Kifo cha Mzee Majuto Kimezima Ndoto Yangu ;-Wema Sepetu.

Mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa msanii mareheme Mzee Majuto alikuwa akiwa bado yye hajatimiza ndoto nae alikuwa akitaka kuikamilisha kabla.

Wema anasema kuwa mwaka mmoja kabla aliwahi kupanga na kuongea na marehemu mzee majuto na wakakubaliana kuwa  watafanya kazi, lakini ikatokea ghafla alipoanza kuumwa na kusumbuliwa na maradhi yaliyomtoa Duniani.

nilipopata taarifa za msiba tu nilijua kuwa wazi ndot yangu imezimika, na kile nilichokuwa nakitaka hakiwezi kufanikiwa kabisa.nilitaka kujipima nione kuwa nikicheza vichekesho na yeye itakuwaje.lakini ndio hivyo tena imeshindikana.

Mzee majuto amefariki wiki iliyopita na kifo chake kimegusa watu wengi nje na ndani ya Tanzania kutokana na ukubwa wa kazi zake alizokuwa akifanya katka tasnia, aligusa maisha ya watu wengi sana hasa kusaidia kuchipua wasanii wachanga.

Wema Sepetu Adaiwa Kumpiga Vibao Chalz Baba Hadharani Kabisa

Muigizaji wa Bongo movie Madam Wema Sepetu amerudi Kwenye headlines Tena huku safari hii akidaiwa kumtandika vibao hadharani aliyekuwa mpenzi wake Chalz Baba.

Global Publishers wanaripoti kuwa tukio hilo lilitokea ukumbi wa burudani wa The Club Legend (zamani Nyumbani Lounge), ambapo Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ilikuwa inafanya shoo ambapo inadaiwa Wema alimpiga vibao Chalz Baba huku kisa kikiwa ni Husna Sajent.

Inadaiwa kuwa Baada ya Chaz Baba kuburudisha jukwaani na wanamuziki wenzake, alishuka na kwenda maliwatoni, wakati akitoka huko alikutana na Wema njiani na baada ya mazungumzo machache watu walishuhudia Wema akimzaba makofi kadhaa Chaz Baba.

Global Publishers lilipojaribu kumsaka Wema na kumuuliza juu ya tukio hilo na kutaka kujua sababu ya kumpiga aliyewahi kuwania mpenzi wake Wena alichomoa na kusema “No Comments”.

Baada ya sakata hilo Gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimsaka Chalz Baba ambaye alifunguka:

Tulikuwa vizuri tu maana jioni tulikuwa naye pamoja kwenye kikao cha kamati ya Miaka Ishirini ya Twanga maana na yeye ni mjumbe, tunategemea kusherekea naye siku hiyo kwa sababu itakuwa ni siku yake ya kuzaliwa pia usiku huo.

Hakukuwa na shida yoyote. Sasa nimeshuka jukwaani naenda maliwatoni mara nikakutana naye akaanza kuniuliza kwa nini Sajenti ananiposti kwenye mitandao ya kijamii na kwa nini tupo karibu.

Mimi nilimjibu kuna shida gani kwa sababu nina uhuru wa kuwa karibu na mtu yeyote yule na yeye hawezi kunipangia masharti kwa sababu si mpenzi wangu.

Nilipomjibu tu hivyo nilishitukia nazabwa makofi kadhaa usoni. Kalala alikuwa karibu ikabidi amtoe. Kiukweli ni kwa sababu ni mwanamke lakini angekuwa mwanaume mwenzangu pangechimbika”.

Steve Nyerere Aongelea Tangazo Lake Kuhusu Ndoa ya Wema.

Mwanabongo movis steve nyerere aliwahi kuweka post moja iliyozua maneno mengi sana katika mitandao ya kijamii kuhusu ndoa ya mwanadada wema sepetu na mwanaume mmoja anejulikana kwa jina la rahul.

Katika posti hiyo,Steve aliandika kuwa ndoa ya mwanadada huyo na Rahul inakuja soon. lakini alipojuwa akiongea na Ayo Tv , Steve alisema kuwa alikuwa anatania kwa lengo la kuwapima watanzania na uwaona watasema nini.

Nilikuwa tu natania , nilikuwa natania kwa sababu nilitaka kuona tempe ya watu, unajua kuwa ukikaa muda mrefu bila utani au kucheka inakuwa sio vizuri na kwa watanzania wanaopedna sana umbea na ndio maana nilitaka tu kuona.Watanzania wengi wanapenda sana umbea , hawapendi kufanya kazi ,kwaio unaangalia tu temper ya watu .

