Diamond Akiri Kumkubali Mrisho Mpoto Kwa Staili Yake Mpya

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemvulia kofia  na kuonyesha kumkubali Msanii Mrisho Mpoto baada Ya staili yake aliyotumia kuimba wimbo alioshirikishwa na Harmonize unaoitwa Nimwage Radhi

Msanii Mrisho Mpoto ameshazoeleka kwa staili yake moja ya uimbaji aliyoitumia Kwenye nyimbo zake maarufu kama Mjomba, Zisonje na Njoo Uzichukue na nyinginezo.

Lakini Kwenye Wimbo Mpya alioshirikishwa na Harmonize ambao sasahivi unafanya vizuri sana Nimwage Radhi Mpoto amekuja kwa staili nyingine kabisa ya kuimba na kuwafurahisha watu wengi ikiwemo Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameshindwa kujizuia na kumwagia sifa Mrisho Mpoto ambapo ameandika:

Kwa kweli Mrisho Mpoto nilikuwa nakuwaza sana, Kwa ufanisi wa serikali hii, ungewezaje kutupa vile vibao vyako vya #MJOMBA #WAITE Na Kadharika…. ila nimeamini kweli Mungu kakutunuku Kipaji na Ubunifu wa Sanaa, Sikutegemea kama UtaniSurprise namna hii… #NimwageRadhi Kali sana?? ….Mdogo angu Mmakonde @harmonize_tz naona Mwaka Huu unahasira nao sana….Kama Naiona hiyo #WasafiFestival Huu Mwaka Sjui hata tuanzie Mkoa gani???,” aliandika Diamond Instagram“.

Wimbo huo umekuwa ukifanya vizuri na kushika chati katika vituo mbali mbali vya habari na hata kushika nafasi za juu katika mtandao wa Youtube.

Mch. Lusekelo-Nampenda Diamond ni Mnyenyekevu, Simpendi Alikiba ni Jeuri

Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC) mchungaji maarufu kama Mzee wa Upako ameetaja Diamond kama msanii anayemkubali.

Mch. Lusekelo amefunguka kwenye kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm ambapo ameweka wazi kuwa anampenda Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu lakini hampendi Ali Kiba kwa sababu ni mjeuri.

Mimi nampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, Simpendi Alikiba kwa sababu ana kiburi, nadhani kwa sababu amekaa Kariakoo”.

Lakini pia Mchungaji huyo hakuishia hapo aliongeza kwa kumsifia Diamond kuwa unyenyekevu wake ndio unamfikisha mbali:

Ukipigia simu Diamond anapokea kwa unyenyekevu ila Alikiba anapokea kwa maringo. Ndio maana Diamond amefika mbali.”

Wasanii hawa wawili wakali wa Bongo fleva wamekuwa wakishindanishwa kwa muda mrefu sana hali iliyosababisha wawili hao kuwa na bifu fulani hivi.

 

Diamond Platnumz: Sina Mpango wa Kuwa Mwanamuziki Milele

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuwa Mwanamuziki maisha yake yote bali ana nia ya kuwa mfanyabiashara hapo baadae.

Diamond ameweka wazi kuwa sio rahisi kwa yeye kuweza kuimba maisha yake yote bali anaamini kuwa kuna kipindi Kitafika atatakiwa kuweka mziki pembeni na Mpango wake ni kuwa mfanyabiashara.

Diamond alifunguka hayo kwenye hafla ya Wasafi Tv iliyofanyika siku chache zilizopita wakati wakizindua kipindi kipya cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo amekiri kuwa muziki ni njia yake ya kujipatia mtaji:

Kazi tunayoifanya sio kwamba Mwenyenzi Mungu anaipenda, kiuhalali haipo hivyo, hivyo tujitahidi kutenda matendo mengi mazuri, tutumie muziki katika njia nzuri.

Mimi vision yangu ni kuwa mfanyabiashara, sina ndoto ya kuimba milele, huwezi kuimba milele, kwa hiyo natumia muziki kesho na keshokutwa iwe ni chanzo cha biashara zangu nyingine na namshukuru Mwenyenzi Mungu siku zinavyozidi kwenda anazidi kunibariki”.

Diamond ni moja kati ya wasanii Tanzania ambaye alifanya mapinduzi makubwa Kwenye sekta ya burudani kwani amefanikiwa kuwa mfanyabiashara mkubwa kuanzia muziki wake lakini pia bidhaa zake kama Diamond Karanga na Chibu Perfume na sasa hivi Wasafi Tv.

