TID Amtupia Dongo Diamond Kwa Kujiita Simba

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kwa Jina la usanii kama Top In Dar (TID) amedai yeye ndiye mwanzilishi wa jina la mnyama.

Hivi siku za karibuni kumekuwa na ugomvi wa marina baina ya wasanii kama juzi tu Afande Sele kamaliza mgogoro na Diamond kisa jina la Simba ambalo kila moja alidai la kwake.

TID ameibuka na kudai yeye ndiye mwanzilishia wa kutumia jina la Simba na hata kudai jina hilo alipewa na mashabiki zake kwa sababu ya kazi zake anazofanya akiwa stejini.

Kwenye mahojiano na kipichi cha On The Street cha ETV, TID amefunguka haya kuhusu jina hilo la mnyama:

Kwa mfano mimi perfomance zangu wanasema ni kali, yaani za kinyama, kwahiyo mimi nilikuwa nafanya kinyama ndipo mashabiki walipo amua kunipa jina la mnyama, mpaka sasa mimi ni mnyama kutoka unyamani.

Lakini sio mbaya sasa hivi nasikia kuna wengine wanajiita Simba, nimewa-inspire kuwa hivyo, kuna wengine ni wakufungwa, lakini ndio mnyama wenyewe”.

TID hana uhusiano Mzuri na WCB kwa ujumla kwani wiki chache tu zilizopita alitoka kutoa povu kwa Wasafi baada ya kudaiwa alikuwa anaomba kazi.

Diamond Amwagia Sifa Kibao Vanessa Mdee

Msanii wa bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameibuka na kumwagia sifa kibao msanii mwenzake Vanessa Mdee na kudai ni mpambanaji sana.

Diamond alifunguka hayo baada ya Vanessa kuwekwa na Wasafi Tv kama Women Crush Wednesday ambapo walimshukiru mchango wake katika Bongo fleva.

Diamond aliandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alifunguka kwa kumtumia ujumbe huu wa shukrani Vanessa:

Vanessa ni moja kati ya waaanii wa kike Kwenye Bongo fleva anayefanya vizuri sana kitaifa na kimataifa na hata albamu yake ya Money Mondays aliyotoa mapema mwaka huu bado inafanya vyema.

Najua Tabia Za Diamond Nikiwa Naye Atanisumbua Sana- Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu kwa mara nyingine amejibu tetesi zilizozagaa kuwa amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Tetesi za Wema kurudiana na Diamond zilianza kuapmba moto Miezi michache iliyopita baada ya Zari kutangaza kuwa alimuacha Diamond baada ya kumuona amekumbatiana na Wema huku akidai wamerudiana Tena.

Lakini Wema siku zote amekuwa akikataa tetesi hizo na kusisitiza kuwa Diamond ni rafiki yake wa karibu tu. Lakini Siku mbili hizi imedaiwa Wema alibeba ujauzito wa Diamond jambo ambalo amelikataa na kusema tayari ana mpenzi wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Wema ameweka wazi kuwa hawezi kurudiana na Diamond kwani anajua tabia zake lakini pia amesema hata akitaka kumuoa hawezi kukubali:

Yaani Diamond, hata aache kila kitu akaniambia sasa Wema nataka kukuoa sitakubali kabisa Alafu nilimpenda zamani, lakini siyo sasa kwa sababu Nasibu nimekaa naye miaka miwili. Najua alivyo na hatanisumbua sana kwa sababu mimi nilimwacha CK kwa ajili yake, matokeo yake akatoka na Meninah (msanii wa Bongo Fleva) na meseji nilizibamba. Kwa hiyo hata kwenye ndoa hawezi kubadilika.

Lakini pia Wema amejitetea kuhusu suala la yeye kuonekana anaenda nyumbani kwa Diamond Madale ni jambo la kawaida kwani alienda kwenye swimming party aliulizwa tu na Diamond kama rafiki yake.

Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Mimba Iliyotoka Na Muhusika Wa Mimba Hiyo

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka kuhusu janga lilompata hivi katibuni baada ya kuweka wazi kuwa mimba aliyokuwa amebeba kwa mara ya pili imetoka Tena.

