Nyimbo za Diamond Zilizofungiwa Zazua Gumzo Bungeni

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige amehoji sababu ya kufungia nyimbo za Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kigezo  cha kukosa maadili baada ya kuziacha zikachezwa kwa muda mrefu hewani.

Wiki chache zilizopita BASATA lilitangaza kufungia nyimbo zaidi ya kumi na tano za wasanii mbali mbali na mmoja ya wasanii aliyefungiwa nyimbo zake ni Diamond Platnumz ambapo alifunguwa nyimbo mbili kwa kigezo cha Kukiuka maadili ya Kitanzania.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, amejibu kuwa Diamond siyo msanii wa kwanza kufungiwa nyimbo zake kwani hata wasanii wa Nigeria, Davido na Wizkid, wamefungiwa nyimbo zao. Pia alimtaja mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo, Kofii Olomide, ambaye wimbo wake wa Ekoti Te umefungiwa nchini humo.
Pamoja na kuibuka wabunge wengi wenye kutaka kutoa taarifa na kuendelea hoja hiyo, Naibu Spika, Tulia Ackson, hakuwapa nafasi.

Diamond na Harmonize Wapania Kuondoa Muziki Wa Nigeria Bongo

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Diamond Platnumz na Harmonize wamekuja na mkakati wa kuua kabisa muziki wa Nigeria ambao umeshika sana kasi nchini Tanzania.

Harmonize amefunguka na kudai wimbo wake mpya wa Kwa ngwaru ni mwanzo mzuri wa kurudisha muziki wa kuchezeka Tanzania ambao kwa kipindi kirefu ulishikiliwa na muziki wa Bongo fleva.

Harmonize amefunguka Kwenye Interview aliyofanya na Radio Five na kudai kuwa nyimbo za kuchezeka Bongo zimepungua kwani ambazo zinazotoka sasa hivi zimepoa kitu ambacho kinafanya nyimbo za wasanii wa Nigeria kupewa nafasi hasa club.

Inafikia wakati tunaona ni lazima tucheze, so tukaona this time around tukija na Kwa Ngwaru kama ngoma nyingi zilitoka kama zimelala ndio maana ukienda club unasikia Wanigeria wakati sisi tunaweza tukafanya muziki mzuri watu wakapenda na wakacheza.

Mwisho wa siku tunapenda tu ngoma zao kwa sababu ya beat lakini lugha hatuijui”.

Harmonize alitoa wimbo huo wa Kwa ngwaru wiki iliyopita na ulitrend kwa wiki nzima Youtube, huu ni wimbo wa pili kwa Harmonize kumshirikisha Diamond ambapo wimbo wa kwanza ilikuwa ni Bado ambao ulifanya vizuri sana.

Amber Lulu- Natamani Sana Kusainiwa WCB

Video vixen maarufu na msanii wa Bongo fleva Amber Lulu amefunguka na kuongelea mipango yake ya kutaka kusaini chini ya label maarufu Bongo WCB inayomilikiwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Amber Lulu ambaye alijulikana kutokana na kuuza Mushi kwenye video za wasanii mbali mbali wa Bongo fleva na vituko vyake. Hivi sasa Amber Lulu kwa hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya jini kisirani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Sam Misago Tv, Amber Lulu amefunguka na kuweka wazi kuwa anatamani sana kufanya kazi chini ya WCB:

Natamani hata kesho niweze kusainiwa WCB na naomba niseme kuwa namtegemea sana Diamond kwa sababu yeye ni kaka yangu ambaye amenitangulia kwaiyo kwa upande wangu nina mipango mingi sana na Diamond na WCB kwa ujumla ingawa najua yeye ana mambo yake na ni mtu mkubwa kumpata inakuwa ngumu lakini natamani siku moja nije kufanya naye kazi na ninatamani niwe msanii wa kwanza kusainiwa WCB baada Queen Darleen”.

Hivi sasa Amber Lulu anafanya vizuri na wimbo wake wa jini kisirani na amekiri msanii anayetamani sana kufanya naye kazi ni Rayvanny kutoka WCB.

 

Majizzo Ampa Tano Diamond na Wasafi Tv

Mkurugenzi na mmiliki wa EFM Radio na TV E, Majizzo amempa pongezi Diamond Platnumz baada ya televisheni stesheni yake ya Wasafi Tv kuanza kufika rasmi .

Siku ya tarehe moja Wasafi Tv ilianza kurysha rasmi matangazo yake Ikiwa ni suala lililosubiriwa kwa hali kubwa na mashabiki wengi ili kuona Diamond Atafanya nini hasa ambacho ni tofauti katika tasnia hii ya burudani.

