Barakah The Prince: Sina Ugomvi Wala Bifu na Alikiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince ameibuka na kudai kuwa hana ugomvi wala bifu na msanii mwenzake Ali Kiba.

Ni wiki chache tu zilizopita Barakah alikuwa anafanya interview na kila kituo na stesheni mbali mbali za media na kudai kuwa Ali Kiba na uongozi wao wote wa Rockstar 4000 ulikuwa unamfanyia zengwe ili kuua mziki wake baada ya kujitoa kwenye label yao.

Barakah aliyesainiwa chini ya label hiyo ya Rockstar 4000 miaka michache iliyopita aliwashangaza watu wengi kwa kile alichodai kuwa anajitoa kwenye label hiyo kisa na mkasa ukiwa uongozi wa label hiyo ukiongozwa na Ali Kiba na Seven Mosha ulikuwa unamzuia kutoa kazi zake na akadai kuwa kwa mwaka mzima ameruhusiwa kutoa nyimbo moja tu.

Kinachojulikana ni kuwa Ali Kiba alishawahi kusema kuwa Barakah ni mtoto tu hana akili, na inasemekana kuwa aliyemfukuza Barakah Rockstar 4000 ni Ali Kiba kutokana na tabia alizokuwa nazo Barakah. Sasa inasemekana kuwa Barakah ameanza tena kujipendekeza kwa Kiba kwani amemposti Alikiba kwenye siku ya birthday na kumtakia maisha marefu lakini hakumjibu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kuptia kipindi cha Enews Barakah amedai kuwa hana ugomvi na bifu na Alikiba kama wengi wanavyodhani;

Mimi sijawahi kuwa na matatizo na Alikiba kabisa wala sijawahi kufikiria kuwa na matatizo naye hayo matatizo ni midomo ya watu tu wanayatengeneza, mimi kutaka kuondoka kwenye kampuni yao ya kazi sio kwamba ndio nina ugomvi nao hii ni kazi tu naweza nikahama ofisi yoyote”.

 

Mama Ashura Azidisha Mashambulizi Dhidi Ya Ali Kiba

Mchekeshaji kutoka Timamu Tv anayejulikana kama Mama Ashura ameibuka tena na kuzidisha mashambulizi yake dhidi ya msanii mkongwe wa Bongo fleva Ali Kiba.

Mama Ashura amekuwa na desturi ya kumkosoa Alikiba tangu alipoweka wazi hisia zake kuwa yeye anaamini Diamond ni msanii mkubwa kuliko Alikiba. Siku ya jumapili na jumatatu alitumia kumkosoa Alikiba kwa performance yake aliyofanya Fiesta na kudai kuwa sio mburudishaji mzuri na wala hajui kuimba live.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mama Ashura ameendelea kufunguka haya kuhusiana na Ali Kiba:

 Unajua uimbaji wa muziki sio ufundi tu wa sauti, maana kuna wanaodhani kwa sababu wana ufundi wa sauti basi mziki wa Bongo wameshauwini. Big NOO yambua jinsi ya kucheza na sauti yako na linganisha na mahitaji ya muziki wako, napendaga kumtolea mfano Mondi sio kwamba pekee anayeweza au anafanya vizuri Laah ila ni mmoja wapo kati ya mfano wa kuigwa. Kipindi anatoka watu wakasema ooh hawezi kuimba anaunga unga vocal zake hazina ufundi, lakini sahivi ule muono umebadilika baada ya watu wa kimataifa kuona uwezo wake wa kucheza na sauti yake ambayo ilisemwa ni ya kuunga unga kiujanja ujanja. Wapo wengi wenye sauti nzuri na wanajua kucheza nazo mfano mwingine ni Barnaba na wengine. Sasa wale wakali wa saute wanavyo jikakamua kuimba ‘halelujah’ kwa kutumia ufundi wao wa halo ya juu”.

 

Christian Bella: Mimi ni Namba Moja Nisifananishwe na Alikiba

Mwanamuziki na mkali wa mziki wa dansi nchini, Christian Bella ameibuka na kudai kuwa yeye ni mwanamuziki namba moja na asifananishwe wala kupambanishwa na mkali mwenzie Ali Kiba.

