Mch. Lusekelo-Nampenda Diamond ni Mnyenyekevu, Simpendi Alikiba ni Jeuri

Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC) mchungaji maarufu kama Mzee wa Upako ameetaja Diamond kama msanii anayemkubali.

Mch. Lusekelo amefunguka kwenye kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm ambapo ameweka wazi kuwa anampenda Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu lakini hampendi Ali Kiba kwa sababu ni mjeuri.

Mimi nampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, Simpendi Alikiba kwa sababu ana kiburi, nadhani kwa sababu amekaa Kariakoo”.

Lakini pia Mchungaji huyo hakuishia hapo aliongeza kwa kumsifia Diamond kuwa unyenyekevu wake ndio unamfikisha mbali:

Ukipigia simu Diamond anapokea kwa unyenyekevu ila Alikiba anapokea kwa maringo. Ndio maana Diamond amefika mbali.”

Wasanii hawa wawili wakali wa Bongo fleva wamekuwa wakishindanishwa kwa muda mrefu sana hali iliyosababisha wawili hao kuwa na bifu fulani hivi.

 

Ali Kiba Atangaza Vita Na Mbwana Samatta Uwanja Wa Taifa

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba anayeendelea kufanya vyema na ngoma yake ya ‘Mbumo wa Radi, atapimana nguvu na mchezo soka la kulipwa Mbwana Samatta uwanja wa Taifa.

Ali Kiba amajulikana kwa uwezo wa kucheza mpira uwanjani na alikwisha weka wazi kuwa ana mapenzi mazito kwa mpira wa miguu na hata kusema asingekuwa msanii basi siku nyingii angekuwa mcheza mpira.

Kwa mara ya kwanza uwezo wa kusakata soka ulionekana Kwenye mechi iliyohusisha wasanii wa Bongo fleva na wasanii wa Bongo movie miaka ya nyuma kidogo.

Habari njema kwa mashabiki zake ni kuwa utamshuhudia Ali Kiba Live kunako dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tarehe 9 juni mwaka huu akiwa na Mshambuliaji wa timu ya taifa na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta.

Ali Kiba ametangaza Habari hiyo njema kwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika ujumbe huu:

Tukutane Taifa naomba unichagulie kikosi bora unacho kikubali kutoka team tofauti katika ligi ya TANZANIA bara.

Wawili hao watakutana kwenye mechi maalumu ya ubalozi wa kujitolea ili kuchangia elimu, hata hivyo orodha ya majina mengine ya wasanii yataendelea kutajwa kadri ya siku zinavyokwenda.

Mbwana Samatta ameandika ujumbe huu kutjibitisha kuwepo katika pambano hilo:

Nimepewa jukumu la kuandaa jeshi la maangamizi mchezaji gani ungependa kumuona siku iyo awe wa sasa au wa zamani?

Billnas Afunguka Kuhusu Ndoa Yake na Jinsi Ali Kiba Alivyohusika

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bill Nas amefunguka na kuweka wazi kwa nini alitangaza ndoa yake mapema mwaka huu.

Bill Nas aliungana na wasanii wengi ambao wametangaza wanatarajia kuuaga ukapera hivi karibuni na kufunga ndoa.

Kwenye Interview yake na Wasafi Tv, Bill Nass amesema kuwa anaamua kuoa kutokana anapenda familia, pia wasanii wanatakiwa kuwa kama watu wengine kwani kufanya hivyo haimaanishi msanii atashuka kimuziki.

Niliposti kuhusu kuoa na pia kuhusu nani nitamuoa nitaamua mimi sio mtu mwingine. Mtu kama Alikiba anaweza kuoa na game yake bado ipo strong kuna kila haja, na pia inatambulisha kwamba ndoa ni jambo muhimu lakini pia sisi ni wasanii na ni watu kama wengine”.

Lakini pia Bill Nas ameweka wazi kuwa siku aliyohudhuria Harusi ya msanii mwenzake Ali Kiba alizidi kupata morali ya kuoa baada ya kuona jinsi mtoto wake alivyokuwa na furaha:

Mtoto wake alikuwa happy sana kwenye ile harusi kwa hiyo ile ilini-impress zaidi”.