Wema amekuwa muwazi sana juu ya kipindi kigumu  akijaribu kutafuta mtoto kwani sio mara ya kwanza kwa Wema kuweka wazi kuwa amepata miscarriage kwani miaka michache iliyopita mimba yake na Idris Sultan ilichoropoka.

Wiki iliyopita Wema Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka wazi machungu yake baada ya kuandika kuwa kwa mara ya pili mimba aliyokuwa amebeba imetoka tena.

Mara moja baada ya habari hizo kusambaaa tetesi nazo zilianza kutembea kuwa muhusika wa mimba hiyo hakuwa mwingine bali ni staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye alisemekana kuwa na Mahusiano naye.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Wema amekataa tetesi hizo na kudai Diamond hakuwa muhusika wa mimba hiyo kabisa na kumtaja mwanaume mwingine:

Hakuna ukweli wowote, ni ya mtu mwingine kabisa Diamond ni Hakuna lolote ila ni mshkaji wangu ambaye si unajua tumezoeana sana!”.

Lakini pia Wema aliweka wazi kuwa mimba yake iitoka muda mrefu uliopita ila aliweka wazi wiki iliyopita:

Kusema ukweli hiyo mimba imetoka karibia mwezi na nusu hivi umepita lakini kilichotokea Mimi niliweka picha moja ya mwanamke mwenye tatizo kama langu la kushika mimba kisha inatoka ndipo nikaandika; ‘My Life Story’.  

Hapo ndipo watu walichukulia kama nimepatwa na janga hilo kwa wakati huu, lakini ukweli ni jambo lililonipata mwezi na nusu uliopita“.

 

Mkubwa Fela- Wanaopenda Kuona Diamond na Ali Kiba Wana Ugomvi Wameumbuka

Sio jambo la siri kuwa Wasanii wakubwa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Ali Kiba hawaivi chungu kimoja ingawa wenyewe kila mmoja kwa wakati wake amesisitiza  kuwa hana bifu na mwenzake.

Siku ya jana Diamond na Ali Kiba walizua gumzo baada ya kuonekana wakipeana mikono na kusalimiana Kwenye msiba wa marehemu Agnes Masogange.

Meneja wa Diamond na mdau wa muziki wa Bongo fleva Saidi Fella maarufu kama Mkubwa Fela amefunguka na kuweka wazi kufurahishwa na kitrndo cha Diamond kusalimiana na Ali Kiba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Mkubwa Fela alifunguka haya:

Naomba nirudie tena niseme kama ninavyosemaga siku zote watu hawa hawanaga matatizo wala ugomvi kwaiyo hiyo ni baraka kwa nchi yetu na hata muziki wetu wa Bongo fleva kwaiyo cha msingi sisi tuombe dua watu waishi kwa usalama na amani tusipende ile watu wachukiane wapende kugombana sawa ni biashara maana mashabiki wanapenda ushabiki lakini haina maana wasanii hawa wachukiane”.

Lakini pia Mkubwa Fella ameongelea umuhimu wa wasanii hao kuonyeshana ushirikiano kwenye matatizo pale walipokutana Kwenye msiba wa Masogange Lakini pia Mkubwa Fela amewashangaa wachochea bifu na kudai wanaumbuka.

 

Zari Adai Hawezi Kudate Mtanzania Tena, Adai Mwanaye Sio wa Tandale

Mfanyabiashara maarufu na baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameibuka na kuapa kuwa hataweza kutembea na mwanaume wa Kitanzania tena.

Zari ameyasema hayo baada ya Kupitia kipindi Kigumu na Ex wake Diamond ambaye alichepuka sana kipindi cha Mahusiano yao ya miaka minne hadi kufikia hatua ya kuzaa nje.

Zari alimwaga Diamond mapema mwaka huu siku ya wapendanao baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Lakini pia Zari ameibuka na kudai kuwa mtoto wake  Tiffah sio wa Tandale hii iliyokea siku chache zilizopita wakati Zari na marafiki zake walipokuwa Kwenye Instagram live.

