Ujumbe wa Wastara kwa Sajuki.

Mwanadada Wastara Sajuki amefunguka na kuandika ujumbe mzito kwa mume wake aliwahi kuwa nae kwa mahusiano kwa mud refu lakini kwa bahatri mbaya mwanaume huyo alifariki Dunia na kumuacha mwanadada huyo akiwa mjane na kuhangaika sana na maisha hasa baada ya kupata ulemavu wa mguu.

Mwanadada huyo anaonyesha kumkumbuka sana mwanaume wake huku akisema kuwa hata watoto wake mara zote wamekuwa wakimuulizia sana baba yao , na hata  kumuita baba yao muongo kwa sababu mara zote amekuwa akiwaambia kuwa atarudi.

Baba, watoto wamekumiss sana watoto wako Farheen anasema urudi basi maana sasahivi huku duniani uongo unaaminika zaidi kuliko ukweli wenyewe. Hujui kama hauwezi kurudi tena na hataki kukubali ukweli nikimwambia uongo ndio ananielewa japo sipendi kuongea uongo. Siku ya kutoka moyoni mwangu ni siku nitakayozikwa. Miss you

 

Wastara Atamani Kufa Baada ya Kupatwa na Majanga

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma amefunguka na kuweka wazi kuwa anapitia kipindi kigumu sana kiasi ya kwamba alitaka kujiua Baada ya kuibiwa kila kitu siku za Hivi karibuni.

Global Publishers wanaripoti kuwa Wastara ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la mguu wake wa kulia kwa muda mrefu baada ya kukatwa, bado amekuwa akipambana kujikimu kimaisha kupitia filamu lakini juzikati watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwake, Sinza-Kwa Remmy jijini Dar na kumuibia vifaa vyote vya ‘production’ pamoja na vitu vingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Wastara alifunguka juu ya majanga yaliyomkuta huku akisema kuwa, imefika wakati anatamani asiwepo duniani:

Napita kwenye wakati mgumu sana jamani, kila likitoka hili, linaingia lingine, natamani hata nijiue. Ni kweli juzi nimeibiwa vifaa vyangu ninavyotumia kuzalishia filamu na vipindi vya TV, vifaa vina thamani kama ya milioni tisa hivi.

Sielewi naanzia wapi, hapa nilipo nina kazi za watu ambazo zilikuwa kwenye ‘external’, nililetewa kwa ajili ya kuwafanyia kazi, wamechukua, kuna vipindi vya TV ambavyo nilikuwa nikivifanya kwa sasa sijui nitarekodi vipi tena, nimechanganyikiwa, natamani niondoke kwenye mgongo wa ardhi”. Lakini pia Wastara ameweka wazi kuwa ameshawashirisha polisi juu ya janga hilo na anaamini ulikuwa ni mchongo wa ndani:

Ishu iko polisi, washukiwa wawili ambao ni mlinzi na kijana mmoja ambaye ananisaidia kazi zangu walikamatwa na kuwekwa ndani kwa siku nne. Yaani kikubwa nipate hata kamera yangu ya kazi maana nafikiria tena mambo ya kukodi kamera, sijui itakuwaje”.

Sijawahi Kuwa na kiben- ten Zaidi ya Bond -Wastara

Msanii wa bongo movies na muziki pia amefunguka na kuwataka watu wasikariri maisha na kuanza kumsema vibaya kwa vitu ambavyo sio vya kweli hasa wale wanaokaa na kumsema kuwa amekuwa na tabia ya kutoak na vijana wenye umri mdogo.

Wastara anasema kuwa hajawahi kuwana mahusiano na vijana wadogo zaidi ya Bond tu na wala hakuna kijana mwingine huku aksiema kuwa katika mahusiano anapenda mtu amzidi yeye miaka miwili au mmoja.

Sijawahi kuwa na mahusiano na kibenten zaidi ya bond amabae alinizidi miaka miwili tu yeye alizaliwa 81 na mimi 83 lakini kutokana na mwili wangu unaniponza naonekana mimi mkubwa lakini sina mazoea ya kutoka na vibenten kama watu wanavyosema.

mimi napenda mtu anizidi na kama atanizidi badi ni mwaka mmoja au miwli kwa bahatai mbaya tu kama inatokea kuwa tunakutana kama ilivyotokea kwa sajuki haikuwa serious lakini ilitengeneza mahusiano mpaka ndoa.

