Mwl Nyerere Alisema Acheni Wakongo Wafundishe Wabongo Muziki:-Nyoshi

Msanii wa muziki wa Dansi Tanzania mwenye asili ya  Congo,Nyoshi el sadaat amefunguka alipokuwa akiongea na clouds media na kusema kuwa katika bandi yake kuna watanzania wengi sana kuliko idadi ya wakongo kwa sababu anataka watanzania pia wajifunze muziki kupitia wao.

Nyoshi ambae wikiend hii anatarajiwa kufanya shoo kubwa sana katika ukumbi wa Escape One anasema kuwa kazi kubwa alionayo ni kuhakikisha kuwa vijana wa kitanzania wanaotaka kujua muziki kupitia yeye wanafanikiwa katika hilo.

baba wa taifa mwalimu nyerere  alishawahi kusema kuwa acheni wakongo wawafundishe muziki wabongo, na ndio maana kwenye band yangu wabongo ni wengi kuliko wakongo.

Nyoshi:-Nikimuoa Gigy Money, Watoto 10 Tutazaa.

Msanii wa miondoko ya dansi nyoshi el-sadaat amefunguka na kuongea yake ya moyoni mwake kuhusu kumpenda sana kimapenzi msanii wa bongo fleva asieishiwa na drama kila siku gigy money ambae amejifungua miezi michache iliyopita.

nyoshi anasema kuwa amekuwa akimpenda ukweli mwanadada huyo na kama asingekuwa amewahiwa na mwanaume mwingine basi angemuoa yeye na hata kuzaa nae watoto 10  kwa sababu ya upendo wake.

Gigy money mimi nina mpendaga sana, nina penda tu yale mambo yake yananivutiaga sana, kwa bahati mbaya ameshagakuolewa  na bwana yake lakini kama angetokea na nini na nini , ningefanya hayo tu na kuamua kumuoa tu kwa sababu si mwanamke kama wanawake wengine tu nashindwaga kumuoa.kwa mfano ningemuoa Gigy money watoto kumi ndio vizuri.

Nyoshi Amjibu Dudu Baya Kuhusu Wasanii wa Dansi kufulia.

Msanii wa dansi nchini Nyoso El Sadaat amemjibu Dudu Baya baada ya msanii huyo wa bongo fleva kuwajia wasaniwa dansi na kuwaambia kuwa wamefulia sasa hivi kwa sababu walizoea kuomba msaada kutoka kwa matajiri na kwa sababu hali ya uchumi sasa hivi kila mtu anajibana na ndio maana hakuna wanachofanya zaidi ya kufulia.

Dudu bata alisema “wasanii wa dansi sasa hivi ni wachafu sana , wamefulia tu hawana tena watu wa kuwaomba ela kabisa.Walikuwa wamezoea kuomba ela , awamu hii wa Magufuli watapata  tabu sana.

Hapo ndipo alipompanikisha Nyoshi na ndipo alipomjibu kuwa wao hawawezi kufulia hata siku moja kwa sababu mabosi wao mpaka sasa wapo na wanaendelea kutoa pesa na hakuna kitu kama icho kinaweza kutokea.

Mabosi wapo na hata uko kuwataja hakumaanishi kwamba tunawabebeleza watupe ela wao huwa wanatoa tu, kama kufulia tungefulia kwenye nguo mngeona tunavaa vibaya mbona tunapiga pamba kama kawaida tu hata hii miwani yangu kuna mtu kaniomba nimpe.