Mameneja Wa Diamond Wadaiwa Kuhusika na Kusambaza Video Ya Ngono Ya Nandy

Kama utakumbuka mwezi uliopita jiji zima lilizizima baada ya video ya ngono iliyomuhusisha msanii wa Bongo fleva Nandy na Billnas kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha skendo kubwa kwa wasanii hao.

Chanzo cha video hiyo hakikujulikana kwa sababu Nandy na Billnas wote walikataa kuhusika na kusambazwa kwa video hiyo lakini aliyeiweka video hiyo Mtandaoni ni kurasa ya Udaku inayojulikana kama UdakuTz.

Sasa tangu wikiendi iliyopita kuna taarifa zilizodai kuwa mmiliki wa kurasa hiyo ya udaku ametekwa na watu wasiojulikana kwani familia yake haijui alipo, mpaka jana ambapo ilidaiwa alichukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano juu ya kuvuja wa  video ile ya Nandy na Billnas.

Lakini taarifa iliyotolewa jana na mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown ni kuwa mmiliki wa kurasa hiyo yupo kituo cha polisi na Kwenye mahojiano hayo amewataja watu waliompa video hiyo avujishe ambao walikuwa ni mameneja wa Diamond ambao mi Salaam SK na Babu Tale.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Soudy Brown aliweka posti hii:

Mpaka sasa haijajulikana kama Watajwa hapo juu  ambao wote ni mameneja wa Diamond wameshatiwa mbaroni au bado.

Lakini pia haijawekwa wazi ni vipi Msanii Diamond anahusika vipi katika hilo lakini yote hii inarudi katika bifu la Diamond na Clouds Media.

Harmonize- Wanaume Waaminifu Africa Wanatoka WCB

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize amefunguka na kudai kuwa wanaume waaminifu kutoka Africa Mashariki wanatoka WCB.

Kwa mara ya kwanza kauli  kama hiyo ilitolewa na mmoja kati ya mameneja wa WCB, Babu Tale mapema mwaka jana ambapo ilipingwa na watu kadhaa ikiwemo Aunty Ezekiel.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia Mambo Mseto, Citizen Radio kuwa kitu hicho ni cha kweli kabisa na uamifu wao umevuka mipaka, sio Bongo tu.

Ni kweli kabisa asilimia mia moja, hamna matukio halafu sisi ndio tunangoza kwa kusalitiwa“.

Kauli hii Inawaacha hoi watu wengi kwa sababu karibia wasanii wote WCB wanakabiliwa na skendo za kuchepuka kuanzia tu na CEO mwenyewe Diamond Platnumz ambaye skendo yake ya kuchepuka na Hamisa wakati yupo na Zari ilitrngeneza headlines.

Wanaume Waaminifi Wanatoka Wcb:- Harmonize

Msanii wa muziki anaefanya vizuri sasa katika tasnia ya muziki Harmonize amefunguka na kusema kuwa wanaume waaminifu na wenye upendo kwa wanawake zao wanatoka katika lebel ya WCB na wala sio kwingineko.

Kauli hiyo ambauo kwa sasa inarudiwa kwa mara ya pili na msanii huyo kwa mara ya kwanza ilisemwa nameneja wao babu take na kusema kuwa hakuna mwanaume wa WCB ambae sio mwaminifu katika mapenzi na kama watu wanataka kuamini hilo wajaribu.

Hivyo kwa kukazia hapo , Harmonize anasema ni kweli kuwa wanaume waaminif wanatoka WCB alipokuwa akiongea na mambo mseto ya citizen radiuo nchini  kenya.

ni kweli kabisa wanaume waaminifu wanatoka wcb  kwa asilimia mia 100 na hamna matukio halafu sisi ndio tunaongoza kwa kusalitiwa 

Alipoulizwa kuhusu mahusiano ya bosi wake Diamond ambae amekuwa na mahusiano na warembo tofauti tofauti Harmonize alijibu kwa kifupi kuwa hawezi kuzungumzia hulo lakini yeye kwa sasa yuko na Sarah tu.

