Baada Ya Kimya Kirefu Alikiba Adokeza Wimbo Mpya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka kuhusu kimya chake baada ya kutotoa nyimbo mpya tangu mwaka jana mwezi wa nane mpaka hivi sasa.

Wimbo wa mwisho Ali Kiba kutoa ulikuwa hit Single yake ‘Seduce me’ tangia hapo mashabiki zake wamekuwa na juu kubwa ya wimbo mpya.

Siku ya Jumapili tarehe 29/4 ilikuwa ni reception ya Harusi yake na hapo aliwang’ata sikio mashabiki zake kwa kukiri kuwa anajua mashabiki zake wana kiu ya nyimbo mpya lakini kuna. Vitu vingine amewaandalia.

Kitu ambacho naweza nikawaeleza tumefanya mambo mengi katika ukimya wangu, najua watu walikuwa wanasubiria wimbo mpya itoke lakini pamoja na hayo kuna vitu vipya nimejihusisha navyo katika biashara ambayo naifanya”.

Ali Kiba alizindua kinywaji chake kipya kinachoenda kwa Jina la Alikiba Mo Faya Energy drink Ikiwa ni moja ya hatua zake za kujiingiza Kwenye ulimwengu wa ujasiriamali.

 

Mkubwa Fela- Wanaopenda Kuona Diamond na Ali Kiba Wana Ugomvi Wameumbuka

Sio jambo la siri kuwa Wasanii wakubwa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Ali Kiba hawaivi chungu kimoja ingawa wenyewe kila mmoja kwa wakati wake amesisitiza  kuwa hana bifu na mwenzake.

Siku ya jana Diamond na Ali Kiba walizua gumzo baada ya kuonekana wakipeana mikono na kusalimiana Kwenye msiba wa marehemu Agnes Masogange.

Meneja wa Diamond na mdau wa muziki wa Bongo fleva Saidi Fella maarufu kama Mkubwa Fela amefunguka na kuweka wazi kufurahishwa na kitrndo cha Diamond kusalimiana na Ali Kiba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Mkubwa Fela alifunguka haya:

Naomba nirudie tena niseme kama ninavyosemaga siku zote watu hawa hawanaga matatizo wala ugomvi kwaiyo hiyo ni baraka kwa nchi yetu na hata muziki wetu wa Bongo fleva kwaiyo cha msingi sisi tuombe dua watu waishi kwa usalama na amani tusipende ile watu wachukiane wapende kugombana sawa ni biashara maana mashabiki wanapenda ushabiki lakini haina maana wasanii hawa wachukiane”.

Lakini pia Mkubwa Fella ameongelea umuhimu wa wasanii hao kuonyeshana ushirikiano kwenye matatizo pale walipokutana Kwenye msiba wa Masogange Lakini pia Mkubwa Fela amewashangaa wachochea bifu na kudai wanaumbuka.

 

Mange Amvaa Jokate Baada Ya Ali Kiba Kuoa Mwanamke Mwingine

Mwanaharakati wa siasa Mtandaoni Mange Kimambi amemvaa Jokate na kumtolea povu zito baada ya aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Ali Kiba kuoa mwanamke mwingine.

Asubuhi ya Leo Ali Kiba Kumuoa mke wake Amina huko Mombasa nchini Kenya lakini Ex wake Jokate anashika headlines ambapo Mange amemjia juu Jokate huku akimcheka kuhusu hilo.

Mange amekuwa akiipinga ndoa hii kufanyika hivi sasa kwa hofu ya kwamba itazima haraka tu zake za Maandamano Lakini pia amekuwa katika vita na Jokate kutokana na Jokate kuwa chama tawala na alikuwa kiongozi.

Mange amemtolea povu zito Jokate huku akihusisha ndoa ya ALi Kiba ambapo kwenye ukurasa wa Instagram wa Jokate aliandika maneno haya:

Ali Kiba Atalipwa Zaidi Ya Milioni 600 na Azam Tv Ili Harusi Yake Irushwe Live

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba amedaiwa kupata dili Nono baada ya kusemekana kuwa amesaini Dili na Azam Tv ambao watarusha harusi yake live kupitia Azam Tv.

Habari zilizo chini ya kapeti kwa hivi sasa zinasema kuwa Azam Tv wamenunua hakimiliki za kurusha harusi ya Alikiba live, dili lenye thamani ya dola za kimarekani 90,000$ ambazo ni zaidi ya milioni 204,331,500.00 za Kitanzania.

