“Naomba msamaha” Comedian Ebitoke apologizes after attacking ex boyfriend new lover

Bongo comedian Ebitoke is one angry woman especially after her ex boyfriend Mlela moved on with a certain video vixen.

The anger and disappointment in her seems to have awaken Ebitoke’s other side forcing her to take action — but not in the best possible way.

Ebitoke with her ex

On Monday the comedian was caught on camera attacking her exes new girlfriend at a conference held at a certain hotel in Dar Es Salaam.

Judging from the videos one can clearly see how the comedian beat up the other lady snatching off her wig in-front of the journalists who had availed themselves for the conference. According to reports Ebitoke left her ex boyfriend’s new lover hurt and traumatized after the attack.

Ebitoke apologizes

With the pressure of facing the law now that she was seen assaulting an innocent person; Ebitoke has now issued an apology for her actions and is willing to solve the matter privately.

Below is  a video of the lass apologizing courtesy of Wasafi TV.

https://www.instagram.com/p/B42Rw91hilJ/?igshid=wmgnfs8ickll

Ebitoke Akiri Kumuiba Mume Wa Mama Ashura

Mchekeshaji maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Anastazia Exavery maarufu kama Ebitoke amefunguka na kukiri kutembea na Mume wa msanii mwenzake Mama Ashura.

Skendo ya Ebitoke kumuiba mume wa Mama Ashura ambaye alikuwa Meneja wao Timamu Tv, Conrad Timoth zilianza Baada ya Mama Ashura kutimuliwa na Ebitoke kuchukua nafasi yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Ebitoke amefunguka kwamba yeye hakumfuata Timoth ili kuwa naye kwenye mahusiano, licha ya kuwa Bosi wake huyo ni mume wa muigizaji mwenzake, Mama Ashura.

Baada ya kuulizwa tetesi za kugombana na Mama Ashura kwa kumchukulia mume, Ebitoke alikiri haya.

Sasa ananimind mimi ndio nilimfuata Timoth nikamwambia njoo kwangu, Haya mambo yalishapitwa na wakati”.

Miezi michache iliyopita Ebitoke alitangaza kuondoka Timamu kwa Timothy na kufanya Sanaa ya kujitegemea muda michache baadae Ashura alionekana tena ndani ya Timamu.

 

 

Ebitoke Ajibu Tetesi za Kujichubua

Siku chache baada ya mwanadada Ebitoke ku-break the internet baada ya kuweka picha katika ukurasa wake akiwa beach, mwanadada huyo aliaandamwa sana kwanza kutokana na kuzoeleka kwake na muonekano wake hakuwahi kuonekana akivaa nguo za wazi kiais icho.

Hata hivyo, mwanadada huyo alisemwa pia kuwa picha hiyo imeonuesha kwa sasa jisni mwanadada huyo alivyojichubua na ngozi yake imebadilika sana sio kama Ebitoke yule aliyekuwa zamani.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, ebitoke amesema kuwa watu hawapaswi kuamini sana kila wanachokiona katika mitandao ya kijamii kwa sababu vitu vingine vimekuwa editing na havina ukweli  wowote.

Katika ukurasa wake Ebitoke aliandika “haya lo nimewawekea rangi yangu ya ukweli, zingine zote fake am still black.mpunguze kusema kuwa najichubua tatizo mnaapenda kuamini  mitandaoni maediting  na usiamini kila unachokiamini.”

Ebitoke Achefua Mashabiki na Picha Yake na Nusu Uchi

Ebitoke ni moja kati ya wasanii ambao hawajawahi kuzoeleka hata mara moja kufanya michezo wanayofanya baadhi ya mambo ikiwa kuweka picha za uchi katika mitandao.

mwanadada huyo ambae ameamua kujiripua na kuamua kuweka picha yake akiwa na beach wear amewakwaza mashabiki zake na kuanza kumwambia kuwa hawajazoea kumuona na mavazi hayo ambayo wamekuwa wakivaa wasani wengine.

Mashabiki hao wameonga mengi na kusema kuwa kutokana na umbo lake hakupaswa kucvaa kitu kama icho huku wengine wakisema kuwa hakuna na haja ya kuharibu historia na hshima ake aliyowahi kuijenga kwa mashabiki zake.

 

Ebitoke Akumbwa na Skendo Ya Kujichubua

Msanii wa maigizo Bongo Annastazia Exavery maarufu kama Ebitoke amejikuta kwenye kituo cha moto Hivi karibuni Baada ya kukumbwa na skendo ya kujichubua.

Taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinadai msanii huyo ameangaliwa sana na mashabiki zake ambao wamedai kuwa anazidi kuwa mweupe kadri siku zinvyozidi kuenda ingawa Ebitoke amekataa kabisa Skendo hizo.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Ebitoke alisema weupe wake umetokana na joto kuwa kali na katika vitu ambavyo hawezi kuvifanya ni kujichubua kwa sababu anaelewa wazi kuwa kuna madhara makubwa endapo atafanya hivyo.

Najua madhara ya kujichubua siwezi kufanya hivyo kama watu wanavyonituhumu, nimebadilika na  mweupe siku hizi tofauti na zamani kwa sababu ya joto tu na siyo vinginevyo”.

 

Ebitoke Akataa Kusema Kilichomtoa Timamu

Mchekeshaji Ebitoke amejikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kupokea lawama nyingi kutoka kwa mashabiki wake kufuatia hatua yake ya kujiondoa kwenye kundi la Timamu.

Licha ya kuandamwa huko, Ebitoke amewaeleza kamwe hatoweza kuwaambia sababu iliyopelekea kujitoa kwenye kundi la Timamu.

Mashabiki wangu mnataka niwafanyie nini ili mridhike maana mmekuwa na Maneno kibao. Mnataka kujua sababu iliyonitoa Timamu?,” .”Itabaki kuwa siri yangu tu na muhusika na sitamani mkaijuia maana ,mtanionea huruma. Punguzeni ukali wa maneno maana hakuna anayependa kuambiwa mabaya kila siku” ameeleza.

Ebitoke alijizolea umaarufu mkubwa ndani ya kundi la Timamu akiwa na wachekeshaji wengine kama Mkaliwenu, Bwana Mjeshi, Mamaa Ashura, kwa sasa Ebitoke ameondoka kwenye kundi hilo.

Ebitoke aliponda penzi la Ben Pol na Anerlisa

Mwanadada kutoka katika kiwanda cha burudani ya vichekesho nchini, Ebitoke ameliponda vikali penzi la msanii ebitoke ambae hapo awali alikuwa akisemwa katika mitandao kuwa ni  mpenzi wake .

Ebitoke anasema kuwa msanii Ben pol hana cha maana hapo zaidi ya kuwa analelewa tu na mwanadada huyo hakunacha zaidi.

Mimi wala sijikisikii vibaya kwa sababu yule ninamuona kama kibenten tu kwaio nabaki nacheka tu,mtu unakula bata na kupelekwa dubai kwa hela gani sasa, wewe si unalelewa tu na unakuwa mbeba pochi tu.

Mahusiano kati a ben pol na ebitoke yalikwa na muda mrefu na yalikuwa yakizungumziwa sana katika mitandao ya kijamii.

 

 

Ebitoke Adai Management Haijawahi Kumpa Gari Wala Nyumba Kama Ilivyodai

Msanii maarufu wa vichekesho katika mitandao ya Kijamii Ebitoke amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi kupewa gari wala nyumba kama ilivyowahi kusikika katika siku za nyuma.

Siku chache zilizopita Ebitoke alitangaza kuachana Rasmi na Management yake ya Timamu ambayo ilikuwa inamsimamia tangu alipoanza kufanya sanaa yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha  Times Fm, Ebitoke amekana taarifa za yeye kupewa gari na Nyumba na Timamu kama ilivyowahi kusikika siku za nyuma:

Hivyo vitu nimekuwa nikiilizwawsana naomba tu leo niseme ukweli siku ya leo, Mimi sijawahi kupewa gari yaani sina gari wala sijapewa nyumba ila nina kiwanja Changu kipo nyumbani karibia namaliza kujenga”.

Ebitoke ameweka wazi kuwa kwa sasa yuko mwenyewe kama yeye tangu alipojiengua Kwenye kundi hilo la Timamu.

Ebitoke Atangaza Kujitoa Timamu Africa

Mchekeshaji aliyejizolea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii ameweka wazi kuwa ameachana Rasmi na Management ambayo ilikuwa inamsimamia Timamu Africa.

Ebitoke ametoa taarifa hizo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameweka wazi sababu ya kuacha kufanya nao kazi ni kwa sababu ya mkataba wao kuisha muda wake.

Napenda kuchukua nafasi hii na kuwatarifu Mashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu, kuanzia sasa nitakua nikifanya kazi zangu nje ya Timamu TV, nikimaanisha mkataba wangu umeisha.

