Pretty Kind Adai Ali Kiba Sio Staa

Video vixen na Msanii wa Bongo fleva Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind ameibuka na kudai Msanii maarufu wa Bongo fleva Ali Kiba sio supa staa kama watu wengi wanavyodhani.

Ali Kiba ni moja kati ya wasanii wa Bongo fleva ambaye amekuwa kwenye chati na amekuwa akiwekwa Kwenye listi ya wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa.

Lakini Pretty Kind ameibuka na kudai kuwa Ali Kiba hana hadhi au status ya kuwa supa staa kwa kuwa hajafabya baadhi ya mambo ambayo yanaweza kumuweka kuwa Staa.

Pretty Kind amefunguka na kusema hawezi kumuweka Ali Kiba Kwenye kundi la mastaa kwa sababu muziki wake haujulikani nchi za nje zaidi ya hapa nyumbani Tanzania:

Mimi ninachoongea ni ukweli na wala sina timu ya aina yoyote ila  Ali Kiba Isupa staa kwa sababu bado hajaitangaza vizuri nchi yetu muziki wake unaojulikana hapa kwetu tu simchukii ila nasema ukweli”.

 

“Ali Kiba ni Msanii Mkubwa na Amenifundisha Mambo Mengi Kwenye Muziki”-Barakah The Prince

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amempa heshima msanii mkongwe wa Bongo fleva Ali Kiba na kudai ni msanii mwenye experience kubwa Kwenye Bongo fleva.

Barakah alikuwa chini ya Label ya Rockstar 4000 ambayo inaendeshwa na Ali Kiba lakini baada ya miaka michache ndani ya Label hiyo BAraka alitangaza kujitoa na kuanza kufanya Muziki wake mwenyewe.

Baada ya kutoka Rockstar Baraka aliwatuhumu kwa kufanya njema mbali mbali za kumrudisha nyuma kimuziki ikiwemo mapema mwaka huu aliwatuhumu kwa kufuta nyimbo zake Youtube.

Lakini sasa inaelekea Baraka amerudi katika nafasi nzuri na Ali Kiba kwani Kwenye Interview yake na kipindi cha refresh cha Wasafi Tv, Baraka amemtaja Ali Kiba kama mtu aliyemfundisha mambo mengi kwenye sanaa kutokana na experience yake;

Ali Kiba ni mkubwa na ana experience Kwenye Industry more than me kwaiyo muda ambao nilikuwa naye nilijifunza vitu vingi Kimuziki na kusema kweli nilikuwa niijua thamani yangu kama msanii na nilijua nini natakiwa kufanya ili kufanikiwa maana yeye ameshakula matunda ya Muziki wetu”.

Barakah amesema kwa sasa hana mpango wa kusainiwa chini ya label yoyote hapa Tanzania labda hapo baadae.

Ali Kiba- Mama Yangu Amenisapoti Kimuziki Kuliko Baba

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘’Mvumo wa Radi’ Ali Kiba amefunguka na kumtaja mama yake mzazi kama mtu ambaye amekuwa akimsapoti kimuziki Kuliko Baba yake.

Ali Kiba amekuwa akionekana akiwa na ukaribu zaidi na mama yake Kuliko na Baba yake hata Kwenye mitandao ya kijamii amekuwa akionekana akiwa karibu na Mama yake.

Ali Kiba ameweka wazi kuwa Mama yake ndiye mtu aliyemsapoti katika mziki wake tangu anaanza Mpaka sasa tofauti na ilivyokuwa kwa Baba yake Mzee Salehe.

Ali Kiba alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo  kimoja cha habari ambapo amefunguka na kusema:

Katika muziki wangu mama yangu ameni support kwa asilimia mia moja tangu naanza Muziki mpaka leo hii”.

Katika jamii zetu za Afrika wazazi wengi wamekuwa wakiamini kuwa muziki au sanaa yoyote ile ni uhuni lakini baadhi ya wasanii kama Ali Kiba wamekuwa wakifuta dhana kutokana na kuwa kioo cha jamii bora na mfano wa kuigwa.