Harusi ya kwanza itakuwa Mombasa tarehe 19, mapokezi Dar tarehe 29 April.

Hakuna chombo kingine cha habari ambacho kitaruhusiwa hata kupiga picha, mambo yote yataripotiwa na Azam Tv.

Lakini pia inasemekana kuwa tayari kuna makampuni 19 makubwa ya East Africa yameshaingia mkataba mkubwa wa kufinance harusi hiyo kitu ambacho kinakadiriwa kuwa Msanii huyo atatengeneza zaidi ya shilingi milioni 600.

Bifu Kati Ya Wanamuziki Ni Muhimu-Country Boy

Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya miondoko ya kurap Ibrahim Mandingo maarufu kama Country Boy ameibuka na kutetea uwepo wa bifu miongoni mwa wasanii.

Bifu ni kitendo cha kutokuwepo maelewano baina ya watu na hii inatumika baina ya wasanii ambapo kwa nchi za nje wasanii hutengeneza bifu ili kuuza kazi zao.

Country Boy amefunguka na kudai bifu ni muhimu katika sanaa na bila kuwepo kwa bifu kunakuwa hakuna msisimko katika kazi za wasanii kwani ushindani unakuwa mdogo.

Kwenye mahojiano aliyofanya  na Star Showbiz, Country Boy alisema kuwa, msisimko kwenye muziki unapungua kwa sababu wanamuziki wengi kwa sasa wanaogopa masuala ya bifu bila kufahamu wanalikosesha soko msisimko ambao ungekuwepo kama kunapotokea tofauti.

Unajua muziki ni mashabiki, sasa kunapokuwa na wanamuziki wawili wana tofauti hata mashabiki wao pia wanakuwa wanashindana na kutamba kuonesha kwamba mwanamuziki wao ni mkali kuliko yule mwingine“.

Kwa upande wa muziki wetu wa Bongo fleva moja kati ya bifu maarufu ni kati ya wasanii Diamond Platnumz na Ali Kiba ambao imesemekana kuwa bifu imewasaidia sana kuuza muziki wao.

Nedy Music Atamani Kufanya Kazi na Alikiba na WCB

Msanii wa Bongo fleva Nedy Music anayefanya vizuri hivi sasa na wimbo wake wa One and only amefungukia mipango yake ya kufanya Kolabo na staa wa Bongo fleva Alikiba Lakini pia kusainiwa WCB.

Nedy Music anayefanya muziki wake chini ya label ya PKP ya msanii Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo itatokea nafasi ya yeye kusainiwa WCB basi ataichukua kwani ni uamuzi wa kibiashara:

Nedy Music amefungukia  kusaini katika label ya WCB amesema ikitokea nafasi hiyo atasaini kwa sababu ni biashara, pia amekanusha taaarifa za kuachana na label yake ya PKP mara baada ya wimbo wake mpya kutoka bila kuwa na logo ya label hiyo.

Kwenye Interview aliyofanya na The Playlist ya Times Fm, Nedy Music aliweka wazi kuwa yupo tayari kufanya kazi na Ali Kiba lakini anataka afanye naye kazi huku watu waone amestahili kufanya naye kazi kwa ajili ya kipaji chake alichonacho na sio sababu anamfahamu tu Kiba basi ndio afanye naye Kolabo:

Unajua usifanye kitu kimazoea, usifanye kitu kwakuwa unajuana na mtu nilitamani watu wajue uwezo wangu, nikiwa na maana hata pale ninapoenda na kazi nataka afanye na mimi basi pawe na urahisi na si kinyonge atafanya kwa kuwa tunajuana, kwa hiyo ni wazo bado lipo na panapo majaliwa litatokea”

.

Ndoa Ya Alikiba Yazidi Kunukia, Tazama Picha Za Mpenzi Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na na Habari za chini ya kapeti zinadai ndoa ni wiki hii hii.

Kwa miezi hii miwili mitatu Kumekuwa na fununu nyingi za Ali Kiba kufunga ndoa ingawa mwenyewe hajawahi hata kumuweka wazi mpenzi wake lakini Kiba picha zimeonekana Kwenye mitandao ya kijamii na inadaiwa huyo ndio bibi harusi.

Habari iliyopo mitandaoni inasemekana kuwa harusi ya Ali Kiba na mrembo huyo inategemea kufungiwa wiki hii ambapo itakuwa ni tarehe 14 na tarehe 15 Mombasa Kenya.