Majizzo amempa tano Diamond kwa kuwa kijana mdogo kuleta kitu kama hiko ambacho kitasaidia kuleta ajira kwa vijana wengi nchini na pia kuleta changamoto katika sekta a hii ya burudani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Majizzo alitiririka haya juu ya ujio wa Wasafi Tv:

Ni mpango mzuri uliochukua na mimi binafsi nakupongeza juu ya kuchagua sekta ya vyombo vya habari, kama vijana ni wajibu wetu kuwahamasisha vijana wengine kufanya kazi kwa bidii ili kujenga taifa letu leo na kizazi cha baadae. Sisi kama “E” tumefanya kidogo na tunaamini kuwa Wasafi (TV na Radio) zitafanya mengi zaidi. Karibu tujenge Tanzania.Karibu kwenye tasnia ya habari @diamondplatnumz“.

 

Kifesi Afukuzwa Kazi na Diamond Baada Ya Kumshauri Arudiane na Zari

Mpiga picha maarufu wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Kifesi amedaiwa kufukuzwa kazi WCB baada ya kumshauri bosi wake arudiane na Zari.

Kifesi alitumia ukurasa wake wa Instagram na kutangaza kuwa ameamua kuacha kazi kama mpiga picha wa Diamond na kujiajiri mwenyewe na kudai anataka kuwa karibu zaidi na Mungu wake kwa kupitia dini yake.

Lakini Mara tu ya habari hiyo kusambaa taarifa mbali mbali kutoka kwa watu wa karibu wa WCB walianza kudai kuwa Kifesi hajaacha kazi bali ametimuliwa na Diamond kwa tabia yake ya kupenda kuingilia maisha binafsi ya bosi wake Diamond.

Kifesi ni mtu ambaye huweka wazi siku zote kuwa anampenda Zari name hata siku alipomuacha Diamond alidai hata Kama wameachana lakini yeye bado anampenda Mama T na kumkubali.

Sasa juzi juzi baada ya Zari kuja Tanzania kusaini dili lake jipya Kifesi alitumia nafasi hiyo kumshauri tena Diamond arudiane na Zari kitendo kinachisemekana kuwa hakikukaa vizuri na Diamond ambapo aliishia kumfukuza kazi.



Jux Amwagia Misifa Lukuki Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa Bongo fleva ambaye anafanya vizuri kwa hivi sasa na ngoma yake ya ‘Fimbo’ amefunguka na kumwagia sifa msanii mwenzake wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Wiki iliyopita Diamond alivunja rekodi kwa kuwa msanii wa Kwanza nchini Africa kwa kufikisha subsribers milioni moja kwenye ukurasa wake wa YouTube huku akiwafunika wasanii wakubwa kama Davido, Wizkid, Fally Ipupa na wengineo:

Jux amefunguka na kumwagia misifa kibao Diamond kwa mafanikio hayo aliyoyapata na kukiri kuwa ni jambo jema kwani kwa upana wake linazidi kuupeleka mbele zaidi mziki wetu wa Bongo fleva.

Jux amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online ambapo alitiririka haya zaidi:

Hiyo ni bahati ambayo sisi Watanzania tumeipata ni kitu kizuri ni sifa pia kwetu kwa sababu kama ni msanii wa Tanzania anakuwa wa kwanza kufanya kitu kama hicho Africa lazima watu watajiuliza huko Tanzania wanafanya mziki gani ndipo wanapoangalia mziki wa Bongo fleva na pia kukutana na wasanii wengine kwa hiyo ni habari njema na sio mchezo maana sio kawaida na watu wasichukulie kawaida maana kuwapata subscribers kama hao kuwapata sio mchezo”.

 

 

Times Fm Yaomba Radhi Baada Ya Interview Ya Diamond

Kituo cha redio cha Times Fm imeomba radhi baada ya Interview yao waliofanya na supastaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz wiki chache zilizopita.

Baada ya Diamond kuachia albamu yake ya ‘A boy From Tandale’ alienda katika kituo cha Times Fm katika kipindi cha The Playlist kwa ajili ya kufanya mapitio ya Albamu yake mpya.

Kwenye Interview hiyo Diamond aliwatolea povu zito BASATA ambayo ilikuwa imefungia nyimbo zake mbili kwa wakati huo ambazo hakuweza kuzifanyia marejeo.

