Prezzo Kafulia Choka Mbaya- Gigy Money

Video vixen na Msanii wa Muzikiwa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameweka wazi msanii kutoka Kenya Prezzo hivi sasa amefulia vibaya mno.

Gigy Money alifunguka hayo wakati anaongelea uhusiano kati ya Rafiki yake Amber Lulu na mpenzi wake Prezzo

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Gigy Money ameweka wazi hivi sasa ukimuona Prezzo siyo yule uliyekuwa unamuona kwenye Tv amekonda vibaya mno yaani kafulia:

Yaani Prezzo kakonda kuliko hata unavyomuona Kwenye picha naona ni stress za kimaisha kwa sababu mimi nimeenda kuperfom juzi juzi Nairobi nimeondoka club nimemuacha Prezzo mpaka asubuhi saa saba za usiku hana direction yoyote.

Alikuwa ana jina zamani sio sasahivi hata wanavyomchukulia huko Nairobi sio tunavyomchukulia sisi huku Bongo yaani amefulia choka mbaya hayupo kwenye peak tena hata huku tunamuongelea sababu ya Amber”.

Gigy Money amedai Kenya wasanii wenye majina ni wasanii kama Nyanshinki, Will Paul, Khaligraph na wengine lakini ukimtaja Prezzo watu watakucheka sana.

Kupunguza Mwili Kunanipa Madili Mengi :-Gigy Money

 

Msanii wa bongo fleva Gigy Money, Amefunguka kuwa yeye kupungua kwake kunampa faida sana katika kupata madili na kuwa mwepesi kwenye show zake.

Akizungumza na eatv.tv Gigy Money amesema kama angeendelea kuwa mnene basi kwenye kutumbuiza jukwaani asingekuwa mwepesi kama alivyo sasa hivi kwa hiyo hapendi kuwa mnene tena.

Gigy Money amesema unene sio mzuri kwa kile alichodai kwamba mtu akiwa mnene anakuwa na mwili usiokuwa na mvuto sana kama ukiwa mwembamba, na pia raha ya kuwa mwembamba unakuwa shapu shapu kwa kila kitu ambacho unakuwa unaitaji kufanya kwa wakati.

Kwanza mimi nafurahia kuwa mwembamba kuliko nilivyokuwa zamani, moja ukiwa mwembamba kwenye ‘show’ unafanya utakavyo tofauti na ukiwa mnene kingine ona mtu kama Vanessa akiwa nafanya ‘show’ hadi una-enjoy kwa hiyo kuwa ki-model pia unapata matangazo mengi” ,amesema Gigy Money.

Ameongeza kwa kusema anapokuwa kwenye jukwaa ana kuwa huru kufanya chochote kuliko zamani alivyokuwa kwa hiyo hapendi kurudi katika hari ile ya zamani ya unene.

“Prezzo Anampenda Amber Lakini Tatizo Hajatulia”- Gigy Money

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefungukia penzi la shoga yake Amber Lulu na mpenzi wake Prezzo.

Siku za hali karibuni kumetokea sintofahamu Kwenye penzi la Msanii Amber Lulu na mpenzi wake Msanii kutoka Kenya Prezzo ambapo imesemekana wawili hao wameachana.

Lakini utata zaidi ulitokea siku mbili hizi baada ya picha kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Prezzo akiwa na mwanamke mwingine wakiwa kitandani.

Baada ya skendo hiyo Amber alitumia mitandao ya kijamii kutangaza kuwa amelitua Penzi lake na Prezzo na kuweka wazi kuwa kwa hivi sasa yupo single.

Kwenye mahojiano na XXL ya Clouds Fm, Rafiki wa karibu wa Amber, Gigy Money amefunguka na kudai Prezzo anampenda Amber Lulu Lakini tatizo lake hawezi kuacha michepuko:

Yaani mshakji (Prezzo) anampenda Amber Lakini ndio hivyo ana mambo mengi yaani amefanya vitu vya ajabu sana rafiki yangu kwa rafiki yangu yaani ana mademu kibao na hivi wapo mbali basi ndio vituko kibao”.

 

Gigy money Asema Haogopi Kupoteza Mashabiki.

Mwanadada Gigy Money amefunguka na kusema kwake wala haogop kupoteza mashabiki kwa sababu anamashabiki wengi sana na hata kama wale wa kwake watapotea lakini bado anamini kuwa na mashabiki wengine wengi kutoka kwa wasanii wengine kama alikiba na diamond.