Wastara amekuwa akisemwa kuwa amekuwa akitembea na vijana wadogo na hata hivi karibuni alikanusha tetesi za kutembea a familia ya kina Alikiba.

 

Wastara Awakana Alikiba na Abdul Kiba

Mwanadada Wastara amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake hajawahi kutamani hata siku moja kutaka  au kutamani kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasani wawili Alikiba au Abdul kiba wasanii ambao pia ni ndugu.

Wastara anasema kuwa hana ukaribu na wasanii hawa wawili kwa sababu  kwa sababu tayari kulishawai kutokea mgogoro kati yao wawili huku wakimtykana sana kwa sababu tu waliwahi kumkuta moja ya  watu wa karibu wa familia ya alikiba akiwa nyumbani kwa wastara na kumzushia mengi.

Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na alikiba au abdul kiba , walikuwa marafiki zangu tu na nilikuja kupoteza moyo wa kuwapost kwa sababu tu  ya timu zao kunitukana sana mitandaoni kwa kitu ambacho wala sikuwa nimekifanya.

Wastara anasema kuwa aliacha urafiki wa wasanii hao wa kimitandao siku nyingi sana ingawa wao bado ni watu wa karibu sana na kila siku mara kwa mara wamekuwa wakiwasiliana.

Mashabiki Wampiga Dongo Wastara Mwezi huu wa Ramadhani.

Mwanadada wastara amekumbwa na maneno mazito katika mitandao ya kijamii baada ya kuweka picha yake akiwa anasali na ndipo watu walipoanza kumshambulia kwa maneno na kumwambia kuwa mtu mwenye imani kweli ya dini hawezi kufabya alivyofanya yeye  wakati anasali.

moja ya shabiki wake wanaomfuata aliandika maneno ya kumshushua wastara huku akisema”sasa wewe unasali au unaonyesha watu kuwa wewe ni mcha mungu na kama unaamua kufanya hivyo kama kuna mashindano basi umechemsha,kila kitu unaweka instagram, eeh umechemsha.”

Mashabiki wamekuwa wakikwerwa na tabia za wasanii kuweka picha na kutangaza kila kitu wanachofanya katika mitandao ya kijamii na kuwatolea maneno makali.

Wastara Agundulika Kuwa na Mpasuko Katika Fuvu la Kichwa.

Msanii wa maigizo nchini Wastara Juma ambae amewasiri jana kutoka nchi India alipouwa amekwenda kwa ajili ya matibabu ametoa taarifa kamili ya matibabu na kusema kuwa anashukuru kwa wote waliokuwa wakimsaidia mpaka kufanikiwa kwenda katika matibabu kwa sababu alikuwa hajiwezi peke yake kiuchumi , lakini alipofika na kufanyiwa vipimo alikuja kugundulika kuwa ana ugonjwa mwingine kichwani.

Wastara anasema kuwa baada ya vipimo alivyopatiwa hospitalini hapo alikuja kubainika kuwa katika fuvu lake la kichwa kuna mpasuko na ndio uliokuwa ukimsababisha kupata maumivu  na kukosa usingizi  hapo awali bila yeye kujitambua.

Ni tatizo ambalo lilikuwa linahitajika kuchukuliwa umakini sana kwa sababu muda mwingi  nilikuwa nikilalamika kukosa usingizi kitu ambacho mimi mwanzoni nilikuwa najua labda ni kutokana na mawazo ya muda mrefu lakini kumbe sivyo hivyo, kwenye fuvu la kichwa kuna mpasuko kwa nje na umesababisha kiuvimbe jambo ambalo lilkuwa linanisababishia kukosa usingizi.

Hata hivyo  pamoja na kusemekana kuwa pesa ya matibabu aliyokuwa amepatiwa haikumtosha kwa matibabu, lakini Wastara anasema kuwa amepatiwa dawa kwa ajili ya kutatua tatizo ilo la maumivu lakini pia kama inawezekana anaweza kupatiwa matibabu mengine hapa nchini.

nimefanikiwa kuapatiw adawa pia ninatakiwa kuzitumia kila baada ya miezi mitatu, na kama kuna uwezekano ninaweza kuata matibabu hata hapa nchini itakuwa vizuri zaidi, wenyewe wamenishauri niweze kupatiwa huduma ya afya kubwa kwa sababu kama kuna ulaima wa kurudi kila baada ya miezi mitatu iwe rahisi kuangalia tatizo lakichwa kwa sababu sio jambo la kulifanyia masihara.