Siku ya jana Diamond alimaliza bifu lake na BASATA na hata Waziri Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri Juliana Shonza na kufungulia nyimbo zake hizo mbili

Barua ya kuomba Radhi kutoka  Times Fm:

Irene Amtupia Dongo Zito Wema Inadaiwa Kisa ni Diamond

Video vixen aliye jizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii Rayvanny Irene, amemtolea povu zito staa wa Bongo movie Wema Sepetu huku ikidaiwa kisa ni penzi la Diamond.

Tangu Zari aweke wazi kuwa kaachana na Diamond na kuwa single Kumekuwa na tetesi nyingi sana kwenye social media juu ya nani hasa anayechukua nafasi ya Zari na moja kati ya Wanawake waliotajwa kuwa na uhusiano na Diamond kwa sasa ni Irene na Wema.

Kuna stori ili trend sana kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma kidogo ambapo ilisemekana kuwa Irene na Wema wamepeana kichapo cha maana baada ya kugongana Madale nyumbani kwa Diamond.

Stori hiyo ilidai kuwa Diamond anatoka na Irene na Wema kwa wakati mmoja na wikiendi hii Irene kamtupia dongo Wema ambapo amemcheka kuwa anajiita African beauty wakati hata kiwanja hana!.

 

African beauty ni wimbo mpya wa Diamond na siku wimbo huo ulipotoka wasanii mbali mbali wa WCB akiwemo Harmonize alimtunuku Wema jina la African beauty jambo ambalo lilimfanya Wema ajitambe kuwa ni African beauty.

Fununu za Irene kuwa na Mahusiano na Diamond zilianza siku nyingi sana wakati bado Diamond yuko na Zari ingawa Diamond alikuwa anakataa kuwa hana Mahusiano naye.

Diamond Aliweka Hadharani Penzi la Mavoko na Lulu Diva

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameliweka hadharani penzi la msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Rich Mavoko na Lulu Diva.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa msanii wa muziki Lulu Diva na Rich Mavoko ni wapenzi ingawa wenyewe wamekataa mara kwa mara kuwa hawana uhusiano wowote.

Lakini Diamond ametoa siri hiyo ya muda mrefu na kulianika penzi hilo Hadharani baada ya kumposti Lulu kwenye ukurasa wake wa Instagram Ikiwa ilikuwa ni birthday ya Lulu  Diva.

Kwenye posti hiyo Diamond aliwataka Rich Mavoko na Lulu Diva waache kujificha na badala yake wakae na wazae mtoto wao:

Pamoja na wawili hao kukataa kuwa walikuwa hawana uhusiano wa kimapenzi lakini mara kwa mara picha zao zilisambaa mitandaoni zilizowaonyesha katika mapozi ya kimahaba.

Baada ya kupewa dongo hilo Lulu Diva alimjibu Diamond kuwa wanataka wajenge kwanza nyumba kabla ya kuanza kuzaa kuwa na familia.

Omarion Akiri Kujisikia Fahari Kuimba Kiswahili

Mwanamuziki wa RnB kutoka Marekani, Omarion amefunguka na kukiri kuwa amejisikia fahari kuimba kwa lugha ya Kiswahili kwenye wimbo wa african Beauty.

Diamond amemshirikisha Omarion kwenye wimbo wake mpya wa African beauty unaopatikana kwenye Album yake ya ‘A boy From Tandale’.

Omarion amefunguka kuhusu kuimba wimbo huo kwa lugha ya kiswahili ambapo amekiri kuwa ni jambo jela kufanya kwa sababu msanii ambaye alikuwa Role model wake Michael Jackson aliimba kiswahili kwenye nyimbo zake zaidi ya mbili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Omarion alifunguka haya kuhusiana wimbo huo:

Penzi ntalipamba ngonjera, Huba kama  Tanga segera kwa viuno vya baikoko kutoka Manzabay, picha twazitwanga kusema, posti insta wanga kuwakera. (Fun fact) Michael Jackson sang Swahili on Liberian Gal and wanna be startin something. What a pleasure I have continuing the work of my musical forefathers M.J connecting my understanding of one another through culture and language it’s all live. I am around the globe with this ?”.

 

Waziri Mwakyembe- Diamond Anaanza Kulewa na Umaarufu

Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Mh. Harrison Mwakyembe, amemuoa juu staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kutokana na kauli zake alizozitoa kwa Naibu Waziri Juliana Shonza.

Dkt. Harrison Mwakyembe ameelezwa kukerwa na kauli alizozitoa Diamond ambazo anaamini zinamdhalilisha Naibu Waziri Juliana Shonza wakati akihojiwa na kipindi cha The Playlist cha Times Fm.

