Ali Kiba ajiunga na gavana wa Mombasa kumfanyia kampeni

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ni rafiki wa dhati wa Ali Kiba. Mara nyingi staa huyo wa Bongo husafiri kuenda Kenya kumtembelea tu gavana huyo.

Jumapili iliyopita Joho aliwafurahisha wafwasi wake alipomuita Ali Kiba kuwatumbuiza, gavana huyo wa Mombasa alikua akifanya kampeni zake Kisauni. Ali Kiba aliimba wimbo maalum ambayo alimtungia gavana huyo.

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho akifanya kampeni zake

“Wa Ganjoni sema! Wa Mvita Sema… Joho Tena!” Ali Kiba aliimba huku akiwaomba wanainchi wampigie kura gavana huyo.

Gavaba huyo wa Mombasa amekua akiwaalika wanamuziki kadhaa kutumbuiza wanainchi akifanya kampeni zake jijini Mombasa.

 

Dadake Diamond – Queen Darleen akana kuwai kuwa mpenzi wa Ali Kiba

Kabla Diamond hajakua nyota Tanzania, Ali Kiba na Queen Darleen walikua marafiki wa dhati. Diamond aliponza kutawala kimuziki, Ali Kiba alianza uadui na yeye kisa kilichosababisha kusambaratika kwa uhusiano wake na Queen Darleen ambaye alisimama na kakake.

Ukaribu wa Queen Darleen na Ali Kiba ulichangia kuzuka uvumi kuwa wawili hao walikua wapenzi, madai ambayo dadake Diamond amepinga.

Queen Darleen na Diamond

“Sio kweli Alikiba hajawahi kuwa bwana wangu, Ali Kiba ni ndugu yangu na tuna heshimiana sana zaidi ya sana. Unajua mimi watu mpaka leo hawajua mwanamume wangu nani, kwa hiyo hata wewe naweza nikazunguka nawe wiki mbili halafu watasema ni wewe. Ali Kiba ni ndugu kabisa, ni mshikaji wangu na ndivyo ilivyokuwa tunazunguka naye sana. Ikumbuke kipindi kile nilikuwa nazunguna na Ali tayari nilikuwa mjamzito kwa hiyo kwa mantiki hiyo basi yule mtoto angekuwa wa Ali Kiba. Nimeambiwa watu wengi bwana angu hadi Dully Sykes wakati ni ndugu. Kipindi hata Nasibu (Diamond) anatoka tukawa tunazunguka naye kumsapoti, watu walisema tena ni bwanagu,” Queen Darleen aliambia EATV.

 

Barakah The Prince amsifu sana Diamond kuliko Ali Kiba akilinganisha mchango wao kwa muziki

Barakah The Prince anatambua kuwa Diamond and Ali Kiba ndo ndume katika ulingo wa muziki Tanzania. Lakini mwimbaji huyo amekiri kuwa Chibu Dangote ndo ndume kamili.

Barakah aliwataja wasanii watatu ambao wako na mchango mkubwa kwenye muziki; Diamond, Ali Kiba na Ommy Dimpoz.

Akiongea na Bongo 5, Barakah alimsifu sana Diamond ambaye alisema ameweka mfano mzuri wa kuigwa na wasanii wote nchini.

“Kwa mfano Bongo kwa mtu kama Ommy Dimpoz, Ommy ni package kabisa ya staa, Diamond ni package na Alikiba ni package iliyokabilika ambayo unaona kabisa huyu ni staa kakamilika. Kwa hiyo kwenye muonekano pia hususan mavazi na mwili lazima mtu uwe makini sana. Diamond ni miongoni mwa mtu ambaye anaowasanua sana watu kwenye vitu, nani alitegemea kama Diamond anaweza kuja na Chibu perfume? Hakuna mtu aliyetegemea, lakini jamaa kaka kafikiria watu wanapenda sana kunukia.