 

Wema Auanika Hadharani Ugonjwa Unaomzuia Kuzaa

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa taarifa za kukatwa utumbo sio za kweli bali ugonjwa wa gumbo unaomsumbua ndio unamnyima mtoto.

Mwezi uliopita taarifa zilienea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema Sepetu anaumwa na yupo hoi kitandani na chanzo cha ugonjwa huo ni kukutwa utumbo ili aweze kupungua.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi, Wema ameanika ugonjwa ambao umekuwa ukimsumbua na kudai ndio unasababisha yeye kukosa mtoto:

Unajua mimi sijakatwa utumbo kama watu wanavyosema; ningekatwa nisingekuwa hivi.

Unajua mimi nilikuwa na tatizo kubwa sana kwa upande wa tumbo langu la uzazi lililosababisha nisiweze kuzaa kwa muda wote huu.

Pia Wema alifunguka jondi ugonjwa huo unekuwa ukimnyima mtoto kwa miaka mingi:

Ngoja niweke wazi leo watu wajue, mimi nina ugonjwa ambao unasababisha mayai yangu ya uzazi kutoboka na kushindwa kupevusha mbegu za uzazi.

Unajua baada ya oparesheni ya India niliporudi nikapata tatizo la kushindwa kupumua vizuri na kingine nikapata maambukizi ya bakteria kwenye kidonda na presha ikawa inashuka.

Naendelea na matibabu lakini tatizo limeanza kupungua nafikiri baada ya mwaka nitakuwa mzima kabisa”.

 

“Sina Mpango wa Kwenda SA Kwenye Birthday Ya Tiffah” Povu la Wema Kwa Zari

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amemwaga povu zito na kudai hataenda Kwenye Birthday party ya Tiffah nchini South Africa.

Wema amefunguka na kusema kuwa hawezi kwenda Afrika Kusini kwenye party ya mtoto huyo kama walivyoalikwa Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika:

God Bless The Next Big Thing… Like Father Like Daughter. On August 6th, A Star was Born… ??????. Msije mkadhani kwenye Party naenda. Wala siendi. I jus wished the lil angel Dats it…!!! ??? #SinagaHianaMie . Maana hamkawii”.

Povu hilo limekuja siku chache baada ya Zari kumwambia Live kabisa Wema na kundi lake la Bongo movie kuwa hawataki nyumbani kwake maaana watamchafulia Nyumba.

Diamond na Zari wanategemea kumfanyia Tiffah bonge la sherehe huko nchini South Africa.

Wema Ajibu Tuhuma za Kuonekana na Wema Hotelini.

Msanii wa bongo fleve Roma amefunguka na kusongelea swala la  picha zilizosambaa akiwa na Wema hotelini huku tetesi kubwa ikiwa ni kwamba msanii huyo na madam walikuwa katika harakati za kufanya wimbo mpya.

Akiongea na waandishi, roma anasema kuwa sio kweli lakini walikutana hotelini hapo ambapo kila mmoja alikwenda kwa ajili ya shughuli zake ndipo walipokutana na kuamua kupga picha.

hiyo stori ya wema nilikutana nae mimi nilipokuwa naenda Ivan,  kula lunch , ndio moja mbili tukawa tumekutana hapo. na tukaanza kupiga stori na ndipo tulipopiga na zile picha.kwaio sio mchongo wa kichupa chochote ni familia tu.

Wiki iliyopt amsanii Roma na Stamina wameachia nyimbo mpya ambayo inafanya vizuri na kusumbua katikia vituo mbalimbali.

Esma Awataja Zari na Wema kuwa na sifa za kuolewa na Diamond.

Esma platinumz ametaa sifa za mwanamke ambae anataka kaka yake amuoe huku akitaja kati ya wanawake wote ambao kaka yake amekuwa nao anaona kuwa Zari na Wema ndio wanaweza kuwa na kaka yake kutokana na sifa walizonazo.

Mwanamke classic, mwanake anaejielewa , mwanamke mwenye akili mwanamke aliyesoma, kwa mfano kama Zari yuko vizuri sana  ni mwanamke anaeielewa na yuko vizuri , pia amesoma lakini pia mwingine Wema, mwanamke ambae shule kidogo imeingia ingia .

Hata baada ya kuwataja wema na zari kama wanawake alioona wanaweza  kuolewa na kaka yake lakini pia esma amesema kuwa ikitokea akaletewa mwanamke tofauti na sifa alizozitaja basi kwake haitakuwa shida ataumia roho lakini baadae  atamzoea.

yoyote atakae niletea kwangu itakuwa sawa tu na siwezi kumsemea ni nai lakini hata kama atamleta na sijamkubali najua roho itaniuma lakini itaenda baadae nitamzoea.