Hizi ni baadhi tu ya picha zinazosemakana ndiye bibi harusi mtarajiwa:

 

 

 

“Sina Bifu na Ali Kiba Ila Kuna Watu Wanatia Chokochoko” – Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz anayeendelea kufanya vizuri na albamu yake mpya ya ‘A boy From Tandale’ amefunguka na kusema hana tatizo na Ali Kiba ila kuna watu wanataka kuwagombanisha.

Diamond na msanii mwenzake wa Bongo fleva Ali Kiba wamesemekana kuwa na bifu kwa muda mrefu sana huku kila mmoja akikataa pembeni kuwa hana bifu na mwenzake lakini vijembe wanavyorushiana vinasema vingine.

Tetesi za wasanii hawa kuwa na bifu zilishika kasi baada ya Alikiba kutoa wimbo wake wa ‘Seduce me’ na Diamond kutoa Zilipendwa kisha kuanza kurushiana maneno Twitter jambo lililopelekea hadi kutukanana.

Lakini jana Kwenye Interview ambayo Diamond alifanya na LilOmmy Kwenye The Playlist alisisitiza kuwa hawana bifu ila kuna muda watu wanakuwa wnawachochea maneno maneno ili kutaka watengeneze bifu.

Unajua watu wanaweza wasiwe na matatizo ila sometimes watu wanakuwa wanatia chokochoko kati yenu na kama wanadamu zinakuja zinawa provoke na mnajikuta mnataka muingie kweli kwenye bifu, lakini baadae mkikaa mnajifikiria kuwa sisi ni watu wazima wenye akili mnajikuta mnagombana halafu wanakuja kufaidika watu wengine kwa sababu mimi kugombana na Ali hakuniongezei chochote kwenye maisha yangu”.

Diamond amesema hawezi kuwa na tatizo na Ali Kiba kwani kila mtu ana mashabiki zake hivyo hana haja ya kuwa na ugomvi naye.

Alikiba, Darassa, Diamond na Vanessa Wang’aa Kwa Tuzo Nchini Uganda

Wanamuziki wakali wa Bongo fleva kama Diamond, Ali kiba, Vanessa Mdee na Darassa wameng’aa kimataifa zaidi baada ya kila mmoja kujishindia tuzo za Hippo nchini Uganda.

Tuzo hizo zilifanyika usiku wa jana nchini Uganda ambapo baadhi ya wasanii waliopata Tuzo kutoka Tanzania ni kama vile Diamond, Ali Kiba, Vanessa Mdee na Darassa.

Vanessa Mdee ameibuka na tuzo ya heshima katika kipengele cha ‘East Africa Best Female Artist’ na Alikiba akiibuka na tuzo ya kipengele cha ‘Song of the Year Tanzania’ kupitia wimbo wake wa Seduce Me.

 

Diamond Platnumz ameshinda tuzo mbili mbili kwenye vipengele vya ‘Africa Song of The Year’ kupitia wimbo wake wa ‘Marry U’ aliomshirikisha Ne-Yo na ‘Best East Africa Video’ kupitia wimbo wa Eneka.

Darassa ameibuka kidedea kwenye kipengele cha ‘East African Super Hit’ na wimbo wake wa Muziki ambao amemshirikisha Ben Pol.

 

Ali Kiba Kufunga Ndoa Siku ya Ijumaa na Mrembo Kutoka Kenya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ali Kiba anadaiwa kajipanga Kusaga ukapera Ijumaa hii kwani anategemea kumuoa mchumba wake ambaye anasemekana kuwa ni Mkenya.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi za Alikiba kuoa na siku ya leo mtandao wa Bongo 5 unaripoti kuwa Ali Kiba atafunga ndoa siku ya Ijumaa tarehe 2/3.

Kumekuwa na taarifa kuwa Ali Kiba amekuwa na uhusiano na binti Kutoka Mombasa Kenya anayejulikana kwa jina moja tu la Amina kwa kipindi kirefu imesemekana Kiba amekuwa na uhusiano na binti huyo.

Tetesi za Kiba kuoa zilianza wiki chache zilizopita baada ya mdogo wa Ali Kiba Abdu Kiba kuliambia gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa kaka yake anatarajiwa kufunga ndoa mwezi marchi mwaka huu.