Wiki kadhaa zilizopita wastara alikuwa akiomba michango kwa ajili ya kufanikisha safari yake ya kupatiwa matibabu ya mguu na mgongo vilivyokuwa vikimsumbua kwa muda mrefu na kufanikiwa kupata ela iliyompeleka mpaka huko lakini jambo lingine limeibuka baada ya kufanyiwa vipimo na kuktwa ana tatizo lingine tena.

Baada ya Kufanikiwa Matibabu,Wastara Kupokelewa Rasmi March 1.

Chama cha waigizaji wilaya ya Kinondoni inatoa wito kwa wasani wote nchi kujitokeza siku ya March 1 kwa ajili ya kumpokea msanii mwenzao Wastara Juma baada ya kufanikiwa kupata matibabu yake aliyokwenda kutibiwa nchini India.Wastara ambae alienda nchin humo mwanzoni mwa mwezi huu anatarajiwa kufika kesho katika uwanja wa ndege wa taifa.

Wastara ambae alikwenda kwa ajili ya matibabu yake baada ya kuhanagika kwa muda mrefu kupata pesa za matibabu yake kufikia hatua mpaka Mh.Rais kuingilia katika michango yake kwa kumuongezea kiasi flani cha pesa amefanikiwa kupata matibabu hivyo anarejea nyumbani .

Akiandika barua kwa wasanii wote, Afisa Habari chama cha Wasanii Kinondoni anawaomba wasanii kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumuona msanii mwenzao na pia kumpa poel na hongera kwa kufanikisha matibabu.

                   TAARIFA KWA UMMA

              Imetolewa leo;

tarehe 26/2/2018

YAH:MAPOKEZI

Chama cha waigizaji Kinondoni,kinapenda kuwajulisha wasanii na watanzania kwa ujumla kutakuwa na mapokezi ya msanii na mwanatasnia mwenzetu  Bi Wastara Juma  yatakayofanyika siku ya Alhamis tarehe 1 March saa saba kamili mchana uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Chama kinawajulisha  na kuwaomba wasanii na wadau wote  wa tasnia kujitokeza  kwa wingi kumlaki muigizaji  mwenzetu na mpendwa wetu Wastara Juma kwa furaha baada ya kufanikiwa  kwa matibabu yake nchini India  katika hospitali ya Sifael  iliyopo mjini Mumbai.UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO I UDHAIFU.PAMOJA TUNAJENGA TASNIA YETU.

Mungu amtie nguvu na amzidishie afya njema…Amin.

Masoud Kaftany

Afisa Habari, Uenezi, Mahusiano na UMMA.

          Chama cha Uigizaji Tanzania.

Hatimaye Wastara Afanikiwa Kwenda Nje Kwa Matibabu.

Msanii wa bongo movies ambae pia kwa sasa amejiingiza katika sanaa ya nyimbo Wastara Juma amefanikiwa kupata ela yote aliyokuwa anatakiwa kuikusanya kwa ajili ya matibabu yake yanayotakiwa kuanza punde atakapofika nje ya nchi.Wastara ambae amekuwa akilia kila siku katika vyombo vya habari ili awezi kupata fedha kwa ajili ya matibabu amesindikizwa jana uwanja wa ndege kwa ajili ya kwenda nchini India.

Akiongea na waandishi wa habari Wastara amewashukuru sana wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kufanikisha ukusanyaji wa fedha hizo ikiwa ni pamoja na Mh.Raisi ambae alitoa zaidi ya milioni 10 kwa ajili ya kuchangia pale panapohitajika.

Nawashukuru sana wananchi na pia vyombo vya habari, kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiongea na kuonekana kwenye vyombo vya habari na ninaamini kuwa bila wao mimi nisingekuwa wastara.bila wao nisingekuwa hapa uwanja wa ndege ninaenda kutibiwa , ninawashukuru sana kwa moyo mkubwa walonionyesha.-Aliongea Wastara huku akilia kwa uchungu.

Wastara amekuwa akilia kwa uda mrefu kutokana na maumivu ya mgongo anayokuwa anayapata kwa muda mrefu sana kutokana na ajali aliyoipta miakamingi na kusababishwa kukatwa mguu wake mmoja na kuwekewa vifaa kwa ajili ya kumsapoti kutembea.