Mke wa Alikiba Adaiwa Kuwa Mjamzito Baada Ya Picha Hii

Mke wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba, Amina Khaleef ameingia Kwenye headlines baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa huenda ni mjamzito baada ya picha yake ya hivi karibuni.

Ali Kiba na mke wake kutoka Mombasa Kenya Amina walifunga ndoa Miezi miwili iliyopita na mara moja Kiba taarifa zilisambaa kuwa Ndoa hiyo imeharakishwa kwa sababu Amina ana kibendi.

Tetesi hizo zimezidi kupambana moto mara baada ya picha mpya ambayo ilipostiwa na Ali Kiba mwenyewe alipokuwa anasheherekea birthday ya Meneja wake Seven Mosha.

Kwenye picha hiyo Alikiba na wanafamilia wote wa RockStars 4000 walionekana katika picha ya pamoja inayodaiwa kupigwa nchini Afrika Kusini.

Usemi wa picha moja ni sawa na maneno 1000 ulidhihirika kwani picha hiyo ilizua gumzo. Hivyo hivyo kwenye picha aliyoipost Alikiba akiwa mke wake, Bi. Amina, meneja wake Seven Mosha pamoja na marafiki zake wengine.

Mpaka sasa Ali Kiba na Mke wake hawajathibitisha taarifa za ujauzito huo na inawezekana asiseme kitu kama inabyojulikana kama Ali kiba huwa ni msiri sana Kwenye mambo yake binafsi hawezi kuyaanika Kwenye mitandao ya kijamii.

Baada Ya Kolabo na Sauti Sol, Tegemea Kolabo Ya Alikiba na Kundi Jingine Kutoka Kenya

Staa wa muziki wa Bongo fleva aliyeendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Mvumo wa radi’ Ali Kiba amedaiwa kuwa yupo njiani kuachia Kolabo yake mpya na kundi la H-art kutoka Kenya.

Bongo 5 wanaripoti kuwa Alikiba ameingia tena studio wikiendi hii nchini Kenya akiwa na kundi la H-Art The Band kuandaa mdundo mpya.

Ali Kiba akiwa na The H-Art Band

Inadaiwa kuwa ngoma hiyo itakuwa ni ya Alikiba akiwa amewashirikisha H-Art The Band na tayari wiki hii wameshamaliza ku-shoot video ya wimbo huo.

Alikiba toka wiki iliyopita yupo nchini Kenya kwa kazi hiyo maalumu ya kuandaa ngoma hiyo na imeandaliwa na producer maarufu nchini Kenya, Cedo.

Kama utakumbuka mara ya mwisho Ali Kiba ametoa wimbo na kundi la muziki kutoka Kenya Sauti Sol wimbo uliotwa ‘Unconditionally Bae’ ulikuwa bonge la hit hivyo tutegemee mambo mazuri kutoka kwa King Kiba.

Ali Kiba Amtaja Ommy Dimpoz Kama Sababu Ya ‘Mo Faya’ Kutoingia Sokoni

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguk na kuweka wazi sababu iliyosababisha kuchelewa kuingia sokoni kwa kinywaji chake cha Mo Faya.

Ali Kiba alizindua rasmi kinywaji chake Miezi Michache iliuopita kwenye hatusi yake lakini tangu hapo kinywaji hicho hakijaonekana Tena kikiwa kinauzwa sokoni.

Kwenye mahojiano na Shilawadu ya Clouds Tv, Ali Kiba ameweka wazi kuwa sababu pekee iliyofanya mpaka kinywaji hivho kuchelewa kuongia sokoni ni maradhi ya msanii Ommy Dimpoz ambaye amemtaja kama balozi wa kinywaji hicho.