Gigy money anasema kuwa hana  wasiwasi kwa sababu wanaompenda wengi ni wanawake na kumpenda kwake ni kutokana na kipaji alichonacho lakini pia watu wengi wamekuwa wakiona vituko vyake na kucheka ambapo kwake yeye ni jambo la furaha na anachoamini ni kwamba yeye ana kipaji na kinamlinda.

Shabiki gani, mimi wa Alikiba wangu, wa Diamond wangu sijui wa nani wangu naanzaje kupoteza mashabiki.napendwa na mademu kuliko wanaume kwa sababu they love my sex, they love music wangu mimi ninafanya watu wafurahi wakiwa instagram, hii ni talent najua siwezi kuwafurahisha watu wote lakini najiamini nini upepo tena sina upepo nina kimbunga.

Gigy Money Asema Hamjui Wema Sepetu

Mwanadada Gigy Money ambae hakosi kuwa na drama kila siku anasema kuwa hamjui mwana dada Wema Sepetu na kwamba yeye ndie msani pekee wa kike ambae anafanya vizuri kwa sasa kuliko msanii mwingine yoyote hapa bongo .

Akiongea kwa kujiamini gigy money anasema kuwa kutokana na madili anayoyapata sasa hivi yanayomuingizia hela hakuna msanii wa kike wa kumlinganisha nae wa sasa.

Swala la gigy money kuwa akisema hawajui baadhi ya mastaa hapa bongo liekuwa la kawaida kwake kutokana na kuwa na tabia ya kusema hivyo mara kwa mara kwa baadhi ya mastaa wakubwa .

Gigy money  ambae baada ya kujifungua alianza kufanya kazi na kusaini mikataba mbalimbali  ya kumuingizia pesa ansema kwa sasa hakuna msanii wa kike bongo anaemfikia.

Gigy Money- Wanaume Wengi Wanalelewa na Wanawake Hakuna Watafutaji

Video vixen maarufu aliyegeukia sanaa ya Bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amedai wa au me wengi Bongo wanajua kulelewa na wanawake hawajui kutafuta wenyewe.

Kwenye Interview yake na Bongo 5, Gigy Money amedai ile dhana kuwa wanaume ndio wanatafuta kwa ajili ya Wanawake imepotea kwani wanaume wengi wanakaaa na kutegemea wake waletewe na Wanawake zao.

Mwanaume wacha wamdharau mwanamke lakini sisi tunachukuwa risk kubwa sana kwenye maisha, mzunguko wa maisha ya mwanamke ni shita tupu ndio maana hata ile nyimbo “Wanaume Tumeumbwa Mateso” siikubaligi.

Wanawake ndio wameumbwa kuteseka, sasa hivi uniambie kuna wanaume wanakula kwa jasho warembo wengi hivi, unanidanganya, wanawake sasa hivi ndio wanatafuta kwa jambo na mateso”.

Kauli hiyo ya Gigy Money imekuja baada ya kurudiana na Baba watoto wake Mo J ambaye aliachana naye mwezi uliopita kwa madai alikuwa hampi huduma zozote zaidi yeye ndio alikuwa a anatoa pesa za matumizi.

 

Nataka Kuanzisha Timu ya Mpira :-Gigy Money

 

Msanii wa Bongo fleva nchini, Gift Mwakyusa ‘Gigy Money’ amefunguka kuwa kupitia watoto wake ana mpango wa kuanzisha timu yake ya mpira kwakuwa, anatarajia kuzaa watoto wengi.

Msanii Gift Mwakyusa maarufu kama ‘Gigy Money’ amesema hayo kwenye KIKAANGONI inayorushwa na EATV kupitia ukurasa wake wa Facebook, ambapo amesema hakumbuki ametoa mimba ngapi kabla ya kufanya maamuzi ya kuzaa na atarajia kuzaa watoto wengi zaidi.