Wema Amjibu Zari “Hatukuomba Kuja South Africa”

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameamua Kuvunja ukimya na kumjibu Zari na kumwambia kiroho safi tu wao hawakuomba kwenda South Africa kwenye birthday ya Tiffah bali walialikwa.

Sakata hilo lilianza baada ya siku ya juzi Meneja wa WCB, Babu Tale kuwakaribisha kamati nzima ya watu walioshughulikia 40 ya mtoto wa Zamaradi ambayo ilijumuisha wasanii mbali mbali wa Bongo movie ikiwemo Wema Sepetu na Aunty Ezekiel kwenye birthday ya Tiffah.

Birthday party ya mtoto wa Diamond na Zari inatarajiwa kufanyika mwezi ujao na wana mpango wa kufanya bonge la party kwaiyo WCB waliamua kuwalipia tickets kamati hiyo ili waende South Africa kwa ajili ya party hiyo.

Lakini Zari hakutaka kabisa watu hao waende kwani siku ya jana alizua gumzo baada ya kubadilisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa hataki watu waende kwa sababu watamchafulia nyumba yake kwaiyo wabaki huku huku Tanzania.

Basi baada ya maneno hayo kutoka kwa Zari Wema alishindwa kujizuia kwani alimjibu kuwa asipanik kwani wao hawakuomba huo mwaliko bali walipewa tu na WCB.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Wema aliandika:

Sema nasikia kama safari ya SA imeleta mtafaruku mtaa fulani…….Jamani hatukuomba halafu kiroho safi tu….”.

 

 

Nitajitahidi Niwe na Roho Mbaya ili Nifanikiwe;-Wema Sepetu

Mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa  mara nyingi sana amekuwa akiowaona watu wenye roho ngumu na ucghoyo wamekuwa wakifanikiwa kitu ambacho kwa upande wake anaona kama hawezi kutokana na ule wema wake kwa watu.

Hata hivyo wema anasema kuwa kwa upande wake yeye inakuwa ngumu kuwa na roho mbaya kwa sababu mungu anakuwa tayari amekuumba hivyo hivyo huwezi kubadilika hata kidogo katika hilo.

Lakini amesema kuwa na yeye atajitahidi kuwa na roho mbaya ili aone kama inawezekana kufanikiwa kama wengine.

Wanasemaga watu wenye roho mbaya wanafanikiwa sana, na mimi roho hiyo sina kwa sababu ninachoamini ni kwamba kama umejariwa roho nzuri basi hiyo ni roho yako tu huna haja ya kuwa na roho nyingine, sometimes roho yangu nzuri inaniponza sana.ila nitajitahidi kujifunza roho mbaya.

Akiongelea kuhusu kesi yake iliyoisha hivi karibuni wema ansema hana la kusema zaidi ya kumshukuru mungu kwa kuwa kipindi icho alikuwa katika wakati mgumu wa kufanya mambo mengi kwa kusua sua.

Harmorapa Adai Moyo Wake Upo Kwa Wema, Achora Tattoo Ya Jina Lake

Msanii wa hip hop Harmorapa ambaye anajizolea umaarufu kwa vituko vyake amefunguka na kudai anampenda Wema na amechora Tattoo mpya ya Jina lake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Harmorapa amefunguka na kudai mwanamke ambaye anajitangaza kuwa ataolewa na Harmorapa ni muongo kwa sababu hana Mahusiano naye.

Harmorapa amefunguka na kudai hana mpango wa kumuoa mwanamke aliyetoka Mwanza kwa ajili yake aliyejitambulisha kwa jina la Khadijah na kudai anataka kumuoa Wema.

Harmorapa amedai kwamba zile picha zinazosambaa Kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa ni clip za Kwenye Movie mpya ambayo amecheza naye lakini sio wapenzi.

Harmorapa amefunguka na kudai hana mpango wa kumuoa mwanamke aliyetoka Mwanza kwa ajili yake aliyejitambulisha kwa jina la Khadijah na kudai anataka kumuoa Wema.

Lakini pia Harmorapa amefungukia mapenzi yake kwa Wema Sepetu na kudai anampenda kupita kiasi na Yupo Tayari kumuoa muda wowote na hata kukiri kuchora Tattoo ya Jina na lake Kwenye shingo.

Siku za nyuma Wema ameshawahi kumtolea povu Harmorapa na kumtaka aache kujitangaza Kwenye vyombo vya habari kuwa anampenda kwani alikuwa anamkera.