Mo Faya zilitakiwa ziingia mtaani toka Idd lakini tumepata mtihani kidogo, mtihani tulioupata ni kwamba balozi wetu (Ommy Dimpoz) anaumwa sana, nasikitika kusema hivyo kwa sababu hali yake si nzuri lakini kila siku kunakuwa na uhafadhali, ndio ninachosubiriwa.

Hali yake ikiwa sawa wakati tunazitambulisha anatakiwa awepo. Tunahitaji hali yake iwe sawa, tunatamani awepo”.

Ommy Dimpoz yupo nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya kufanyiwa matibabu baada ya kufanyiwa operesheni mwezi uliopita.

Lakini pia Ali Kiba amekana tetesi zilizokuwa zimesambaa kuwa vinywaji hivyo vimepigwa stop na Serikali kutokana na kukosa ubora.

Gigy Money-Nilitembea na Ali Kiba Pamoja na Abdu Kiba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ametoa kali baada ya kukiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Staa wa Bongo fleva Ali Kiba pamoja na mdogo wake Abdu Kiba.

Gigy Money ameweka wazi kuwa ametembea na ndugu hao wawili lakini sio kwa wakati mmoja bali ilikuwa ni nyakati tofauti maana alikutana nao tofauti tofauti.

Gigy Money alifunguka hayo Kwenye Interview yake na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv ambapo alikiri kuwa wakati anaanza Mahusiano nao hakujua kuwa walikuwa ni ndugu:

 Kweli nilitembea nao mbona kawaida kwani nilikutana nao muda mmoja? Kwanza nilivyotembea nao sikuwa najua kama ndugu.

Halafu isitoshe mimi sina makosa mwenye makosa ni Ali Kiba kwani alijua natembea na mdogo bado akanitaka”.

Gigy Money ameanika kuwa Mahusiano Yake na Ali Kiba na Abdu Kiba yalikuwa siku nyingi kabla hajaanza kuwa video vixen ambapo enzi hizo alikuwa anakutana na wasanii club ambapo alikuwa anapenda kutembea na wasanii.

Nuh Mziwanda- Sina Bifu na Diamond Ila Sina Ukaribu Naye Pia

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amefunguka na kudai jana bifu na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Nuh ambaye ameshafanya ngoma na Ali Kiba aliomshirikisha katika wimbo wake wa Jike Shupa amefunguka na kusema hata kama hajawahi kufanya ngoma na Diamond haimaanishi wana bifu.

Mziwanda alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online pale alipotakiwa kujibu tetesi kama ana tatizo lolote na Diamond:

Mimi sina bifu na Msanii yoyote na wala sina bifu na Diamond wala sina ugomvi naye unajua yule mchizi sana na tulishawahi kufanya vitu vingi sana lakini muda nakumbuka Times hafanyi shoo zake tulikutana Dodoma tukafanya shoo yake kwaiyo ni mtu ambaye yuko Poa lakini hatuna mawasiliano wala ukaribu wowote.

Lakini pia Mziwanda ameweka wazi kuwa kama ikitokea nafasi ya kufanya kazi na Diamond basi atafuata taratibu za kwenda Kwenye uongozi wake na kuomba Kolabo.

Kutokana na Bifu lililopo kati ya Diamond na Ali Kiba, wasanii wanaofanya kazi na wasanii hao hujikuta wakichagua upande wa kuwa na hivyo Mziwanda baada ya kufanya Kolabo na Ali Kiba alidaiwa kuwa na bifu na Diamond.

 

Kolabo Yangu na Ali Kiba Imenipa Mafanikio Makubwa-Nuh Mziwanda

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amefunguka na kudai wimbo wake wa ‘Jike shupa’ aliomshirikisha Ali Kiba ndio wimbo wake uliompa mafanikio makubwa.

Mwezi uliopita Nuh Mziwanda alianika Rasmi mjengo wake mpya ambao alikuwa anajenga na sasa anaweka wazi kuwa pesa za mjengo huo zinatoka katika ile Kolabo na Ali Kiba ambayo ilimpa Tour nchi nzima.