Baada ya kipindi cha ‘cheche’ kuingia mtaani na kuhoji watu ili kuuliza watu nani mkali wa ‘vocal’ kati ya Ali Kiba na Christian Bella na majibu kurudi huku watu wengi wakimpigia kura Ali Kiba kuwa ni mkali kuliko Christian Bella na kuibuka mshindi kitendo ambacho Bella alionesha kutokuridhika na kusema Kiba ni mkubwa katika mziki wake wa Bongo fleva lakini na yeye mkubwa kwenye mziki wake wa dansi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Christian Bella alifunguka haya kuhusiana na ushindindani huo dhidi ya Kiba.

Unajua huo ni mtazamo wa shabiki waliyemhoji huyo walimhoji anamkubali msanii wake kila msanii ana mashabiki wake na mimi najua watu mliowahoji wanaweza wakawa mashabiki wanaompenda Alikiba na mimi sijawahi kusema kuwa Alikiba sio msanii mzuri kwaiyo mtu akisema kuwa ni msanii mzuri siyo vibaya kwanza sijawahi kujali sijui umsifie mtu zaidi yangu eti nione vibaya?Noo ila kama mlipiga kura mkaona Kiba ni zaidi sio vibaya siwezi kukataa maoni ya wale ila ukweli wangu hata ukimhoji Kiba hawezi kusema kuwa ananishinda mimi hats siku moja never! Alafu Ali hawezi kunizidi mimi na mimi siwezi kumzidi yeye hata siku moja”.

Pia Bella amekiri kuwa ni vigumu kumshindanisha yeye na Alikiba kwa sababu wanafanya aina mbili za mziki zilizo tofauti kabisa na hivyo hawawezi kupambanishwa kwani Kiba anafanya Bongo fleva na yeye anafanya mziki wa Dansi na kila mmoja ni mkali katika kitengo chake.

Ali Kiba Amjia Juu Shabiki Wake Baada Ya Kumuita ‘Mungu’

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri nangoma yake ya ‘seduce me’ amemjia juu shabiki wake baada ya kumuita Mungu wa Bongo fleva.

Baada ya Ali Kiba kuposti picha kwenye ukurasa wake wa instagram, shabiki huyo alijulikana kama Kiba Salu aliacha ujumbe chini ya picha hiyo na kuandika ‘Bongo fleva God’ Kitu ambacho hakikumpendeza Ali Kiba na kumjia juu shabiki huyo na kumuandikia:

Kiba Salu naomba msiniite hivyo wala siwezi kuwa hivyo wala siwezi kukibali kuitwa hivyo imani yetu hairuhusu kujiita au kuitwa na mtu yoyote jina la Muumba, Tafadhali”.

Ai Kiba alitokwa na povu hill baada ya kuitwa Mungu wa Bongo fleva kitu alichosema hakiruhusiwi kwa imani yake ya kidini ya Kiislamu kwani Mungu ni mmoja tu na binadamu hawezi kuwa Mungu.

Ali Kiba ambaye amekuwa kimya kwa kipindi kidogo tangu alipoachia nyimbo yake iliyovunja rekodi ya ‘seduce me’ mwezi wa septemba mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ali Kiba aliweka picha akiwa visiwani Zanzibar ambapi inasemekana kuwa yupo katika hatua za kutengeneza nyimbo take mpya itakayotoka hivi karibuni.

Caroline Joseph Amefunguka Kuhusu Tetesi Za Ujauzito Wa Alikiba

Mwanadada Caroline Joseph ameongelea tetesi zilizomkabili mtandaoni kuhusu yeye kutangaza kuwa ana ujauzito wa mwanamuziki Ali Saleh kiba.

Ni wiki chache tu zimepita tangu mwanamuziki Ali Kiba akumbwe na skendo ya picha zilizosambaa mtandaoni zinazomuonesha yeye na mwanadada Caroline wakiwa chumbani wamepiga picha pamoja, lakini haraka sana msemaji wa Kiba aliibuka na kusema Kiba hana uhusiano wowote na yule dada ila tu nishabiki aliyemfata kupiga picha kama walivyo mashabiki wengine.

Wiki iliyopita kuna picha ya ‘Ultrasound’ ya mtoto iliyodaiwa kuwekwa na Caroline mtandaoni akidai kuwa anatarajia kujifungua mtoto wa kike wa Kiba.

Picha iliyodaiwa kupostiwa na Caroline akidai ni ultrasound ya ujauzito wake

Caroline amefunguka kuhusu sakata hilo lililokiki mtandaoni amesema ameshtushwa na habari hizo zilizosambaa kwani sio za kweli na anamheshimu Kiba kama kaka na ndugu yake.