 

Ali Kiba Amedai Kuwa Hata Kama Ni Staa Hawezi Kuishi Maisha Ya Kujionyesha

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kudai kuwa pamoja na kuwa na umaarufu mkubwa lakini hataweza kuishi maisha ya kujionyesha mbele za watu.

Lakini pia Ali Kiba ameonekana kuwatupia Dongo wasanii wenzake wanaoishi maisha ya kujionyesha (show off) na kudai kuwa kuna maisha ya kuishi kama staa Lakini pia kuna maisha ya kuigiza kuwa staa.

Ali Kiba amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Dj  Show ya Radio One ambapo amedai maisha anayoishi ndio yana manufaa sana kwa mashabiki zake ambao walimuwezesha kufika hapo.

Kuna maisha ya ustaa na kuna maisha ya kawaida na kuna maisha ya kuigiza kuwa staa. Mimi sijachagua in nature nipo hivyo, Watanzania walinipokea katika hali ambayo kiukweli haisemeki sasa hii leo nije nibadilike, so nisingependa kumshawishi shabiki yangu kwa namna yoyote ile kuwa nimebadilika kwa sasa hivi.

Kwa hiyo ule wivu wa kumfanya mtu anze kunichukia kwamba Ali amekuwa hivi na hivi, hapana!. Mimi ni staa, mimi ni supa staa nitafanya, ninaishi maisha ambayo nimechagua lakini bado nitaendea ku-humble kwa watu“.

Ali Kiba ameendelea na media tour kwa ajili ya kutangaza Single yake mpya ya ‘Mvumo wa radi’ ambayo imeendelea kushikilia namba moja Kwenye mtandao wa Youtube.

Alikiba Akataa Kufanya Kazi na Abby Skillz

Msanii wa bongo fleva anavuma kwa sasa na wimbo wa mvumo wa radi amefunguka na kusema kuwa kamwe hawezi na hataki kufanya kazi na msanii Abby Skillz au kumsaini katika lebel yake ya King’s music kwa sababu yeye ndie alimsaida mpka kutokea katika muziki hivyo kumuajiri katika lebel hiyo ni kama kumshushia heshima msanii huyo.

Akiongea na Planet Bongo msanii Alikiba alisema kuwa ni kweli kuna kipindi ilisiskiaka kuwa Abby Skillz alikuwa amesainiwa katika lebel hiyo lakini baadae waliona kuwa msanii huyo ikasikika kuwa msaii huyo hayupo tena katika lebl hiyo.

kwakweli niliweza kumsaini abby skillz kwenye lebl yangu lakini niliona kama vile simtendei haki kabisa,kwa sababu yeye ndie alieniingiza katika game ya muziki na kuona mwanga katika muziki kwaio nikaona ni bora abby ajitegemee yeye kama yeye tu.

kwa sababu ukiwa katika kings music kuna baadhi ya asilimia zitakuwa zinatoka , kwaio mimi niliona siwezi kumfanyia hivyo yeye ni bora afanye kazi mwenywe lakini tutakuwa tunafanya kazi pamoja lakini sio chini ya lebel.

 

 

Ex wa Ali Kiba Sabby Angel Amtolea Povu Zito Staa Huyo

Muigizaji wa Bongo movie Sabby Angel ameibuka na kumtolea povu zito Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba baada ya kauli tata aliyoitoa kuhusu warembo wa Bongo.

Sabby Angel alishawahi kukiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ali Kiba siku za nyuma kidogo ameshindwa kuvumilia na kumpa ukweli Staa Huyo aliyeoa hivi karibuni.

Hivi karibuni Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Ali Kiba alifunguka kuwa sababu ya yeye kuwaacha warembo wote wa Bongo na kwenda kuoa Kenya ni kwa sababu wasichana wengi wakibongo wanaendekeza vigodoro na wengi sio wasomi.

Sabby Angel ameonekana kukasirishwa na kauli hiyo kutoka kwa mpenzi wake wa zamani na ameandika ujumbe huu:

Ni jambo la Kheri kwa Ali K kuoa lakini sijapenda comment yake eti kusema eti Tanzania hakuna wanawake wasomi wa kuoa.