Wastara aliamua kufunguka katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhgusushida yake hiyo kuwa peke yake hatoweza kufanikiwa kupata ela zinazohitajika kwa matibabu hivyo aliwaomba wananchi wamsaidia kumchangia na kupata ela hizo,ombi amablo lilipokelewa vizuri na wananchi na viongozi mbalimbali na kumsaidia kupata fedha hizo.

Wastara: Sijawahi Kuwadanganya Watanzania Kuhusu Ugonjwa Wangu

MuigIzaji wa bongo movie Wastara Juma amefunguka na kusema kuwa hajawahi kuudanganya umma wa Watanzania kuhusu ugonjwa wake unaomsumbua.

Wiki chache zilizopita Wastara aliulilia umma wa Watanzania umsaidie chochote kitu ili aweze kwenda kusafiri nje ya nchi ili akapate matibabu kwa ajili ya mguu wake unaomsumbua kwa hivi sasa.

Wastara anasumbuliwa sana na mguu huo ambao ulikatwa miaka michache iliyopita baada ya kupata ajali ya gari. Miaka ya hivi karibuni Wastara amekuwa akilalamika kuwa mguu huo unamsumbua sana hadi kupelekea kusababisha maumivu kwa miguu yote.

Baada ya kuenda kwenye vyombo vya habari na kuomba msaada kupelekea Watanzania kumchangia mamilioni na pia hata Raisi Magufuli kumchangia milioni kumi na tano kuna baadhi ya habari zilizodai kuwa Wastara ni tapeli na anatumia mguu wake ili apate pesa ambazo atazitumia kwa ajili ya maslahi yake binafsi na biashara zake.

Wastara amekana tuhuma hizo na kwenye mahojiano na Millard Ayo Wastara amesisitiza kuwa hajawahi hata siku moja kudanganya Watanzania kuhusu mguu wake:

Kwanza mimi siwezi kuwalazimisha watu waamini kile ninachokisema ila siku zote naamini kwamba halafu watu wote wanaoongea na kudai mimi ni muongo na siumwi hawajawahi hata siku moja kuja kuniona wala kushuhudia matatizo yangu hawezi kujua mimi naishije nasikitika sana kusikia taarifa hizo mimi sijawahi hata siku moja kudanganya kuhusu ugonjwa wangu lakini hasa sijawahi kuwadanganya Watanzania kuhusu ugonjwa wangu”.

Mange Kimambi amemtuhumu Wastara kwa kudanganya kuhusu ugonjwa wake mara ya mwisho alipochangiwa kwani alisema anaumwa na kupelekwa India Lakini aliporudi zilipotakiwa risiti hakuwa nazo ndipo ilipojulikana kuwa alienda Muscat kununua vitu vya Dukani kwake tuhuma ambazo Wastara amezikataa.

JPM Asikia Kilio cha Wastara

bBada ya kilio cha muda mrefu na kuwa akituma ujumbe mara kadhaa kwa watu mbalimbali, wastara sasa anaweza kupata tumaini la matibabu yake kutokana na mafanikio aliyoyapata leo ya kupokea kiasi cha shilingu million 15 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Magufuli.

Watu mbalimbali wamekuwa wakimchangia msanii huyu kwa ajili ya kukamilisha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya matibabu yake yaliyotakiwa kanza tangu mwaka uliopoita lakini alishindwa kuhudhuria matibabu hayo kwa sababu ya uhaba wa fedha.

Wastara anaomba hela za matibabu ya mguu wake ambao unampa maumivu makali ya mgongo kwa muda mrefu na alipaswa kurudu india alipokuwa maetiwa mara ya kwanza na kupewa mguu wa bandia.

Wastara alipata ajali ya pikipiki akiwa na marehemu mume wake mwaka 2012, na kukatwa mguu ambapo baadae aliwekewa mguu wa bandia lakini alipaswa kuwa anarudi kliniki nchini humu kila baada ya muda fulani lakini swala hilo lilishindikana mwaka jana kutokana na uahaba wa fedha.

Akipokea fedha hizo kutoka kwa katibu wa Raisi mh,ngusa samike wastara ametoa shukrani zake za dhati kwa Mh.Raisi na mkewe kwa kuona kilio chake na kumfikiria kwa kumpa msaada.

Wastara Amedai Michango Anayopewa na Wananchi Inaibiwa

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajuki amefunguka na kudai kuwa michango aliyokuwa anachangiwa na wasamaria wema inaibiwa.