Baraka The Prince

“Nampongeza sana Diamond, ni mtu ambaye anatumia nafasi yake aliyopo sasa hivi vizuri. Kwa hiyo sitaki kusema kuwa watu wengi wanafanya kwa kuwa yeye kafanya, no lakini uyeye anaweza akawa anawapa watu mioyo ya kuthubutu. Unajua mtu mpaka kurizki na kuweka hela yake nyingi kwenye brand ya nguo au nini, ujue hapo umerizki na biashara ina mambo mawili, kuna kunyanyuka na kuna kuanguka.

“Mtu mpaka uweze kurizki lazima uone mfano kwa mtu, huwezi kurizki tu, kwa hiyo yeye ni miongoni mwa watu wanaowapa watu moyo na kuona kumbe kitu hiki unaweza kukifanya na kitu hiki na kikawezekana na tukabiga mitonyo na maisha yetu yakawa mazuri,” Barakah alisema.

 

 

Ali Kiba akiri kuwa Barakah The Prince ako na akili za kitoto

Wambeya wanasema kuwa urafiki baina ya Ali Kiba na Barakah The Prince unadidimia kwasababu ya bifu kati ya Baraka na Ommy Dimpoz.

Inasemekana kuwa ukaribu wa Dimpoz na Ali Kiba umechangia kuzorota kwa urafiki baina ya Kiba na Baraka kwasababu Dimpoz na Baraka hawali sahani moja kwa sasa.

Barakah The Prince na Ali Kiba

Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Ali Kiba alikiri kuwa Barakah The Prince ako na akili za kitoto ndio maana kuna maadhi ya mambo yanaibuka kwamba haelewani na baadhi ya wasanii wenzake.

“Mimi nadhani ni utoto tu, nadhani ni umri tu lakini Baraka yupo vizuri, ni mtu anayesikiliza na ana rekebishika. Muda mwingine labda umri ndio unampeleka lakini muda mwingine mtoto akifanya jambo unamwambia. Ni mdogo wetu tutamwelimisha na sidhani kama anamchukia Ommy Dimpoz labda ni maneno tu ya mtaani,” Ali Kiba alisema.

 

Ali Kiba atangazwa rasmi miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000

Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television ni kampuni inayojulikana dunia nzima kwa kutengeneza vipindi vya wanamuziki kutoka nchi mbalimbali na kuvisambaza katika vituo vya runinga vya kimataifa.

Ali Kiba, Lady Jaydee na Barakah The Prince ndo wasanii kutoka Tanzania ambao wamejiunga na Rockstar4000 Music Entertainment.

Ali Kiba amekua Rockstar4000 Music Entertainment kwa takribani miaka 6; usiku wa jana staa huyo alitangazwa rasmi miongoni mwa wamiliki wa kampuni hio.

Tofauti na kuwa miongoni mwa wamiliki wa Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television, Ali Kiba pia anakuwa Director of Music and Talents kwa kampuni hio.

 

Ali Kiba afunguka kuhusu mipango aliyonayo na lebo yake

Watu wengi ata hawajui kama Ali Kiba ako na lebo yake. Staa huyo ako na wasanii ambao amewasaini kwa lebo yake ambayo sio maarufu.

Wasafi inayomilikiwa na Diamond ndo lebo ambayo inajulikana sana Tanzania na ata nje ya nchi hii. La kushangaza ni kuwa Ali Kiba anamiliki lebo yake.

Akiongea na Mzazi Willy Tuva katika kipindi cha Mambo Mseto ya Citizen Radio, Ali Kiba alifunguka kuhusu lebo yake na mipango yake kuhusu lebo hio.

“Mimi nilisha kuwa na lebo muda mrefu sana, sema kazi zangu hazikuwa za matangazo kama hivyo. Ni muda mrefu nimeanza kufanya muziki na kusaidia watu sio leo, toka nipo katika game kabla sijapumzika nilikuwa na lebo yangu ya muziki lakini haikuwa inatangazwa. Sasa hivi kila kitu kipo kwenye utandawazi, kila mtu anatakiwa kujua Alikiba ana lebo na anafanya hivi na hivi.