Wamekua wema na wenye UPENDO KWANGU SIKU ZOTE. Pia Napenda kuwashukuru Mashabiki zangu kwa kipindi chote ambapo mmekua mkinisapot na kufurahishamwa na kazi zangu ?”.

Lakini pia Ebitoke ametoa shukrani zake za dhati kwa management yake hiyo ambayo pia imesimamia comedians maarufu kama Mama Ashura na Mkali wao.

Shukukran ZANGU ZA Dhati kwa Manager wangu ?@timothconrad kwa kunilea vyema nitakupenda siku zote Maana bila wewe nisingekua mimi. @bwanamjeshi, @mr_beneficial, @chidi_luba nawashukuru sana kwa upendo mlionao kwangu tangu tumeanza kufanya kazi mpaka sasa, nyie ni familia yangu, tutaendelea kusapotiana kama familia ❤”.

 

Ebitoke Atangaza Kutoka Kabisa Timamu

Msanii wa maigizo ya vichekesho, Anastasia Exavery maarufu kama Ebitoke ambaye amekuwa akifanya kazi Timamu TV ametangaza kuondoka kuifanyia kazi TV hiyo mara baada ya mkataba wake kumalizika.Ebitoke amesema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram na kudai kuwa kwa sasa atakuwa anafanya kazi na TV nyingine.

”Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu mashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu, Kuanzia sasa nitakuwa nikifanya kazi zangu nje ya Timamu TV nikimaanisha mkataba wangu na Timamu TV umeisha” ameandika Ebitoke.

Aidha ametoa shukrani zake za dhati kwa uongozi mzima wa Timamu TV kwa kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanafanya kazi nzuri, lakini pia amewashukuru wafanyakazi wenzake ambao amekuwa akishirikiana nao katika kutengeneza maigizo mafupi ya vichekesho ambao ni @ Bwanamjeshi na @Mr. Beneficial.
Mbali na hatua hiyo  Ebitoke ameenda mbali zaidi kwa kufuta video zake zote za kazi alizofanya akiwa chini ya uongozi wa Timamu TV kwenye ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi Milioni 1.
Aidha hajasema baada ya kumaliza mkataba wake na Timamu TV atasajiliwa na TV gani nyingine kuendeleza fani yake ya uchekeshaji.

Ebitoke Amuomba Msamaha Shilole Baada Ya Kudai Sio Msanii

Mchekeshaji mwenye vituko kutoka Timami Tv, Ebitoke amesanda na kumuomba msamaha msanii wa Bongo fleva Shilole baada ya kupewa kichambo cha haja.

Siku chache zilizopita Ebitoke alitamka Kwenye Interview aliyokuwa anafanya na kusema hajui kama Shilole ni Mwanamuziki au ni mama ntiliye na hata kusema kuwa hajui nyimbo yake hata moja.

Baada ya kuongea maneno hayo Shilole alimjia juu na kumrushia maneno huku akidai hawezi kubishana na Ebitoke kwani siyo level zake kabisa kwani hadhi zao haziendani.

Baada ya kupokea kichambo hiko Ebitoke ameibuka na kumuomba msamaha Shilole na kusisitiza kuwa maneno aliyoongea yalikuzwa na watu matandoni kwani anajua kuwa SHilole ni msanii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Ebitoke alifunguka haya:

Unajua watu wanajua kukuza maneno sana ila mimi niliongea kutokana na kazi anayozozifanya nyimbo zake mbona mimi nazijua kama ile wa kigoli si wimbo wake ule? Mi naujua na ninajua ni msanii kwaiyo mimi naomba tu anisamehe tu”.

 

Wanja Umenipa Heshima na Kazi-Ebitoke

Mwanadada mchekeshaji kutoka timamu Ebitoke  ameweka siri ya mafanikio yake katika kazi na kusema kuwa  tabia yake ya kipekee na ubunifu wa kupaka wanja wa kuukoleza ndio uliompa kazi, jina na ajira katika tasnia ya maigizo.

Ebitoke anasea kuwa yeye hawezi kufanya make up kama watu wengine wanapokuwa katika lication kwa sababu wanja ndio kitambulisho chake kikubwa katika kazi yake, na kusem akuwa endapo atabadilisha aina ya kujiremba na kuanza kupaka tofauti basi atasahaulika kabisa.

Ninauheshimu sana wanja kwa sababu ndio ulionipa maisha ,hata akaunti yangu ya benki inafanya vizuri sana na nimetimiza ndoto zangu nyingi tu kwasababu ya huu wanja ingawa watu watakuwa hawauelewi.