Diamond Atangaza Kuja na Reality Show Ya Maisha Ya WCB

Staa wa Muziki wa Bongo fleva na CEO wa label ya WCB m, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa reality show kitakachoonyesha maisha halisi ya Label yake ya WCB.

Diamond ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa habari hiyo njema kwenda kwa mashabiki zake.

Kipindi hiko ambacho kitaonyesha maisha halisi ya kundi Zima la WCB kinatarajiwa kurushwa Wasafi Tv hapo siku za mbeleni.

Diamond alitoa taarifa hiyo alipokuwa njiani kuelekea nchini Uingereza ambapo anaenda kupiga shoo yake ya ‘A boy From Tandale’ ambapo aliandika:

Moja ya kitu ambacho nakisubiri kwa hamu ni ndani ya Wasafi Tv ni reality show ya WCB Wasafi…..wacha wamalize kutest signal zao wamwage maji tuoge kama kambale…. Na mnatujuaga siye hatujui kuficha yote mtayaona”.

 

 

TID Amtupia Dongo Diamond Kwa Kujiita Simba

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kwa Jina la usanii kama Top In Dar (TID) amedai yeye ndiye mwanzilishi wa jina la mnyama.

Hivi siku za karibuni kumekuwa na ugomvi wa marina baina ya wasanii kama juzi tu Afande Sele kamaliza mgogoro na Diamond kisa jina la Simba ambalo kila moja alidai la kwake.

TID ameibuka na kudai yeye ndiye mwanzilishia wa kutumia jina la Simba na hata kudai jina hilo alipewa na mashabiki zake kwa sababu ya kazi zake anazofanya akiwa stejini.

Kwenye mahojiano na kipichi cha On The Street cha ETV, TID amefunguka haya kuhusu jina hilo la mnyama:

Kwa mfano mimi perfomance zangu wanasema ni kali, yaani za kinyama, kwahiyo mimi nilikuwa nafanya kinyama ndipo mashabiki walipo amua kunipa jina la mnyama, mpaka sasa mimi ni mnyama kutoka unyamani.

Lakini sio mbaya sasa hivi nasikia kuna wengine wanajiita Simba, nimewa-inspire kuwa hivyo, kuna wengine ni wakufungwa, lakini ndio mnyama wenyewe”.

TID hana uhusiano Mzuri na WCB kwa ujumla kwani wiki chache tu zilizopita alitoka kutoa povu kwa Wasafi baada ya kudaiwa alikuwa anaomba kazi.

Baada Ya Tetesi Za Kusainiwa WCB, Barakah The Prince Azungumza

Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefungukia tetesi ambazo zimekuwa zikisambaa kwa muda mrefu sasa kuwa amejiunga na label ya WCB.

Tetesi za Barakah kusainiwa WCB zilianza kushika kazi siku za hivi karibuni baada ya kuonekana ana ukaribu na wasanii wa label hiyo na hata wadau wa WCB.

Lakini tetesi hizi ziishika hatamu zaidi pale Barakah alipodaiwa kutengeneza kiki ya uongo ya Rommy kumtongoza mpenzi wake Naj ilimradi watangaze ngoma yao mpya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Rick media, Barakah The Prince amekana tetesi za yeye kujiunga WCB na kudai ni marafiki tu wa karibu:

Hapana, WCB ni kama familia yangu, mara nyingi hata mameneja wa WCB ndio wanakuwa wananiongoza na kunielekeza nifanye nini.

“Kwa hiyo tumeamua kuwa kama familia na kuna wasanii wengi wanafanya vizuri, lakini sio kwamba nipo chini ya WCB, no siyo kweli“.

Hapo nyuma Barakah hakuwa na ukaribu na WCB mpaka pale alipojitoa Kwenye label ya Rockstar 4000 ya Ali Kiba.

Nedy Music Atamani Kufanya Kazi na Alikiba na WCB

Msanii wa Bongo fleva Nedy Music anayefanya vizuri hivi sasa na wimbo wake wa One and only amefungukia mipango yake ya kufanya Kolabo na staa wa Bongo fleva Alikiba Lakini pia kusainiwa WCB.