Mameneja Wa Diamond Wadaiwa Kuhusika na Kusambaza Video Ya Ngono Ya Nandy

Kama utakumbuka mwezi uliopita jiji zima lilizizima baada ya video ya ngono iliyomuhusisha msanii wa Bongo fleva Nandy na Billnas kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha skendo kubwa kwa wasanii hao.

Chanzo cha video hiyo hakikujulikana kwa sababu Nandy na Billnas wote walikataa kuhusika na kusambazwa kwa video hiyo lakini aliyeiweka video hiyo Mtandaoni ni kurasa ya Udaku inayojulikana kama UdakuTz.

Sasa tangu wikiendi iliyopita kuna taarifa zilizodai kuwa mmiliki wa kurasa hiyo ya udaku ametekwa na watu wasiojulikana kwani familia yake haijui alipo, mpaka jana ambapo ilidaiwa alichukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano juu ya kuvuja wa  video ile ya Nandy na Billnas.

Lakini taarifa iliyotolewa jana na mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown ni kuwa mmiliki wa kurasa hiyo yupo kituo cha polisi na Kwenye mahojiano hayo amewataja watu waliompa video hiyo avujishe ambao walikuwa ni mameneja wa Diamond ambao mi Salaam SK na Babu Tale.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Soudy Brown aliweka posti hii:

Mpaka sasa haijajulikana kama Watajwa hapo juu  ambao wote ni mameneja wa Diamond wameshatiwa mbaroni au bado.

Lakini pia haijawekwa wazi ni vipi Msanii Diamond anahusika vipi katika hilo lakini yote hii inarudi katika bifu la Diamond na Clouds Media.

Wasafi Tv Wazindua Kipindi Cha Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani (+picha)

Kituo cha televisheni cha Wasafi Tv kinachomilikiwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, siku ya jana kimetangaza ujio wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Siku ya jana Wasafi Tv walifanya uzinduzi wa kipindi hiko kitakachoitwa Nyumba ya Imani ambacho kitakuwa maalumu kabisa kwa waislamu wote katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kitakachorushwa Wasafi Tv.

Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Wasafi Tv Mbezi beach na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali walioalikwa kwa ajili ya kupata futari.

Hizi ni baadhi ya picha za hafla hiyo:

 

Harmonize- Wanaume Waaminifu Africa Wanatoka WCB

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize amefunguka na kudai kuwa wanaume waaminifu kutoka Africa Mashariki wanatoka WCB.

Kwa mara ya kwanza kauli  kama hiyo ilitolewa na mmoja kati ya mameneja wa WCB, Babu Tale mapema mwaka jana ambapo ilipingwa na watu kadhaa ikiwemo Aunty Ezekiel.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia Mambo Mseto, Citizen Radio kuwa kitu hicho ni cha kweli kabisa na uamifu wao umevuka mipaka, sio Bongo tu.

Ni kweli kabisa asilimia mia moja, hamna matukio halafu sisi ndio tunangoza kwa kusalitiwa“.

Kauli hii Inawaacha hoi watu wengi kwa sababu karibia wasanii wote WCB wanakabiliwa na skendo za kuchepuka kuanzia tu na CEO mwenyewe Diamond Platnumz ambaye skendo yake ya kuchepuka na Hamisa wakati yupo na Zari ilitrngeneza headlines.

Mama Diamond Athibitisha Kumpa Kipigo Cha Mbwa Mwizi Hamisa Mobetto

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra au maarufu kama Mara Diamond amethibitisha kumpa kipigo cha mbwa mwizi mkwe wake Hamisa Mobetto.

Mwanzoni mwa wiki hii kuna stori ilisambaa kuwa Mama Diamond kampa kipigo kizito Hamisa baada ya Kumekuwa nyumbani kwa Diamond Madale hadi kuacha wigi lake.

Mama Diamond amethibitisha habari hizo kwenye mahojiano aliyofanya na Globa Publishers ambapo ameweka wazi kuwa hampendi na hataki hata kumuona nyumbani kwake:

Ni kweli nilimpiga na wigi nikamvua na hayo  mambo ya kumfuata mzazi mwenzie ni huko, pale Madale ni kwangu na simtaki nyumbani kwangu kabisa.