Shilole Amjibu Ebitoke na Kudai Sio Hadhi Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amemjia juu msanii wa vichekesho kutoka Timamu Tv, Ebitoke na kusema sio mtu wa hadhi yake.

Siku ya jana Ebitoke alimuongelea Shilole Kwenye Interview yake na kudai hajui nyumimbo hata moja ya Shilole kwa sababu hajui kama ni msanii au ni mama ntiliye.

Kwenye mahojiano na EATV, Shilole amesema hawezi kubishana na mtu kama Ebitoke kwa kuwa hana pesa na pia sio level zake na pia kama anatafuta kiki basi yeye hatoi kiki sahivi:

Nyumbani kwake ananitazama kila siku, wengine wanapenda wanisikie nikiongea, mimi siwezi kuongea na mtu ambaye hana hela, lakini wakati huo ananijua na ananiangalia kwenye tv sebuleni kwake, mimi sitoi kiki sasa hivi“.

Mbali na kuwa msanii Lakini pia Shilole ni mjasiriamali ambapo anamiliki mgahawa wake unaoitwa Shishi Food.

Ebitoke- Shilole Sio Msanii Bali ni Mama Ntiliye

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv, Ebitoke ameibuka na kumtolea povu zito Shilole huku akidai kuwa hamuelewi kama ni msanii au mama ntiliye maana hajui kazi yake hata moja.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Shabiki mmoja alimtaka ataje wimbo mmoja wa Shilole na kuuimba ndipo aliposema hajui wimbo wake hata mmoja kwani hajui kama ni msanii au ni mama ntiliye:

Labda unitajie nyimbo zake mimi sijui kazi zake mimi najuaga  yeye ni mpishi tu ila hapa Kwenye nyimbo mtanisamehe kwa kweli sizijui nyimbo zake…..Nisiwe muongo naongea ukweli wala sio kiki kama mlivyozoea mambo ya kiki siku hizi nimeacha”.

Shilole mbali ya kuwa msanii wa Bongo fleva Lakini pia ni mfanyabiashara ambaye anamiliki mgahawa wake unaoitwa Shishi Food ambapo anauza vyakula mbali mbali.

 

Ebitoke- Namchukia Sana Mange Kimambi

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv, Ebitoke amefunguka na kuweka wazi kuwa hampendi kabisa Mwanaharakati wa mambo ya siasa mitandaoni Mange Kimambi.

Kama utakumbuka siku za nyuma Ebitoke alishawahi kuingia Kwenye headlines baada ya Mange kutangaza kuwa Anatembea na bosi wa Timamu Tv ambaye ni mume wa msanii mwenzake Mama Ashura na hadi kusababisha Mama Ashura kufukuzwa.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Ebitoke aliulizwa anamchukuliaje Mange Kimambi na mara moja alitiririka jinsi anavyomchukia:

Yaani katika watu ambao siwezi kiwazungumzia ni huyo, Kwanza huyo Dada mimi simpendi, ameshawahi kuongia kwenye anga zangu lakini hata kabla ya hapo nilikuwaga simpendi.

Halafu siwezi kumkubali yule dada maana hanisidii kitu chochote mimi naona anawasaidia watu wengine, Mimi sipendi mambo yake na wala sikapendi na wala sipendi vimtu vinavyoongea sana “.

Lakini pia Ebitoke amesisitiza taarifa alizozieneza Mange hazikuwa na ukweli hata kidogo kwani yeye na Mama Ashura wako vizuri kabisa ingawa sio marafiki.

Hakuna Msanii wa Kike Anaenipa Shida:Ebitoke

Msanii wa kike wa maigizo ya vichekesho nchini, Ebitoke amekiri kuwa hakuna msanii wakike yeyote bongo anaempa shida wala kuwaza kuwa anaweza kushindana nae kwa sasa kwa sababu yeye anajiamini na anajua kuwa hakuna anaeweza kumpita kwa kipaji.

Akiulizwa na bongo5 usiku wa kutolewa ka tuzo za sinema zetu ebitoke alisema “hakuna msanii wa kike anaenipa shida kabisa , sijamuona bado labda mimi mwenyewe”

Akiendelea kuongea, ebitoke pia alitoa taarifa kuhusu kuzushiwa kutoka kimapenzi na mdogo wake Ben Pol anaeitwa Wyce ambae ameweza kuwa video queen katika video yake mpya.

