Muonekano wa Msanii Ndio Unaouza Kazi zake.:-Tammy the Baddest

Msaii wa rap wa kike nchini Tanzania , Tammy the Baddest amefunguka na kusema kuwa kwa kawaida kitu kikubwa kinachoweza kuuza kazi ya msanii ni muonekano wake kwanza kabla ya kazi yake yenyewe.Na hii inakufanya watu wakuone kuwa wa thamani hata kutamani kufanya kazi na wewe.

Msanii kama msanii hasa mtoto wa kike ni lazima uwe full package,sio uonekane tu unafanya muziki basi, no! u have to sale.ili kuuza ni lazima uwe na muonekano mzuri , ili hata kama unashida mtu aone mmmh yani kumpa show tammy kwa kiasi fulani , hapana.

Tammy pia amesema kuwa hata yeye amekuwa akijari sana muonekano wake ingawa kuna muda inampa changamoto kwa sababu mashabiki na watu wanaomuona wanahisi kama ana ela sana.

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo,‘Tammy The Baddest’ aeleza kwanini anapenda nguo fupi fupi

Kama mnamjua Tamara Ally ‘Tammy The Baddest’ basi unaelewa mavazi ambayo yeye huyavaa kwenye video zake. Si siri kuwa anapenda vitu fupi ambazo humuacha akikaa ni kama yuko uchi, lakini hiki ni kitu cha kawaida kwake.

Katika interview na Global Publishers msanii huyu alisema kuwa yeye amezoea mavazi ya aina hii na hata akiwa nyumbani kwao na wazazi wake yeye huvaa hivi kwani wamemzoea nahata hivyo si ajabu kitu cha ajabu.

Tammy
Tammy

Aliendelea kusema kuwa kukaa nusu utupu anajichukulia poa kwani ni kawaida mwanamke kujiachia na lifestyle yake.

“Mchumba utupu mara kwa mara kuwa ni mazoea.kukaa nusu utupu wangu mwenyewe ananichukulia poa kwani ni kawaida mwanamke kujiachia just life style tu, hata kwenye video yangu (Mtoto wa Kike) nimeonesha hadi nguo ya ndani mbona ni vitu vya kawaida tu jamani.”

Sasa hivi anapepea na nyimbo yake mpya ya Mtoto wa Kike ambayo yeye pia anaonekana kuwa nusu uchi.