Ali Kiba pia anadaiwa kuonekana Moombasa mara kwa mara kwa ajili ya kukicheki jiko lake lakini pia ametajwa kuwa na urafiki wa karibu na gavana wa mji huo, Joho

Ali Kiba Azidi Kupaa na Kuenda Level Nyingine

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘seduce me’ Ali Kiba amezidi kukaa juu zaidi kwenye chati hasa mwaka huu wa 2018 unaonekana utakuwa mwaka mzuri kwa Ali Kiba.

Ali Kiba ni moja ya wasanii Bongo fleva ambaye ni msiri sana katika mambo yake binafsi watu wengi wanafahamu kuhusu kazi zake binafsi lakini ni ngumu sana kujua nini kinaendelea katika maisha yake binafsi au hata katika kazi zake binafsi.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Ali Kiba anakuja na bidhaa zake sokoni ambapo ilisemekana anaweza akawa mmiliki au balozi wa bidhaa kadhaa lakini hakuna siku ambayo Ali Kiba aliweza kuthibitisha taarifa hizo.

Lakini huu mwaka ni lazima utakuwa mwaka wa Ali Kiba kutengeneza pesa ingawa anafanya mambo kimya kimya kwa sasa lakini kuna video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyoonyesha Energy drink inayoitwa ‘Mo Faya’ ambayo ilikuwa na jina la  Alikiba na Sura ya Alikiba.

Lakini Mpaka sasa haijawekwa wazi kama yeye ni mmiliki wa kinywaji hiko au ni balozi wa kinywaji hiko lakini kitu ambacho kinajulikana na ukweli juu yake kutoka katika mtandao wa Dizzim Online ni kuwa mmiliki wa kinywaji hiko anaitwa Dj Sbu ambaye ni mkazi wa South Africa ambaye ameonekana mara kadhaa na Ali Kiba. Ali kiba ataungana na ulimwengu wa wasanii wafanyabiashara kama Diamond, Vanessa na Jux.

Vanessa Mdee: Mimi ni Shabiki wa Ali Kiba, Niliyoongea Yaligeuzwa

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri sana hivi sasa Vanessa Mdee amefunguka na kusema amesikitishwa na watu kugeuza maneno aliyoyasema na kufanya yawe negative wakati yeye hana tatizo na staa wa Bongo fleva Ali Kiba.

Wiki hii Vanessa Mdee alikamata headlines kwa maneno aliyosema kuhusu mastaa Diamond Platnumz na Ali Kiba ambapo alidai kuwa baada ya kutembelea nchini Nigeria na kuenda kwenye kumbi mbali mbali za starehe amegundua kuwa hawapigi sana nyimbo za nje ya nchi yao na alisikia nyimbo mbili tu kibongo ambazo ni za kwake na Diamond ambazo wote wameshirikishwa kwenye nyimbo hizo na Wanaigeria wenyewe.

Lakini alipoulizwa kama amesikia nyimbo za Ali Kiba zikipigwa Vanessa alisema hapana hakusikia nyimbo ya Ali Kiba basi baada ya kusema hayo mashabiki wa Ali Kiba walimjia juu Vanessa na kusema kama Ali Kiba sio maarufu Nigeria kama anavyodai mbona ameshinda tuzo nchini Nigeria?.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na mashabiki wa Ali Kiba wanazidi kumtolea povu aliandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Nilivyokuwa nazungumza hiyo ishu nilikuwa nazungumza kitu kikubwa zaidi lakini wenye akili zao wamegeuza imekuwa hivyo na ukiangalia lengo la jibu langu lilikuwa kuwahamashisha Watanzania wapromote na kuuthamini zaidi muziki wa nyumbani wenzetu Wanigeria ndivyo wanavyofanya sasa hapo wapi nimeudiss mziki wa Ali Kiba? Alafu Kiba anajua mimi shabiki yake sasa tutafika kweli kila neno linageuzwa kuwa baya na negative wakati nilikuwa nashedd light kwa hii ishu jamani?”.

Vanessa aliyaongea hayo alipokuwa nchini Nigeria ambapo yupo kwenye media tour kwa ajili ya kutangaza Albamu yake mpya inayoitwa Money Mondays.

Ali Kiba Aibuka Kidedea Tena Amgaragaza Diamond na Wasanii Wengine Kibao

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Ali Kiba ameibuka kidedea kwa kutajwa kama msanii mwenyewe ushawishi mkubwa Tanzania.

Tuzo hizo zinazojulikana kama 100 Most Influential Youth zilizoandaliwa na Advance Media organization zilitangazwa rasmi mwaka Jana na mastaa kibao walitajwa kuwania tuzo hizo.