Sina mimba jamani na wala sina uhusiano na Kiba, kuna mtu amefungua akaunti feki kwa kutumia jina langu kwenye mtandao wa Instagram Ambaye anasema ana ujauzito wa Kiba na ameweka picha zangu eti na ultrasound ya mtoto tumboni na kusema Princess Kiba anakuja! Kiukweli imeniuma sana maana imenipa usumbufu hivyo nimeenda kuripoti polisi katika kitengo cha makosa ya kimtandao (cyber crimes)na wako kwenye uchunguzi wa kumpata huyo mtu aliyetumia jina langu na kuweka picha zangu kunichafua ili achukuliwe hatua”.

Pia, Caroline aliweka wazi kuwa amekuwa akipokea meseji za vitisho kwenye simu yake kwa namba ngeni Kwamba watamfanyia kitu kibaya kwa kuwa anamchafua Kiba kwa kusema ana mimba yake.

Nimepokea vitisho kwenye Simu yangu kuwa watanipoteza kwasababu namchafua Alikiba lakini nimekuwa nikiwaambia waangalie kwenye Instagram mimi natumia jina la Dorothea Caroline 9, huyo aliyeweka hiyo picha Hana 9 mwishoni. Nimeamua kwenda polisi ili huyo mtu akamatwe maana naweza kupatwa na jambo baya Wakati sina hatia yoyote Huyo mtu inawezekana anatafuta wafuasi kwaajili ya kufanya biashara zake”.

Ali Kiba alikataa kujibu tuhuma hizo hata kupitua meneja wake alipotafutwa alikataa kuongelea suala hill.

Elimu ni Muhimu Kwa Wasanii Ili Kuondoa Ujinga- Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Ali Kiba ameongelea umuhimu wa elimu kwa wasanii.

Wasanii wengi wakishaingia kwenye sanaa yoyote wakapata njia ya kuingiza kipato wanaona hakuna umuhimu wa kusoma au kupata elimu ya darasani.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ali kiba aliongeza kuwa elimu inatoa ujinga na hivyo ni muhimu kwa wasanii wote kupata elimu.

Ukiwa na elimu kama wewe ni msanii ni rahisi kuonyesha watu ubongo wako ukoje, kwa sababu mkasa na visa vipo na maneno yapo lakini utamfanya mtu afikirie huyu mtu aliwaza nini, unajua ubongo wako ukiwa active utaweza kufikiria vitu vya msingi zaidi, achana na watu wanaoimba ujinga, ni kwasababu tu ya talent lakini elimu ni ya muhimu sana kwenye kila kitu”.

Ni kawaida kwa wasanii wengi kudai kuwa hawadhani kama kuna umuhimu wa kupata elimu ya darasani na hasa wakipata mafanikio lakini pia kuna wasanii wachache waliofanikiwa kupata elimu ya juu mfano wasanii kama Mwana Fa, Nikki Wa pili, Jokate na wengine wengi.

Je una maoni gani juu suala hili la elimu kwa wasanii, je unahisi kuna umuhimu wowote kwa wasanii kupata elimu?

Tafadhali toa maoni yako.

Ali Kiba Aweka Wazi Wasanii Anaotaka Kuwasaini Rockstar 4000

Msanii wa Bongo fleva Ali Kiba ambaye amesainiwa chini ya label ya Rockstar 4000 amefunguka kuwa wana mpango wa kuendelea kusaini wasanii wengi wenye vipaji chini ya label.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5, Ali Kiba alikiri kuwa hawezi kutangaza hadharani rasmi  kwa sasa kwani bado hawajakamilisha kila kitu lakini baadhi ya wasanii ambao wana mpango nao au aliowagusia ni pamoja na Aslay, Abdu Kiba , Abby skill na Jokate.

“Ni ngumu kuwataja kwa saivi kwasababu hatujawa introduce lakini Abdu Kiba yupo na Abby skills pia bila shaka nina uhakika naye atakuwepo”.

Ali Kiba alipouliza kuhusiana na Aslay kama wana mpango wakumchukua kutokana na kipaji chake, Ali Kiba amekiri kumkubali sana Aslay.

