Nikki Mbishi Amjibu Dudubaya Kuwatetea Chege na Madee.

Siku chache zilizopita , msanii Dudubaya alitoa mapovu kuhusu wimbo wa madee na chege na kuwaambia kuwa wamekuwa wakifanya kazi zao huku wakijikita sana katika maazi ya kiafrika ya kusini kuliko ya kitanzania .Imekuwa kawaida kwa msanii Dudubaya kuwa akiponda nyimbo za wasanii wengine na kusema kuwa hawajui kufanya kazi za muziki.

Sasa basi amneno hayo yamemgusa , nikki mbishi na hivyo ameamua kumjibu  Dudubaya kwa kile alichokisema kuhusu Madee na Chege na kumwambia kuwa kama anaona wenzake wamekuwa wakikosea basi anatakiwa kutoa mfano wa hivyo vitu vizuri ili wasanii wengne wamuige na sio kukaa anaponda bila yeye kufanya kitu chochote.

unajua saa zingine kukaa unaongelea miziki ya watu wengine wakati wewe mwenyewe haujatoa kitu ambacho kiko perfect tukisikie, tuonyeshe basi mamba, dudabaya kwamba jiwe langu hili hapa sijaiga south wala wapi nyie mnaonaje, maana mimi ninaamini sana kwenye kutoa kazi kuliko kukaa kimya na kukosoa.

Nikki Atoa msimamo wake kuhusu maelezo ya BASATA

Msanii wa muzik nchini  nikki mbishi anaonekana kuwa na hasira na kukata tamaaa baada ya kuongea maoni yake baada ya BASATA  kuongea yao kuhusu muziki.

Rapper Nikki Mbishi kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa kwa sasa wasanii wa muziki watafute kazi nyingine ya kufanya kwani ya sanaa ya muziki nchini imeshakufa na hakuna namna.

Kwanza kampuni zenyewe hazitoi deals kwa wasanii directly mpaka middleman ahusike na analipwa cha udalali bado BASATA nao wanataka hapo hapo duh, wasanii tutafute cha kufanya sanaa ishakufa, chemchemi za mapato zinazidi kukauka..Ukisoma ajira hakuna,ukijiajiri vikwazo juu ya vikwazo mpaka ujasiriamali unakushinda,mbona awamu tutarudi vijijini kuchoma mkaa na Best Nasso japo Wizara ya mali asili na utalii nayo itakuja kubana tena.“amesema Nikki Mbishi na kuifungukia serikali.

Laiti Serikali ingetazama uwiano wa waajiriwa na waliojiajiri isingeweka terms kandamizi kiasi cha watu kujipiga mpaka risasi wenyewe maana tunakoelekea Mungu sitiri..Nchi yako mwenyewe ila unaweza hata kukufuru ukajiuliza “Hivi mimi nafanya nini hapa Duniani?”. Kuna siku biashara ya muziki wetu itakuwa kama ile ya kuuza madawa ya kulevya tu,maana utaambiwa santuri zako zote HARAM.“ameandika Nikki Mbishi.

Kwa upande mwingine Nikki wa Mbishi ameenda mbali zaidi na kudai kuwa kama kungelikuwa na uwezekano basi Mungu angepeleka miaka 20 mbele ili kuwe na uwezekano wa kuivunja BASATA kwani haipo kwa ajili ya kulea wasanii.

Mungu angepeleka mbele miaka hata 20 leo iwe 2038 labda tungeanua matanga ya mawazo mfu tupate mawazo mapya yenye manufaa kwa kizazi kilichopo..Vunja BASATA jenga hata BAR watu walewe maana haitulei bali inatutesa tu,“ameandika Nikki Mbishi

Mitandao ya Kijamii Inaleta Wivu Baina ya Watu:-Nikki Mbishi

Msanii wa rap nchini , Nikki mbishi amefunguka na kutoa maoni yake juu ya athari kuwa zinazoletwa na mitandao ya kijamii  nchini hasa kwa wasanii ambao wanakuwa wanasikiliza sana maneno ya mitandaoni.

