Thea na Mike Sangu Bado Mahabani Hata Baada Ya Ndoa Kuvunjika

Msanii mkongwe wa Bongo movie Salome Urassa maarufu kama Thea na aliyekuwa mume wake ambaye pia ni Msanii Mike Sangu wamedaiwa kuwa bado wanapendana licha ya ndoa ya kuvunjika.

Thea na Mike Sangu walikuwa kwenye ndoa Lakini waliishia kutengana kwa muda mrefu, juzikati walionesha kuwa bado wanapendana kwa kui­tana majina matamu, kitu ambacho kiliwaacha wengi mido­mo wazi.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa tukio hilo lilichukua nafasi maeneo ya Yombo Dovya jijini Dar ambapo wasanii hao walikwenda kutoa msaada kwa Hamisi, mtoto anayesumbuliwa na uvimbe.

Ilikuwa hivi; wakiwa eneo hilo mmoja wa wasanii alimtania Thea na kumwambia kuwa, Mike anamuita. Bila ku­tarajia Thea alimsogelea Mike na kumuuliza kwa sauti iliyotokea puani; ‘Eti kweli unaniita mume wangu?’

Maneno hayo yaliyotoka kwa sauti ya kimahaba yaliwafanya wasa­nii waliokuwa eneo hilo kuamini kuwa bado wawili hao wanapendana na huenda siku moja wakarudiana kwani waswahili wanasema; penzi la kweli halifi.

Mike Adai Kuwa Hataki Hata Kusikia Suala La Ndoa

Msanii wa filamu za Bongo movie Mike Sangu amefunguka na kusema wazi wazi kuwa hataki hata kusikia Suala kufunga ndoa kwa muda mrefu sana.

Mike amesema kuwa sio kwamba haoni wanawake wa kuoa tangu atengane na mkewe msanii mwenzake wa Bongo movie, Salome Urassa ‘Thea’ bali hana hamu na ndoa tena kwani imemkinahi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Mike alisema kuwa anakutana na wanawake wengi ambao angetaka kuingia nao kwenye ndoa asingeshindwa lakini wito wa kuoa umepotea moyoni mwake.

Kiukweli sina hamu ya kuoa tena mpaka moyo wangu utaka­pokubali, ni kama ndoa imeniki­nahi hivi na si kwamba sina wa kuwaoa, wapo wengi lakini bado siko tayari“.

Mike na Thea waliachana miaka kadhaa ya nyuma ambapo walikuwa bonge la varangati na kuanika mambo yao katika magazeti ya udaku.

Tumbo Kubwa La Thea Lazua Utata

Muigizaji mkongwe wa filamu za Bongo movie Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea alizua gumzo mbele ya hadhara Baada ya kuonekana kuwa na tumbo kubwa kupitiliza.

Kutokana na kitambi hicho mara moja kuna taarifa zilisambaa kwamba huenda mwanamama huyo ni mjamzito na watu wengi ndiyo maana tumbo limemtoka hivyo au kama ni kuridhika na maisha basi ameridhika kwelikweli.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers  na kuulizwa kuhusiana na madai kwamba ni mjamzito au laa, Thea alikuwa na haya ya kusema:

Jamani sina ujauzito, hili tumbo ni kwamba nimenenepa tu, yaani nimeridhika na maisha ninayoishi lakini kama watu Wananichuria haina shida kwa sababu kuzaa ni jambo jema sana.”

Mashabiki wengi walionekana kuuponda muonekano wa Thea na kumkosoa kwa kujiachia na kunenepeana tu na kupoteza mvuto Wake Kama msanii.

 

Thea Apewa Ruksa Ya Kuolewa na Mumewe

Muigizaji wa Bongo movie Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea amepewa ruksa ya Kuolewa Tena na mume wake Michael Sangu ‘Mike’ baada ya kutangaza nia ya kutaka ndoa.

Mike na Thea walifunga ndoa miaka kadhaa iliyopita lakini baada ya kushindwana kukaa kwenye ndoa na kuachana Thea alitangaza kuwa anataka Kuolewa na mwanaume mwingine jambo ambalo mume wake Mike hana tatizo nalo.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mike amesema Thea ana uhuru hata wa kuolewa au kuzaa na mwa­naume yeyote anayemtaka kwani yuko huru hakuna sheria yoyote inayo­mbana kwa kuwa wakati wanafunga ndoa katika Kanisa Katoliki, walifunga ya mseto hivyo muigizaji huyo akawa anaendelea kusali kwenye kanisa la kilokole alikokuwa tangu mwanzo.