Nyumba ni yangu na katika ujenzi nilikuwa namshirikisha sana mama yangu, yeye ndio aliyekuwa anashughulika na mafundi. Mimi sikuwa nafuatilia, kipindi kile ndio nilikuwa nimeachia Jike Shupa, nilifanya tour Tanzania nzima, chaka to chaka wilaya kwa wilaya.

Nilikuwa nikipata pesa yangu kidogo kidogo namtumia mama anajenga, kwa hiyo mimi narudi huku nakuta nyumba imefika sehemu nzuri kwa sababu nakumbuka nilikaa miezi mitatu”.

Kolabo hiyo ndio moja ya nyimbo pekee ya Mziwanda aliyofanya vizuri kwani ina viewers milioni mbili Kwenye mtandao wa Youtube.

Mr. Blue Awainulia Mikono Ali Kiba na Diamond

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khery Sameer  au maarufu kama Mr. Blue amewainulia mikono mastaa wa Bongo fleva Diamond na Ali Kiba.

Mr. Blue amefunguka na kuweka wazi kuwa anaona kabisa kuna vitu vya Ziada vinavyowafanya Ali Kiba na Diamond wazidi kupata mafanikio katika tasnia hii.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mr Blue amesema wanamuziki wengi chipukizi hutamani kuwa kama wawili hao bila kufahamu mbali na kufanya muziki wanajituma, wana nidhamu na wana malengo ya kufika

Unajua wengi hutamani kuwa kama fulani kwenye muziki hasa watu wanaofanya vizuri zaidi kwa sasa kama Diamond na Kiba, lakini bila kufahamu kwamba ili ufanikiwe ni lazima uwe na vitu vya ziada mbali na kuimba kawaida.

Kwa ushauri wangu, wanamuziki chipukizi waangalie ni vitu gani vya ziada wanavyo wanamuziki wanaotamani kuwa kama wao wavifuate na wataweza kufika kule wanako kuhitaji”.

Ni wiki chache tu zilizopita Mr. Blue alikana taarifa za  kuwa ana bifu na Diamond baada ya tetesi za muda mrefu zilizodai hivyo.

Ali Kiba Ampeleka Mzazi Mwenzake Mahakamani Akidai Kudhalilishwa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba anadaiwa kumburuza mzazi mwenzake mahakamani na kumtuhumu kwa kumdhalilisha.

Mwezi uliopita habari zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Ali Kiba ameburuzwa mahakamani na mzazi mwenzake aliyetambulika kwa jina la Devotha.

Ali Kiba na mwanamke huyo wamezaa mtoto mmoja lakini madai ya mwanadada huyo ni kuwa Kiba alimtelekeza mtoto huyo na kukataa kumpa matunzo baada ya yeye kumchukua kutoka kwa mama yake Ali Kiba alipokuwa anaishi.

Baada ya kuzozana kwa muda mrefu Kwenye mitandao ya kijamii mwanamke huyo alimfungulia kesi Ali Kiba Kwenye mahakama ya watoto Kisutu na mara moja Kiba alitakiwa kufanya DNA.

Lakini sasa inasemekana kuwa Ali Kiba amemfungulia kesi mzazi mwenzake kwenye kituo cha polisi cha Osterbay akidai kuwa amedhalilishwa na mwanamke huyo.

Kiba amesema Kitendo Cha mzazi mwenzake kuongea na vyombo vya habari ni Kitendo Cha kumdhalilisha yeye.

Mzazi mwenzake na Kiba alifanya Interview na Millard Ayo wiki chache zilizopita ambapo alifunguka Mazito Kuhusu Mahusiano Yake na Ali Kiba mpaka kufikia kuzaa naye na sasa kumtelekeza mtoto.