Baadhi ya Mastaa walioshindanishwa katika tuzo hizo ni pamoja na Alikiba, Jokate, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Idris Sultan, Faraja Nyalandu, Nancy Sumari, Dina Marios, Millard Ayo na wengineo wengi.

Siku ya Jana ilitangazwa rasmi kuwa Ali Kiba amembwaga hasimu wake namba moja Diamond baada ya kutajwa kuwa ndio msanii mwenye ushawishi Mkubwa sana na kupewa medani ya sanaa na burudani katika tuzo za advance media 2017/2018.

Matokeo ya kura zilizokuwa zikipigwa za 50 Most Influential Tanzanians (vijana 50 wenye Ushawishi zaidi) yametoka na katika kipengele cha burudani (Entertainment) Mshindi ni Ali Kiba huku akimshinda hasimu wake Mkubwa Diamond ambaye yeye amechukua nafasi ya pili , akifuatiwanam Wema Sepetu aliyechukua nafasi ya tatu huku nafasi ya nne imechukuliwa na mchekeshaji Joti na nafasi ya tano imechukuliwa na Vanessa mdee huku Jokate Mwegelo akichukua nafasi ya sita .

Baada ya ushindi huo Ali Kiba alitumia ukurasa wake wa Instagram kuandika salamu zake za shukrani kwa mashabiki zake baada ya kumpigia kura:

 

Thank you for voting for me to become the most influential Young Tanzanian in Entertainment Industry Nawashukuru sana #Kingkiba”.

 

 

Hivi Ndivyo Ali Kiba na Diamond Walivyojaza Nyomi la Watu Kwenye Show za Kenya na Rwanda (picha na video)

Wasanii wakali wa Bongo fleva wanaozidi kufanya vizuri Diamond Platnumz na Ali Kiba, wamedhihirisha ukubwa wa muziki wao kila mmoja kwa wakati wake.

Mwishoni mwa wiki hii iliyopita wasanii wote wawili walikuwa na shoo nje ya nchi ambapo Diamond alikuwa na shoo ya kufunga mwak nchini Kenya, Naivasha na Ali Kiba alikuwa na shoo nchini Rwanda.

Ali Kiba

Alikiba alidhihirisha ukubwa wa muziki wake baada ya kupiga shoo ya peke yake nchini Rwanda iliyovuta watu wengi ambapo ilisemekana kuwa Kiba alipiga bonge la shoo kwenye uwanja huo wa mpira ambao alijaza mashabiki walioenda kumuona akitumbuiza.

Hizi ni baadhi ya picha na video zinazomuonyesha Kiba akitumbuiza sherehe yake ya kufunga mwaka na Kiba:

 

 

 

  1. Diamond Platnumz

Diamond alizidi kudhihirisha ukubwa wa muziki wake nje ya nchi baada ya kupiga bonge la shoo la kimataifa nchini Kenya katika mji wa Naivasha ambapo katika ukumbi huo aliopiga shoo naweza thubutu na kusema kuwa Alijaza maana kulikuwa bonge la nyomi la watu.

Hizi ni baadhi ya picha na video zinazoonyesha nyomi la Watu walioenda kwenye show ya Diamond;

 

Ali Kiba Awataka Radhi Mashabiki Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa Ali Kiba amefunguka na kiwataka radhi mashabiki zake wote.

Ali Kiba aliomba radhi baada ya kushindwa kutimiza ahadi yake ya kufanya tamasha la Funga mwaka na King Kiba baada ya kudai kupatwa na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake na hivyo kupalelekea kukosa kishiriki tamasha hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ali Kiba aliandika ujumbe huo wa msamaha na kuonyesha kusikitishwa na kitendo cha kishindwa kushiriki tamasha hilo:

Hello fans  natumaini kila mmoja wenu amekuwa na wakati mzuri katika kipindi hiki cha sikuku ningependa kuchukua nafasi hii kiwaomba radhi kwa kishindwa kuwatimizia kifanya Funga mwaka na King Koba kama ilovyohaidiwa. Haikuwa lengo langu ila kuna mambo yamejitokeza  yaliyo nje ya uwezo wangu ambayo yamesababisha kitoweza kufanyika kwa tukio letu ambalo lingehusisha uzinduzi wa bidhaa zangu na wimbo wangu mpya. Hata hivi karibuni Mungu akijaalia ntawapa taarifa ya namna tutakavyoufungua mwaka  asanteni sana kwa ushirikiano na support mnayonipa kila siku Mungu awabariki sana”.