Mama Diamond aliulizwa sababu gani hasa ilimfanya amchukie Mobetto na alifunguka haya:

Kitendo cha kuniitia mimi Shilawadu (kipindi cha udaku cha Televisheni ya Clouds) kilinikera sana halafu nikaanza kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini pia Mama Diamond aliweka wazi kuwa baada ya kumtembezea kipigo Hamisa alimvua wigi ndipo Diamond alikuja kumuamulia:

Mama Diamond ameweka wazi hamtaki Mobetto na  kama mwanaye atakuwa na Mahusiano naye basi hawataelewana:

Kwanza tu siyo mwanamke wa kuoa (wife material) hajui kutandika hata kitanda wala kufanya tu usafi ni shida.

Yaani atajua yeye mwenyewe maana mimi ndiyo nimemzaa Diamond na siyo yeye sasa sijui nani ana nguvu hapo.

Siwezi kukanyaga kwenye  harusi yao hata siku moja watasherekea wenyewe”.

Mama Diamond ameweka wazi kuwa anataka Mwanayr amletee mwanamke mwingine anayejiheshimu na sio Mobetto.

Hatimaye Diamond Amuweka Mtoto Wake na Hamisa Mtandaoni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz anayefanya vizuri na kibao chake cha kwangwaru ametengeneza gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha ya mtoto wake na Hamisa.

Hatimaye kwa mara ya kwanza Diamond ameposti picha ya kwanza ya mtoto wake Dylan ambaye amezaa na Hamisa.

Tangu Dylan azaliwe kulikuwa na mgogoro kati ya Diamond na Hamisa hii ilitokana na Hamisa kuanika video na picha zao za faragha Wakati huo Diamond alikuwepo na Ex wake Zari.

Tangu hapo kilichofuata kilikuwa ni kurushiana vijembe Mtandaoni na kupelekana mahakamani na hata Hamisa alisema kuwa Diamond alikuwa hataki kumuona mwanaye na hata kumuhudumia.

Lakini tangu taarifa za Diamond na Hamisa kurudiana zienee inaelekea mambo yamekuwa tofauti kwani Diamond amesemekana hata kumuona mtoto wake na hata jana kwa mara ya kwanza aliweza kumposti mtoto wake Kwenye ukurasa wake wa Snapchat:

 

Esma- Wema Ndio Ana Mapenzi Ya Kweli Alimpenda Naseeb Sio Diamond

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amemwagia sifa kibao aliyekuwa wifi yake Wema Sepetu kwa kudai ndio mwanamke aliyempenda kweli Diamond.

Kama utakumbuka Wema na Diamond walikuwa wapenzi kwa muda mrefu tangu Wema alipokuwa Miss Tanzania kwa kipindi hiko Diamond alikuwa ndio anaanza muziki.

 

Esma alianza kwa kumposti  Wema na  kuanza kumsifia kuwa amependeza na mavazi yake ya kinigeria ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka posti:

Baada ya posti hiyo kuzua gumzo baada ya Esma kuendelea kuitana wifi na Wema hata baada ya Wema kuachana na kaka yake Diamond, na Esma alifunga kazi kwa kumwagia sifa Wema huku akikiri yeye ndio wifi aliyempenda kweli Diamond kwani alianza naye mapenzi wakati hana kitu mpaka leo staa.

Wema uwifi hauishi leo wee ndio forever wiii wa kihistoria mtoto wa watu unajua kuishi ulimpenda Naseeb na sio Diamond”.

 

Pamoja na kwamba Wema aliachana na Diamond muda mrefu uliopita lakini amekuwa bado karibu sana na familia yao.

Baba Diamond Amsifu Mama Diamond Kwa Hili

Baba mzazi wa Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ Mzee Adul Juma amemwagia sifa kibao mzazi mwenzake Mama Diamond baada ya kumuanika Kwenye mtandao wa Instagram.

Global Publishers wanaripoti kuwa wazazi Diamond wapo katika nafasi nzuri hivi sasa baada ya kuwepo kwa sintofahamu baina yao kwa kipindi kirefu.

Mzee Abdul aliingia kwenye bifu zito na Diamond baada ya kumtuhumu kutomjali kwa sababu tu ana ugomvi na mama yake mzazi, (Bi Sandra) hali iliyosababisha staa huyo kumchunia kwa muda mrefu.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu huku kila mmoja akikwepa kumzungumzia mwenzake kwa vyovyote, juzikati Bi Sandra alionesha ‘kusanda’ kwa kuamua kumuanika mzee Abdul mitandaoni.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Bi Sandra, aliweka picha ya muda mrefu ya mzee Abdul akiwa amembeba Diamond alipokuwa mdogo, kitendo kilichofanya komenti kibao kujazana katika ukurasa huo.