Bonafsi kama mtu umeamua kuoa we oa tu kwa manufaa yako lakini sio kukashifu wanawake wote. Kwani hapo wakati anatoka na hao wanawake wa Kitanzania hauona hayo mapungufu? Kwani watu wanaoa vyeti? Wanaoa kukimu mahitaji yao binafsi na kuzaana?.

Hiyo ni kumaanisha hata wazazi wetu wa kike na hata mama yake ni wale wale it is very immature”.

Ali Kiba alifunga ndoa na binti kutoka Mombasa Kenya wiki chache zilizopita.

Ali Kiba Awatupia Dongo Wasanii Wanaonunua ‘Views’ Youtube

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Mvumo wa radi’ amedai kuwa kuna wasanii wenzake ambao wana tabia ya kununua viewers (watazamaji) Youtube.

Ali Kiba alipatwa na sakata hilo la views huko Youtube baada ya video yake kuanza kupoteza watazamaji badala ya kuongezeka kitu kilichodaiwa kuwa ni figisu figisu tu alizofanyiwa na watu.

Kwenye Interview aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Ali Kiba alikiri wazi wazi kabisa kuna wasanii ambao wana tabia ya kununua views Youtube ilimradi tu wavunje rekodi jambo ambalo hawezi kufanya maana ni utoto:

Tunajua kabisa kuna hizi bisness za kuweka maroboti katika hizi YouTube, watu wanajifanya wana views wengi na nini. Hivi vitu vipo, tena vipo!, vipo sana tu!, vipo tena sana boss!

Eeeh, wananunua lakini kwa mimi binafsi naona ni utoto, mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu, kwanini nidanganye watu“.

Lakini pia Ali Kiba amepasua kuwa hizo views za Youtube hazimsumbui sana kwani ana njia zake nyingine za kumpatia pesa Kwenye muziki na sio Youtube tu.

Haijaathiri chochote, watu wamepata walichokuwa wanataka na sio mimi nategemea pesa kutoka YouTube viwership, hapana!. Ninachotaka kwangu ni mashabiki wangu waridhike waelewe kabisa wana-deal na msanii wa aina gani“.

 

Ali Kiba Afunguka Baada Ya Kuburuzwa Mahakamani Kisa Kutelekeza Mtoto

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Mvumo wa radi’ amefunguka na kujibu tuhuma za kutelekeza mtoto hadi kupelekea kufikishwa mahakamani.

Wiki iliyopita kuna habari ilitawala vyombo vya habari kuwa Ali Kiba amefikishwa mahakamani na mzazi mwenzake anayeitwa Khadija aliyezaa naye mtoto mmoja kwa kudaiwa Kutompa matunzo mtoto huyo.

Kwenye Interview  na Kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Kiba amedai mzazi mwenzake huyo aliinyanyasa sana familia yake kwa sababu alikuwa hataki kabisa mtoto aishi kwa upande wa wazazi wake.

Mtoto nilikuwa namlea vizuri tu, kila wikiendi alikuwa anakuja nyumbani na kama kumuhudumia natimiza majukumu yangu, sijajua sababu ya mwenzangu kuniletea fujo ila sijawahi kupelekwa Polisi.

Mimi niliiona kwenye gazeti, hayo malalamiko yapo Ustawi wa Jamii, haya yalitokana na mama yule alivyokuwa akitunyanyasa sisi sote familia yetu kuuhusu kukaa na mtoto ama kumuona.”.

Lakini pia Alikiba amesema amefurahi kuitwa mahakamani kwani haelewi mpaka sasa lengo la mzazi mwenzake huku akidai kuna kipindi mtoto anafikia hadi hatua anataja jina lingine la baba yake kitu ambacho kilimfanya aache kutoa huduma kwa mtoto.

Mimi nilikuwa nataka ifike huko ilipofika (Mahakamani), sababu haiwezekani kama kumuhudumia mimi nilikuwa namhudumia tena vizuri tu. Mtoto nimemtoa kwenye shule aliyokuwa akisoma, nikampeleka shule ya gharama zaidi ya mara tatu ya ile aliyokuwa akisoma mwanzo. Sasa yanapotokea haya nashindwa kuelewa lengo lake ni ini?”