“Aslay ni msanii mzuri sana na anafanya kazi yake vizuri sana na anapendwa na watu na anaimba vizuri na ana talent na ni kweli Rockstar inachukuaga wasanii wenye vipaji kama Aslay lakini hatuja Fanya mazungumzo na Aslay bado lakini tunavyosema bado maana yake kuna nia huko mbeleni”.

Lakini pia Ali Kiba aliongelea kumsaini Mwana Dada Jokate ambaye pia alikuwa mpenzi wake na alifunguka:

“Jokate bado hajasaini lakini huwa anapendelea kuimba lakini ni mtu wa karibu wa rockstar anapendaga kutupa ushauri saa nyingine lakini pia ana talent ya kuimba na pia mda wowote akiwa tayari bila shaka tutamsaini”.

 

Ali Kiba ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Seduce me’ alioutoa mwezi uliopita.

Gigy Money Adai Wimbo Wake Ni Mkali Kuliko Seduce Me ya Ali Kiba

Video queen maarufu aliyepenya kwenye muziki Gigy Money anayetesa na wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nampa papa’ ameingia tena kwenye vichwa vya habari baada ya kudai kuwa wimbo wake huo ni mkali kuliko wimbo wa Alikiba.

Ali Kiba ambaye kwa sasa bado anafanya vizuri na wimbo wake wa Seduce me alioutoa mwezi uliopita amekuwa akipata maoni mbalimbali juu ya wimbo huo kutoka kwa wasanii mbalimbali mmoja wapo akiwemo Gigy Money.

Kwenye Mahojiano aliyoyafanya na kituo cha redio cha East Africa kupitia kipindi chao cha Planet Bongo Gigy Money alifunguka kuwa kwa maoni yake na watu wengi anaona Nampa papa ni kali sana kuliko Seduce me ya Ali Kiba.

“Ni hivi Seduce me na ngoma yangu nampa papa yangu kali, ndiyo Nampa papa kali kuliko seduce me yaani itakaa muda mrefu kwenye chati sema tu watu hawataki kukubali hill kwa sababu Alikiba ni msanii mkubwa alafu alikaa kimya muda mrefu mashabiki walimmiss sana alafu huwezi kusikiliza seduce me zaidi ya mara tano lakini papa unaweza kusikiliza siku nzima”.

Alimalizia kusema Gigy Money

Je ni kweli unahisi wimbo wa Gigy Money ni ni mkali kuliko seduce me ya Ali Kiba?

Mange Kimambi: Diamond Kaweka Rekodi Feki

Mange Kimambi ameibuka upya na kudai kuwa rekodi ambayo Diamond Platnumz ameweka ni feki Hili limekuja baada ya Diamond kuachia wimbo wake mpya siku mbili zilizopita uitwao Hallelujah aliomshirikisha  mwanamuziki Morgan Heritage, wimbo huo ulifanikiwa kufikisha jumla ya views million mbili kwenye mtandao wa Youtube ndani ya siku moja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange alifunguka yafuatayo juu ya suala hilo;

“#IssaFakeRecord Amenunua viewers huo ndo ukweli!!! Samahani kwa ntakaowakwaza…. Baba Dully ajifunze kukubali na kushindwa sometimes, hakuwa na haja ya kununua viewers ili tu avunje rekodi ya Ali Kiba”.

Mange aliendelea kusimamia msimamo wake juu ya suala hilo japokuwa alipokea ushindani mkubwa shidi ya mashabiki wa Diamond ambao walimlaani vikali;

“Mtanitukana sana Team Diamond ila wote mnajua kuwa sisemagi uwongo na maneno yangu kwa njia moja au nyingine huwa lazima mwisho wa siku yawe ya kweli! Naamini soon mtakuja kujua kuwa Mange aliwaambia ukweli kuwa Diamond alinunua viewers! Leo mtanichamba ila siku moja ukweli utajulikana. Haiwezekani nyimbo imetrend namba moja Tanzania peke yake ikapata waangaliaji milioni moja ndani ya masaa kum na tano wakati Seduce me iliyotrens Afrika Mashariki nzima ilipata waangaliaji milioni moj ndani ya masaa thelathini na nane, it doesnt make sense ata all #fact”.

Diamond alivunja rekodi hiyo iliyowekwa na hasimu wake Ali Kiba ambaye kwa kupitia wimbo wake wa seduce me alifikisha waangaliaji milioni 1 ndani ya masaa 38 na Diamond juzi alifikisha waangaliaji wa Video yake hiyo milioni 2 ndani ya siku moja.