Wastara aliiomba jamii ya Watanzania wamsaidie kupata pesa ambayo itamsaidia kwenda kutibiwa mguu wake ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu, Wastara pia aliiomba serikali imsaidie kupata matibabu zaidi kwani amedai maumivu makubwa zaidi aliyapata wakati wa kampeni.

Wastara alianza kusumbuliwa na mguu miaka kadhaa iliyopita baada ya kupata ajali ya gari iliyopelekea kukatwa mguu mmoja na hivyo kupelekea ukilema wa mguu mmoja. Lakini baada ya kuwa mlemavu Wastara alidai kuwa mguu ule uliokatwa na ambao mzima yote kwa mpigo ikaanza kumsumbua.

Baada ya kuomba msaada huo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari Wastara alianza kupata michango kutoka kwa watu mbali mbali lakini kwenye mahojiano na Global publishers Wastara amedai kuwa amekuwa akidhulumiwa pesa zake bila kuelewa zinaenda wapi:

Inavyoonekana kuna pesa zangu nyingi Sana zimeibiwa tangu nimetangaza kuomba msaada, kwani kuna kipindi hapo kati pesa ziliingia sana kisha zikakata nilikaa kama siku tisa hazikuingia watu wakawa wananiambia wametuma. Nilipoenda Tigo wakaniambia kuna jam kubwa sana na pesa kule wakiziangalia wanaziona nyingi sana lakini kwenye laini yangu sioni kitu ikabidi niwaambie wanisaidie na waliniambia kwa siku nilikuwa napokea milioni tatu lakini cha ajabu kwangu salio naona laki mbili na nusu tu kwaiyo hapo kuna kitu kabisa Kama sio wajanja wa mjini wameshahack sijui”

Lakini pia Wastara amesema kuwa anasikitishwa na watu Wanaosema yeye kageuza michango ya watu mtaji kwani sio kweli na mguu wake umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu sasa.

 

Nicole Awaomba Wasanii Wamkomboe Wastara.

Msanii wa bongo movie ambae pia alishawahi kutwaa taji la Miss Shinyanga, Nicole Franklyn amewaomba wasanii wote nchi kuwa na moyo wa kujitolea na kumsaidia msanii mwenzao Wastara Juma ambae anaomba msaada kwa ajili ya kwenda nje kwa ajili ya matibabu yake ya mguu.

Msanii huyo wa bongo movie anaomba wasanii waache kinyongo na kumsaidia msanii mwenzao kwa sababu matatizo yanaweza kumkumba mtu yoyote na hakuna anaeijua kesho yake.nicole anasema kuwa hata kama kuna mtu alishawahi kuwa na kinyongo na Wastara haina haja ya kuangalia makosa bali kusameheana na kusaidia katika matatizo.

ninawasihi na kuwaomba wasanii wenzangu tuungane kumchangia wastara, ili aweze kukamilisha ela yake kwa ajili ya matibabu yake.Ninaamini sapoti ya wasanii aliyopewa bado haitoshi kabisa kwa sababu tukiamka wote atafanikiwa.hata kama kuna mtu anakisasi kwa sasa aweke kando tu  kwa sababu matatizo yanaweza kumfika mtu yoyote.

Wastara amekuwa akiomba msaada kwa muda mrefu ili kukamilisha fedha zinazohitajika kwa matibabu ya mguu wake inayohitaji zaidi ya milioni 30.wastara anatakiwa kurudi nchini india ili aweze kufanyiwa matibab hayo ili kuondokana na maumivu ya mgongo yanayompata kwa kumrudia rudia kila muda.

Hata hivyo bado inasemekana kuwa muamko wa wasanii wenzake na Wastara ni mdogo sana kulingana na hali za wasanii na wingi wao katika tasnia hiyo.Inaaminika kuwa kama wasanii wote wataguswa na tatizo hilo itasaidia kufanikisha na kumsaidia wastara.

“Nina Maumivu Makali, Sitafuti Kiki” – Wastara

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma amefunguka tena na kuulilia uma wa Watanzania na kuwasihi wamsaidie kwa sababu yeye ni mgonjwa na yupo kwenye mauivu makali sana na kuwasihi kuwa hatafuti kiki kama watu wengi wanavyodai.

