Dogo Janja Asipoachana na Irene Uwoya Ataishia Kufa- Mo Music

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Mo Music ameibuka na kumpa ushauri Dogo Janja na kumtaka kuachana na Mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya.

Sio Siri ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja imetengenwza sana headlines siku za hivi Karibuni ambapo imekuwa ikisemekana Dogo Janja kapokonywa Mke na vigogo wenye pesa zao wanaoweza kumlea mtoto mzuri kama Irene.

Tetesi hizi zimepelekea Dogo Janja kuonekana kama mtu mwenye msongo wa mawazo kiasi ya kwamba kuonekana kwa Mwanasaiokolojia siku chache zilizopita.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Mo Music ameibuka na kumshauri msanii mwenzake kuachana na Uwoya kwani asipofabya hivyo anamtabiria kukutana na Kifo mbeleni.

Unajua vitu vingine watu wanajitakia wenyewe ningekuwa mimi ndio Dogo Janja nisingejiingiza kule kwa sababu ingawa wanaweza mapenzi sio umri lakini Hizi nyingine zinakuja kama laana angeatakiwa kuwa na mtu wa umri wake lakini sahivi ni kama vile pressure inamuendesha kuwa na mtu kama yule.

Nimesikia tetesi kama hawaishi wote nyumba moja sasa ndio ndoa gani hiyo lakini mimi kama kaka yake namshauri ajitulize na atulize akili ajue jinsi ya kucheza na familia yake lakini akiendelea huvyo hivyo ataendelea kuugua kupata presha mwisho wa siku Kifo kabisa”.

 

Mo Music Awatolea Povu Wanaosema Kapotea

Msanii wa muzic wa bongo fleva Moshi Matemi, maarufu kama Mo Music ameibuka na kuwatolea povu baadhi ya masgabiki wanaosema kuwa kwa sasa amefuia tangu wimbo wake wa kibajaji umetoka umekuwa haufanyi vizuri katika vyombo mbalimbali hivyo inasemekana kuwa ameamua kufuga kuku na kuachana na muziki.

Hata hivyo baada ya kutafuta na kuulizwa kuhusu tetesi hizo , mwana muzi huyo alidai kuwa kwake yeye game la muziki bado changa na wala hawezi kufulia sasa hivi, na wanaoisema wimbo wa kibajaji haujfanya vizuri ni muongo kwa sababu wimbo huo umekuwa ukipigwa sehemu mbalimbali  na swala la kuuza na kufuga kuku ilo ni jambo la kawaida kwake.

Mimi nimepotea? kivipi mbona nyimbo zangu zinapigwa sana radioni,na hata kama nitafuga hao kuku unaosema kwani cha ajabu hapo ni kipi?ninachojua mimi ni kuwa kibajaji imefanya vizuri tu, na hata game kwangu bado naliona changa.hao wanaoeneza maneno ya umbe a waendelee tu lakini ole wake nije nimgundueanasambaza maneno hayo.-Alifunguka Mo-Music.

Mashabiki wengi wamekuwa wakifatilia saa pale wanapoonda msanii wao yuko kimya kwa muda mrefu , ingawa jambo hilo huwa zuri wa sababu unampa msanii hamasa ya kufanya kazi, lakini pia inasaidia kuleta ushindani katika game.

Dini Yamnyima Mo-Music Mchumba wa Kuoa.

Msanii wa muziki wa bongo, Moshi Katemi maarufu kama Mo Music jina la kisanii, amejikuta akiingia katika wakati mgumu wa kupoteza mwanamke wake wa kuoa na kunyanganywa mwanamke huyo na mwanaume mwingine kutokana na tofauti za kidini.

Mo Music ambae amekuwa katika mawazo ya muda mrefu na kukosa furaha alimpoteza mpenzi wake huyo wa siku wa  nyingi aliyekuwa akijulikana kwa jina la Iptsam na walikuwa tayari wana mipango ya kuoana lakini baada ya kutokea mvutano wa kidini ndege huyo aliamua kupeperuka na kwenda kwai mwanaume mwingine anaendana nae kidini.

Akiongea na GPL, moja ya watu wa karibu wa Mo Music ambae ndio kilikuwa chanzo kikubwa cha habari hii alisema kuwa Mo Music alikuwa tayari ameshatoa mpaka mahari kwa wazazi wa mwanadada huyo nyumbani kwao  lakini tatizo likaja katika dini kwa sababu Mo Music ni mkristo na mwanadada ni muislamu  huku wote wakiwa hawajaridhika kutoka katika dini zao yaani hakuna akiyetaka kubadilisha dini na kumfuata mwenzake.

Baada ya kuvutana kwa muda mrefu binti huyo aliamua kuchumbiwa na mwanaume mwingine na kuolewa kabisa huku akimuacha Mo Muzic soremba bila hata kurudisha mahari.