 

Miziki ya Ali Kiba na Mwana FA Yatambulika Kimataifa Zaidi

Wanamuziki Ali Kiba na Mwana FA wamekula shavu zito baada miziki yao wanayofanya kutambulika na wasanii wakubwa wa Marekani.

Mwanamuziki Ali Kiba ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Seduce me’ ameula kwani wimbo wake huo umekuwa miongon ati ya nyimbo zilizochezwa na DJ katika uzinduzi wa wa bidhaa za mbalimbali za BallyxSwizz zinazomilikiwa na mwanamuziki na producer mkubwa Marekani Swizzbeats ambaye pia ni mumu wa mwanamuziki mkubwa duniani Alicia Keys.

Model wa kimataifa toka Tanzania Flaviana Matata ambaye alikuwa mmoja wa wahudhuriaji katika sherehe hiyo alituma clip ya video katika mtandao wake wa twitter na kuandika

“When you go to support a friend and his DJ plays Tanzanian music Swiss Beats thanks for support”.

Pia katika sherehe hiyo model Flaviana Matata alikutana na Mwanamuziki maarufu anayeenda kwa jina la ‘Fabolous’ ambaye alitaja mistari ya ‘Unanijua unanisikia’ ambayo inapatikana katika nyimbo ya Mwana FA inayoitwa Unanijua unanisika katika hali ya kuonyesha furaha yake na shukrani Mwana FA aliyumia mtandao wa twitter kumshukuru rapper huyo na model huyo kwa kumfikishia ujumbe huo.

Hiyo yote inaonesha ni kwa jinsi gani muziki haujalishi lugha inayotumika kwani Faboulous hajui kiswahili lakini ametokea kuvutiwa na wimbo huo pamoja na kutokujua maana ya wimbo huo pia ni vizuri kuona lugha yetu inakua zaidi.

 

Faiza Ally: Alikiba Anafanya Muziki Mzuri Kuliko Diamond

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Faiza Ally ameibuka tena na kudai kuwa anauelewa zaidi muziki anaofanya Ali Kiba kuliko muziki anaofanya Diamond Platnumz.

Katika mahojiano aliyoyafanya na TBC Faiza alidai kuwa wasanii wote wawili wanajitahidi katika kufanya muziki kwani wana vipaji tofauti kwani mmoja ni muimbaji na mwingine ni mburudishaji.

Faiza aliendelea kusema:

“Kwanza kati ya muziki wa Diamond na Ali Kiba , naupenda zaidi muziki wa Ali Kiba, muziki wake ni mzuri kuliko Diamond, kwani Diamond ni ile full entertainment ukimwangalia tu unatabasamu lakini Ali Kiba ana muziki mzuri. Nikizungumzia mtu aliyeutoa mziki akaupa heshima mpaka akampa changamoto Kiba na yeye akasimama mpaka tukaanza kumuona kwenye hali ya tofauti ni Diamond”.

Faiza ni moja ya watu ambao msimamo wake umekuwa ukibadilika kuhusu nani ni bora kati ya Diamond na Ali Kiba kwani mara kwa mara amekuwa akibadilika kwani leo anaweza akasema Diamond na kesho atasema kuwa ni Ali Kiba.

Lakini yote kwa yote ushindani huu ndo unafanya muziki wetu kuwa bora zaidi kwani Ali Kiba asingekuwa na changamoto kutoka kwa Diamond asinge kuwa bora alivyo sasa na hivyo hivyo kwa Diamond asingepata changamoto kutoka kwa Ali Kiba basi asingejitahidi kutupa muziki mzuri zaidi tunaopata leo hii.

Alikiba Aongelea Umuhimu Wa Kutumia Kiswahili Kwenye Nyimbo Zake Badala ya Kingereza

Mwanamuziki anayefanya vizuri kwenye Bongo fleva na kutamba na nyimbo yake ya ‘Seduce me’ Alikiba amefunguka kuwa haoni sababu ya kuacha kutumia kiswahili katika nyimbo zake inasaidia kukuza lugha yetu ya taifa na pia mashabiki ambao pia hawajui kiswahili wanaimba nyimbo zake zote.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni East Africa Alikiba alisema haoni sababu za kutotumia Kiswahili kwani ni moja kati ya lugha kubwa sana;

“Hakuna kizuizi cha lugha kwenye muziki zamani tulikuwa tunapenda miziki ya kilingala laakini tulikuwa hatujui nini wanaimba, tulikuwa tunapenda miziki kutoka Congo lakini hatuelewi wanaimba nini bado mpaka sasa kuna watu wanapenda miziki ya kizungu lakini hawaelewi kizungu hivyo hakuna kizuizi cha lugha kwenye muziki. Kiswahili ni lugha kubwa Afrika na tunapendelea kuimba kiswahili tunakuza lugha yetu kwanza mimi najivunia kuwa mswahili nasaidia kukuza lugha yangu ya Kiswahili ifike kote inapotakiwa kufika kwasababu tayari ni lugha kubwa duniani”.