Wiki chache zilizopita Wastara aliomba msaada kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwaomba watanzania wamsaidie kumchangia kiasi cha shilingi milioni 37 za Kitanzania ambazo zitatumika kwa ajili ya matiibabu ya miguu yake na mgongo ambao amedai umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Lakini baada ya kutangaza kuwa anahitaji msaada kumekuwa na muitikio tofauti kabisa kutoka kwa watu huku kila mmoja akiongea lake huku watu wengi wakisema kuwa Wastara amefanya vile ili kutafuta kiki kwa sababu anaweza kujihudumia mwenyewe.

Wastara amefunguka kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Friday Night Night Live cha East Africa TV na kusema kuwa anapata maumivu makali yanayotokana na kuumwa huku watu wakisema anatafuta kiki, anahitaji msaada wa Watanzania:

Yaani hapa mtu anaweza akaniumiza kwa maneno anaweza akaniumiza kwa vitendo Kwa sababu yeye anaamini kwa kichwa chake na mawazo yake kwamba yule mtu anaamini kuwa mimi nimelala kitandani siumwi au nimepotea kwenye sanaa natafuta kiki, kiki ya kujifunua nguo nikapiga picha mguu wangu ambao umekatika kwenye gazeti? Jamani hii sio kiki nipo kwenye maumivu makali na ninahitaji msaada wenu lakini pia siwezi kulazimisha mtu kuamini au hata wasanii wenzangu kuamini kuwa naumwa”.

Wastara alianza kusumbuliwa na matatizo ya mguu miaka michache iliyopita baada ya kupata ajali ya gari ambayo ilimpelekea kukatwa mguu mmoja lakini miaka ya hivi karibuni alianza kusumbuliwa na mguu mwingine ambapo pia amekuwa akipatwa na maumivu ya mgongo.

 

 

Waziri Mwakyembe Amtembelea Wastara na Kutoa Msaada wa Matibabu.

Waziri wa sanaa , habari na michezo Mh.Harison Mwakyembe amekwenda kumtembelea msanii wa bongo movies Wastara Juma nyumbani kwake na kumjulia hali lakini pia ameweza kumsaidia kutoa shilingi mil.1 kwa ajili ya kuchangia fedha za matitabu zinazotakiwa kwa mwanadada huyo kwenda India kwa ajili ya matibabu yake. Mh.Waziri mwakyembe ambae aliambata na  katibu wa bodi ya filamu  walifika mpaka nyumbani kwake kwa ajili ya kumjulia hali msanii huyo.

Hata hivyo Waziri Mwakyembe amewaomba wasanii wote nchini kuwa na moyo wa kujitolea na kumsaidia Wastara Juma ambae anahitaji mili37 kwa ajili ya kurudi katika hospitali aliyokuwa akitibiwa hapo mwanzo kwa ajili ya kubadilishiwa baaadhi ya vifaa mwilini mwake vinavyomfaya aweze kutembea vizuri lakini pia  kuondoa maumivu makali anayokuwa anayapata kwa sasa maeneo ya mgongoni kwa muda mrefu na kusabaisha kuzimia kwa muda kutokana na maumivu hayo.

Uwepo wa Mh,Waziri nyumbani kwa Wastara kuna kuja baada ya msanii huyo kuamua kufunguka katika vyombo vya habari kuhusu hali yake hiyo baada ya kupata ajali ya pikipiki miaka kama  minne iliyopita na kumsababisha kukatwa mguu na ndipo alipowekewa mguu wa bandia ambao unahitaji kuhudhuria kliniki mara kwa mara lakini awamu hii alishindwa kurudi kutokana  na kushindwa kupata fedha za kumrudisha hospitalini huko.

Alipokuwa akiuulizwa kuhusu muamko wa watu na wasanii wenzake katika kuchangia  msaada huo , Wastara alisema anashukuru watanzania  wote ambao wamekuwa na moyo wa kujitolea kwa sababu wa sasa msaada wake unatoka mikononi mwa watu ingawa bado muamko wa wasanii wenzake unakuwa mdogo.

 

Wastara Azidi Kumlilia Marehemu Sajuki

Muigizaji wa bongo movie Wastara Juma au maarufu Kama Wastara Sajuki amezidi kumuomboleza na kumlilia aliyekuwa mume wake marehemu Sajuki aliyeaga dunia miaka michache iliyopita.