Zari alifunguka na kusema mtoto wake Tiffah anashindwa kutofautisha kati ya R na L tabia ambayo ameirithi kutoka kwa Upande wa Baba yake kwani Watanzania wengi hawawezi kutofautisha R na L na wengi wao wanamuita Zali badala ya zari.

Ndipo mmoja kati ya marafiki wa Zari alisema Tiffah ni wa Tandale Lakini mara moja Zari alikataa na kusema mwanaye sio wa Tandale.

Tandale ndipo Diamond na familia yake walipokulia na hajawahi hata mara moja kukataa asili yake na hata albamu yake inaitwa ‘A boy From Tandale’.

Diamond Akiri Kuwa Yeye ni Bingwa Wa Kiki na Drama

Supastaa wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekiri kuwa yeye ni bingwa wa kutafuta kiki mitandaoni Lakini pia anajulikana kwa kuwa na drama zisizoisha.

Diamond amekiri hayo kwenye mkutano aliofanya na waandishi habari siku ya jana katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kujuzwa mambo kadhaa kuhusu sheria za mitandao.

Diamond ameongea hayo na kuomba radhi kwa mashabiki zake na serikali baada ya kuachia video mbili tofauti zilizomuonyesha akiwa na wanawake wawili huku akifanya matendo yaliyotafsiriwa kinyume na maadili ya Kitanzania.

Na mimi ni miongoni mwa mabingwa wa kiki, najikubali, najua kabisa drama ninazo kila siku lakini tunaziweka vipi zisiende kuwatia dosari viongozi ambao wanapambana kuhakikisha sanaa yetu inafika mbali,

Kwa sababu ikienda kwa mazingira ambayo yalikuwa yamezoeleka huko nyuma unawavunja moyo viongozi ambao wanapigania sanaa ifike mbali”.

Lakini pia kwenye mkutano huo pia Nandy aliomba radhi pia kwa kusambaza video yake ya chumbani na Billnas ambayo ilivuja wiki chache zilizopita.

Ujumbe Wa Diamond Kwa Ali Kiba Baada Ya Kuoa

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameweka bifu pembeni na kumpongeza msanii mwenzake Ali Kiba baada ya kufunga ndoa siku ya jana.

Diamond na Alikiba wamekuwa kwenye bifu la muda mrefu ambapo lilisababisha kugawa mashabiki zao lakini hivi katibuni Diamond aliweka wazi kuwa hana bifu na Ali Kiba.

Jana ilikuwa siku ya shamra shamra kwa Alikiba kwani alifunga ndoa mjini Mombasa Kenya na mkewe Bi. Amina na ilikuwa ni harusi iliyozua gumzo sana Kwenye mitandao ya kijamii.

Diamond hakuona hiyana kumpongeza Ali Kiba na alimtumia ujumbe wa pongezi Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

Wadau nimeambiwa King Kiba kaoa leo mumfikishie salamu zangu za ndoa njema na maisha yenye furaha Amani na baraka tele”.

Baada ya kumtumia ujumbe huo pia Mama mzazi wa Diamond na familia yake wote walimposti Ali Kiba na kumpongeza.

Nuh Mziwanda Amtaka Diamond Aache Kudhalilisha Wanawake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amemjia juu msanii mwenzake Diamond Platnumz na kumtaka aache vitendo vyake anavyofanya vinavyopelekea kudhalilisha wanawake.

Nih ameongelea kitendo cha Diamond kusabaza video Kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wanawake wawili tofauti katika usiku mmoja kama udhalilishaji wa wanawake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Nuh Mziwanda amedai kitendo alichokifanya Diamond sio cha kiungwana kwani wanawake wote ni kama mama zetu hivyo tunapaswa kuwaheshimu.

Ni lazima tuwaheshimu wanawake maana ndio waliotuzaa na waliotuleta duniani kwaiyo automatically ni watu wa kuwaheshimu na hiyo ni nguvu ambayo Mwenyezi Mungu kaiweka kwaiyo huwezi ukarekodi vitu kama vile alafu ukaviweka Kwenye mitandao inakuwa inaleta picha mbaya kama vile dada zetu hawana thamani kitu ambacho sio cha kweli”.