Nedy Music anayefanya muziki wake chini ya label ya PKP ya msanii Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo itatokea nafasi ya yeye kusainiwa WCB basi ataichukua kwani ni uamuzi wa kibiashara:

Nedy Music amefungukia  kusaini katika label ya WCB amesema ikitokea nafasi hiyo atasaini kwa sababu ni biashara, pia amekanusha taaarifa za kuachana na label yake ya PKP mara baada ya wimbo wake mpya kutoka bila kuwa na logo ya label hiyo.

Kwenye Interview aliyofanya na The Playlist ya Times Fm, Nedy Music aliweka wazi kuwa yupo tayari kufanya kazi na Ali Kiba lakini anataka afanye naye kazi huku watu waone amestahili kufanya naye kazi kwa ajili ya kipaji chake alichonacho na sio sababu anamfahamu tu Kiba basi ndio afanye naye Kolabo:

Unajua usifanye kitu kimazoea, usifanye kitu kwakuwa unajuana na mtu nilitamani watu wajue uwezo wangu, nikiwa na maana hata pale ninapoenda na kazi nataka afanye na mimi basi pawe na urahisi na si kinyonge atafanya kwa kuwa tunajuana, kwa hiyo ni wazo bado lipo na panapo majaliwa litatokea”

.

Dansa Wa Diamond Akumbwa na Skendo Ya Kutelekeza Mtoto

Dansa kutoka WCB ambaye mchezo shoo wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zungu amekumbwa na skendo ya kuwa mmoja kati ya wanaume waliotelekeza watoto wao Dar.

Siku ya jumatatu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliwakusanya wanawake wote ambao wametelekezwa na wanaume ambao wamezaa nao ambapo hawawahudumii watoto wao.

Mmoja kati ya Wanawake waliojitokeza ni mwanamke ambaye alijitambilisha kama mzazi mwenza wa Dansa wa  Diamond anayejulikana kama Zungu ambapo amedai alimtelekeza yeye pamoja na mtoto wake baada ta kuachana ambapo amekuwa hataki kumtunza mtoto wake.

Baada ya tuhuma hizo Zungu alitafutwa na Timamu Tv ambapo amefunguka na kusema yule mwanamke ana matatizo ya akili pia ni mkorofi na amedai kuwa hajawahi kumkataa mtoto wake na amesema yupo tayari hata leo kwenda kwa Makonda na kujielezea na kama ikitokea anatakiwa amchukue mtoto wake amesema yupo tayari kumlea mwanaye mwenyewe.

NInastahili Kuwa Msanii Wa WCB- Mbosso

Mwanamuziki wa Bongo fleva Marombosso maarufu kama Mbosso ambaye amesainiwa chini ya label ya WCB amefunguka na kusema kuna muda utafika watu wote watajua kuwa anastahili kuwa msanii wa WCB.

Mbosso amefunguka hayo baada ya kuona kuwa anakosolewa sana na baadhi ya watu ambao wanaona kama hana kipaji kikubwa cha kuweza kuwa msanii wa label hiyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na TBC Fm, Mbosso amefunguka na kuongea mengi kuhusiana na uwezo wake katika label hiyo:

Kuna muda unaweza ukafanya kitu kwako wewe kipo sawa na unajaribu kukiwakilisha kwa njia iliyo sawa lakini inafikia hatua anaona hakiko sawa anafikia hatua hata ya kukutukana matusi, inafikia hatua mtu anakutukana mpaka matusi ya mama yako.

Lakini huwezi kumzuia mtu kufanya hivyo vitu ila kuna muda utafiki kila mtu atajua Mbosso kumbe anastahili kuwa WCB au anastahili kupewa hiki ambacho anapewa sasa hivi“.

Mbosso alijipatia umaarufu wakati alipokuwa katika kundi la Yamoto Band, Baada ya kundi hilo kuvunjika Mbosso alijiunga na timu nzima ya WCB rasmi mwaka huu tarehe 28 januari.