Nikki anasema kuwa moja ya athari kubwa ya mitandao ya kijamii ni kuleta wivu  na chuki kwa watu wanaoitumia kutokana na amneno yanayokuwa wakizushwa na pengine kusambaa  kwa kasi katika mitandao ya kijamii huku maneno hayo mengine yakiwa yanachafua jina la wahusika,

Nikki anasema kuwa kuna watu pia wamekuwa na taia ya kujitangaza kuwa wana mali nyingi na kuwafanya wenzao kuwaonea wivu hata kuwachukia  na mwisho wa siku kuna kuwa hakuna ukweli owowte juu ya umiliki wa mali hizo.

Mitandao ya kijamii inajenga wivu miongoni mwa watu,unakuta mtu anajitangaza mara ana hiki mara ana kile watu wanajikuta wanapata chuki na kuanza kumchukia kumbe hana hata kitu ni maisha ya mtandaoni tu.

 

Nikki Mbishi- Watangazaji Acheni Kuuliza Maswali ya Diamond na Ali Kiba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nikki Mbishi amefunguka kuhusu kuchoshwa na Watangazaji wa vyombo vya habari ambao wamekazania maswali ya Diamond na Ali Kiba.

Diamond na Ali Kiba ni wasanii wakubwa kabisa wa Bongo fleva Lakini pia bifu walilonalo limekuwa likileta mgawanyo baina ya wasanii mbali mbali.

Hivyo ni swali la kawaida kwa wasanii kuulizwa kama wanapenda muziki wa Diamond au Ali Kiba lakini swali hilo limeonekana lumkera Nikki Mbishi ambaye amemwaga povu zito.

Nikki Mbishi amesema katika interview maswali kuhusu Diamond na Alikiba ndio hushamiri ila anachojivunia ni kwamba na yeye uhoji pia.

Kwenye m ukurasa wake wa twitter Nikki Mbishi amefunguka haya:

Kila interview wanauliza “Una mpango wowote wa kufanya ngoma na Ali Kiba au Diamond?” Hapo basi mtangazaji ndio anajiona kamaliza mwenyewe…#UFALA

Wakiitwa wengine interviews wanahojiwa ila nikiitwa mimi nawahoji wao ndio maana wanakuwa mabubu nikitimba….I’m proud of it. Great monday to all pointless and dumb presenters out there,peace!”.

 

Bongo Movie Wanadai Haki Zao Wanasahau Kazi Zao Mbovu-Nikki Mbishi

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya rap, Nikki Mbishi amewatushia wasanii wa tasnia ya filamu Tanzania Bongo movie na kuwataka waache kulalamika kuhusu kazi zao wakati kazi zao mbovu.

Nikki Mbishi alitoa kombora hilo alipokuwa anafanya Interview na Bongo 5 ambapo aliulizwa kama tuzo zilizoanza za SZIFF zitasaidia kuinua tasnia ya Bongo movie ambayo imekuwa ikizorotw:

Jamani saa nyingine tuseme ukweli tu hawa wasanii wanalalamika wanadai haki zao lakini kitu ambacho mimi naamini ni kuwa mnalalamikia nini maslahi yapi ambayo  hayaendani kabisa na ubora wa kazi zenu? Kazi mbovu alafu mnalalamika nini badala mkae mjijenge mtoe kazi za maana”.

Siku za hivi karibuni kuna sintofahamu ambazo zimetokea ambapo tangu tuzo za SZIFF zifanyike kuna mkanganyiko umetokea miongoni mwa wasanii wa Bongo movie ambapo kila mmoja anataka ashinde tuzo.

Tumeteswa Sana na Media Nyingine, Asante WASAFI Tv Kwa Kuleta Usawa-Nikki Mbishi

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap kuchana Nikki Mbishi ameibuka na kuimwagia sifa lukuki Wasafi Tv baada ya kupiga nyimbo yake.