Mange- Wimbo Mpya Wa Ali Kiba Umebuma

Mwanaharakati wa mambo ya siasa Mtandaoni mwanadada Mange Kimambi amemlipua staa wa Bongo fleva Ali kiba na kusema wimbo wake mpya unaojulikana kama ‘Mvumo wa Radi’ umebuma vibaya mno.

Siku ya Ijumaa Ali Kiba aliachia wimbo wake mpya kwa mara ya kwanza Kupitia kipindi cha XXL ya Clouds Fm lakini wimbo huo umepatwa na masahibu na kudaiwa kufanyiwa figisu figisu na watu wasiojulikana Kwenye mtandao wa Youtube.

Mange ameibuka na kumpa za Uso Ali Kiba kuwa wimbo wake wa Mvumo wa radi umebuma lakini amemtaka asikate tamaa kwani wasanii wengi wanatoa nyimbo na zinabuma na hata akamtolea mfano Diamond na kudai Albamu yake ya A boy From Tandale ilibuma pia.

 

 

Baada Ya Video Ya Ali Kiba Kubaniwa Youtube Amefunguka Haya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka kuhusiana na ngoma yake mpya ya Mvumo wa radhi aliyoiachia siku ya Ijumaa.

Kumekuwa na taarifa kuwa Ali Kiba amefanyiwa figisu figisu na watu fulani kwani tangu Jumamosi Kumekuwa na na tatizo la views (watazamaji) wamekuwa hawaongezeki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ali kiba amerikiri tatizo hilo na kusema kuwa wanafanya jitihada kadhaa ili suala hilo likae sawa:

Tunafahamu tatizo la kutokuongezeka kwa views kwenye akaunti ya YouTube ya ALIKIBA, na tupo kwenye mawasiliano ya moja kwa moja na makao makuu ya YouTube Africa ambao wanafanya kila jitihada kutatua tatizo hili kwa haraka iwezekanavyo. Shukrani kwa uvumilivu wenu na support mnayoendelea kutupa! Endeleeni kuangalia video ya Mvumo wa Radi”.

Video ya Mvumo wa Radi tangu jana Mei 12, 2018 imekuwa namba moja kwenye Trending ya video zinazotazamwa zaidi Tanzania na mpaka sasa bado ipo namba moja lakini tangu jana licha ya kuwa namba moja bado views wanaongezeka taratibu sana ukilinganisha na siku ya Ijumaa.

Ali Kiba Hana Mpango Wa Kuongeza Mke Mwingine

Staa wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuongeza mke mwingine.

Ali Kiba alifunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv ambapo anafanya media tour kwa ajili ya kinywaji chake cha Mo faya na Single mpya anayotegemea kufanya:

Kwenye Interview hiyo aliulizwa na shabiki kama ana mpango wa kumuoa Jokate maana yeye ni muislamu anaruhusiwa kuoa wake wanne.

Jamani tuheshimiane mimi nimeshaoa Jamani”.

Lakini pia Kwenye mahojiano Ali Kiba aliweka wazi kuwa sababu kubwa yeye hana skendo za Kwenye magazeti ni kwa sababu hapendelei kujiweka Kwenye nafasi zitakazoweza kusababisha skendo kama vile sio mtu wa kwenda Kwenye kumbi za starehe labda iwe ni kuperfom Lakini pia hanywi pombe.

Mwanamke Aliyemburuza Ali Kiba Mahakamani Afunguka

Siku chache zilizopita stori iliyopamba vichwa vya habari ni kuwa staa wa muziki Ali Kiba alipelekwa mahakamani na mama mtoto wake anayeitwa Hadija Hassan,na sasa mwanamke huyo anafunguka kuhusu kesi hiyo.

Global Publishers wanaripoti kutoka kwa chanzo makini kilicho karibu na familia ya Kiba  kuwa, mwanamama huyo ambaye ni mzazi mwenza wa Kiba alipatwa na hasira baada ya kusikia msanii huyo anaoa hivyo akaamua kwenda kumchukua mtoto wake ambaye alikuwa anaishi na baba yake huyo.