“Nipo na wasanii ambao nimewasaini lakini bado sija watangaza wala kutoa kazi zao, tupo kwenye procsess za mwisho kwa sababu kila mtu kasharekodi nyimbo yake bado kushoot video ndio tuwatangazie watu,” Ali Kiba alifunguka baada ya kuulizwa kama angefungua lebo kama baadhi ya wasanii wengine wakubwa.

 

Picha 10 za mtoto wa Ali Kiba ambazo ni dhibitisho kuwa anang’ara kuliko wasanii wengi wa Bongo

Wasanii wengi Tanzania hawajaekeza katika muonekano wao wa kimavazi; Diamond Ali Kiba, Dogo Njanja ni miongoni mwa wasanii wa Bongo ambao wanajulikana kung’ara sana kimavazi.

Inaonekana Ali Kiba anamfunza mwanawe Prince Sameer Ali Kiba jinsi ya kung’ara. Prince Sameer tayari anavutia kwa mavazi yake ilhali yeye bado ni mchanga.

Tazama picha za Prince Sameer hapo chini:

Dully Sykes aeleza kwanini anaegemea upande wa Diamond badala ya Ali Kiba

Dully Sykes ameshawahi kushirikiana na Ali Kiba na Diamond kuachia nyimbo; ‘Kuteseka Nimechoka’ (na Ali Kiba) na ‘Utamu’ (na Dianond na Ommy Dimpoz).

Sykes pia amejaribu mara nyingi kuwapatanisha Diamond na Ali Kiba lakini kila mara alipojaribu juhudi zake ziliambulia patupu.

Dully Sykes na Diamond

Akiongea kwenye kipindi cha 180 Power cha Sibuka FM, Dully Sykes alifunguka na kusema kuwa anaegemea upande ya Diamond kuliko upande wa Ali Kiba.

Mwimbaji huyo alieleza kuwa upande wa Ali Kiba hawataki kuwa karibu lakini upande wa Diamond wanamuonyesha upendo

“Upande wa Alikiba hawataki kuwa karibu na mimi ila upande wa Diamond wapo karibu na mimi, sababu hao wapo karibu na mimi na wao wananionyesha upendo ndio maana nipo karibu nao na sina tatizo na Ali Kiba wala Diamond,” alisema Dully Sykes.

 

Jacqueline Wolper afunguka kuhusu mpenzi wake wa kitambo – Ali Kiba

Kabla ya Harmonize kuponyoka naye, Ali Kiba ndo alikua mpenzi wake muigizaji wa filamu za Bongo – Jacqueline Wolper.

Mbaka sahi Wolper anakumbuka mambo mazuri kuhusu ex wake Ali Kiba – muigizaji huyo hakuwa na mabaya ya kusema kuhusu Ali Kiba alipomuongelea kwenye mahojiano na gazeti la Amani.

Jacqueline Wolper

Mambo mawili anayoyapenda Wolper kuhusu Ali Kiba ni upole na unyenyekevu wa superstar huyo, vitu ambavyo Wolper anasema wanaume wengine aliyokutana nao hawana.

“Mengi nakumbuka, kikubwa ni upole wake pamoja na unyenyekevu. Ni tofauti na wanaume wengine ambao nimewahi kukutana nao,” muigizaji huyo ameliambia gazeti la Amani.

 

TIDAL – tovuti ya kuuza muziki inayomilikiwa na Jay Z yamsifu sana Ali Kiba

TIDAL inatambua Ali Kiba, Mtanzania huyo alisifiwa sana na tovuti hiyo ya kimataifa ambayo huuza muziki ya wasanii wanaotajika ulimwengu nzima.

TIDAL , ambayo inamilikiwa na Jay Z, ilimsifu Ali Kiba wakati akishiriki katika moja ya tamasha la muziki ambalo lilifanyika London nchini Uingereza wiki iliyopita.

Jay Z

“The unstoppable AliKiba is live right now in London” mtandao wa TIDAL uliandika wakati Alikiba akitumbuiza kwenye stage.