Tangu kitendo hiko kitokee siku chache zilizopita tayari Diamond ameshachukuliwa hatua za kisheria na Waziri amehaidi atafikishwa mahakamani kwa kitendo hiko alichofanya.

Baada Ya Kuachiwa Kwa Dhamana, Diamond Kuhojiwa Tena na Polisi

Mwanamuziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz anatarajiwa kuhojiwa Tena na polisi baada ya kuachiwa kwa dhamana hapo jana.

Siku ya jana tarehe 17 April Diamond alishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano baada ya kusambaza video yake yake chafu ya chumbani ambazo hazikuwa na maadili Kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kushikiliwa kwa Diamond hapo jana kwa ajili ya mahojiano ila sasa ameachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi zaidi unaendelea na utakapokamilika ataitwa tena polisi kwa mahojiano.

Taarifa za kuhojiwa Diamond na Polisi simesikika kwa mara ya kwanza leo Bungeni ambapo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema Polisi walimkamata Diamond hapo jana, pia aliangiza msanii Nandy nae ahojiwe.

Siku ya Jumapili Diamond aliwashangaza watu wengi ikiwemo kuwakasirisha mashabiki zake baada ya video zake akiwa na wasichana wawili tofauti huku mmoja akiwa mzazi mwenzake Hamisa Mobetto kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.

Diamond Afikishwa Polisi Baada Ya Video Yake Kuvuja Mtandaoni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefikishwa polisi jana kwa ajili ya mahojiano baada ya kusambaa kwa video zake zisizo na maadili katika mitandao ya kijamii.

Jamiiforum wnaripoti kuwa hayo yalisemwa na Waziri wa habari, Michezo, Utamaduni na sanaa Dr.  Harrison Mwakyembe akiwa bungeni wakati akijibu swali juu ya kanuni za maudhi ya Mitandaoni aliloulizwa na Mbunge Goodluck Mlinga.

Aidha Dkt. Mwakyembe amesema Msanii Faustina Charles (Nandy) naye atahojiwa na Polisi kufuatia video yake ya faragha akiwa na Msanii mwenzake Billnass kusambaa mitandaoni.

Waziri Mwakyembe amesema kwa sasa wanaangalia  taratibu za kuwafikisha mahakamani.

Bifu Kati Ya Wanamuziki Ni Muhimu-Country Boy

Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya miondoko ya kurap Ibrahim Mandingo maarufu kama Country Boy ameibuka na kutetea uwepo wa bifu miongoni mwa wasanii.

Bifu ni kitendo cha kutokuwepo maelewano baina ya watu na hii inatumika baina ya wasanii ambapo kwa nchi za nje wasanii hutengeneza bifu ili kuuza kazi zao.

Country Boy amefunguka na kudai bifu ni muhimu katika sanaa na bila kuwepo kwa bifu kunakuwa hakuna msisimko katika kazi za wasanii kwani ushindani unakuwa mdogo.

Kwenye mahojiano aliyofanya  na Star Showbiz, Country Boy alisema kuwa, msisimko kwenye muziki unapungua kwa sababu wanamuziki wengi kwa sasa wanaogopa masuala ya bifu bila kufahamu wanalikosesha soko msisimko ambao ungekuwepo kama kunapotokea tofauti.

Unajua muziki ni mashabiki, sasa kunapokuwa na wanamuziki wawili wana tofauti hata mashabiki wao pia wanakuwa wanashindana na kutamba kuonesha kwamba mwanamuziki wao ni mkali kuliko yule mwingine“.

Kwa upande wa muziki wetu wa Bongo fleva moja kati ya bifu maarufu ni kati ya wasanii Diamond Platnumz na Ali Kiba ambao imesemekana kuwa bifu imewasaidia sana kuuza muziki wao.

Diamond Endelea Kuwatumia Hao Wanawake Maana Hawajielewi Lakini Kumbuka Kutumia Kondomu- Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Shamsa Ford Amefunguka na kudai kuwa sio kweli kwamba Diamond anawadhalilisha wanawake ambao wanatoka nao kimapenzi kwa kusambaza video zao mtandaoni.