Ali Kiba ameonekana kukasirishwa na mambo yake binafsi ya kifamilia kuanikwa Kwenye mitandao ya kijamii ukitegemea hasa kwa sababu yeye ni mtu mkimya asiyependa kuanika mambo yake Mtandaoni.

Ali Kiba Ampeleka Mzazi Mwenzake Mahakamani Akidai Kudhalilishwa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba anadaiwa kumburuza mzazi mwenzake mahakamani na kumtuhumu kwa kumdhalilisha.

Mwezi uliopita habari zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Ali Kiba ameburuzwa mahakamani na mzazi mwenzake aliyetambulika kwa jina la Devotha.

Ali Kiba na mwanamke huyo wamezaa mtoto mmoja lakini madai ya mwanadada huyo ni kuwa Kiba alimtelekeza mtoto huyo na kukataa kumpa matunzo baada ya yeye kumchukua kutoka kwa mama yake Ali Kiba alipokuwa anaishi.

Baada ya kuzozana kwa muda mrefu Kwenye mitandao ya kijamii mwanamke huyo alimfungulia kesi Ali Kiba Kwenye mahakama ya watoto Kisutu na mara moja Kiba alitakiwa kufanya DNA.

Lakini sasa inasemekana kuwa Ali Kiba amemfungulia kesi mzazi mwenzake kwenye kituo cha polisi cha Osterbay akidai kuwa amedhalilishwa na mwanamke huyo.

Kiba amesema Kitendo Cha mzazi mwenzake kuongea na vyombo vya habari ni Kitendo Cha kumdhalilisha yeye.

Mzazi mwenzake na Kiba alifanya Interview na Millard Ayo wiki chache zilizopita ambapo alifunguka Mazito Kuhusu Mahusiano Yake na Ali Kiba mpaka kufikia kuzaa naye na sasa kumtelekeza mtoto.

Ali Kiba ameonekana kukasirishwa na mambo yake binafsi ya kifamilia kuanikwa Kwenye mitandao ya kijamii ukitegemea hasa kwa sababu yeye ni mtu mkimya asiyependa kuanika mambo yake Mtandaoni.

Ali Kiba- Dini Yangu Hainiruhusu Kumposti Marehemu Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Staa wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Mvumo wa Radi’ Ali Kiba amefunguka na kusema hawezi kuposti marehemu Kwenye mitandao ya kijamii kwani dini yake hairuhusu.

Siku ya jana msanii wa Bongo fleva Sam wa Ukweli aliyejuliakana zaidi kwa nyimbo yake ‘Sina raha’ na ‘Huku kwetu’ alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.

Wasanii mbali mbali walijitokeza kuonyesha masikitiko yao ikiwemo kumposti katika mitandao ya kijamii lakini Ali Kiba hakufanya jambo lili pekee a watu kumjia juu msanii huyo.

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari, Ali Kiba anafunguka na kusema sababu pekee iliyompelekea asimposti Sam wa Ukweli ni kwa sababu za kidini ambazo hazimruhusu kumuanika marehemu:

Nataka niliweke hili sawa kwa jamii mimi dini yangu hairuhusu kumposti marehemu katika mitandao ya kijamii ndio maana watu huwa hawaoni mimi nikiposti lakini huwa marina salamu za rambi rambi kwa familia na si kwa kujionyesha kwa sababu sio lazima na haturuhusiwi  kufanya vitu kama hivyo lakini leo hii ningependa kusema kweli ndugu na jamaa na mashabiki wa Sam wa Ukweli, Nimeguswa na msiba ambao umetokea jana na Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mahala pema peponi Inshallah”.

 

ShiiKANE- Tunatamani Kufanya Kazi na Diamond Lakini Ali Kiba Kwanza

Mastaa wa muziki kutoka Nigeria ShiiKANE wamefunguka na kuweka wazi kuwa wanatamani sana kufanya kazi na Diamond lakini mpaka wakishafanya kazi na Ali Kiba Kwanza.