Wasanii wakubwa kama P Square, Davido, Awilo Logomba, Sarkodie, Cassper Nyovest na wengine pia walitumbuiza mashabiki katika tamasha hilo la muziki.

 

Shilole: Mimi namkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko Ali Kiba

Shilole ameeleza sababu ya kumkubali Diamond Platnumz kuliko Ali Kiba – wawili hao (Ali Kiba na Diamond) ni maadui wakubwa kimuziki.

Nani kati Diamond na Ali Kiba ndo mfalme wa muziki Tanzania? Mjadala huu huzua utata kila mara unapoulizwa. Mashabiki wa Diamond watasema Simba ndo anaweza na wale wa Ali Kiba watasema yeye ndo bingwa.

Zuwena Muhamed alimaarufu kama Shilole amesema yeye ni Team Diamond Platnumz. Akiongea kwenye kipindi cha Kikaangoni live kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, Shilole alisema yeye anamkubali sana Diamond.

“Mimi namkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko Alikiba, nampenda Diamond kutoka na mambo yake na vile alivyo, kwa hiyo kila mtu ana watu anaowakubali na kuwapenda” alisema Shilole.

Ruby amkana Ali Kiba

Hellen George maarufu kama Ruby amefunguka na kuweka wazi uhusiono wake na staa wa Bongofleva Ali Kiba. Uvumi mitendao ulikuwa unasema kuwa Ruby na Ali Kiba ni wapenzi.

Akiongea na Swaggaz, Ruby alisema hana ukaribu wowote na hit make huyo wa ‘Aje’. Mrembo huyo alisema hata hajawahi kuwa na mawasiliano na Kiba.

Ruby

Rubi alipuuza uvumi mitendaoni kuhusi uhusiano wake na Ali Kiba, alisema kuwa watu walishawahi sema yupo karibu sana na Diamond Platnumz .

“Na mimi taarifa hizo nimekuwa nikiziona kama wewe ulivyoziona, sioni jipya kwasababu walishawahi kusema kuwa nipo karibu sana na Diamond, sasa wamegeukia kwa Kiba ambaye hata mawasiliano yake sijawahi kuwa nayo,” Ruby alisema.

 

Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers amlenga Ali Kiba baada ya kumkosoa Babu Tale

Eric Shigongo, mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, alianza mgogoro na Wafasi alipodai kuwa Diamond anaingizwa shimoni na Naseeb Abdul, Babu Tale na Salaam.

Madai yake Shigongo yalimkera sana Babu Tale na kumlazimu kumwonya kutoingilia biashara yake na kuwachafulia jina wasanii wake.

Soma pia: Meneja wa Diamond Babu Tale amrarua mmiliki wa kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo

Mfanyabiashara huyo sasa amefunguka na kuamua kumshauri Alikiba kuhusiana na muziki wake na namna ambavyo anatakiwa kuishi kwa mipango ili hata siku asipokuwepo kwenye ramani ya muziki awe na maisha yenye tija kulingana na kazi alizofanya nyuma.

“Kwanza kabisa nianze kwa kukiri kuwa sikuwahi kukutana na Alikiba ana kwa ana mpaka miezi miwili iliyopita nikiwa katika Hotel ya Double Tree, iliyopo Masaki, Jijini Dar es salaam. Nilikwenda pale kwa ajili ya chakula cha mchana na mke wangu. Muda mfupi tu baada ya sisi kuingia walifika Alikiba na meneja wake Christine Mosha (Seven) wakaja moja kwa moja kwenye kona tuliyokaa na kutusalimia. Kitu cha kwanza nilichojifunza na kukipenda kwa Alikiba ni unyenyekevu, kijana huyu ni mnyenyekevu mnoooo! Kitu hiki peke yake ukiachana na muziki wake kilinifanya nimpende Kiba. Walipoondoka mimi na mke wangu wote tulikiri KIBA NI MNYEYEKEVU NA NDIYO SABABU AMEFANIKIWA SANA KATIKA MUZIKI.