Hali ilikuwa poa, mimi na yeye tulikuwa tunavaaa uhalisia tu hakuna mapenzi pale,na kuhusu lile kiss hakuna kitu ila director alituambia tuvae uhalisia tu ili kitu kiwe kizuri.

Ebitokea Aongelea Kutoka na Mume wa Mama Ashura

Mwanamaigizo upande wa vichekesho kutoka katika kundi la Timamu, Ebitoke amefunguka na kuongelea tetesi za muda kidogo ambazo zinamtuhumu yeye kuwa amekuwa katika uhusiano wa kimapezni na bosi wake ambae pia ni mume wa mama Ashura.

kwa wale wanaosema kuwa eti mimi nimempindua hiyo sio kweli wakati yupo tumemficha sehemu, tutamleta tu.Mama Ashura yupo ila kwa sasa anaendelea na mambo mengi, tutamleta tu atarudi na watu wataendelea kumuona kama zamani ila kwa sasa hivi yupo kidogo kuna mambo anayafanya.

Tetesi zilizokuwa zimeenea katika mitandao ilikuwa ni kwamba Ebitoke amekuwa akitoka kimapenzi na mume wa Mama Ashura kitu kilichopelekea wasanii hao kugombana na hata mama Ashura kuacha kufanya kazi katika kundi lao na kwa sababu walikuwa wakikaa nyumba moja basi Mama Ashura ilibidi kuwapisha wawili hao.

Ebitoke Amefungukia Tuhuma za Kuiba Mume wa Mama Ashura

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv Ebitoke amefungukia tuhuma ambazo zimekuwa zikimuandama kwa muda sasa kuwa yeye na mchekeshaji mwenzake Mama Ashura wana bifu baada ya kumuibia mume.

Ebitoke  alijipatia umaarufu siku za nyuma Kutokana na vituko vyake na make up yake ya sioni ameongelea habari ambazo zinaongelewa sana mtandaoni kuwa ameiba mume wa Mama Ashura ambaye amezaa naye.

Miezi michache iliyopita Mange Kimambi alivunja bonge la habari iliyowashangaza watu wengi kuwa Ebitoke anamchukua mume wa Mama Ashura ambaye pia ni Bosi wao anayewasimamia kazi zao pale Timamu Tv.

Pia ilisemekana kuwa tangu Ebitoke amchukue mume wa Mama Ashura wamekuwa kwenye bifu kali na pia ilisemekana kuwa Mama Ashura amekuwa akiteswa sana na mwanaume huyo.

Tangu taarifa hizi zienee Mama Ashura amekuwa haonekani Tena kwenye mitandao ya kijamii kama zamani na kuna hata taarifa kuwa hivi sasa mrefu kuzaa hapo Timamu Tv.

Ebitoke alifanya Interview na Millard Ayo Tv ambazo alipoulizwa kuhusu ishu yake ya Kumuona mume wa Mama Ashura alikataa kata kata kujibu tuhuma hizo:

Bwana hayo mambo mi sitaki kuyaongelea yaani ukiniuliza kuhusu huyo mtu sina cha kujibu lakini yupo tu mbona sema sitaki kumuongelea kabisa”.

Hata Ebitoke alivyobanwa na ndugu mtangazaji aeleze Mama Ashura alipo alikata kuendelea kufanya Interview na kuondoka.

Ebitoke Akumbwa Na Tuhuma za Kuiba Mume wa Mama Ashura

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini kutokea katika kundi la timamu Ebitoke  ametuhumiwa kuhusishwa na kuvunjika kwa ndoa ya msanii mwenzie Mama Ashura wa kundi hilohilo kwa kutembea na mume wake.Tuhuma hizo ziliibuka juzi kati mbaada ya mwana harakati Mange Kimambi kuamua kusema siri hiyo ambayo ilikuwa imejificha kwa  muda mrefu na kutoa hadi video zinazomuonyesha Mama Ashura akiwa barabarani na mtoto wake wa kiume wakiangaika baada ya kufukuzwa katika nyumba hiyo.

Ebitoke anaedaiwa kuwa alikuwa akikaa kwenye nyumba ya Mama Ashura na mume kwa muda kidogo ikiwa ni kama kumsaidia mahali pa kuishi aliamua kumgeuzia kibao shoga yake huyo na kutembea na mume wake ambae pia ndio meneja wa kazi zao za uchekeshaji.

Mpaka sasa inavyosemekana ni kwamba baada ya Mama Ashura kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe, Ebitoke ndio amekuwa mama mwenye nyumba hiyo na kumuacha rafiki yake akiangaika na mtoto barabarani.