Wasanii hao watatu wanaounda kundi hilo la ShiiKANE wapo nchini Tanzania kutoka nchini Nigeria kwa ajili ya kufanya kazi na baadhi ya wasanii wa nchini hapa Lakini pia kwa ajili ya kutangaza muziki wao.

Wasanii hao wamekiri kuwa wanatamani kufanya kazi na wasanii wa Bongo Diamond na Ali Kiba lakini mmoja wa wadada wa kundi hilo Shay amekiri kuwa wanataka kufanya kazi na Ali Kiba kwanza.

Wasanii hao walifunguka hayo Kwenye mahojiano waliofanya na Bongo 5:

Tunatamani kufanya kazi na mtu kama Diamond ila kwanza Alikiba kisha Diamond ila tayari tumesha fanya kazi na Chin Bees ambaye ametufundisha Kiswahili kidogo katika kazi tuliyofanya“.

Lakini pia mbali na Diamond na Ali Kiba ShiiKANE wamesema Msanii wanaye ramani kufanya naye kazi ni Vanessa Mdee kwani wamekiri wanavutiwa na kazi zake sauti  yake na hata urembo wake.

Mchungaji Lusekelo Awashauri Diamond na Ali Kiba Waache Uzinzi

Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC) mchungaji maarufu anayejulikana kama Mzee wa Upako amewataka wasanii Diamond Platnumz na Ali Kiba waache uzinzi.

Siku chache zilizopita Mchungaji Lusekelo alitengeneza headlines baada ya kusema kuwa anamkubali sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu na akamkosoa Ali Kiba kuwa ni mjeuri.

Kwenye Interview yake na Millard Ayo Tv, Mchungaji Lusekelo amesema hawezi akakaa na kujibizana na Diamond wala Ali Kiba kwa sababu wote ni watoto sana kwake anaweza kuwazaa.

Lakini pia Mchungaji Lusekelo amewapa ushauri wasanii hao na kuwataka  waache uzinzi kwani maisha ni mafupi:

Muache uzinzi haya maisha ni mafupi sio leo una mke huyu kesho una mke yule mtakufa!.

Mimi ni Mzee ingawa sio Mzee sana lakini nimeishi maisha marefy lakini tumeona wanamuziki wengi walikuwa lile juu wanakuja wanaporomoka na mwenye akili hujifunza Kupitia makosa ya watu wengine lakini mjinga hujifunza kwa makosa yake mwenyewe”.

Lakini pia Mchungaji Lusekelo aliwataja wasanii wengine ambao anawakubali mbali na Diamond ambao ni Ben Pol, Darassa, Mrisho Mpoto na Malaika.

Ali KIba Atangaza Ujio Wa Albamu Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba ametangaza rasmi ujio wa Albamu yake mpya mapema mwaka huu.

Kwa wiki kadhaa sasa Ali Kiba amekuwa akifanya vizuri na ngoma yake ya ‘Mvumo wa radi’ ingawa hajatoa Albamu  yoyote kwa miaka ya hivi karibuni.

Kwenye Interview yake na ITV, Ali Kiba ametangaza ujio wa Albamu hiyo mapema mwaka huu na kuwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula.

Lakini pia Kiba ameweka wazi kuwa maandalizi ya Albamu hiyo yameshaanza kufanyika tayari kabisa kwa ajili ya kuwafikia mashabiki.

Albamu naweza nikaachia mwaka huu nipo katika kumalizia japokuwa tayari nipo na nyimbo ila nataka kila kitu kitoke kikiwa perfect”.

Lakini pia Ali Kiba Ameongeza kuwa albamu hiyo itauzwa kwa njia ya online na kawaida, yaani hard copy.

Mwaka huu wasanii wengi wamejitosa na kuanza kuuza Tena Albamu baada ya kuacha kufanya hivyo kwa miaka mingi ambapo wasanii kama Diamond, Vanessa Mdee, Chin bees wameshatoa Albamu zao ambazo zipo sokoni.