Shigongo

“Alikiba, meneja wake na Watanzania wenzangu lazima mnisikilize hapa; MAFANIKIO MAISHANI HUJA NA KITU NYUMA YAKE, mara nyingi kitu hicho huwa kuwapuuza na kuwadharau waliokufikisha ulipo. Kuwatenga bila kufahamu hao ndiyo wanunuzi wa kazi zako ama wasikilizaji wa muziki wako na wakikuachia tu utatumbukia shimoni na huo ndiyo utakuwa mwisho wako. Ali kiba anapaswa kufahamu kwamba hawezi kuwa Champion for life, hata akiwa bora kiasi gani lazima siku moja atakuja mtu bora zaidi yake. Kabla ya Chris Brown alikuwepo Usher Raymond, kabla ya Rihanna alikuwepo Beyoncé, kabla ya Floyd Maywether alikuwepo Mike Tyson, kila zama na bingwa wake. Leo ni Kiba kesho atakuwa mwingine” alisema Shigongo.

Shigongo aelekeza mawaidha yake kutoka Diamond na kuipelekea Ali Kiba..hivi ndivo alivyo mshauri kuhusu wazazi wake

Mmamiliki wa Global publishers bado anaendelea kutoa mawaidha yake kwa wasanii wa Tanzania.

Alianza na Diamond ambapo alitukatanwa na mashabiki na sasa ako kwenye Ali Kiba ambapo alizungumzia mambo mengi mpaka ile ya kifamilia.

Hivi ndivyo alivyomweleza Ali Kiba:

1. ‘Detachment from fans’, hii ina maana ya kujitenga kutoka kwa mashabiki zake. Linaweza kuonekana kuwa jambo dogo lakini limekuwa likiwaangusha wanamuziki wengi duniani. Hili ni la kwanza ambalo anatakiwa kujiepusha nalo kama atataka kuwa juu kwa kipindi kirefu.
2. Ali ni mnyenyekevu, hataki makuu lakini kwa kazi yake ilivyo inambidi kidogo aongeze thamani, hapa nina maana kwamba Ali ajiepushe na suala la kusafiri bila meneja anapokuwa ndani au nje ya nchi kwenye shoo. Simaanishi kwamba hasafiri naye, hapana, namaanisha kwamba asifikirie kutokusafiri naye kwani hii huongeza thamani ya msanii anapoongozana na timu yake, hasa meneja au mameneja.

3. Asiyumbishwe na ushindani. Huu upo kote duniani na ndiyo maana ni rahisi kusikia Nicki Minaj anashindana na Iggy Azalea. Anachotakiwa ni kuweka chapa zake katika aina fulani ya muziki ili vizazi vijavyo viweze kumkumbuka kwa muziki wake fulani kama anavyojulikana Michael Jackson kwa muziki wa Pop.

4. Afanye sana kazi za kijamii. Hili linaonekana kuwa jambo dogo sana lakini unapoamua kufanya kazi za kijamii inakuweka karibu na mashabiki zako na pia unabarikiwa kulingana na kile unachokifanya.
5. Asiweke nguvu zake nyingi katika mambo yasiyokuwa na tija. Hili huwa linamfanya mwanamuziki kupotea haraka. Skendo hazikufanyi kusikika bali zinakufanya kupotea kwani mashabiki zako watakuwa wanahitaji muziki, hawahusikii inavyotakiwa, skendo zinakuwa nyingi kuliko kazi. Kiba amejulikana kwa sababu ya muziki, hajajulikana kwa sababu ya skendo, waliosikika kwa skendo acha wafanye skendo ila kama umejulikana kupitia muziki, fanya muziki.