Nasibu kichwa na mzee Abdul…namuona Nillan Mtupu”.

Lakini pia gazeti hilo lilipomsaka Baba Diamond alifunguka na kuonyesha kufurahishwa kwa kitendo hiko na kumwagia sifa Mama Diamond:

Kama mama Diamond kafanya hivyo, basi ujue mimi ni mzazi mwenzake, Diamond tumemlea, tumeishi naye kwa muda mrefu na hayo masuala mengine yaliotokea kipindi cha katikati ni ya kifamilia tu na naimani ni mapito“.

 

Hamisa Mobetto Awajia Juu Watu Wanaombeza Kisa Amezaa na Wanaume Wenye Hela

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Haida Mobetto amewajia juu watu wanaombeza baada ya kusema kuwa yeye sio Single mothers.

Siku ya juzi ilikuwa ni Mother’s Day/ siku ya Mama duniani na Hamisa aliweka wazi kuwa yeye sio Single mother kwa sababu anasaidiwa kulea watoto wake na Baba watoto wake.

Hamisa ana watoto wawili ambapo mtoto wake wa kwanza Fantansy amezaa na Majizzo na mtoto wake wa pili Dylan amezaaa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Lakini baada ya video hiyo kuingia mtandaoni watu walianza kumsema vibaya kutokana na yeye kuongelea suala lake la kuzaa na wanaume wawili tofauti ambao wote ameweka wazi wana uwezo.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Hamisa altoa povu hili:

Mnatakiwa mjua kwamba Fancy na Dee Mungu ndo alipanga wazazi wa hawa watoto wawe nani..hasira zenu please msinimalizie mie mtoto wa marehemu Mzee hassan..Its getting boring now.”

 

 

 

 

Diamond Asisitiza Kuwa Nillan Ni Mtoto Wake Sio Wa Ivan

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kuuanika ukweli wazi kabisa kuwa Nillan ni mtoto wake na sio mtoto wa Marehemu Ivan Semwanga kama wengi wanavyodai.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi zinazodai kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond ambapo ilidaiwa kuwa Zari alichepuka na Ivan kipindi yuko na Diamond ndio akamzaa Nillan.

Diamond ameamua kuzima kabisa tetesi hizo na kuanika kuwa Nillan ni mtoto wake na kuwataka mashabiki wasilete uchonganishi Kwenye familia yake hasa kwa wanaye.

Siku ya jana Mama Diamond aliposti picha ya Baba Diamond akiwa amembeba Diamond wakati mdogo na Diamond alikomenti kwenye picha hiyo kuwa anataka aonganishe picha hiyo na ya Nillan ili watu waone jinsi walivyofanana na kuacha kusema yule sio mtoto wake.

 

Dah hii picha nilikuwa naitafuta sana…kuna picha moja nimembeba Nillan kama hivyo nilikuwa nazimix niwawekee maboya wanaokazana kusema Nillan sio mwanangu…mxiew”.

Lakini pia Diamond alimtolea povu zito shabiki na kumta asimgombanishe na watoto wake:

Usiniletee uchanganishi na matimu yenu kwa wanangu…watoto wote ni wangu Tiffah, Nillan, Dylan… hivyo yaani”.

 

Waziri Mwakyembe Azidi Kumfagilia Diamond

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezidi kumfagilia staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kudai kuwa yupo Kwenye listi ya wasanii 10 duniani wenye Sauti nzuri.

Mwakyembe amesema hayo kwenye mahojiano yake na kipindi cha KAA HAPA cha Mrisho Mpoto na kueleza kuwa Diamond kwenye video zake hana haja ya kutumia picha za ajabu ajabu kwani sauti yake ni dhahabu inajiuza.

“Kwenye tasnia yetu ya sanaa  vijana wetu  nyimbo nzuri sana, wana vipaji vya hali ya juu. kinacholeta matatizo hapa ni  picha ambazo haziendani na maadili yetu, kuchanganya na utupu ndani yake hivi vitu kwa kweli wafanye wengine lakini sio hapa. Tuchukulie kijana kama Diamond sauti yeke pekee yake inatosha kabisa kumuuza. Ukisema wasanii 10 duniani tuwe wakweli tuu! wenye sauti nzuri, Diamond huwezi kumtoa pale. Lakini huitaji kuuza ukaongeza na picha za ajabu ajabu wanaofanya hivyo ni wale wenye mapungufu ili kuficha ma’flat flat kwenye nyimbo zao Diamond yeye haitaji kufanya hivyo”.