Aunty Ezekiel Awatolea Povu Wanaohoji Ukaribu Wake na Zari Pamoja na Wema

Msanii filamu za kibongo Aunty Ezekiel amemwaga povu kwa mashabiki Kwenye mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakimsema na kumuita Yuda kwa kitendo chake cha kuwa na ukaribu na Wema pamoja na Zari.

Mashabiki Kwenye mtandao wa Instagram ambao wamegawanyika Kwenye team Wema na Team Zari wamekuwa wakimpiga majungu Aunty na kumuita Yuda msaliti baada ya kutangaza kwenda nchini South Africa kushiriki birthday ya Tiffah.

Kwenye mahojiano na gazeti la na Amani, Aunty alisema majungu hayo yameanza mitandaoni baada ya kusikia amealikwa kwenda kwenye bethidei ya mtoto wa Zari, Tiffah inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao lakini kamwe majungu hayo hayamsumbui.

Ifike mahali tufunge mjadala, kila siku ni Aunt kuwa karibu na Zari, Wema kama ni bethidei nitaenda tu. Hawa wote ni marafiki zangu sasa siwezi kubagua kwa kuwa eti Wema aliachana na Diamond wakati kule kwa kina Diamond pia kuna mpenzi wangu Iyobo na isitoshe Zari ni wifi yangu kwa upande mwingine“.

Kwa miaka mingi Zari na Wema wamekuwa kama paka na panya kwa ajili ya kugombea penzi la Diamond kwaiyo kitendo cha Aunty kusema anaenda Kwenye sherehe ya mtoto wa Zari kiliwashangaza watu wengi hasa kwa sababu Aunty rafiki yake kipenzo ni Wema.

Diamond Kuwakutanisha Wema na Zari Nchini South Africa

Ikiwa siku zinakaribia kuelekea birthday party ya mtoto wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Bosslady Zarinah Hassan, Diamond anatarajiwa kuwakutanisha Zari na Wema nchini Afrika ya Kusini.

Diamond Kupitia uongozi wa label yake ya WCB imetangaza kusafiri na Wema Sepetu ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wanakamati wa birthday party ya Tiffah Dangote.

WCB wamesema wataisafirisha kamati hiyo kwa kuwa wameipenda na wanaona ni jambo zuri kwenda kushiriki nao kwenye shughuli hiyo. Mastaa wengine ambao wanaunda kamati hiyo ni Shamsa Ford, Shilole, Irene Paul, Irene Uwoya, Lamata, Kajala Masanja pamoja na wengine wengi.

Wema pamoja na wanakamati wengine ambao siku ya jana walikuwa wanakamati katika arobaini ya mtoto wa Zamaradi wamepokea mualiko huo uliowasilishwa na Meneja wa Diamond Babu Tale.

Diamond ameitaja Birthday party ya Tiffah  kama  sherehe ya mwaka ambapo pia amehaidi kuwalipia mashabiki kadhaa kwa ajili ya kwenda kuhudhuria.

Wema Angeshindwa Kulipa Faini Ya Milioni 2 Ningemlipia Mimi- Kajala

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo msanii mwenzake Wema Sepetu angeshindwa kulipa faini ya milioni 2 basi angamlipia yeye.

Miaka ya nyuma Wema alishawahi kumtupia Kajala faini ya shilingi milioni 13 ambayo iliweza kumsaidia kutokwenda jela kwa miaka saba kutokana na kesi yake ya utapeli.

Lakini tangu miaka hiyo Wema na Kajala walikuja kugombana na kuwa maadui wakubwa na juzi ilikuwa zamu ya Wema ambaye alihukumiwa kwenda jela kwa mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni 2.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Kajala ambaye kwa sasa yupo nchini Dubai, alisema kuwa kama angetakiwa kusaidia kumlipia Wema faini hiyo asingekuwa na tatizo, angemlipia.

Ningejua na kuwa na hakika Wema hawezi kulipa hiyo faini, ningemlipia hata kama ni kwa kukopa hizo pesa, lakini mimi sikuwepo nchini wakati Wema anahukumiwa.

Lakini pia Kajala ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa zinazosambaa kuwa amemtelekeza rafiki yake Wema:

Jamani mimi naona watu wanasema sikuonekana mahakamani, lakini hawajui kama nipo au sipo, hata hivyo kama ingehitaji faini ambayo kubwa kwa kweli mimi nisingeshindwa hata ya kukopa ningemlipia.

Sio kwamba sikuwa napenda kwenda mahakamani kuungana naye, kulikuwa na vitu vinaendelea kwa upande wangu hivyo ikaniwia vigumu”.

