Mfahamu Mmiliki wa Wasafi tv na Muandaaji wa Wasafi Festival

Mara  nyingi watu wamekuwa wakijiuliza hasa kutokana na taarifa zinazosambaa katika itadano kuhusu umiliki wa televisheni ya Wasafi Festival ambayo haina muda mrefu tangu kuanza kufanya kazi.

Basi katika moja ya magazeti ya kuaminika gazeti la Mwananchi linatoa tarifa kuwa wasafi tv imekuwa na hisaya watu watatu tofauti ambapo, mmoja wapo ni Juhayna Zughalulu 53%, Diamond Platinumz 43% na  Ali khatib dai 2%.

Hivyo basi mwenye hisa kubwa ndio mmmilkki halali wa kampuni hiyo ambae ni juhayna zughalulu, je juhayna ni nani? hilo ni swali la kujiuliza lakini rudi katika kumbukumbu zako na utajua hayo yote.

Juhayna ni mke halali kabisa wa bwana joseph kusaga ambae ni mmiliki mwenzi wa clouds media , hivyo basi kumbe hata wasafi tv ina mkono wa clouds media.

hivyo basi hata kwa kuangalia , utakuja kujua kuwa kuna muingiliano mkubwa kati ya wasafi tv na clouds media, alkini pia maswali yanazidi kutanda kwa mashabiki kuwa kma wawili hawa wana muingiliano kwanini basi kunakuwa na ushindani kati ya wasafi na clouds ?haa nibaadhi ya maswali ya kujiuza lakini yanakosa majibu kwa sababu kama kweli wawili hawa wanataka kufanya kazi ya kuleta burudani basi walitakiwa kuingiliana na kufanya kazi pamoja ili kufanikisha lengo lao.

 

 

 

 

 

Wasafi Tv Wazindua Kipindi Cha Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani (+picha)

Kituo cha televisheni cha Wasafi Tv kinachomilikiwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, siku ya jana kimetangaza ujio wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Siku ya jana Wasafi Tv walifanya uzinduzi wa kipindi hiko kitakachoitwa Nyumba ya Imani ambacho kitakuwa maalumu kabisa kwa waislamu wote katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kitakachorushwa Wasafi Tv.

Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Wasafi Tv Mbezi beach na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali walioalikwa kwa ajili ya kupata futari.

Hizi ni baadhi ya picha za hafla hiyo:

 

Tumeteswa Sana na Media Nyingine, Asante WASAFI Tv Kwa Kuleta Usawa-Nikki Mbishi

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap kuchana Nikki Mbishi ameibuka na kuimwagia sifa lukuki Wasafi Tv baada ya kupiga nyimbo yake.

Nikki Mbishi amefunguka na kudai kuwa amefurahishwa na mwanzo mzuri wa Wasafi Tv kwani imeonekana kupiga nyimbo za wasanii mbali mbali bila ubaguzi wala upendeleo wowote.

Nikki Mbishi amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika waraka huu kuisifia Wasafi Tv:

Asante Wasafi TV nyie mmecheza wimbo wangu #NIMEKUMISS bila hata mimi kuwaletea, najua ndio mnaanza ila msisahau kuendelea hivi hivi. Hakuna kitu kinachojenga na kuimarisha misingi ya sanaa kama ushindani wenye usawa “Fair Competition” hii inamaanisha anayestahili na apate na asiyestahili akose japo fitna zipo tu.

Tumeshuhudia umwinyi na ubeberu kwa kipindi kirefu sana,wapo ambao walitaka uMungu mtu lakini walijishtukia wakabwaga na wengine walibwagwa na hiyo ni kwa sababu ya kuleta umatabaka wa kanda fulani na kanda fulani na kujuanajuana sana kiasi kwamba akina sisi tusiofungamana nao tukaishia kutengwa na kuonekana “VINEGA” Kila la kheri kwenye hii ligi ya mbuzi kuna siku daraja litapanda tutacheza ya ng’ombe na mpaka tembo nini simba. Ipo siku watajihoji na kujijibu wenyewe“.

Wasafi Tv imeonekana kupiga nyimbo ambazo ni za wasanii ambao ni wazi kabisa wana bifu na Diamond kama vile Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Lady JD, Nay wa Mitego na wengineo.