Diamond alizua gumzo hili siku ya jana bada ya video zake kusambaa mtandaoni akiwa na Hamisa Mobetto chumbani wakikumbatiana na wakati huo huo akiwa na binti wa kizungu wakiwa pamoja chumbani pia Wakila denda na uchafu mwingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Shamsa aliulizwa nini maoni yake juu ya jambo hilo na alifunguka na kumtaka Diamond aendelee kutoka na wanawake tofauti tofauti kwa kuwa hawajitambui huku amtahadharisha kutumia kondom ili kuepuka magonjwa na zinaa.

Mwanaume hawezi kukufanya mwanamke ikawa chombo cha starehe inategemea mwenyewe na akili yako kama unataka kuchezewa utachezewa kama unataka kuwa mwanamke wa muhimu kwake utakuwa inategemea mwenyewe unajiweka wapi kwaiyo mimi siwezi kumlaumu Diamond kama anawatumia maana wenyewe ndio wameweka mazingira hayo kwa nini asitumie nafasi? Ila mimi namshauri Diamond awale tu hao wasichana ila akumbuke kutumia kondomu maana magonjwa mengi”.

 

 

Diamond na Mzungu Wake Wakifanya Yao (+Video)

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amezidi kuzua gumzo na kutengeneza headlines baada ya kuachia video nyingine akiwa na msichana wa kizungu.

Msichana huyo ambaye hajajulikana jina mpaka hivi sasa pia ameonekana kwenye video mpya ya Diamond na Harmonize ya wimbo unaoitwa Kwangaru.

Video hizo zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii zinamuonyesha Diamond akiwa na msichana huyo wa kizungu huku wakikumbatiana na kupeana mabusu moto moto:

 

 

 

 

 

Diamond Awakosoa Watu Waliodhani Huu Utakuwa Mwaka Wake wa Mwisho Kimafanikio

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amewazodoa wale wote waliohisi huu utakuwa mwaka wake wa mwisho kimafanikio.

Diamond ambaye umeuonyesha ulimwengu kuwa hakuna kitu kinachomshinda kufanya kuanzia kuwa mmiliki wa record label kubwa Tanzania WCB na hivi sasa mmiliki wa Kituo cha televisheni cha WASAFI TV.

Diamond amesema kuwa jakuna kinachoshindikana  kama utaweka juhudi ya kweli na kazi katika kile unachokifanya basi mafanikio ni lazima Diamond ameyadhihirusha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka posti mbili.

Posti ya kwanza Diamond ametoa ahadi jinsi Wasafi Tv itakapotoa usawa kwa wasanii wote bila ubaguzi na kumpa nafasi ya kweli kila mwanasanaa:

Lakini pia katika posti yake ya pili Diamond ameongelea ujasiri alionao na huo ndio unampa mafanikio kwani anapenda kuthubutu kufanya mambo ambayo wengine wanadhani hayawezekani na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kukata tamaa bali ana Songa mbele kutafuta mafanikio.

Dansa Wa Diamond Akumbwa na Skendo Ya Kutelekeza Mtoto

Dansa kutoka WCB ambaye mchezo shoo wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zungu amekumbwa na skendo ya kuwa mmoja kati ya wanaume waliotelekeza watoto wao Dar.

Siku ya jumatatu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliwakusanya wanawake wote ambao wametelekezwa na wanaume ambao wamezaa nao ambapo hawawahudumii watoto wao.

Mmoja kati ya Wanawake waliojitokeza ni mwanamke ambaye alijitambilisha kama mzazi mwenza wa Dansa wa  Diamond anayejulikana kama Zungu ambapo amedai alimtelekeza yeye pamoja na mtoto wake baada ta kuachana ambapo amekuwa hataki kumtunza mtoto wake.

Baada ya tuhuma hizo Zungu alitafutwa na Timamu Tv ambapo amefunguka na kusema yule mwanamke ana matatizo ya akili pia ni mkorofi na amedai kuwa hajawahi kumkataa mtoto wake na amesema yupo tayari hata leo kwenda kwa Makonda na kujielezea na kama ikitokea anatakiwa amchukue mtoto wake amesema yupo tayari kumlea mwanaye mwenyewe.