Jacqueline Mengi Ashinda Tuzo Nchini Marekani

Mke wa Mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi, Jacqueline Mengi ameshinda tuzo ya Stevie Awards za mambo ya biashara kama Mjasiriamali wa mwaka katika kategori ya uzalishaji Kupitia kampuni yake ya Amorette Ltd.

Jacqueline atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoberfest 20 mwaka huu mjini London, Uingereza.

Jacqueline Mengi ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Amorette, Akizungumzia ushindi wake Kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema amefurahishwa na ushindi huo ukionesha Mchango wake unatambuliwa duniani.

https://www.instagram.com/p/BmXY5kWne4b/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=12k8naxmkbk85

Roma Atasitisha Zoezi la Kutoa Nyimbo Baada Ya Brazil Kufunga

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Roma Mkatoliki amesema anafuata ahadi yake na kusema hataweza kutoa nyimbo kwa sababu Brazil wameshinda.

Siku ya leo kabla ya mechi ya Kombe la dunia kati ya Mexico na Brazil  Roma alitangaza Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa endapo Brazili akifungwa basi ataachia ngoma yake mpya.

Na baada ya matokeo kutoka na Brazil kumfunga Mexico Roma aliweka wImazi kuwa hataweza tena kuachia wimbo mpya.

Lakini Kama Utakumbuka katika michuano ya mwaka 2014 Roma aliahidi endapo Brazil itafungwa na Ujerumani atahama Tongwe Records na kwenda Sharobaro Records.

Maneno Matamu Ya Jacqueline Mengi Kwa Mume Wake

Siku ya jana kulikuwa na uzinduzi wa kitabu cha Mkurugenzi wa IPP na Mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi.

Kitabu hicho ambacho kitaelezea historia yake yote ya maisha yake kuanzia kukulia katika hali ya kimaskini mpaka kufikia kuwa Bilionea kwa hivi sasa.

Kitabu hicho kinachoitwa ‘I can I must I will’ kimeelezea maisha magumu aliyopitia, Dkt. Mengi amesema katika maisha yake alishawahi kulala chini lakini hakukata tamaa na ndio maana akapata msukumo wa kuandika kitabu hicho.

Maisha yangu awali nililala chini, wageni wangu walikuwa Panya na Mende lakini baadae nilipokua nikasema ninaweza kuondokana na umasikini na niliweza”.

Baada ya tukio hilo zito lililohudhuriwa na hata Raisi wa Tanzania John Magufuli, Mke wa Dr. Mengi, Mrembo Jacqueline Mengi aliandika maneno haya matamu kwa mume wake Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.