Pia Alikiba alisema haoni sababu ya kuacha kutumia Kiswahili kwa kuhofia kuwa mashabiki wake wa nchi za nje ya Afrika Mashariki hawataelewa kwani ameshafanya matamasha kwenye nchi ambazo watu hawaongei Kiswahili kabisa na bado watu wanaimba nyimbo zake pamoja na kwamba hawaelewi wanaimba nini hata kama maneno mengine wanashindwa kuyasema vizuri lakini bado wanajitahidi kuimba naye.

Kumekuwa na dhana nyingi sana ambapo wasanii wanaona bora kutumia kingereza kuimba kwenye nyimbo zao ili ziweze kusika kimataifa zaidi lakini tunasahau kuwa muziki ni sanaa ambayo inavutia kwa vitu vingi ukiachana na maneno yanayoimbwa msikilizaji anaweza kuvutiwa na  biti inayotumika pia vyombo vilivyomo kwenye nyimbo na hasa sauti inayoimba kwaiyo kwa maoni yangu ni vema kuendeleza kutumia Kiswahili ili tuikuze lugha yetu ya taifa.

Picha za Alikiba na Shabiki Zilizozua Utata Mtandaoni

Mwanamuziki Alikiba alizua utata baada ya picha zake na shabiki wake kuvuja mtandaoni. Alikiba alikuwepo jijini Mwanza kwa ajili ya tamasha la Fiesta lililofanyika jana lakini picha alizopiga na msichana ambaye hakutambulika mara moja zilileta utata kidogo miongoni mwa watu hasa sababu ya pozi tata za picha hizo. Huku kila mtu akisema lake mtandaoni hakuna mtu aliyemtambua mwanadada yule.

Hizi ni baadhi ya picha hizo zilizozua utata:

1.
2.
3.

Picha hizo zilizomuonyesha katika mapozi mbalimbali na mwanadada huyo ziliamsha minong’ono baada ya mashabiki kuanza kudhani kuwa ni mpenzi wake, lakini baada ya muda chanzo cha karibu cha Alikiba kiliachia picha huku kikisisitiza kuwa Ali hana uhusiano wowote na mdada yule zaidi ya urafiki wa kawaida tu.

Upande wa Alikiba waliachia picha hizi pia;

1.
2.

Msemaji wa Alikiba alisistiza kuwa hizo picha zote zilipigwa kwa wakati mmoja akijibu maswali ya watu kuwa ni kwanini alipiga picha na msichana chumbani, “Hizo picha zote zilikuwa ni Alikiba akipiga na mashabiki zake waliomfata kuomba picha za pamoja”. Ali kiba alimaliza kiu ya wakazi wa Mwanza kwa kupiga bonge la shoo.

Dkt. Mwakyembe- Sioni Sababu ya Kuwasuluhisha Diamond na Alikiba

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo mheshimiwa Harison Mwakyembe amefunguka kuhusu ugomvi unaoendelea kati ya wasanii wawili wakubwa Tanzania Ali kiba na Diamond Platnumz ambapo amesema kuwa hatarajii kuwapatanisha tena kama alivyohaidi mwanzoni.

Wadau mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva walimuomba waziri Mwakyembe aingilie kati beef hilo la wasanii hao wawili ambao kwa muda mrefu wamekuwa hawapatani huku sababu kamili ya ugomvi huo ikiwa haijajulikana huku watu wengi wakihisi bifu hilo limetokana na ushindani wa kimuziki baina yao. Bifu lao lilionekana dhahiri pale ambapo Ali kiba alitoa wimbo wa ‘Saduce me’ na kupokelewa vizuri na mashabiki wake ndipo Diamond naye alipoamua kutoa nyimbo yake mpya ya Zilipendwa masaa machache baadae ambazo ziliingia kwenye ushindani mkali kwenye mtandao wa youtube.