6. Awasaidie wazazi wake kwa kila kitu. Wazazi ndiyo nguzo muhimu sana hapa duniani. Unaweza kuona unafanikiwa lakini unapomwacha mzazi ni lazima kutakuwa na vitu vibaya vitatokea, huwezi kuviona sasa hivi, kuna siku ukishaanza kushuka, kuna sauti moja ya upole itasikika moyoni mwako, itakwambia kwamba tatizo halikuwa kukosa thamani, halikuwa kukosa mapromota, tatizo kubwa lilikuwa ni mama au baba kwani Mungu aliwachagua hao wawe wazazi wako kwa makusudi yake.

7. Nilipokutana na Seven na kuzungumza naye, nilibahatika kumwambia kuhusu gharama kubwa, kwa unyenyekevu mwingi, alikiri kuwepo kitu hicho na ndiyo maana shoo zake si nyingi sana nyumbani. Namnukuu Seven: “Ni kweli Eric, gharama zipo juu lakini ndivyo tunavyotoza hata huko nje. Ili kidogo tufanye shoo za kutosha hapa nyumbani, basi wadhamini wajitokeze wengi japo na sisi gharama zishuke kwa kuwa wakijitokeza wengi, na sisi tutaingiza kingi hivyo hata malipo yatakuwa madogo. Kama akija mdhamini mmoja, inajulikana kwamba lazima shoo iwe ya gharama sana. Lakini mbali na hilo Eric, naandaa kufanya shoo za hisani mara kwa mara ili kuisaidia jamii kwani naamini itamfanya Ali kuwa karibu na mashabiki zake.”

Aliendelea kuongea kwamba malipo ya nyumbani yana kila sababu ya kushushwa kwa kuwa Tanzania ipo chini kiuchumi, si kama Afrika Kusini au nchi za Ulaya. Mashabiki watuelewe tu kwamba tunajua kwamba wanatofautiana kifedha, hatuwezi kuwatenga kwa kuwa wote ni mashabiki zetu, tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha shoo zinamfikia kila mtu,” alimalizia Seven.

Diamond amrai Ali Kiba kuweka muziki wake wasafi.com

Akiongea kwenye mahojiano ya kipindi cha 360 cha Clouds FM, Diamond Platnumz alikiri kwamba hana tatizo na Ali Kiba. Diamond na Kiba wamekuwa na beef zito sana kwa takribani miaka mitatu.

Diamond aliambia Clouds FM kwamba anaheshimu Ali Kiba, alifunguka na kusema kwamba uongozi wake uko katika mazungumzo na uongozi wa Ali Kiba ili Kiba aweze kuuza nyimbo zake kwenye mtandao wa wasafidotcom ambao ni mradi mpya wa Diamond.

Ali Kiba and Diamond TBT

Baadaye usiku kupitia akaunti yake ya Instagram, Ali Kiba aliandika caption zenye utata zilizotafsiriwa na mashabiki na wadau mbalimbali kuwa zimelenga kujibu maneno hayo ya Diamond Platnumz.

“Waambie Wasituzoee kabisa MAZOEA kuzoeana ?? @billnass #alikibaworldtour2k17 #KingKiba,” Ali Kiba aliandika.

Watu wengi wanaamini kwamba Diamond anahitaji amani na Ali Kiba kwasababu za kibiashara zaidi. Iwapo Ali Kiba atakubali kuuza wimbo zake wasafi.com, Diamond atafaidika zaidi kwasababu Ali Kiba ako na wafwasi wengi.

 

Picha 7 za dadake Ali Kiba zinazoonyesha urembo wake ata akivaa buibui

Watu wengi wanamfahamu Ali Kiba and ndugu yake Abdu Kiba, lakini wengi hawatambui kwamba superstar huyu wa Bongo fleva ako na dada.

Ali Kiba na Abdu Kiba wote ni waimbaji lakini dada yao, Zabibu, si msanii. Zabibu ameonekana na ndugu yake Ali Kiba mara mingi wakiwa pamoja wakihuduria shuguli tofauti tofauti.

Ingiwa Zabibu huvaa mavazi za kisasa, mwana dada huyo pia huvaa buibui. Na ata akivaa mavazi yake ya kidini bado urembo wake huonekana tu.

Tazama picha zilizo chini: