Roma Atoa Kituko cha Video ya Parapanda ku-shoot-iwa Mbinguni.

Msanii Roma mkatoliki amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hawataweza kuachia  wimbo wa parapanda kwa sasa kwa sababu bado wako na idea ya kufanya hivyo.

msanii huyo anasema kuwa wamkeuwa wakiangaika sana kufanya hivyo mara nyingi na  ma-director tofauti na kufikia uafaka kuwa wanataka kufanya video hiyo mbinguni laki wanaweza wakienda huko watarudije huko.

baadae wimbo uliruhusiwa na ukandelea tu vizuri lakini hapo kweny video tuseme tu ukweli kuwa tulikosa kabisa idea  ya video ya parapanda kabisa ambayo ingeweza kuwaridhisha watu wakaipenda , na tulishare na madsirector wengi sana kuhusu idea ya video iyo na tkakosa lakini mwisho wa siku kuna waliosema mmh labda twende mbinguni, na nikawaambia kwenda rahisi ila kutudi itakuwaje kufanya show.

Mpaka sasa video hiyo haijatoka na kwa mujibu wa Roma ni kwamba bado amekuwa akisubiri kwa sababu hawaba idea ya wimbo huo.

Alichosema Roma Kuhusu Fiesta na Kutokuwepo kwa Ruge,

Msanii wa muziki wa hip hop nchini, Roma Mkatoliki amefunguka na kusema kuwa mara zote amekuwa  akisikia kuhusu matatzio yaayotokea katika matamasha mbaimbali hasa hili la fiesta na kwa uwezo alionao Ruge amekuwa akijitahidi kuya-solve matatizo hayo lakini mwaka huu imeshindikana kwa sababu Ruge hayupo,

Roma anasema ameuwa akim-miss sana ruge kila mar lakini baada ya kufungiwa kwa fiesta abakuta anam-miss zaid kwa sababu angekuwa ana uweoz wa kuoambana angepambana kama anavyofanya wakati wote.

katika ukurasa wake, Roma aliandika “kwa uzoefu wangu wa kile kiwanja cha Leaders m kila mara  hizo zimekuwa za miaka mingi lakini ruge huwa anapambana mpaka tunafanikiwa , huwa ninam-iss siku zote lakini kwa hili nimem-miss zaidi.”

Nilipiga Stop Kitendo Cha Wema Kuwepo Kwenye Video Ya Roma-Mke Wa Roma

Wasanii wa hip hop wanaounda kundi la Rostam Roma Mkatoliki na Stamina wameachia kazi yao mpya “Kaolewa” ambayo mpaka sasa inafanya vizuri kwa hewa.

Kwenye video hiyo yupo msanii wa Bongo movie Nisha ambaye amecheza uhusika wa Mwajuma lakini inadaiwa uhusika huo alitakiwa acheze Wema Sepetu lakini Mke wa Roma alikataza kitendo hiko.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Mke wa Roma amefunguka na kuweka wazi kuwa alimkataza mume wake kumtumia Wema Sepetu kwa sababu aliamini Nisha angefanya kazi nzuri zaidi na kuvaa uhusika:

Wakati wanaenda kushoot video nililetewa option ya video Queen wenyewe walikuwa wanataka kumchukua Wema Sepetu nikawaambia Hapana Wema hayupo Kwenye uhusika wa hiyo nyimbo yenu nikawaambia kama mnataka Msanii atakayevaa uhusika vyema basi mchukueni Nisha, na kweli Nisha amevaa uhusika vizuri sana na video imependeza”.

Wema Sepetu ameshawahi kuonekana kwenye video ya wimbo wa Diamond tu na alishawahi kusema hawezi kufanya video za wasanii wengi.

Video ya wimbo wa Rostam ‘Kaolewa’ inaendelea kufanya vyema na sasa inashika chati kwa kutrend namba 3.

Roma Amuanika Mtoto Hadharani Kwa Mara Ya Kwanza

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kuchana Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki amemuweka mtoto wake hadharani kwa mara ya kwanza tangu azaliwe Miezi michache iliyopita.

Roma na mke wake Nancy walijaliwa kupata mtoto wao huyo wa Pili ambaye ni wa kike ambaye anaitwa Ivy lakini kutoka na ukimya wao mtoto huyo hajawahi kuonekana Kwenye mitandao ya kijamii.

BAADA ya kumficha kwa kipindi cha miezi sita, Roma Mkatoliki’ ameamua kumuanika mwanaye wa kike, Ivy. Ishu hiyo imetokea juzikati, baada ya Star Showbiz kumtimbia nyumbani kwake, Mbezi- Jogoo jijini Dar ambapo alikuwa akifanya sherehe ya kumbatiza mtoto huyo.

Nimekuwa siyo mtu wa kuanika anika hovyo maisha yangu na wanangu lakini kwa kuwa umetokea haina jinsi, huyu hapa ni Ivy, leo ndiyo amebatizwa rasmi“.

Msanii huyo ambaye Yupo Kwenye kikundi na msanii mwenzake Stamina ‘Rostam’ wanafanya vyema na ngoma yao ya Parapanda.

“BASATA Mnaua Sanaa, Ubunifu na Vipaji”- Roma

Msanii wa muzili kutoka kundi la ROSTAM, Toma Mkatoliki amewatolea uvivu Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) baada ya kufungiwa nyimbo yao mpya.

Roma Mkatoliki amemwaga povu hilo baada ya ya yeye na msanii mwenzake Stamina kufikishwa BASATA siku ya jana baada ya kuachia wimbo wao wa Parapanda.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Roma ameandika na kudai kuhuzunishwa na jinsi BASATA wamekuwa wakifanya maamuzi yao juu ya kazi za wasanii.

Roma ameandika kuwa BASATA inaua Sanaa, Ubunifu na vipaji na kudai hachukizwi na BASATA bali anachukizwa na utendaji kazi wao pia akawataka mashabiki zake watoe maoni huku akisisitiza haoni kama wimbo wao wa parapanda ulikuwa na sababu za kufungiwa.

Roma- Ndoa Haiwezi Kunifelisha Kimuziki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba na miondoko ya Hip Hop, Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki ameibuka na kudai kuwa kama msanii sio lazima ufelishwe na ndoa.

Imekuwa jambo la kawaida kwa wasanii wengi Kwenye tasnia hii kupotea katika muziki au sanaa nyingine mara tu pale wanapoingia ndani ya ndoa iwe mwanamke au mwanamke.

Kutokana na dhana hiyo imekuwa ikidaiwa kuwa msanii hawezi kufanya muziki kama yuko ndani ya ndoa au kama akishaoa au akishaolewa basi atapotea Kwenye muziki.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Roma kwa upande wake amekataa dhana hiyo na kuweka wazi kuwa kila kitu ni kujipanga ingawa kuna changamoto katika ndoa lakini hawezi kuacha muziki bali anazipigania.

Changamoto ni nyingi, lakini ili kuziepuka wakati wa kazi huwa ninaacha mambo ya ndoa pembeni na kupiga kazi. Siwezi kuacha kukesha studio kwa sababu ya ndoa. Siwezi kuacha kupiga shoo kwa sababu ya ndoa”.

Lakini Roma aliendelea kufunguka kwa kuwapa somo wasanii wenzake juu ya ndoa na sanaa:

Kwa hiyo watu wengi waliofeli kisa ndoa, hapa nitaweka wazi kwamba walishindwa kumentaini hapo. Katika maelewano na watu wao wa karibu hasa kwenye kazi zao.Wake wanashindwa kuwaelewa wanaume wao na kuwaacha wafanye kazi kama ilivyokuwa awali kabla ya kuwa nao. Hapo ndipo inapokuwa tatizo. Lakini kwa upande wangu mke wangu ni muelewa sana”.

 

Kala Jeremiah Akana Kuwa na Bifu na Roma

Msanii mkongwe wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana Kala Jeremiah amekana kabisa tetesi zinazodai kuwa ana bifu na Msanii mwenzake Roma Mkatoliki.

Habari za wasanii hao kuwa na bifu zilianza baada ya wasanii hao kupunguza ukaribu waliokuwa nao zamani na hata kutopeana sapoti katika kazi zao Ikiwa ni pamoja na kutopostiana Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Roma amedai kuwa hana bifu lolote na Roma bali ni marafiki wazuri bado:

Hapana sina bifu na R.O.M.A yeye kwangu ni kama ndugu na hatuna tofauti zozote zile na sina background hasa ishu hiyo iliibukia wapi.

Hatuna bifu. Kwanza R.O.M.A kwa sasa ana kundi, kwa hiyo muda mwingi unakuta anafanya mambo yake na kundi lake. Hatuambatani tena ni kama ambavyo unaweza usimuone R.O.M.A na ndugu yake yeyote wakimbatana, lakini ukamuona na Stamina. Utasema haelewani na ndugu zake? Kuna muda tunaonana na mambo mengine yanaendelea, lakini si kwamba tuna tofauti. Kuhusu mitandaoni, ukitazama Instagram, kwanza ni kama hayupo vile, kwa hiyo tupo sawa”.

Lakini pia Kala alicheka baada ya kusikia tetesi kuwa eti hawaelewani sababu ya penzi la Dayna Nyange ambapo amesisitiza kuwa wapo vizuri tu.

Wasanii Wakongwe Hawapewi Nafasi Kwenye Media- Roma

Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa staili yake yake ya kipekee ya kuchana Roma Mkatoliki amefunguka na kuweka wazi kuwa wasanii wakongwe wengi hawapewi nafasi Kwenye vyombo vya habari.

Roma amedai kuwa ndio maana wasanii wengi wa zamani hawapendi kuitwa wakongwe kwani wanajua wazi hawatopata airtime kama wasanii wengine.

Kwenye mahojiano na Friday Night Live ya East Africa Tv, Roma amesema hiyo ni sababu kubwa wasanii wengi wanalikwepa jina hilo:

Unafikiri ishu ni ukongwe, wala si hivyo, ishu ni kuna baadhi ya makundi hayapewi nafasi kwenye media house, mchongo ndio upo hapo, hizo nyingine zote mchongoma tu.

Snoop Dog ni mzee anafanya mchongo na Wiz Khalifa, kwanini Mox asifanye mchongo na Country Boy halafu ukawa kweli mchongo lakini sisi tunakuja kuitafsiri mkongwe hana nafasi kwenye generation ya sasa hivi which is total wrong”.

Wasanii wengi wakongwe waliowahi kufanya vyema Kwenye gemu hapo nyuma wamekuwa wakilalamika kukosa nafasi ya kurudi kwenye chati ambayo imekaliwa na wasanii wengi wapya wanaofanya vizuri zaidi.

Moni Awatolea Povu Zito Mashabiki Zake

Msanii wa Bongo fleva anafanya miondoko ya kurap Awadhi Mtezo maarufu kama Moni Central Zone amewatolea povu zito mashabiki zake ambao wamemtuhunu kwa kutegemea kiki ndio afanye muziki.

Kumekuwa na trend kubwa kwa hivi sasa kwa wasanii wa Bongo fleva kupenda kiki yaani msanii anakuwa haoni kama muziki wake utafanya vizuri bila kiki na kabisa anapanga kabla hajatoa wimbo lazima atengeneze kiki wakuusindikiza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Star Showbiz, baada ya kuulizwa kuhusu komenti hizo za mashabiki kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, ambao walidai hivi karibuni alipokuwa anataka kupushi ngoma yake mpya ya Mwaah, alitumia kiki ya ugomvi na mwanamuziki Roma alifunguka hivi:

Hata siku moja sitegemei kiki. Muziki wangu ni mzuri na unajiuza wenyewe. Kikubwa kilichokuwepo kwa sababu nilikuwa karibu na R.O.M.A, mambo yalikuwa hayaendi vizuri kwa sababu alikuwa anaonekana yeye tu na si mimi, lakini baada ya kila mtu kuchukua time yake, kwa sasa naonekana mwenyewe na si kwamba nategemea kiki”.

 

Roma akamilisha Usajiri BASATA.

Msanii Roma Mkatoliki maefanikisha jukumu lake la kujisajili kama msanii rasmi wa tanzania katika tasnia ya muziki na kuwa kwa sasa anatambulika na BASATA na kazi zak zitakuwa zinzlindwa na baraza hilo.

Hayo yamekamilika siku ya march 5 mwaka huu baada ya kuagizwa kufanya hivyo na baraza siku chache zilizopita ambapo msanii huyo alikutana na uongozi wa BASATA  na Naibu waziri wa habari kwa ajili ya kuzngumza mambo mbalimbali na pia kuongelea swala lake  la kugfungiwa kwa muziki wake na yeye pia kufanya kazi za sanaa.

Roma ambae alikuwa amefungiwa kutokana na wimbo wake kukosa maadili na alipotakiwa kuurekebisha alichelewa kufanya hivyo lakini baadae alikuja na kutambua kosa lake hivyo kukaa chini na mamlaka husika hivyo kupata kibali cha kurudi kazini na kusamehewa adhabu yake.

Akiongea na waandishi wa habari katika usajiri huo, katibu mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza anasema kuwa “tunawaomba sana wasanii waje  kufanya usajiri na pia kuleta nyimbo zake kukaguliwa mashairi ili kupelekwa kwa public  na pia hata wa kazi za filamu ninawaomba sana kuna mamlaka husika “

Roma na Pretty Kindy Kurudi Katika Muziki, Diamond Apewa Onyo.

Jana siku ya tarehe 29 March Waziri Mwakyembe alitoa tamko lake kuhusu swala la kufungia wasanii na nyimbo zao na kusema kuwa hakuna msanii yoyote anaechukiwa na basata lakini wanaamua kufanya hayo kwa sababu wanataka muziki wa tanzania kufika mbali zaidi na kwamba wasanii wanapoona wamba wamekosea basi ni bora  kurudi BASATA  ili kuyazungumza na sio kuanza kuonge katika mitandao.

Kuhusu Diamond, Mwakyemeb amesema kuwa kosa kubwa la Diamond ilikuwa ni kujibizana na Naibu waziri katika mitandao ilhali kulikuwa na uwezekana na kukaa na kuyamzliza.

Akiongezea na kuto habari za furaha kwa mashabiki na wasanii pia , Jh juliana Shonza amesema kuwa waliamua kukaa chini na kupitia maelezo na maombi ya Pretty Kindy ambae pia alifungiwa kwa miezi sita lakini kutokana na mwenendo wake inaonyesha kuwa kuna kitu amejifunza lakini pia ameweza kutimiza yale yote aliokuwa aeambiwa ayafute hivyo wameona kulikio kumpunguzia adhabu kama alivyoomba ni bora kumsamahe kabisa.

Kwa upande wa Roma, Mh Shonza anasema kuwa roma pia aliandika barua kwa baraza ili kuangalia kwa adhabu yake upya nandio baraza lilipoamua kutoa msamaha lakini kukubaliana kuwa nyimbo yake ya kiba100 kutopigwa kwa mfumo wa sauti au video mpaka pale itakapofanyiwa marekebisho yanayotakiwa.

Hata hivyo wasanii hao walipopata nafasi ya kuongea na media kwa upande wa Pretty Kindy anasema anashukuru sana Mungu kwa kutolewa kwaadhabu yake kwa sababu kwa muda uliowekwa ilikuwa ni vigumu sana , nae Roma amewaomba mashabiki na vyombo mbalimbali kutokuuucheza wimbo huo mpaka utakapofanyiwa marekebisho.

Roma: BASATA Nipunguzieni Adhabu Mtaniua Njaa

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap Roma Mkatoliki amefunguka na kuiangukia kwa mahojiano BASATA huku akiomba apunguziwe adhabu.

Mwezi uliopita Roma pamoja na wasanii wenzake wa Bongo fleva walifungiwa nyimbo zao na BASATA kwa kudai maudhui yake hayana maadili ya Kitanzania, lakini Roma alitangazwa kufungiwa kabisa kufanya sanaa kwa muda wa miezi Sita.

BASATA ikiwemo wazi kuwa imemfungia Roma kutokana na wimbo wake wa ‘kibamia’ ambao walimwambia mara kadhaa aubadilishe lakini aligoma na kila walivyomuita alikataa kutokea.

Siku ya jana Roma na mtoto wake Ivan walifanya Interview na XXL ya Clouds Fm na aliomba BASATA impunguzie adhabu yake kwani hali yake ya kiuchumi sio njema kabisa:

Haya yote yanaongeleka, lengo ni Roma aendelee kufanya muziki wake kwa sababu muziki unamsaidia kama ajira, nyuma ya Roma kuna watu ambao anawasaidia. Kwahiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu Roma aendelee na muziki wake ili maisha yake yaendelee

Tena nikitoka hapa nitawasiliana na Katibu mkuu wa Basata najua atanisikiliza, pia nimesikia Jumatatu kuna mkutano wa wasanii wote na BASATA utafanyikia pale BASATA, zote ni katika njia ya kwenda kuyaongelea haya mambo, lengo tuwe chombo kimoja”.

Lakini pia kilichokamata hisia za watu wengi ni pale mtoto wa Roma, Ivan alipoulizwa kwa nini hakwenda shule siku ile ndipo alipojibu “Sijakwenda shule leo Baba hana hela”.

 

Fid Q Aingilia Kati Sakata la Roma na BASATA.

Rapa Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q ameamua kuchukua jukumu la kuanzisha mazungumzo na Baraza la Sanaa Tanzania baada ya kutolewa kwa adhabu kwa msanii mwenzake wa muziki Roma Mkatoliki na kumfungia kwa kipindi cha miezi sita kutokufanya kazi yoyote ya muziki.

Fid Q alikuwa ni mtu wa kwanza kuonyesha hisia zake za kuumia na hukumu hiyo huku akiamini kuwa miezi sita ni minhi sana kwa msanii roma kutokana na ukweli kwamba msanii huyo ana familia yenye mke na watoto wanaomtegemea kupitia kazi hiyo.

waswahili wanasema mambo ya kusadifu ni kutosheleza haja  ya chunguni , yale yaletayo faida  kama chakula n.k, tunaomba mturuhusu tuje tujadili hii sheria ya kifungo upya siu ya jumatatu ili kumuokoa baba anayetegemewa na familia kwa kupitia sanaa.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Baraza la Sanaa pia lilimaua kumjibu Fid Q na kumtaka akaribie kwa ajili ya mazungumzo ya swala la msanii huyo.

milango iko wazi muda wote,Baraza limesukumwa kuundwa kwa umoja  wa wasanii na kujenga mfumo rasmi wa mawasiliano na majadiliano .bahati mbaya wasanii wengi bado wako nje ya mfumo huo.Limekuwa  likiitisha vikao vya mashauriano , lakini mahudhurio yamekuwa hafifu .Kupitia umoja uliopo karibuni.

BAVICHA Wamtaka Naibu Waziri Kutengua Kauli ya Kumfungia Roma.

Baraza la Vijana  Chadema wamemtaka Naibu Waziri  Habari, Utamaduni na Michezo kutengua kauli yake ya kumfungia msanii wa muziki wa kizazi kipya Roma Mkatoliki  kwa kuwa sio jukumu lake kumfungia msanii huyo au msaniii yoyote.

BAVICHA  wamedai kuwa jukumu la kuwafungia wasani linatoka kwa BASATA hivyo wameshangazwa na kitendo cha Mh Juliana Shonza  kuingilia kati swala hilo na kutangaza kufanya maamuzi hayo yeye kama yeye kwa sababu hakupaswa kutangaza.

Serikali hii haioni kuwa kuna kila sababu kwa sababu hali ya uchumi ni mbaya , lakini leo unamsimamisha msanii  asifanye kazi ambayo anaitegemea kwa miezi sita , kwanza sheri haimoi mamlaka Waziri , mamlaka hiyo ameitoa wapi waziri?

mamlaka hiyo ipo kwa  BASATA yeye kazi yake ni kuisimamia BASATA  tu  aielekeze BASATA  wafanye kazi gani  na sio yeye Naibu Waziri, Sisi  kama baraza tunaona kama naibu waziri kwakweli amepotoka.Naibu Waziri amekosea na tumesikitishwa sana na tuna kila sababu ya kusema kuwa tunakemea.Serikali na Waziri mwenye zamana hiyo wanapaswa kutengua maamuzi hayo  na wale waliochelewa mpaka nyimbo hizo zikapigwa zaidi ya mwaka mmoja wanapaswa kupewa adhabu pia.

Lakini pia BAVICHA wamewataka BARAZA na naibu waziri kutokufanya kazi kwa kushinikizwa na watu  binafsi.H hata hivyo msemaji  huyo wa BAVICHA  Bwana  Sosopi amesema kuwa hakuna mtanzania anaetaka  kuvunjwa kwa maadili  lakini inabidi BASATA watoe hukumu  pale panapostahili.

Mpaka sasa Roma hajajitokeza kuongelea swala hilo ingawa kumekuwa na watu wengi nyuma yake wakimsapoti, lakini inasemekana kuwa msanii huyo kwa sasa yupo nje ya nchi kikazi.

BASATA Wamfungia Roma Mkatoliki Miezi Sita

Msanii wa hip-hop nchi Roma Mkatoliki afungiwa kwa muda wa miezi sita (6) kutokufanya kazi yoyote mpaka kifungo hicho kitakapoisha baada ya miezi hiyo kwa kosa la kutotii amri aliyokuwa amepewa na baraza la sanaa tanznaia siku za nyuma alipotakiwa kurekebisha baadhi ya maneno katika wimbo wake wa kibamia aliyomshirikisha satmina pamoja na maua sama.

Matukio ya kufungiwa kwa wasanii yameanza kufululiza ikiwa ni kuhakikisha kuwa nyimbo za Tanzania zinakuwa na maadili ambapo siku ya jana nyimbo zisizopungua kumi zilifungiwa kucghezwa katika vituo mbalimbali kwa kusemekana kuwa zimekuwa hazina maaadili ya kusikilizwa na watanzania.

Kibamia ni moja ya nyimbo zilizofungiwa jana na kufatiwa na kufungiwa kwa msanii mwenyewe siku ya leo baada ya kuonekana kushindwa kutumia muda aliokuwa amepewa kwa ajili ya kufanya marekebisho ya maudhui ya wimbo huo.

 

 

Roma Atuhumiwa Kuwa na Urafiki wa Mashaka

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Roma Mkatoliki anadaiwa kuwa mbali na watu ambao alishawahi kufanya nao kazi na kuwa marafiki zake hapo awali.msanii huo anadaiwa kuwatenga na kutokujali urafiki ambao walishawahi kuutengeneza na kuwafaidisha kimuziki.

Msanii Roma anadaiwa kuanzisha urafiki na watu wengi nahata wengine kufanmya nao kazi lakini mwisho wa siku anazinguana nao na kuwatupilia mbali kabisa bila kujali kile walichokitengeneza.Msanii huyo inasemekana alianzisha urafiki na Mose mtambo na kuwa karibu sana lakini baadae walikuja wakazinguana na baadae alikuja kuwa karibuna Dayna Nyange lakini walikuja wakazinguana tena.

Roma pia alikuwa rafiki wa karibu wa msanii Kala Jeremiah  ambapo kipindi cha urafiki wao ndipo Roma alikuwa akifunga ndoa, Kala alitoa sapoti kubwa sana katika harusi hiyo lakini kitu cha kushangaza sasa hivi ni kama wamepotezana kabisa ,sasa hivi wako na project na Stamina lakini unakoelekea ni kufa kwa sababu wanazinguana sana.

Hata alipotafutwa kuulizwa kuhusu swala hilo roma alitakia kujibu mashtaka hayo lakini alianza kucheka na kisha kujibu”hizo habari umezitoa wapi, nani kakwambia , sikiliza nikwambie tangu nimeanza musiki  huu sijawahi kuzinguana na mwana yoyote kwaio hizo habari hazina ukweli.

Kumekuwa na skendo nyingi sana za wasanii kuwa katika mahusiano ya kirafiki na hata kufanya kazi nyingi nzuri za kufanikiwa pamoja lakini pia bila kujali kuwa urafiki huo unaweza kuwafikisha mbali kimaslahi wanakuja  kugombana na kusahau yale waliofanya nyuma.

Ujumbe wa Roma Mkatoliki kwa wasanii wa Bongo: Muache kutegemea media

Roma Mkatoliki ametoa ujumbe kwa wasanii wa wenzake, staa huyo anayetamba kwa wa wimbo mpya ‘Zimbabwe’ amewataka wasanii wa Bongo waache kutegemea media kupush ngoma zao.

Akiongea na The Playlist ya Times FM, Roma alisema kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao wanapata upendeleo wa ngoma zao kupata airtime katika media.

Rapa huyo alionya kuwa mtindo huo ni hatari kwani wasanii hao wanapobwagwa na media mara nyingi huwa wanavyoshindwa kuishi kabisa.

“Yeah, off course asilimia mia moja kuna wasanii wanabebwa na media na pale media inapokata mirija utaona the way wanavyoshindwa kuishi kitu ambacho si kizuri, nashauri mtu atumie kipaji chake halafu aweze kujua at any time unaweza ukabwagwa na media halafu ukatakiwa usimame wewe kama wewe sasa kitaa unacho?, kwa sababu mimi naamini cha kwanza kitaa. Kitaa kikikuelewe media ni bless tu, utakuta ni Miaka minne/mitano wimbo wangu haujaingia kwenye chart za top ten lakini nikidondoka kwenye show na huo wimbo, bwana wee!!, kwa hiyo ile show yangu ya Mbagala ndio top ten yangu,” Alisema Roma.

 

Nay Wa Mitego: Nliumizwa sana na maneno ya Roma Mkatoliki

Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay Wa Mitego amefunguka kuhusu bifu yake na Roma Mkatoliki iliyoonza baada ya Roma kutekwa nyara miezi kadhaa iliyopita.

Roma aliongea maneno ya kumkashifu Nay Wa Mitego mara baada ya yeye kuachiliwa na watu waliomteka nyara akiwa na wenzake kwa studio yake.

Nay Wa Mitego

Nay ata hivyo hana machungu na Roma, rapa huyo alisema yeye bado anamtakia mema Roma hata kama maneno aliyosema juu yake yalimuuma sana.

“Roma anatakiwa ajue kwamba mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao walishinda kutwa nzima kwenye studio yake ya Tongwe Records na kituo cha polisi, toka siku aliyotekwa hadi siku aliyopatikana, lengo likiwa ni kutaka kujua tunasaidiana vipi ili aweze kupatikana. Akitaka kuthibitisha hilo amuulize mkewe, lakini nikashangaa baada ya kupatikana eti akanikashifu, kila nikikumbuka inaniumiza, sema mimi ni mwanaume siweki vitu rohoni, na pia nimeipenda sana ngoma yake ya Zimbabwe, Roma ni rapa mkali, sina kipingamizi juu ya hilo,” amesema Nay Wa Mitego.

Roma Mkatoliki

 

Mke wa Roma amchana mrembo aliyemkalia Roma akitumbuiza jukuwaani hivi karibuni

Kuolewa na msanii ni kitu ngumu sana kwani unapaswa kuwa na subra ya kuelewa kuwa hiyo pia ni kazi. Hata hivyo mke wa Roma ameonyesha kukerwa na mwanamke aliyemkalia Roma wakati alipokuwa akipiga show yake ya kwanza tangu tokeo lake la kutekwa miezi kadhaa iliyopita.

Mrembo huyu alifunguka kuhusu tekeo hilo kupitia mtandao wake wa Instagram huku akisema kuwa alitamani sana kupanda jukwaani kumshusha yule binti….aliandika kusema,

 

Kuwa Na Mume Msanii Wakati Mwingine Ni #Stress Nyie Acheni Tu Jamani!!!
.
.
Aaaf kuna vibinti ndiyo kama vinafanya makusudi

Kama Huyu!!!
Nilitamani Nipande Jukwaani Nikamshushe.
Sijui Hata alivyombeba alimpeleka wapi!!!!
.
.
Aaaah Ntafanyaje Mie Na Ndiyo Kazi Inayonifanya Niende Saloon!! .
.
By the way uliua…Show nzuri kama kawaida yako
Cc @usimsahau_mchizi_roma@usimsahau_mchizi_roma

Hata hivyo mashabiki wengi walimuunga mkono huku wengine wakimwambia kuwa mambo Kama hayo hutendeka lakini ikiwa Roma ni wake hakuna mwanamke yeyote anaweza kumchukua.

Tazama video hiyo hapa;

https://youtu.be/VA66Muo5-KE

Roma aweka wazi kuwa amewasamehea na kuwasahau waliohusika na kutekwa kwani

Roma ambaye ni msanii wa hiphop bongo alitekwa miezi kadhaa iliyopita lakini akapatikana baada ya siku kadhaa kitu ambacho yeye Kama mwanadamu hajaweza kusahau.

Hivi karibuni akizungumza na Times FM, Roma alifunguka kudai kuwa tangu awachiliwe serikali ya Tanzania haikumsaidia kwa njia yoyote. Msanii huyu alisema kuwa familia, marafiki na mashabiki ndio walisimama na yeye hadi kupona kwake. Alipoulizwa ikiwa Serikali ilimjulia hali wala kumshughulikia alijibu kwa kusema,

“Lahashaa! Hapana juu kwa juu tuu polisi, polisi Mwananyamala PF3 sijui nini ile, baada ya pale nikajiongoza mimi mwenyewe na familia yangu,so ikawa hivyo tuu“

Hata hivyo Roma alisema kuwa ameshawasamehe na amewasahau wote waliohusika na kutekwa kwake.

“Yaliyopita yamepita tunasamehe,tunasahau waliohusika Mungu atawahukumu na mkono wake na Mungu atupe neema uvumilivu na neema ya kuwasamehe…Lakini usidanganyike na mtu anakwambia sijui alikuja akatoa bugana lake au sijui akatoa hela ya panadol, Lahashaa!“

Roma Mkatoliki arejelea kazi yake ya ualimu

Watu wengi hawakua wanajua kazi aliyokuwa akifanya Roma Mkatoliki kabla ya kujiunga na sanaa. Rapa huyo anarudi shuleni kwa muda mfupi.

Roma alikua mwalimu wa somo la Hisabati kabla ya kuamua kuanza kuangusha mistari kwa ngoma zake za kuvutia.

Rapa huyo alienda kufunza hisabati katika shule ya msingi ya Mchikichini iliyopo Mbagala-Kibondemaji jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Showbiz Xtra kabla ya kuelekea shuleni, Roma alisema kuwa ameamua kuchukua nafasi hiyo kwanza kujikumbushia kazi yake ya ualimu.

“Somo la hisabati ni miongoni mwa masomo yanayotengwa sana na wanafunzi wengi hivyo basi nikiwa kama mwalimu niliyepitia kufundisha somo hili, nimeona vyema kuhamasisha wanafunzi walipende na kuliamini. Nitagawa vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba na pia kuwafundisha somo hilo. Kila mmoja nitahakikisha amehamasika na somo hili na kulipenda kama masomo mengine,” alisema Roma.

 

Roma Mkatoliki aeleza kwanini muziki wake sio chanzo cha yeye kutekwa nyara

Rapa Roma Mkatoliki na wenzake walitekwa nyara wiki kadhaa zilizopita wakiwa kwenye studio. Kupotea kwa Roma kulizua utata, watu wengi waliamini kuwa muziki anaoufanya Roma ndo ulikua chanzo cha yeye kutekwa nyara.

Roma alisemekana kuwa aliukosoa serikali kupitia mistari zake kwa wimbo wake, watu wengi walihusisha tukio la kupotea kwake na muziki anaoufanya.

Lakini akizungumuza katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV, Roma alikana dhana hilo. Alisema muziki wake hauvunji sheria yoyote.

“Kwanza niweke sawa, naamini katika muziki ninaofanya na naamini sijafanya kitu kibaya, sivunji sheria na wala siongei maneno mabaya

“Naumia sana nikiona mtu anautafsiri vibaya muziki wangu. Mimi sifungamani na upande wowote, hata ukiniuliza kadi ya chama mimi sina kadi ya chama chochote. Kwa sababu nikichukua kadi ya chama chako utasema nimekuwa mwanafamilia wako wewe ni baba ukikosea nitakunyooshea vipi kidole?. Kwa hiyo napata sana ukakasi nikiona watu Roma wanamtafsiri tofauti, naumia sana,”alisema Roma.

“Nliamini kuwa sitakuwa na wewe” Mke wa Roma Mkatoliki aeleza hofu iliompata baada ya bwana wake kupotea

Wiki chache zilizopita Roma Mkatoliki alitekwa nyara na watu wasiojulikana alipokua kwenye studio. Msanii huyo aliachiliwa huru baada ya wasanii kulalamika.

Soma pia: Roma Mkatoliki aelezea yote yaliyomfanyakia baada ya kutekwa

Mke wa Roma Mkatoliki, Nancy, alisherekea siku ya kuzaliwa kwake Jumapili hii Aprili 23. Nancy aliongelea kupotea kwa mumewe.

Alisema kuwa alikata tamaa kumpata mume wake baada ya siku kadhaa kupita bila kuskia lolote kutoka kwa polisi ama watu waliomteka nyara mumewe.

Nancy na Roma Mkatoliki

“lifika wakati nilikata tamaa na kuamini kuwa sitakuwa na wewe katika sikukuu ya kumbukumbu yangu ya kuzaliwa ya mwaka huu!! Lakini Mungu Baba Wa Mbinguni akasema no. #MyBirthday2017,” aliandika Nancy kwenye Instagram.

 

Mke wa Roma Mkatoliki azungumza mara ya kwanza baada ya mumewe kutekwa

Ni wiki chache tu kutoka Roma Mkatoliki awachilie huru baada ya kutekwa na watu asiyewatambua.

Alitekwa kwenye sttudio yake lakini baada ya kulalamika kwingi kwa wa Tanzania akaachiliwa.

Sasa amo nyumbani ana pumzika na mke wake Nancy Mshana amezugumza kwa mara ya kwanza kutoka muwewe atekwe.

Mrembo huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.

“(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.Ameen” Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki.

Bali na hilo amewashukuru wa Tanzania wote ambao wamesimama na familia yake wakati huu mgumu.

Mke wa Roma aeleza alivyozunguka vituo vyote vya polisi kumtafuta mumewe ambaye hajulikani aliko

Mke wa Roma, Nancy amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya mumewe, Roma kupotea. Kulingana na stori mitandaoni kuna fununu kuwa Roma na rafiki yake walichukuliwa na polisi wakiwa studio za Tongwe Record Masaki jijini Dar es Salaam.

Kama Watanzania wenzake Nancy hafahamu alipo mumewe ambaye ni baba ya mtoto wake, Ivan. Akizungumza na wanahabari, Nancy ameeleza kuwa amemtafuta mume wake katika vituo vya polisi lakini kila andako hakuna anayerecords za Roma Kutiwa mbaroni. Alisema,

Mimi kama mke wa Roma mara ya mwisho niliwasiliana na mume wangu jana saa kumi na mbili jioni, akaniambia anaelekea Tongwe Records kwajili ya kazi zake za kila siku. Baada ya hapo sikuwa nampata tena kwenye simu lakini nikachukulia ni kawaida tu simu imezima, nimekuja kuamka saa 7 nikapokea simu kutoka kwa rafiki yake akaniambia uko na Roma nikamwambia hapana alikuwa Tongwe, akaniambia kuna taarifa kwenye mitandanao na mimi nikaingia nikakuta hizo taarifa kama walizopata watu wengine. Baada ya hapo nikaanza kutafuta watu wa kunisaidia, baadhi ya ndugu zangu wameangaika vituo vyote vya polisi Roma hayupo, hadi sasa hivi sifahamu yuko wapi, kwa ufupi sina ninachokijua wala ninachokifahamu. Jitihada zangu za kutafuta kwenye vituo vyote vya polisi nimemaliza.

Hivi sasa watanzania kwa ujumla wameungana mikono katika jitihada za kumtafuta Roma ambaye mpaka sasa hajulikani aliko.

“Uoga ni uzembe” Babu Tale amtaje anayemlaumu kwa kupotea kwa Roma Mkatoliki

Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wamepotea bila ya yeyote kujua nani aliwateke, wamepelekwa wapi na nia yao ni ipi.

Wasanii wengi wamehofia usalama wa Roma na wenzake kwasababu hata polisi hawajui nani aliwateka. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

Roma Mkatoliki

Babu Tale, meneja wa Diamond, ameweka wazi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ndiye anafaa kulaumiwa kwa kupotea kwa Roma.

Babu Tale amemtaka Makonda awaeleze Watanzania kule Roma alipo, anasema kuwa yeye ndiye kiongozi wa kamati ya usalama Dar es Salaam kwahivyo anafaa ajue Roma alipo.

Paul Makonda

Uoga ni uzembe me nazani mwenye jukumu la kujua Roma yupo wapi ni Mkuu wa koa sababu yeye ndio kiongozi wa kamati ya usalama ya mkoa sasa ikiwa tumezunguka vituo vyote vya polisi na mwenzetu atumuoni nani wa kumfuata kumwambia tunamtaka mwenzetu kama sio @paulmakonda me naanza hili bila uoga mkuu wa mkoa naomba utusaidie kutuambia mnzetu @roma2030 alipo. Tukutane Tongwe mida hii me nipo kwa foleni wakuu #uogauzembe#freeroma,” Babu Tale aliandika kwa Instagram.

 

Diamond, Babu Tale, Vanessa Mdee, Professor Jay wahofia usalama wa Roma Mkatoliki na wenzake waliotekwa usiku wa Jumatano

Rapper Roma Mkatoliki na vijana wengine walitekwa usiku wa Jumatano wakati walipokuwa studio ya Tongwe Records. Watu wasiojulikana walipotea na Roma na wenzake.

Mpaka sasa bado hakuna anayejua wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi. Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

Roma Mkatoliki

Wasanii kadhaa wamekashifu kitendo hicho:

Professor Jay: ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU… Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana.. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!

Diamond: Wakati mwingine natafakari sijui hata wapi tunaelekea… lla kwakuwa Mwenyezi Mungu ndio Mpangaji wa yote basi naamini hata hili litapita tu… Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya @roma2030 na wanamziki wenzetu wote ambao hadi sasa haijajulikana walipo..

Vanessa Mdee: Wherever you are, God is Bigger than, Stronger than, Realer than all the other forces that be. Stay UP brother @roma2030 #VivaRoma #FreeRoma #FreeMoni roho inauma na nimetoka kumsikiliza mkeo redioni hajui hata ulipo sasa ndiyo nini ?????is this where we are at now? Ma studio yanavamiwa, watu wanakamatwa kama wanyama pori. Aaaarrrrgh

AY: Vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka tujue hali za wasanii wenzetu wako kwenye hali gani..@romamkatoliki Mungu yupo pamoja nanyi awaepushie lolote baya.. @tongwerecords @j_murder_tongwe

Babu Tale: Baba wa familia kupotea kama kuku na sisi wadau kuishi kupost tu hii sizani kama itatusaidia tuamke sote kwa pamoja saa sita mchana tukutane Tongwe Record tujue mstakabal wa mwenzetu @professorjaytz @efm_93.7 @cloudsfmtz #freeroma

 

Baada ya Nay wa Mitego, Wasanii wengine wawili mashuhuri kukamatwa

Huzuni imejaa Tanzania nzima baada ya ripoti kutokea kwamba wasanii wengine wawili walikamtwa usiku tulioamkia.

Roma mkatoliki alikamatwa jana kwenye Tongwe Records na mpaka wakati huu hakuna anayejua akuwepo.

“Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana..

Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!” professor Jay alitangaza kwenye instagram.

Wasanii wengi ikuwepo Nay wa Mitego wamekashifu tendo hilo.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.