Sikumbuki ni mimba ngapi nimewahi kutoa ila sio ufahari sikuwa na uwezo wa kulea lakini saivi nazaa na nina mpango wa kuanzisha timu ya mpira kupitia watoto wangu”, amesema Gigy.
Gigy ameongeza kuwa alijifikiria kutoa ujauzito wa mtoto wake wa sasa lakini hakufanikiwa kufanya hivyo, na kuanzia sasa ameamua kuzaa kwakuwa anaweza kulea

Gigy Money-Nilitembea na Ali Kiba Pamoja na Abdu Kiba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ametoa kali baada ya kukiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Staa wa Bongo fleva Ali Kiba pamoja na mdogo wake Abdu Kiba.

Gigy Money ameweka wazi kuwa ametembea na ndugu hao wawili lakini sio kwa wakati mmoja bali ilikuwa ni nyakati tofauti maana alikutana nao tofauti tofauti.

Gigy Money alifunguka hayo Kwenye Interview yake na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv ambapo alikiri kuwa wakati anaanza Mahusiano nao hakujua kuwa walikuwa ni ndugu:

 Kweli nilitembea nao mbona kawaida kwani nilikutana nao muda mmoja? Kwanza nilivyotembea nao sikuwa najua kama ndugu.

Halafu isitoshe mimi sina makosa mwenye makosa ni Ali Kiba kwani alijua natembea na mdogo bado akanitaka”.

Gigy Money ameanika kuwa Mahusiano Yake na Ali Kiba na Abdu Kiba yalikuwa siku nyingi kabla hajaanza kuwa video vixen ambapo enzi hizo alikuwa anakutana na wasanii club ambapo alikuwa anapenda kutembea na wasanii.

Gigy Money Ajutia Kuanika Listi Ya Wanaume Aliotembea Nao

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kuelezea majuto yake kuhusiana na uamuzi wake wa kutaja orodha ya wanaume aliowahi kubanjuka nao.

Siku za nyuma Gigy Money aliwahi kutengeneza headlines baada ya kutaja listi nzima ya wanaume aliowahi kuwa na Mahusiano nao ambapo ndani yake kulikuwa na wasanii kadhaa.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Gigy Money amekiri anajutia kutaja orodha hiyo ya wanaume kwani mpaka leo kuna wanaume wanaogopa kumtongoza kwa kuogopa kuanikwa.

Kuwataja wanaume nilipitaga nao najutiaga sana, inafanya kuna muda nikose vitu vya maana kwa kuogopa kuwa nitaropoka. Kumbe ule ni utoto na ni foolish age kila mtu lazima apitie hata uikimbie ni bora uipitie ukubwani usiirudie. Kwahiyo najutia kuwataja wanaume niliowahi kutembea nao ila sijutii kupitia ile hatua“.

Listi ya wanaume wa Gigy Money ilijumuisha mastaa wa muziki wa Bongo Fleva na watangazaji wa Redio na Tv.

Namjua Stan Kabla ya Moj ;-Mama Gigy Money

Mama mzazi wa msanii Gigy Money amefunguka na kusema kuwa kabla hata hajaanza kumjua moJ ambae ndie inasemekana kuwa baba wa mtoto wa Gigy Money ingawa yeye mwenyewe anakataa na kusema kuwa mtoto huyo sio wa moj na kusema kuwa ni mtoto wa mwanaume mwingine.

Mama yake Gigy Money anasema kuwa kabla hajaletewa kutambulishwa moJ alishawahi kutambulishwa stan na mtoto wake, mimi namjua stan kabla hata ya huyo moJ . moJ mimi nimeenda kumkuta kwa gigy nyumban kuna kipindi mwanangu aliumwa ndio nikamkuta huko.

Mama Gigy Money anasema “kosa kubwa alilowahi kulifanya moj  aliwahi kumpiga sana mwanangu na nikampeleka kiyuo cha polisi mabatini lakini after two day nikawakuta wako pamoja sasa ningefanyaje,kwaio hapo kosa likawa la kwangu mimi nimeonekana nina kiherehere kampiga mwanangu kaumia na tayari alikuwa na mimba.Kitu kikubwa ninachoumia kwa moj ni kwamba alikuwa akimpiga sana mwanangu.

Nilimuuliza Gigy hii mimba ya nani akaniambia mama hii mimba ina baba lakini mimi nina mpenda sana moJ , kwaio hata moj anakaa  na Gigy lakini anajua mimba sio ya kwake.

 

Nai Adai Gigy Money ni Mnafiki na Sio Rafiki Mzuri Kwake

Video vixen maarufu Bongo Nai ambaye pia ni mpenzi wa msanii wa Bongo fleva Moni Centrozone ameibuka na kumtolea povu Gigy Money kwa kudai sio rafiki mzuri.

Gigy Money na Nai walionekana kuwa na ukaribu mkubwa siku za hivi karibuni hasa baada ya Gigy Money kuachana na Mo j na Nai kuachana na Moni centrozone.

Lakini ukaribu huo uliingia mdudu baada ya habari kusambaa kuwa Gigy anatoka na Moni na hata alibadilisha jina lake na kujiita Gigy Centrozone Kwenye Instagram.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, NAi anafunguka na kuweka wazi kuwa ameumizwa na kitendo kilichofanywa na Gigy Money ambaye amekiri kuwa sio rafiki mzuri kwake:

Gigy sio rafiki mzuri kwangu kwa sababu ni mtu ambaye anajaribu kuniongelea vibaya hata kwa Moni ambaye alimposti na kujibadilisha jina na pia kajaribu kumpelekea vitu vya uongo vingi ambavyo vimetufanya mimi na Moni mpaka sasa hatupo sawa.

Na pia naweza kudiriki kusema kuwa Gigy sio rafiki wa kweli kwangu hivyo nimemuweka pembeni nina maisha yangu mwenyewe sihitaji watu wanafiki”.

Nai amekiri kuwa Gigy Money alimtafuta ili wayamalize lakini amesema hataki Tena urafiki naye kwani ameharibu uhusiano wake na mpenzi wake Moni.

Nai Adai Gigy Money ni Mnafiki na Sio Rafiki Mzuri Kwake

Video vixen maarufu Bongo Nai ambaye pia ni mpenzi wa msanii wa Bongo fleva Moni Centrozone ameibuka na kumtolea povu Gigy Money kwa kudai sio rafiki mzuri.

Gigy Money na Nai walionekana kuwa na ukaribu mkubwa siku za hivi karibuni hasa baada ya Gigy Money kuachana na Mo j na Nai kuachana na Moni centrozone.

Lakini ukaribu huo uliingia mdudu baada ya habari kusambaa kuwa Gigy anatoka na Moni na hata alibadilisha jina lake na kujiita Gigy Centrozone Kwenye Instagram.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, NAi anafunguka na kuweka wazi kuwa ameumizwa na kitendo kilichofanywa na Gigy Money ambaye amekiri kuwa sio rafiki mzuri kwake:

Gigy sio rafiki mzuri kwangu kwa sababu ni mtu ambaye anajaribu kuniongelea vibaya hata kwa Moni ambaye alimposti na kujibadilisha jina na pia kajaribu kumpelekea vitu vya uongo vingi ambavyo vimetufanya mimi na Moni mpaka sasa hatupo sawa.

Na pia naweza kudiriki kusema kuwa Gigy sio rafiki wa kweli kwangu hivyo nimemuweka pembeni nina maisha yangu mwenyewe sihitaji watu wanafiki”.

Nai amekiri kuwa Gigy Money alimtafuta ili wayamalize lakini amesema hataki Tena urafiki naye kwani ameharibu uhusiano wake na mpenzi wake Moni.

Kim Nana Awatolea Povu Gigy Money na Lynn

Video Queen anayefanya vizuri kwa hivi sasa Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana amewapa kichambo cha maaana warembo wenzake Lynn na Gigy Money baada ya kurushiana matusi.

Wiki iliyopita kuna video clip ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyowaonyesha Gigy Money na Lynn wakiwa wanarushiana mitusi mizito mizito na hata kudaiwa kupigana.

Kim Nana amewatolea povu wasichana hao kwa kitendo walichofanya mbele ya jamii huku akidai jambo hilo linawafanya watu wawaone walio katika fani ya uvideo Queen ni wahuni tu kama wao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,  Kim Nana alisema hakufurahishwa na wauza nyago hao kusemeana mbovu hadharani kwani ingekuwa vema wakaitana pembeni na kugombana pasipo kuwapa watu faida hasa ikichukuliwa kuwa, wao ni kioo cha jamii.

Unajua wameshindwa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii na  maneno waliyokuwa wakirushiana yanafanya watu waidharau fani yetu na kuona kuwa ni ya kihuni kutokana na kuropoka ovyo mbele za watu“.