Amber Lulu- Natamani Sana Kusainiwa WCB

Video vixen maarufu na msanii wa Bongo fleva Amber Lulu amefunguka na kuongelea mipango yake ya kutaka kusaini chini ya label maarufu Bongo WCB inayomilikiwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Amber Lulu ambaye alijulikana kutokana na kuuza Mushi kwenye video za wasanii mbali mbali wa Bongo fleva na vituko vyake. Hivi sasa Amber Lulu kwa hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya jini kisirani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Sam Misago Tv, Amber Lulu amefunguka na kuweka wazi kuwa anatamani sana kufanya kazi chini ya WCB:

Natamani hata kesho niweze kusainiwa WCB na naomba niseme kuwa namtegemea sana Diamond kwa sababu yeye ni kaka yangu ambaye amenitangulia kwaiyo kwa upande wangu nina mipango mingi sana na Diamond na WCB kwa ujumla ingawa najua yeye ana mambo yake na ni mtu mkubwa kumpata inakuwa ngumu lakini natamani siku moja nije kufanya naye kazi na ninatamani niwe msanii wa kwanza kusainiwa WCB baada Queen Darleen”.

Hivi sasa Amber Lulu anafanya vizuri na wimbo wake wa jini kisirani na amekiri msanii anayetamani sana kufanya naye kazi ni Rayvanny kutoka WCB.

 

Diamond na WCB Wamuegemea RC Makonda

Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa label maarufu ya WCB, Diamond Platnumz na timu yake nzima imefunguka na kusema inamtegemea Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kusimamia suala la nyimbo kufungwa.

Siku chache zilizopita Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza rasmi kuwa jumla ya nyimbo 13 za wasanii mbali mbali zimefungiwa akiwemo Diamond ambaye alifungiwa nyimbo zake mbili ambazo ni Halelujah na Waka waka.

Tangu taarifa zisambae kuwa nyimbo mbili za Diamond zimefungiwa Kumekuwa na hisia hasi juu ya suala hilo na sio ndani tu ya Tanzania bali hata kwa mashabiki walio nje ya Tanzania.

Lakini tangu sakata hilo litokee Diamond hajaongelea chochote kuhusiana na ishu hii lakini uongozi wake meneja wake Salaam Sk amefunguka na kusema hawawezi kuongelea suala hilo ila kama kuna mtu ana maswali juu ya hilo akaongee na malezi wao RC Makonda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Salaam SK aliandika ujumbe huu juu ya ishu hiyo:

Habari za muda huu waungwana, Tumepigiwa simu na waandishi wa habari kila kona kuhusu nyimbo mbili za Diamond zilizofungiwa, nimeona kama taasisi huwaga tunafanya vitu kwa kutokukurupuka sie kama WCB tulipoona taasisi yetu inakuwa kubwa tukaomba ulezi kwa Paul Makonda ambaye ni kiongozi wa serikali mwenye kupenda maendeleo ya vijana kwaiyo nyimbo zote za WCB kabla ya kutoka lazima azipitie, kuna nyimbo nyingi ameshazizuia na zinazotoka ameziridhia yeye binafsi zitoke, kwaiyo sioni sababu ya nyimbo ya halelujah na wakawaka kufungiwa kama inavyosemekana  maana sisi hatujapata barua ya nyimbo hizo kufungiwa na kama zimefungiwa mlezi wetu ataongea zaidi”.

 

 

Zamaradi Mketema Kuoneka Mubashara Ndani ya Wasafi Tv

Muigizaji mkongwe Zamaradi Mketema amethibitishwa kuanza kuonekana live kama mtangazaji katika redio station na televisheni station mpya ya Wasafi Tv and Radio inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz.

Suala hili Limekuja baada ya ukimya mrefu aliokuwa nao Zamaradi Kwenye anga ya utangazaji. Mara baada ya Zamaradi kumuacha aliyekuwa mpenzi wake na Baba watoto wake mkurugenzi wa Clouds Fm Ruge Mutahaba na kuolewa na mwanaume mwingine mwaka jana Zamaradi aliacha kazi Clouds Fm pia.

Mapema mwaka huu kuna tetesi zilisambaa kuwa Zamaradi atajiunga kwenye redio mpya ya Diamond lakini zilikuwa ni tetesi tu lakini mpaka jana usiku tunaweza kuthibitisha kuwa ni taarifa za kweli kabisa na mpaka hivi sasa Zamaradi yupo na timu nzima ya WCB.