Dkt. Mwakyembe amefunguka na kudai anaona staa huyo wa Bongo fleva ameanza kulewa umaarufu hadi kufikia hatua ya kumdhalilisha kiongozi wa serikali:

Dkt. Mwakyembe ameongea haya na Global Publishers:

Kama ni vikao na wasanii tumefanya vingi sana, lakini Diamond haudhurii vikao hivyo sio wajibu wa serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, however popular he is hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalumu kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond sio kiongozi wa shirikisho la muziki wala msemaji wa Chama cha muziki wa kizazi kipya kuwasemea Wenzake. Si busara kwake kushindana na serikali na kama ana ushauri basi atoe kistaarabu utazingatiwa lakini si kwa kumshambulia Naibu Waziri kwa dharau na kejeli jinsi alivyofanya sijafurahishwa hata kidogo”.

 

Diamond Amtolea Uvivu Naibu Waziri Shonza Baada Ya Kufungia Nyimbo Zake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemtolea povu zito Naibu Waziri wa Habari Butudani na Michezo Bi. Juliana Shonza baada ya kufungiwa nyimbo zake mbili.

Mwezi uliopita BASATA walitangaza kufungia nyimbo zaidi ya kumi na tano na moja kati ya nyimbo mbili zilizofungiwa ni za Diamond na hata kuwafungia wasanii kama Roma kufanya shughuli zozote za kimuziki kwa miezi Sita.

Kwenye mahojiano aliyofanya juzi kwenye kipindi cha The Playlist cha Times Fm Diamond aliongelea suala hilo kwa jazba na kuweka wazi kuwa haoni hatari kufungiwa nyimbo hizo kwani hakumpunguziii kitu kwani ataenda kuzi perform nje ya nchi.

Inawezekana Mh. Waziri wa habari amenizidi elimu, mamlaka inawezekana kanizidi kwenye umri lakini Kwenye elimu ya sanaa ya Tanzania nimemzidi apende akatae apende akatae akinichukia mimi sijali”.

Baada ya kutoa povu hilo juzi, Naibu Waziri Juliana Shonza hakutoa majibu yoyote kuhusiana na madai ya Diamond.

Diamond ameonekana kukerwa na majibu ya Naibu Waziri Shonza ambayo amekuwa akiyatoa kuhusu kufungia nyimbo za wasanii bila ya kuwapa taarifa sahihi kabla ya zoezi hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Diana alimtolea uvivu na kumuandikia ujumbe huu:

.

“Sina Bifu na Ali Kiba Ila Kuna Watu Wanatia Chokochoko” – Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz anayeendelea kufanya vizuri na albamu yake mpya ya ‘A boy From Tandale’ amefunguka na kusema hana tatizo na Ali Kiba ila kuna watu wanataka kuwagombanisha.

Diamond na msanii mwenzake wa Bongo fleva Ali Kiba wamesemekana kuwa na bifu kwa muda mrefu sana huku kila mmoja akikataa pembeni kuwa hana bifu na mwenzake lakini vijembe wanavyorushiana vinasema vingine.

Tetesi za wasanii hawa kuwa na bifu zilishika kasi baada ya Alikiba kutoa wimbo wake wa ‘Seduce me’ na Diamond kutoa Zilipendwa kisha kuanza kurushiana maneno Twitter jambo lililopelekea hadi kutukanana.

Lakini jana Kwenye Interview ambayo Diamond alifanya na LilOmmy Kwenye The Playlist alisisitiza kuwa hawana bifu ila kuna muda watu wanakuwa wnawachochea maneno maneno ili kutaka watengeneze bifu.

Unajua watu wanaweza wasiwe na matatizo ila sometimes watu wanakuwa wanatia chokochoko kati yenu na kama wanadamu zinakuja zinawa provoke na mnajikuta mnataka muingie kweli kwenye bifu, lakini baadae mkikaa mnajifikiria kuwa sisi ni watu wazima wenye akili mnajikuta mnagombana halafu wanakuja kufaidika watu wengine kwa sababu mimi kugombana na Ali hakuniongezei chochote kwenye maisha yangu”.

Diamond amesema hawezi kuwa na tatizo na Ali Kiba kwani kila mtu ana mashabiki zake hivyo hana haja ya kuwa na ugomvi naye.

“Nyimbo Zangu Kufungiwa Hakunipunguzii Kitu”-Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz anayefanya vizuri na albamu yake mpya ya ‘A boy from Tandale’ amefunguka na kudai kufungiwa kwa nyimbo zake mbili hakumpunguzii kitu.