Unajua huyo Hadija alianza figisufigisu mara baada ya kusikia Kiba yupo kwenye maandalizi ya ndoa ndipo akaanza kudai mtoto na kwenda kumchukua kwa nguvu nyumbani kwa akina Kiba alikokuwa akiishi maeneo ya Kariakoo jijini Dar.

Sasa hapo ndipo ugomvi ulipoanza kwa kuwa hakupendezwa na kitendo hicho cha Kiba kumuoa mwanamke mwingine na hakuwa tayari kuona mwanaye akilelewa na mama wa kambo. Yaani kitendo cha Kiba kuoa ndiyo sababu kubwa ya haya yote“.

Baada ya Tuhuma hizo, Risasi Mchanganyiko lilimsaka Hadija na alifunguka haya kuhusu ishu hiyo:

Siyo kweli kwamba nilianza figisufigisu baada ya kusikia Kiba anaoa, bali niliamua kwenda kumchukua mwanangu kwa sababu nyingi sana. Hakuna anayeweza kujua na siwezi kuzungumza sana maana ni mambo ya kifamilia na familia zina mambo mengi sana.

Isitoshe mwanangu bado ni mdogo hajafikisha umri wa miaka saba bado ndiyo maana nikaona ni vyema kukaa na mwanangu kwa kuwa nilikuwa siridhishwi na malezi aliyokuwa akipata, nikaongea na baba yake, nikamchukua mtoto wangu na hapo ndipo mambo yalipobadilika“.

 

Jokate Akimbia Mitandao Ya Kijamii Baada Ya Ali Kiba Kuoa

Msanii na mfanyabiashara maarufu mitandaoni Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amepotea kabisa Kwenye mitandao ya kijamii tangu aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Ali Kiba alivyofunga ndoa.

Jokate na Ali Kiba walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu lakini mwaka jana mwishoni habari zilisambaa kuwa wameachana ingawa hakuna aliyethibitisha taarifa hizo.

Ali Kiba alifunga ndoa na Amina Khalef tarehe April  19 / 2018 Mombasa nchini Kenya na kiukweli Jokate aliandamwa sana na mashabiki juu ya ali Kiba kuoa mwanamke mwingine.

Siku ya shughuli ya Alikiba Jokate aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagram na kuambatanisha na caption iliyosomeka; LoL (Laugh Out Loud). Post hiyo ya Jokate ilienda mbali sana baada ya watu kuhusisha na hatua aliyochukua Alikiba ya kufunga ndoa.

Sasa basi, tangu April 20, 2018 siku moja baada ya Alikiba kufunga ndoa Jokate hajaonekana katika mtandao huo wa Instagram, hivyo hivyo katika mtandao wa Twitter na Facebook, mashabiki wanahoji ukimya wake umesababishwa na nini?.

Ingawa na Jokate aliweka wazi siku yake ya birthday kuwa anategemea Kuolewa mwaka huu.

Nandy Amnyooshea Mikono Ali Kiba Akiri Kumkubali

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT Nandy amekiri kuwa pamoja na mambo mengine yote na maneno yakiwekwa pembeni staa wa Bongo fleva Ali Kiba amemu-insipire sana kwa kinywaji chake.

Nandy amekiri kuwa hatua aliyofikia Ali Kiba ya kuingiza kinywaji chake mtaani ambayo ni Energy drink ni hatua kubwa sana ambayo imempa changamoto hata yeye ya kufanya makubwa zaidi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na The Playlist ya Times, Nandy amekiri kuwa kupitia Kiba ni vizuri wasanii wengi wakajifunza kuwa ni vizuri kuwekeza nje ya muziki.

Ameni-inspire kwa kinywaji kwa sababu ukiangalia the package ya kinywaji chake jinsi ilivyo ni project fulani ambayo ipo serious”.

Lakini pia Nandy ameongelea uwekezaji wa wasanii wengine kama Diamond Platnumz ambaye ni mmoja kati ya msanii Lakini pia mfanyabiashara.