 

Wema Sepetu na Diamond Platnumz Wang’ara Tuzo Za Kimataifa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu wamezidi kuipeperusha Bendera ya taifa baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo za IARA Awards.

Wema Sepetu ambaye tayari ni Muigizaji bora wa kike katika tuzo za SZIFF amefanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo za International Achievement Recognition Awards (IARA) Kupitia Movie yake ya Heaven Sent.

Wema amechagulia kushindana katika kipengele cha Best International Actress huku akichuana na wasanii wengine wanne kutoka Africa ambao ni Joselyn Dumas kutoka Ghana, Amal Bouchoucha kutoka Algeria, Omotola Jalade kutoka Nigeria, Pearl Thusi kutoka South Africa na Tatiana Manslay kutoka Canada.

Kupitia page yake ya instagram Wema ameshukuru kwa kuweza kupata nafasi hiyo na kuwapa ujumbe mashabiki zake waendelee kumpigia kura kwa wingi  ili aweze kubeba tuzo hiyo:

And We are Nominated again…. Heaven Sent is still going places my loves…let’s keep on voting nawapenda nawajua Kwenye sekta ya kupiga kura tupo vizuri, tuseme INshalllah”.

Lakini pia Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekuwa nominated katika kipengele cha Best Male  International Artist huku akiwa anachuana na wasanii kama vile Davido, MOhamed Abbas, LA Foune, Mr. P, Medikal, Black Coffee pamoja na Casper nyovest.

“Mimi na Wema Tutaenda Kumtembelea Muna Labda Tufukuzwe”- Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere ameweka wazi kuwa hana kinyongo na Muna hata baada ya povu alilomtolea Povu Kwa waandishi wa habari Lakini ameshapanga kwenda kumtembelea.

Sakata hili lilianza wiki chache Kwenye msiba wa mtoto wa Muna ambapo Steve alionekana kuingilia mambo ya kifamilia ya Muna na kutangaza Kwenye mitandao ya kijamii taarifa ambayo Muna amedai haikua ya kweli.

Lakini siku ya jana Steve ametangaza kumsamehe Muna na kudai anajua hiki ni kipindi kigumu kwa Muna kwani bado anamuomboleza mtoto wake hivyo haoni sababu ya kuweka kinyongo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Steve  amedai kuwa yote ambayo ameongea Muna siku ya jana kuhusu yeye sio ya kweli na tayari ameshamsaheme ambapo amepanga safari ya kwenda kumtembelea akiwa na Wema Sepetu.

https://www.instagram.com/p/BlaXDuthZLR/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1lebqzhdtqbzi

Mambo Ya Fashion Yataka Kumdhalilisha Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amedaiwa kutaka kudhalilishwa na fashion baada ya kutaka kudondoka Kwenye steji baada ya kuvaa viatu viewfinder na vyenye kisigino chembamba.

Global Publishers wanaripoti kuwa sakata hilo lilitokea wikiendi iliyopita mashindano ya Miss Morogoro 2018 ambapo alialikwa kama mmoja wa majaji.

Awali saa 6 usiku wakati Wema akiingia katika Ukumbi wa Hoteli ya Morogoro lilipofanyika shindano hilo alionekana akiwa amevalia gauni refu la rangi ya gold huku chini akiwa ametinga viatu virefu vilivyompa wakati mgumu kutembea kwa mikogo. Hata hivyo staa huyo alifanikiwa kufika kwenye meza iliyoandaliwa kwa ajili ya majaji na kukaa lakini shughuli ilikuwa pale ambapo alitakiwa kupanda jukwaa kutoa neno.

Wakati akielekea kwenye ngazi za kupandia jukwaani, Wema alionekana kuyumba na kutaka kupiga mwereka lakini mmoja wa watu waliokuwa karibu yake waliwahi kumzuia na ndipo aliposhikiliwa na kupandishwa. Hata hivyo, hali iliendelea kuwa tete baada ya staa huyo kufika ngazi ya pili ya jukwaa ambapo aliyumba tena na ndipo mtangazaji wa Redio Planet FM ya Moro, Warda Makongwa akaongeza nguvu na kumfikisha jukwaani salama.

Wakati wa kushuka ili kumuepushia aibu staa huyo, wadada wawili walionekana kumshika mikono na kushuka naye taratibu huku mtangazaji wa Redio Clouds FM, Gardner G Habash naye akiongeza nguvu. Mbali na viatu kumuumbua Wema, umbo lake namba nane lililokuwa limejengeka vilivyo kutokana na gauni alilokuwa amevaa lilikuwa gumzo na wengi waliibua gumzo kutokana na msambwanda wa mrembo huyo.