Suala hili limekuja baada ya serikali kuingilia kati kazi za wasanii mbali mbali na hata kufungia baadhi ya wasanii kama Roma Mkatoliki na baadae kumfungulia.

Waziri Mwakyembe amesisitiza kuwa serikali haina ugomvi wowote na wasanii bali wapo katika jitihada za kulinda maadili ya nchi yetu.

 

Nandy Amnyooshea Mikono Ali Kiba Akiri Kumkubali

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT Nandy amekiri kuwa pamoja na mambo mengine yote na maneno yakiwekwa pembeni staa wa Bongo fleva Ali Kiba amemu-insipire sana kwa kinywaji chake.

Nandy amekiri kuwa hatua aliyofikia Ali Kiba ya kuingiza kinywaji chake mtaani ambayo ni Energy drink ni hatua kubwa sana ambayo imempa changamoto hata yeye ya kufanya makubwa zaidi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na The Playlist ya Times, Nandy amekiri kuwa kupitia Kiba ni vizuri wasanii wengi wakajifunza kuwa ni vizuri kuwekeza nje ya muziki.

Ameni-inspire kwa kinywaji kwa sababu ukiangalia the package ya kinywaji chake jinsi ilivyo ni project fulani ambayo ipo serious”.

Lakini pia Nandy ameongelea uwekezaji wa wasanii wengine kama Diamond Platnumz ambaye ni mmoja kati ya msanii Lakini pia mfanyabiashara.

Tunaambiwa nje ya kuimba tunatakiwa tuwekeze nje ya muziki wetu na ndicho hiki kaka zetu wanafanya ukimuangalia kama Diamond, Alikiba ni vitu ambavyo wanatuhamasisha”.

Kwa hivi sasa Nandy anafanya vizuri sana ngoma yake ya Ninogeshe inayoshika namba moja kwenye mtandao wa Youtube.

Tunda- Sina Bifu na Hamisa

Video vixen maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Tunda Sebastian ameibuka na kuweka wazi kuwa hana bifu lolote na Hamisa Mobetto na wala hajawahi kugombana naye.

Tunda na Hamisa walisemekana lies Kwenye bifu zito siku za nyuma na ikidaiwa kisa kilikuwa ni penzi la staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Inajulikana wazi kuwa Hamisa ana uhusiano na Diamond na hata kuzaa naye mtoto mmoja lakini hapo nyuma ilishasemekana kuwa Tunda alikuwa ana uhusiano na Diamond kwa muda mrefu.

Kuwepo kwa bifu hilo kulithibitika baada ya Tunda kutumia mtandao wa kijamii kumfikishia Ujumbe Hamisa Miezi kadhaa iliyopita na kusema kuwa Diamond hamtaki lakini anajipendekeza.

Lakini pia siku zilizopita Tunda alimpiga Dongo Zito Hamisa baada ya kusikia karudisha majeshi kwa Diamond ambapo alidai ni mjinga kwa kurudiana na Diamond.

Siku ya juzi Tunda kawatolea povu zito watu walioandika stori kuwa yeye na Hamisa wana bifu ambapo amedai kuwa hana ugomvi wowote na Hamisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tunda aliandika ujumbe huu huku akisisitiza kuwa hana bifu na Hamisa:

Hamisa hajawahi kujibu tuhuma zozote na Tunda na hata kumrushia maneno Kwenye mitandao ya kijamii.

Diamond Atangaza Kuja na Reality Show Ya Maisha Ya WCB

Staa wa Muziki wa Bongo fleva na CEO wa label ya WCB m, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa reality show kitakachoonyesha maisha halisi ya Label yake ya WCB.

Diamond ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa habari hiyo njema kwenda kwa mashabiki zake.

Kipindi hiko ambacho kitaonyesha maisha halisi ya kundi Zima la WCB kinatarajiwa kurushwa Wasafi Tv hapo siku za mbeleni.

Diamond alitoa taarifa hiyo alipokuwa njiani kuelekea nchini Uingereza ambapo anaenda kupiga shoo yake ya ‘A boy From Tandale’ ambapo aliandika:

Moja ya kitu ambacho nakisubiri kwa hamu ni ndani ya Wasafi Tv ni reality show ya WCB Wasafi…..wacha wamalize kutest signal zao wamwage maji tuoge kama kambale…. Na mnatujuaga siye hatujui kuficha yote mtayaona”.