Baada ya mwandishi kupata habari hIzo aliaamua kumtafuta moja kwa moja mhusika mkuu wa jambo hilo ambae ni mo muzic  ili kujua ukweli wa tukio hilo.dah umenitonesha kidonda klichoanza kupoa, ni kweli kabisa kuwa demu yule kaolewa  wiki iliyopita,kitendo cha kubadilisha dini kwangu kingewakera wazazi wangu, na ndio maana nikawa nasuasua na tupo kwenye mvutano waturudishie mahari yeti lakini wanauzungusha.-Alifunguka Mo-Music

Mo Music sasa hivi nafanya vizuri na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Kibajaji.

Mo-Music Ampongeza Aliyeamua Kumtuliza Gigy Money

Msanii wa kizazi kipya nchi Mo-Music amefunguka na kusema kuwa ameshangzwa sana baada ya kuona picha za msanii wa kike Gigy Money zilikuwa zikimuonyesha kuwa  ana mimba ukizingatia mwanadada mwenyewe alikuwa machachari na hakutegema kama mwanadada huyo atapata mimba hivi karibuni.

Mo-Music anasema kuwa hakuwahi kufikiria kuwa Gigy money atabeba mimba hivi karibuni ukizingatia kuwa alikuwa akisema kuwa hawezi kuwa katika mahusiano na mwanaume ambae hana ela lakini kitu cha ajabu ni kwamba mwanaume aliempa mimba ni wa kawaida sana hata halingani na maneno ya mwanadada huyo.

Hilo swala la Gigy Money limenikosha sana ,kwanza  alikuwa anasema anapenda mwanaume tajiri lakini jamaa mwenyewe alienae ana maisha ya kawaida tu, pia nampongeza sana jamaa kwa kuamua kumtuliza na mpaka sasa ameamua kuzaa.nawasihii na wasanii wengine wa kike waige mfano wake waache kuchoropoa mimba.

Gigy Money ambae kwa sasa ana mimba ya miezi saba alikuwa hataki kabisa kujulikana kuwa ni mjamzito lakini siri ilikuja kufichuka siku alitakiwa kuripoti katika baraza la sanaa nchini kutokana na kesi ya kuvaa nguo zeney kuvunja maadili ndipo aliposhangaza watu wengi baada ya kutokea akionekana katika hali hiyo ya ujauzito.

Hata hivyo watu wengi wamekuwa wakimshangaa na hata kumpongeza mwanaume aliyekuwa nae kutokana na ukweli kuwa Gigy Money ni moja ya wanawake waliokuwa wkaijitapa kuwa katika mapenzi wanajali sana malsahi ya ela kuliko kitu kingine.

Gigy Money akionekana kuwa mjamzito.

Gigy Money akiwa na mwanaume wake.

Mo Music Ndani Ya Bifu Zito na Timbulo

Mwanamuziki wa bongo fleva aliyetamba na vibao kama ‘basi nenda’ No music amefunguka na kudai kuwa anahisi kuwa Timbulo ana bifu naye kwa sababu amekuwa hapokei Simu yake akimtafuta.

Mo music alikuwa chini ya management ya Timbulo na McDenis lakini baada ya muda alihama na kuhamia management nyingine lakini baada ya kuhama aliamua kumaliza bifu na msanii mwenzie Timbulo lakini cha ajabu ameshangaa kuona kuwa anampotezea na kukataa kupokea Simu yake ili waweze maliza tofauti zao.

Mo music ameyaongea hayo kwenye mahojiano na Lilommy ambapo alifunguka mambo yafuatayo;

Kwanza mimi sijawahu kuwa na bifu na Timbulo maana mimi sijawahi kumchunia ila mwenzangu nimejaribu sana kumtafuta nimejaribu sana kumpigia Simu lakini anakuwa hapokei simu yangu lakini mimi namheshimu sana Timbulo maana ni moja ya watu wameweza kunisaidia mimi kuwa Mo music na pia ni kaka yangu alafu isitoshe amewahi kuwa kwenye gemu kuliko mimi kwaiyo kilichotokea ilikuwa ni misunderstanding kati yangu na yeye mimi nilikosea lakini na yeye pia alikosea baadhi ya vitu ambapo kuna mambo aliyazungumza kwenye media badala ya kunitafuta mimi kama mdogo wake tuyamalize wenyewe kwangu mimi niliona kama ameni disrespect kwa kweli”.

Timbulo alipotafutwa ili aongelee ishu hiyo alifunguka na kudai kuwa yeye binafsi hana tatizo na Mo music ila kama kweli hajamkosea ni kwanini ameenda kumuomba radhi redioni?Timbulo amedai kuwa tangu Mo music amehama uongozi amekuwa akitafuta kiki kupitia jina lake.