni kuwa na mtoto, wasingefanya hivyo…huwezi amini kabisa kuwa  furaja ya kuwa na mtoto kwa mawanamke ni zaidi ya changamoto.-Alifunguka Rose Ndauka.

Hata hivyo inabidi wanawake na wasanii wa kike wajue kuwa  uwezekano wa kuzaa na kuwez kumaintain mwili wako kurudi katika hali ya kawaida, lakini pia wakiwa kama vioo katika jamii tunazoishi kwa sababu wanakuwa wakiangaliwa an watu wengi wanapaswa kufanya yale ambae yanawapendaza jamii.

 

Kifo Cha Kanumba ni Kikubwa Kuliko Hukumu Aliyoipata Lulu- Rose Ndauka

Mwigizaji wa filamu za Bongo Rose Ndauka amefunguka na kudai kuwa kifo cha Kanumba ni kikubwa kuliko hukumu ya kuua bila kukusudia aliyopewa muigizaji Lulu Michael.

Elizabeth Michael ‘Lulu’ amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mapema wiki hii baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Steven Kanumba.

Kwenye mahojiano ambayo Rose Ndauka alifanya na Millard Ayo alifunguk yafiluatayo kuhusu kifo cha Kanumba kilichotokea miaka mitano iliyopita na hukumu ya Lulu:

Hili jambo lililotokea limenigusa kwa sababu najifunza mambo mengi najifunza kuwa kwenye maisha kuna kitu kinaweza kukukuta ambacho hujawahi kutarajia lakini vile vile kimenigusa kwa sababu pengo la Steven Kanumba halijaweza kufutika hasa kwenye mioyo ya Watanzania wengi, nikijiongelea mimi kama msanii lakini pia nikiongelea Watanzania waliokuwa wanapenda filamu za Steven Kanumba lakini pia kwa upande mwingine kimenigusa kwa sababu Lulu bado ni binti mdogo lakini mwisho wa siku Mungu ana mipango yake”.

Lakini pia Rose ameongelea kuhusu post yake aliyoiweka kwenye kurasa yake ya Instagram na waty wengi kutafsiri kuwa alikuwa upande Wa Kanumba:

Kwenye ile posti nilikuwa namaanisha kwamba vijana tujifunze kutokana na tukio zima  lililotokea kwa Kanumba na kusababisha kifo chake lakini vile vile kwa upande mwingine like tukio limemsababishia kifungo msanii Lulu Michael lakini piano lulu anatakiwa amuombe sana Mungu kwani hakuna linalomshinda kila kitu kinawezekana lakini pia atatumikia kifumgo kitapita lakini Kanumba ameenda moja kwa moja kwaiyo pia hiyo miaka miwili haiwezi kulipiza maisha ya Kanumba aliyopoteza muhimu ni kusameheana na kuendelea na maisha”.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.