Tunaambiwa nje ya kuimba tunatakiwa tuwekeze nje ya muziki wetu na ndicho hiki kaka zetu wanafanya ukimuangalia kama Diamond, Alikiba ni vitu ambavyo wanatuhamasisha”.

Kwa hivi sasa Nandy anafanya vizuri sana ngoma yake ya Ninogeshe inayoshika namba moja kwenye mtandao wa Youtube.

Billnas Afungukia Mahusiano Yake na Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Billnas amefunguka na kuweka wazi kabisa uhusiano wake na staa wa Bongo fleva Ali Kiba.

Billnas amerudi Kwenye headlines huku safari hii Ikiwa ni uhusiano wake wa kikazi na Ali Kiba. Siku chache zilizopita kuna taarifa za sintofahamu zilisambaa kumuhusu Billnas na Ali Kiba.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Billnas amefunguka kuhusu tetesi zilizodai kuna ngoma kati yake na Alikiba inakuja.

Nina Mahusiano mazuri na Ali Kiba na huwa ananishauri mambo mengi katika kazi zangu na hata muda mwingine huwa tunataniana naamini anakubali kazi zangu maana huwa nikiachia ngoma ananiambia mdogo wangu hapo freshi au kazia buti sehemu fulani.

Sitaki kuliweka sana hilo mbele ila watu wajue tunayo mahusiano mazuri kama nilivyo na mahusiano mazuri na wasanii wengine“.

Billnas anayefanya Muziki wake katika miondoko ya kurap anafanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Tagi Ubavu”.

 

Bongo Movie Wamwaga Povu Baada Ya Kukosa Mualiko Kwenye Harusi Ya Alikiba

Wiki iliyopita ilikuwa ni harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na mpenzi wake Amina Khalef iliyofanyika Kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Global Publishers inaripoti kuwa Wasanii wa Bongo movie wamemjia juu Ali Kiba kwa kitendo cha kutowaalika Kwenye harusi yake.

GP inaendelea kudai kuwa Msanii mmoja maarufu ameibuka na kudai wameumizwa na kitendo cha kutengwa kabisa Kwenye shughuli hiyo:

Yaani harusi ilipopita, tukafanya tathimini na kuangalia idadi ya watu waliohudhuria. Tukagundua wengi ni mastaa wa Bongo Fleva, watangazaji na wadau wengine wasiohusiana na Bongo Muvi.

Kwa kweli tukagundua jamaa ni mbaguzi. Hakuwa fair, alipaswa kuwaalika angalau mastaa wachache wa Bongo Muvi kuonesha ushirikiano, mbona sisi kwenye mambo yetu huwa tunaalika watu wote?”.

Inadaiwa gazeti la Amani lilifanya uchunguzi na kugundua Kinabalu waraka ulioandikwa na wasanii hao, uliosomeka hivi:

Sisi Bongo Muvi tumekuwa tukishiriki matukio mengi ya wasanii wa Bongo Fleva iwe harusi, misiba na hata maradhi, lakini kwa tukio la AliKiba tumejiuliza sana, wasanii kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Aunt Ezekiel, JB, Dk. Cheni, Ray, Richie, Gabo nk. ambao hata wachache chini ya hapo walifaa kualikwa.

Tulimuona Esha Buheti lakini najua yule ni mwana familia kwa upande flani, sijajua ni kipi kimetokea kiasi cha kutokualikwa sisi, lakini kwenye video zao wamekuwa wakitualika ili tupendezeshe video zao, na hata kututaja ndani ya nyimbo zao,”

Lakini pia gazeti hilo liliwahoji wasanii kadhaa ili kupata mtazamo wao juu ya hilo na waliongea haya:

Aunt: Nisingependa kabisa kuongelea kuhusu hilo.

Wolper: Kwa kweli sikupewa mualiko lakini pia nilikuwa naumwa.

Steve Nyerere: Siwezi kulalamikia kutoalikwa kwenye harusi japo najua hayo mambo ya utimu yanaweza kuingia.

Ali Kiba alipotafutwa kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo hakuweza kupatikana.