Mh. Mwakyembe amesema;

“Kama kuna ushindani kati ya Ali Kiba na Diamond ambao ni kiweledi, kitaaluma basi mimi nafikiri tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha waendelee kushindana vizuri ili tupate miziki mizito.kwa hiyo mimi nawaomba watanzania wachukulie mvutano huo ni mzuri katika tasnia, mradi mimi sijasikia watu wameshikiana mapanga”.

Pia Dkt. Mwakyembe amesisitiza kuwa ahadi yake aliyoitoa mwanzoni ya kutaka kuwaita Diamond na Alikiba ili kufanya wimbo kwa pamoja iko pale pale kwani anaamini wote ni vijana wenye vipaji na watafanya kazi nzuri kwa pamoja ila tu kwa sasa wakati haujafika.

Mashabiki wengi wa Diamond wamekuwa wakimtuhumu Alikiba kwa kung’aa kupitia Diamond yaani kuwa asingekuwa na bifu na Diamond Alikiba asingesikika yaani anafaidika zaidi na bifu hilo.

Je wewe unaonaje je ni kweli tuhuma hizo za Alikiba kung’aa kupitia Diamond? Na je wasanii hawa wanahitaji kuendelea kuwa na bifu au wapatane tu? Tafadhali toa maoni yako hapo chini.

Lady Jay Dee Aikataa Rockstar 4000 ya Alikiba

Baada ya kusambaa kwa  taarifa za Lady Jay Dee kujitoa kwenye Label kubwa Africa ya Rockstar 4000 imbayo pia inawasimamia Ali Kiba na Ommy Dimpoz mapya yaibuka.

Akiongea na Bongo 5 mtu wa karibu wa msanii huyo amedai, Jide hajawahi kusaini mkataba na label hiyo kwa maana hakuna picha zilizowahi kuonyesha mkataba  huo, alikuwa anafanya kazi na Seven Mosha ambaye ni boss wa label hiyo Kama rafiki yake wa muda mrefu aliyekuwa anamsaidia kazi katika mziki wake.

“Nafikiri kaamua ka Continue reading “Lady Jay Dee Aikataa Rockstar 4000 ya Alikiba”

“Muda wa Ali kuoa sasa umefika” Familia ya Ali Kiba wamtaka afunge ndoa na Jokate Mwegelo

Mamake na dadake Ali Kiba wametoa kauli zao kuhusu staa huyo kufunga ndoa. Wawili hao walisema muda umefika kwa Ali Kiba kuoa.

Akiongea na Global Publishers, mamake Ali Kiba alisema kuwa mwanawe anahitaji mke wa kumchungia watoto wake wanne ambao walizaliwa na wanawake tofauti.

“Mimi kama mzazi, ninaona muda wa Ali kuoa sasa umefika maana kama ni maisha ya ujana amesha­fanya kila kitu, ana watoto wanne na kila mmoja na mama yake, ni vi­zuri sasa akachukua mke ili aweze kuwalea hawa watoto wake. Mimi kama mzazi huu ndiyo msimamo wangu, ninamtaka ata­fakari na kuchukua uamuzi mara moja, maana ingawa siyo vizuri kwa mzazi kumpangia mtoto wake cha kufanya, lakini inapofikia suala la kuoa ni muhimu ukasimama na ku­toa msimamo, wakati wa kuoa ume­fika,” alisema mamake Ali Kiba.

Dadake Ali Kiba – Zabibu alisema kuwa Jokate Mwegelo ndo mwanamke ambaye Ali Kiba anafaa kufanga naye ndoa. Zabibu alimsifu Jokate kwa kusema kuwa ni msichana mwenye busara.

Jokate Mwegelo

“Mimi namchukulia Jokate kivingine kabisa, ni msichana mwenye busara zake na amekuwa kama mshauri wangu wa karibu mno, ningetamani angekuwa mke halali wa kaka yangu kwa sababu ana vigezo vyote vya kuwa hivyo. Kwa kuwa kaka yangu bado hajaoa, ninaomba kila kukicha na­fasi hiyo ichukuliwe na Jokate kwa sababu ni mwanamke anayestahi­li kuipata nafasi hiyo ya kuwa wifi yangu,” alisema Zabibu ambaye pia ni rafiki wa mastaa wengi,”alisema Zabibu.