Thea yuko huru kuolewa au kuzaa hata na wanaume kumi maana hakuna kinachomzuia, shida iko kwangu maana dini ya Katoliki inatambua ndoa moja tu ambayo nili­funga naye na hatujawahi kuibatilisha”.

Kwenye mahojiano na Global Publishers wiki chache zilizopita Thea alitangaza nia ya Kuolewa baada ya kupata mwanaume mwingine.

Ndoa Ya Thea na Mike Yafika Pabaya

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea amekiri ndoa yake na Muigizaji mwenzake Michael Sangu kufika  sehemu mbaya na kutaka ivunjike kanisani.

Thea amefunguka kuhusu ugumu aliopitia katika ndoa yake na jinsi alivyoichoka mpaka kufikia hatua ya kutaka Kubeba mimba ya mwanaume mwingine ili mradi tu Ndoa hiyo iweze kuvunjika.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Thea alisema utaratibu wa ndoa za Kikristo hautambui talaka ndiyo maana tangu amemwagana na mumewe hajaolewa kwa sababu ya kifungo hicho cha sheria za dini ambapo sasa ameamua ‘kujilipua’ ili apate mume mwingine.

Unajua kanisani kama mmetengana na mume halafu ukaenda kuzaa na mwanaume mwingine ndoa inakuwa imeshavunjika tayari, sasa hivi nina mpenzi na ninataka nibebe mimba yake; hapo ndiyo ndoa na Mike itakuwa imefikia ukingoni”.

 

Hakuna Msanii Anaenipa Changamoto-Thea

mwanadada mkongwe kutoka bongo movies amefunguka na kusema kuwa amekuwa katika tasnia ya filamu kwa zaidi ya miaka 20  kwaio hakuna msanii anaempa changamoto  katika kazi za sanaa kwa sasa kwa sababu anajiamini na kazi zake.

Thea anasema kuwa amekuwa ni msanii anaejitahidi sana ku-maintain sanaa yake kwa kutengeneza filamu zenye ubira ili kuendlea kuwaweka mashabiki wake wasiondoke wala kumchoka na kazi zake.

Nina miaka 20 katika game na sina changamoto yoyote inayonisumbua  kwa mastaa wa sasa lakini kitu ninachowaambia tu ni kwamba wajitahidi na kukaza buti kwa sababu game ni gumu kwa miaka hii ukiwa unafanya kazi na bado zikawa zinakulipa  ni ngumu sana.

Thea anasema kuwa katikakazi zake alizofanya ambazo ziko zaidi ya 50 amekuwa akiipendelea sana filamu yake yan ya sengito.

Hata hivo thea ansea kuwa mara nyingi hutumia muda wake kuhakiksha kuwa kazi zak za sanaa zinakuwa sawa uhuki akitolea mfano na kusema kuwa kama hana kazi za filamu hulala saa sita lakini kama anakuwa na kazi huweza kulala hata saa9.

 

Sijawahi Kunyakua Bwana Wa Mtu- Thea

Msanii mkongwe wa Bongo movie Salome Urassa maarufu kwa Jina la usanii kama Thea, amefunguka na kuweka wazi kuwa katika maisha yake hajawahi hata siku moja kunyakua bwana wa mtu.

Watu maarufu hasa Kwenye tasnia ya Bongo fleva na Bongo movie wamekuwa wakinyosheana vidole na kutuhumiana kwa vitendo vya kuchukuliana mabwana au wanaume.

Kwenye mahojiano  na Za Motomoto News, Thea aliweka wazi kuwa, suala la kuibiana mabwana halipo kwa wasanii tu, bali ni kwa jamii nzima, lakini kwa upande wake hajawahi  kumzunguka mtu kwa kuwa hiyo ni tabia ya mtu na kwake haipo.

Kiukweli tangu niyajue mapenzi, sijawahi kuiba bwana wa mtu kwa sababu siyo tabia yangu na siwezi kufanya hivyo, wanaochukua mabwana za watu ni tabia zao ambazo huwezi kuzibadilisha na hii haipo kwa wasanii tu, bali ni kwa jamii kwa jumla kwani tumekuwa tukisikia sana ila kwa wasanii wanaonekana zaidi kutokana na majina waliyonayo”.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.