Wiki chache zilizopita BASATA ilifungia nyimbo kumi na tano za wasanii mbali mbali wa Bongo fleva kwa kudai zimekiuka maadili ya Kitanzania na moja ya wasanii hao ni Diamond ambaye alifungiwa nyimbo mbili Wakawaka na Halelujah.

Kwenye Interview aliyofanya na The Playlist ya Times Fm Diamond amefunguka na kudai yeye kufungiwa nyimbo zake hakumpunguzii kitu zaidi ni kama kumkomoa na kurudisha nyuma jitihada za kukuza mziki huu wa Bongo fleva.

Suala si kufungia tu nyimbo, mimi ukinifungia nyimbo hainipunguzii kitu nikienda nje naenda nai-perform ukiwa hutaki sinaondoka tu naenda nchi nyingine, kwa hiyo ni kukaa tuzungumze, tuelekezane lakini tusifanye kama kukomoana, hapana, tufanye katika mazingira ambayo yatasaidia sanaa ikue“.

Bongo Flava naijua kweli kweli, halafu kama mimi ni mtu ambaye siogopi kwenda jela kwa ajili ya Bongo Flava, siogopi kufanya chochote kwa sababu ndio Baba yangu na Mama yangu ndio nimefanya hadi nimefika hapa, kwa hiyo unapo-deal na sanaa yangu hakikisha unafanya kitu ambacho kipo sahihi usikurupuke kwa sababu una mamlaka”.

Diamond pia amesema hivi sasa jitihada zake anazielekeza kwenye uzinduzi wa radio station na television station zake za Wasafi TV na Wasafi Radio pamoja na kuhakikisha albamu yake inafanya vizuri sokoni.

Alikiba, Darassa, Diamond na Vanessa Wang’aa Kwa Tuzo Nchini Uganda

Wanamuziki wakali wa Bongo fleva kama Diamond, Ali kiba, Vanessa Mdee na Darassa wameng’aa kimataifa zaidi baada ya kila mmoja kujishindia tuzo za Hippo nchini Uganda.

Tuzo hizo zilifanyika usiku wa jana nchini Uganda ambapo baadhi ya wasanii waliopata Tuzo kutoka Tanzania ni kama vile Diamond, Ali Kiba, Vanessa Mdee na Darassa.

Vanessa Mdee ameibuka na tuzo ya heshima katika kipengele cha ‘East Africa Best Female Artist’ na Alikiba akiibuka na tuzo ya kipengele cha ‘Song of the Year Tanzania’ kupitia wimbo wake wa Seduce Me.

 

Diamond Platnumz ameshinda tuzo mbili mbili kwenye vipengele vya ‘Africa Song of The Year’ kupitia wimbo wake wa ‘Marry U’ aliomshirikisha Ne-Yo na ‘Best East Africa Video’ kupitia wimbo wa Eneka.

Darassa ameibuka kidedea kwenye kipengele cha ‘East African Super Hit’ na wimbo wake wa Muziki ambao amemshirikisha Ben Pol.

 

Penny- Ningemzalia Diamond Lakini Alikuwa Hajatulia

Mtangazaji maarufu Penny au maarufu kama Vj Penny amefunguka kuhusu uhusiano wake na staa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz ambapo amekiri kuwa endapo angekuwa ametulia angemzalia.

Penny na Diamond walikuwa na uhusiano wa kimapenzi miaka michache iliyopita na kuna wakati ilisemekana kuwa Penny alikuwa amembebea mimba Diamond lakini baadae habari zilienea kuwa alichoropoa mimba hiyo.

Diamond na Penny enzi za mapenzi yao

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda Penny amefunguka kuwa sababu iliyomfanya mpaka hakuzaa na Diamond kipindi cha Mahusiano yao ni kutotulia kwake:

Mimi napenda sana mtoto ndoto yangu ni siku moja nije kuwa mama lakini pia nataka mwanaume ambaye nitazaa naye awe baba bora kwa mwanangu. Kwa kipindi kile niliposhika mimba ya Diamond siwezi kusema sana kuhusu yeye lakini ningeweza kumzalia lakini alikuwa ana mambo mengi”.

Lakini pia Penny alipoulizwa anamshauri Diamond amuoe nani kati ya Wema na Zari kwani alitangaza kuoa mwaka huu Penny alifunguka:

Kwanza yeye aangalie mwanamke anayempenda kwa dhati, anayejua familia na kumshauri vyema katika kazi zake na pia asithamini sana starehe badala ya maendeleo”.

Penny amesisitiza kuwa kamwe hawezi tena kurudiana na Diamond kwani kila mtu ameshakuwa na maisha yake na yeye ana mpenzi wake.