Hamornize alithibitisha taarifa hizi kwa kuweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram na kusindikizwa na ujumbe wa kumkaribisha Zamaradi ndani ya Wasafi Tv:

Let’s go Mama Juju welcome to th Family Wasafi Tv”.

Zamaradi na Diamond Pamoja na timu nzima ya WCB wapo visiwani Zanzibar kwa ajili kufanya zoezi la kusaka vipaji vipya vya watangazaji ambao watafanya kazi katika kituo hicho kipya cha Wasafi tv.

 

Picha za Wema,Esma na Wcb Zazua Mjadala Mitandaoni.

Huku bado mahusiano ya kimapenzi katika ya Diamond na Zari yakiwa bado hayajakaa sawa baada ya Zari kusema kuwa hana mapezni tena na Diamond Platinumz kutokana na kuwa na tetesi nyingi za kuwa na wanaume tofauti tofauti, huku upande wa pili mambo yanazidi kupamba moto kutokana na ukaribu walionao Wema Sepetu na Esma Platinuzm .

Wema Sepetu ambae ni miss tanzania inasemekana kuwa ni ndo chanzo kikubwa cha kuwafanya Zari na Diamond kuachana baada ya kuonekana kuwa karibu na Diamond siku za hivi karibuni anazidi kuoneka kuwa karibu na wasanii wa wcb na  dada yake Diamond ambae pia siku za nyuma ilisemekana kuwa hayupo kribu na kaka yake wala aliyekuwa wifi yake (Zari) kwa madai kuwa wawili hao walikuwa wana mgogoro.

Tetesi za Esma kuwa na chuki na Zari zinaanza kuthibitika kwa sababu ya ukaribu mkubwa aliyonao na wema ambapo hapo mwanzo kipindi mwanadada huyo amegombana na Diamond hawakuwa kama walivyo sasa na hata kuanza kuonekana katika events mbalimbali za lebo hiyo.

wakioenaka kuwa karibu siku ya uzinduzi wa club ya Rommy Jonnes inayojulikana kama Octagon, Wema Sepetu alikuwa karibu na kila msanii kutoka wcb, huku kampani yake kubwa ikiwa na Esma ambae ni dada yake na Diamond.

                                                                

Wema sepetu akiwa na wasanii wa wcb.

                                                                        

                                                                Alichoweka Esma snapchart

 

                                                         Alichokipost Wema snapchart .

Diamond Kuipeleka Wcb Nje ya Tanzania.

Inavyosemekana kuwa Wcb ndio lebo kubwa nchini na nje ya nchi kwa ukubwa na kudumu katika industry ya muziki, wasanii wengi wanataka kuwa  kama Diamond katika msimamo wa kutaka kuimarisha lebo zao.

Hata lebo nyingi zilizoanzishwa sasa zimekuwa zikiiga mfano mzuri wa diamond platinuzm katika kutengeneza lebo na kuisimamai kama anavyosimamaia Diamond platinumz.Yeye mwenye we huwa anasema kuwa kitu kikubwa kinachofanya lebo yake kuweza kukua na kuendekla hata wasanii wake wote kufanikiwa ni kwa sababu wasanii hao wanaheshimu kazi hiyo kwa sababu ndio inayowapa kula na kutunza famila zao.

Msanii huyo mkubwa na meneja wa lebo hiyo siku ya tarehe 15 February, alitangaza kuwa wanaangalia mbele katika kuipeleka lwbo ya wasafi mele zaidi wakianzania na nchini kenya.lengo kubwa ni kusaidia wasanii wengi zaidi Afrika katika kuwatoa kimuziki ili waweze kufanikiwa na kukuza muziki wa afrika.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, diamond platinumz anawaalika watu wote kujua kuwa lebo ya wcb imekuwa na sasa inaaanza kutanuka na kuchukua wasanii nje ya Tanzania kwa ajili ya kufanya nao kazi”as we are abaout to launch  wcb wasafi branch in Kenya , pls help me tag all tarented artist in kenya you would like to besigned under Wcb_wasafi (kama mnavyofahamu kuwa mwaka huu wasafi tunatarajia kufungua tawi jipya nchini kenya , maalumu kwa ajili ya kunyanyua wasaniiwengne vijana  tokea mtaani…tafadhali naoma nisaidie kuwatag vijana wote wenye vipaji Kenya .