 

Gigy Money Adai Eti Diamond ni Baba Wa Mtoto Wake

Msanii wa Bongo Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amerudi tena Kwenye headlines huku safari hii akidai Baba wa mtoto wake MK staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Gugy Money alijifungua mwezi uliopita lakini tangu ajifungue aliweka wazi kuwa hamjui baba wa mtoto wake kwani kipindi anapata mimba alikuwa Anatembea na wanaume wawili ambao alisema ni Mo J na Stan.

Lakini sahivi Gigy ameibuka na jipya akidai Baba wa mtoto wake pia anaweza kuwa Diamond Platnumz ambaye siku za nyuma zilishawahi kusikika tetesi kuwa aliwahi kuchepuka naye.

Gigy Money amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Dizzim Online ambapo aliulizwa nani ni Baba wa mtoto na alifunguka:

Mo J sio Baba wa mtoto nilishasema Baba wa mtoto anaitwa Naseeb Juma Abdul au Diamond ambaye nanona bora yeye awe Baba kwa sababu ni Mlezi wa wana alafu na mimi mwenyewe Mlezi wa wana alafu kingine anapenda watoto alafu alishanichanaga Gigy ukizaa we niambie tu kwa wiki shilingi ngapi”.

Gugy Money amekuwa sana Kwenye headlines tangu ajifungue kwani ni wikiendi iliyopita inasemekana alipeana kichapo cha mwizi na mrembo Irene club.

Bifu la Gigy Money na Irene Lapamba Moto

Msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money aliyewahi kufanya vyema na ngoma yake ya ‘Papa’ amejikuta Kwenye bifu zito na video Queen Irene wa Kwenye wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’.

Siku ya jana kuna video ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyowaonyesha warembo hao wawili wakirushiana maneno ya kejeli na matusi ambapo inadaiwa wawili hao walipeana kichapo cha haja.

Kisa cha ugomvi wao kinawemekana kuwa ni kugombania mwanaume Lakini pia inasemekana kuwa kisa ni Diamond kwani Gigy Money ni rafiki wa karibu wa Mobetto ambaye ni mpenzi wa Diamond Lakini pia inasemekana Diamond anatoka na Irene.

Gigy Money na Irene walianza kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii muda mrefu lakini hatimaye bifu lao lilichukua sura mpya baada ya wawili hao kukutana Uso kwa Uso wikiendi iliyoisha.

Gigy Money Ametangaza Tena vita na Irene ambapo kupitia ukurasa wake wa Snapchat ameandika ujumbe huu:

Mrembo Kim Nana Adai Amber Lulu na Gigy Maney Sio Level Zake

Video Queen anayekuja kwa kiasi ya ajabu Kwenye tasnia Lilian Paul Kessy maarufu kama Kima Nana amewaponda vibaya mno wasanii Amber Lulu na Gigi Money huku akidai hawafai kuwa mavideo vixen.

Kim Nana alijizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video za wanamuziki kama Beka Flavor ameibuka na kudai mavideo Queen hao ambao wameongia Kwenye Bongo fleva hawakuwa level zake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, amefunguka na kudai ni bora wadada hao walivyoingia Kwenye muziki kwani hawakuwa na mvuto wa kuwa wauza sura wa Kwenye video:

Amber Lulu na Gigy Money hawanivutii kabisa na hawana mvuto wa kuwa ma-video queen. Bora ‘wa-stick’ hukohuko kwenye muziki walikokimbilia”.

Lakini pia mrembo huyo alijitamba ni bora kuliko mavideo Queen wote kwa Bongo kwa sababu ana muonekano wa kuwa hivyo tofauti na ilivyokuwa kwa Gigy Money na Amber Lulu.

Amber Lulu

Kim Nana alipoulizwa kuhusu tuhuma za mavideo Queen wengi Bongo kutembea na wasanii mbali mbali ili wapate umaarufu alikataa na kudai yeye yupo kikazi zaidi hana time hiyo:

Mimi ninajiheshimu, nikiitwa na mwanamuziki kuhusu kazi, tunafanya halafu basi. Tutaendelea kuwasiliana kwenye mambo mengine, lakini siyo mapenzi. Sijawahi kutoka kimapenzi na staa yeyote Bongo na sitarajii hilo kwa sababu kuwa na uhusiano na mastaa kuna-umiza kichwa. Wengi hawa-jatulia“.