Nikki Mbishi amefunguka na kudai kuwa amefurahishwa na mwanzo mzuri wa Wasafi Tv kwani imeonekana kupiga nyimbo za wasanii mbali mbali bila ubaguzi wala upendeleo wowote.

Nikki Mbishi amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika waraka huu kuisifia Wasafi Tv:

Asante Wasafi TV nyie mmecheza wimbo wangu #NIMEKUMISS bila hata mimi kuwaletea, najua ndio mnaanza ila msisahau kuendelea hivi hivi. Hakuna kitu kinachojenga na kuimarisha misingi ya sanaa kama ushindani wenye usawa “Fair Competition” hii inamaanisha anayestahili na apate na asiyestahili akose japo fitna zipo tu.

Tumeshuhudia umwinyi na ubeberu kwa kipindi kirefu sana,wapo ambao walitaka uMungu mtu lakini walijishtukia wakabwaga na wengine walibwagwa na hiyo ni kwa sababu ya kuleta umatabaka wa kanda fulani na kanda fulani na kujuanajuana sana kiasi kwamba akina sisi tusiofungamana nao tukaishia kutengwa na kuonekana “VINEGA” Kila la kheri kwenye hii ligi ya mbuzi kuna siku daraja litapanda tutacheza ya ng’ombe na mpaka tembo nini simba. Ipo siku watajihoji na kujijibu wenyewe“.

Wasafi Tv imeonekana kupiga nyimbo ambazo ni za wasanii ambao ni wazi kabisa wana bifu na Diamond kama vile Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Lady JD, Nay wa Mitego na wengineo.

Nikki Mbishi Awa-mind Wasanii Wanaotengeneza Muziki kwa Kiki

Msanii mkongwe wa muziki wa hip-hop nchini, nikki mbishi amefunguka na kusema kuwa amekuwa akichukizwa sana na wasanii ambao wamekuwa wakitengeneza muziki wao kupitia kiki ambazo muda mwingine zinakuwa hazina msingi wowote.

Nikki anasema kuwa wasanii wengi sasa hivi hawafanyi kazi kabisa zitakazo wavutia mashabiki, badala yake wanakuwa wanajiingiza katika maswala ya ajabu ili kupata kiki ili wimbo wake ukitoka basi aweze kupata mashabiki wengi kitu ambacho hawezi kukifanya katika kazi zake.

kuna wakati ulifika au sijui kama bado huo muda bado upo,matukio ya kisiasa yalianza kufunika matukio ya kimuziki mtu anatoa ngoma yako alafu anataka kusikia mambo yako mengine .

Akiongezea kuhusu uwepo wa matukio ya kisiasa kwa wasanii ,nikki anasema kuwa wasanii wengi wamejikuta wakijihusishwa na matukio ya kutekwa na kupotea ili anaporudi anakuwa tayari ameshatengeneza attention kwa mashabiki zake.

Ilifika sehemu ikawa kwamba mtu anaona kutekwa na kupotea kwenda kusikojulikana ndio kiki inayoweza kumfanya auze,inaonekana kama hiyo ndio dili ,kwaio kila mtu anajifanya kama vile ndio kapotea , katekwa , mara sijui kausishwa na mambo gani  na serikali ilimradi iwe hivyo tu.

Wasanii wengi bongo wamekuwa na tabia ya kutengeneza skendo kubwa itakayo muhusu yeye au watu wake wa karibu ili kuwavutia watu na kumfanya apate watu wengi watakao kuwa wanamfuta , hii inamfanya apat mashabiki wengi kiasi kwamba akiachia wimbo wake mpya inakuwa ni rahisi kuuza.Kitu ambacho Nikki Mbishi amekuwa akikipinga kabisa.

Hivi sasa Nikki Mbishi anafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na wimbo wake wa Nimekumiss.