 

Mange Kimambi Aibua Mapya Ugomvi wa Shilawadu na Mose Iyobo

Siku chache zimepita tangu kutokee ugomvi kati ya Moze Iyobo na waandaaji wa kipindi cha shilawadu(Soudy brown na Qwisar), ambapo baada ya waandaaji hao kutaka kufany interview na Aunty Ezekil kuhusu ugomvi aliokuwa nao na mrembo Tunda walifika katika pub yake na kumkuta Mose Iyobo ambae kwa inavyosemekana ni kuwa waandaaji hao walivamiwa na kupigwa vibaya na mzazi mwenzie na Aunty Ezekiel.

lakini wakiwa katikati ya kipindi cha shikawadu,Aunty Ezekiel aliwapigia simu waandaaji hao na kuwaomba radhi kuwa kitu hicho hakitajirudia lakini pia alimuombea mzazi mweznie msamaha na kusema atakapo rudi kutoka China watakuja kuyaongea na kuyamaliza.

Siku ya jana wasanii na wacheza dance wa wcb, walikuwa wakipost picha nyingi kuonyesha kuwa walikuwa pamoja na rc wa dar es salaam.ambapo baada ya picha hizo nyingi kusambaa katika mitandoa ya kijamii mange kimambi aliibuka na lake na kusema kuwa wasanii hao walialikwa kwa  mkuu wa mko kwa ajili ya kuwapongeza kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwapiga shilawadu.

Katika ukurasa wake wa Instagram Mange Kimambi aliandika,ndo wameenda kupongezwa na mkuu wa mkoa kwa kuwapiga shilawadu.ila sijui bashite angewafanya ni  shilawadu kama Magu angemruhusu  kuwanyoosha.

Ugomvi huo wa Mose na shilawadu unahusishwa na ugomvi kati ya shilawadu na mh makonda siku za nyuma na kusemekana kuwa kipigo cha shilawadu juzi ni kutokana na kutumwa na mkuu wa mkoa huyo ili kuwakomesha zaidi.

Hata hivyo bado kunaonekana vita ya  maneno inaendelea kati  kundi la wcb na waandaaji wa kipindi hicho huku wakitupiaa madongo gizani.

 

 

 

Meneja wa Diamond Agundua Njama za Kumshusha Diamond

Meneja wa msanii mkubwa Tanznaia na afrika kwa  amefunguka  na kutoa siri juu ya njama za kumshusha msanii  Diamond platinumz zinazofanywa chinichini kwa ajili ya kumshusha na kumuua msanii huyo kimuziki.

Sallam Sk anasema kuwa kuna watu wamekuwa na njama za kumshusha Diamond kwa kumpakazia skendo mbalimbali lakini hawataweza kwa kipindi hiki cha utawala wa raisi magufuli kwa sababu hakuna atakaeweza.

katika ukurasa wake wa instagram sallam sk ameandika”kumbe tatizo ni kumpoteza huyo kijana, waambie familia yako na wazazi wako waliokuleta kuwa huyo mtoto kaletwa duniani kwa makusdi katika maisha haya.ili kuleta ukombozi wa dhuluma uliokuwa ukitendeka katika taifa hili.unatakiwa kujua kwamba hili taifa sasa raisi wake anaitwa John Pombe Magufuli’

Hivi karibuni dimaond amekuwa akikumbwa na skendo nyingi sana ambazo kwa kawaida zingeweza kumchafua hata kufanya kazi zake za muziki kutokufanya vizuri kabisa.Na skendo kubwa alikuwa nayo ni ile ya kutembea na wanawake tofauti tofauti lakini inaovyosemekana yupo mtu nyuma ya pazia anayepigana kuua muziki wa Diamond.

Kumekuwa na maneno madogo madogo yanayoendelea katika mitandao na captions tofauti tofauti katika page za wasanii na waandishi wa Clouds Tv hasa wale wa kipind cha shilawadu .