Sajuki Juma alikuwa maarufu Kama muigizaji wa Bongo movie aliaga dunia miaka michache iliyopita alipokuwa njiani kwenye ndege kwaajili ya kusafirishwa kwenda nchini India kwa matibabu zaidi kwa maradhi ya Kansa yaliyo kuwa yanamtatiza kwa wakati ule.

Sajuki na Wastara mbali ya kuwa maarufu kwa sababu wote wawili walikuwa waigizaji kutoka katika tasnia ya Bongo movie, lakini walipata umaarufu zaidi baada ya kupata ajali ya gari na Wastara kukatwa mguu na kuwa kilema kitendo ambacho wengi walifikiri kingepelekea Sajuki kumkimbia Wastara lakini ilikuwa tofauti kwani pamoja na ulemavu wake Sajuki alimuoa Wastara.

Tangu kifo chake kitokee Wastara ameshafunga ndoa mbili na zote zimeishia kwenye talaka kitendo ambacho mara kwa Mara kimemfanya amkumbuke marehemu muewe Sajuki ambaye walitengana na kifo tu.

Siku chache zilizopita Wastara amemkumbuka tena marehemu Sajuki ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram alimuandikia ujumbe huu kwa ajili ya kuuanza mwaka 2018;

Siku inaishaje leo Farhen karidhika kusherehekea sherehe ya baba yake kwa kubadilisha nguo na kumposti amefurahi mwenyewe, bilakujua leo sio siku ya sherehe ya baba yake Bali ni kumbukumbu ya kutoweka kwake duniani Mungu ni wetu sote…ewe unichukiae uniombee kwa Mungu nisimame tena uzipate baraka zake usifurahi kuanguka .

 

 

Wastara Afunguka Siri Ya Kutokukata Tamaa Baada Ya Kupata Matatizo

Mwanadada msanii  mkongwe Tanzania  Wastara Sajuki ,ambae  alipitia magumu mpaka hapa alipofikia amefunguka na kuelezea maisha ya ke na magumu aliyoyapitia tangu alipopata ajali yake yeye na mumewe na baadae mume wake kuumwa na kulazwa kwa muda mrefu sana na hatimaye kuaga Dunia.

Wwanadada huyo ambae ni muigizaji, lakini pia ni mwimbaji na mjasiriamali lakini kwa sasa pia ameonyesha uwezo wake mkubwa wa kuingia katka siasa na kufanya vizuri . Wastara ameamua kuongea na kuwashauri wanawake wengine wasikate tamaa baada ya kupata matatizo hayo kwa sababu yeye pamoja na kupata matatizo hayo hakuwahi kukata tamaa bali iliendelea kumpa chachu ya maendeleo.

Wastara anaeleza kuwa kipindi anaanza sanaa tayari alikuwa ni mfanya bashara lakini hakukata tamaa na kuacha biashara yake kwa sababu alijua vitu vyote viwili akiweza kuvimudu basi ataweza kufanya vizuri.Akiendelea kuongezea kuhusu mahangaiko yake Wastara anasema

kweli tangu nimepata ajali  matatizo mengi sana yalijitokeza,unajua siku napata ajali ndio ilikuwa siku ambayo nilitakiwa nikanunue gauni langu la harusi.kwaio mipango mingi ilivurugika na hata nilipokatwa mguu nilifunga ndoa baadae mume wangu akanza kuuumwa na nilingaika nae sana lakini yote kheri namshukuru Mungu.

Kwangu mimi sijioni kama mlemavu kabisa, na ndio maana unaona ninaigiza na na kushiriki katika  mambo mengine  mengi ya mikakati ya kimaisha  ikiwepo siasa na jamii , kwaio nawasihi waache kulitafuta tatizo lao  na badala yake watafute  namana na suluhu ya kukabiliana na matatizo hayo.

Hata hivyo Wastara ambae hivi karibuni ametoa wimbo unaowahamasisha wanawake amesema kuwa ameamua kuongea na wanawake wenzie  ili kujikita katika kupambana na ndoto zao , lakini pia nyimbo hiyo sio kwa wanawake tu bali hata kwa wanaume ambao wanakata tamaa mapema waaachena huo wimbo unawahusu.

Wastara anaongezea na kusema kuwa wanawake wengi wanakuwa na visingizo kuwa wanashindwa kuanzisha biashara kwa kisingizio cha kuwa na mitaji , lakini anachowaambia ni kuwa kitu kikubwa nai kuwa na wazo zuri la biashara kwanza.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.