Tetesi hizo zinadai kuwa hata baada ya Mama Ashura kufukuzwa , hakuruhuiswa kuondoka na kitu chochote na kwamba hata akaunti zao za mitandao ya kijamii meneja wao huyo ndie anaezimiliki hivyo hawajui hata neno la siri la kuingilia katika akaunti zao.

Ni kawaida kwa wasanii bongo kupinduana na kuchukuliana mabwana  hata kama wawili hao wanakuwa ni marafii sana, na hii inafanya kuharibu kazi zao na mahusiano yao mazuri katika kazi yanakuwa yanaishia hapo .

 

Ebitoke Aongelea Kuhusu Ukimya Wake

Alipoanza kujulikana katika tasnia ya sana alikuwa ni moja ya wasanii wasioisha kutajwa midomoni mwa watu lakini hivi karibuni ameonekana kupoa kidogo , badhi ya mashabiki wameanza kusema kuwa labda na yeye amefulia na zile kiki  alizokuwa anatafuta zimekwisha lakini msanii huyo wa maigizo ya vichekesho kwa jina la Anastazia Xavery akijulikana kwa jina  maarufu la Ebitoke amekana swala hilo na kusema kuwa yupo sana katika game na wala hategemei kuacha kazi yake kwa sabau ni kipaji alichozaliwa nacho.

Ebitoke amesema kuwa tangu amezaliwa, amezaliwa kwa ajili ya kazi ya kuchekesha kwaiyo ni kitu kilichopo katika damu yake na hawezi kuacha na kwa sasa ana madude mengi ya hatari bado hajayaonesha  ila anaomba watu wamvumilie kwa sababu amekuwa akitingwa na majukumu ya hapa na pale lakini ataibuka hivi karibuni.

ha! ha! haa!  mimi sio rahisi kupotea kihivyo kama watu  mnavyofikiria aisee, niko na madude mengi sana ya hatari  bado sijayaachia, sema kuna baaadhi ya majukumu ya kikazi kwa sasa ninayafanya.-Alifunguka Ebitoke

juzi juzi katika moja ya majukwaa ya matamasha ya fiesta ambalo hivi karibuni linafikia ukingoni Ebitoke alionekana katika jukwaa akiwa na msanii Ben Pol wakiombana na msamaha na kutangaza kusameheana na kurudiana hivyo zile tetesi za kuwa wameachana kufutika tena masikioni pa watu ambapo kwa muda kidogo wawili hao walionekana kuwa mbalimbali na kusemekana kuwa walikuwa wamegombana.

Ingawa Ben Pol mwenyewe amekuwa akikanusha habari za kuwa na mahusianao na mwanadada huyo lakini Ebitoke kila siku amekuwa akisema anampenda sana Ben Pol.

Napenda Mwanamke Anayejiamini- Ben Pol

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Bernad Paulo maarufu kama Ben Pol amefunguka kuhusu aina ya mwanamke anayempenda. Mwana muziki huyo amekuwa katika vichwa vya habari sana kutokana na kutajwa na mchekeshaji maarufu Anastazia Kisaveli ‘Ebitoke’.

Ebitoke amemtaja mara kwa mara kwamba anampenda kimapenzi Ben Pol lakini kijana huyo amepotezea. Katika mahojiano yake aliyoyafanya hivi karibuni Ben Pol aliweka wazi kuwa hana muda wa kumuongelea Ebitoke kwani kulitokea mvurugano baada ya Meneja wa Ebitoke kutoka Timamu tv kudai kuwa alimlipa Ben Pol kiasi cha shilingi milioni tatu ili tu aonekane na Ebitoke katika mitandao ya kijamii lakini Ben Pol amekataa tuhuma hizo.

Ben Pol ameweka wazi kuwa kitu pekee anachoangalia kwa mwanamke ili awe naye kimapenzi ni lazima awe najiamini pindi wanapokuwa kwenye maongezi.

“Endapo nikimpenda msichana kitu kikubwa ninachoangalia ni ‘confidence’ yake hasa pindi tukiwa tunachat, usmart, umakini na uharaka wa kujibu vitu unavyokuwa unaulizwa kwa wakati huo”.

Ben Pol ni moja kati ya wanamuzi wanaopendwa sana na wadada yaani mashabiki wake wengi ni wasichana kutokana na aina ya muziki anayoimba hata pia na muonekano wake . Hivi sasa Ben Pol anatamba na nyimbo yake mpya inayoitwa kidume aliyomshirikisha mwanamuziki kutoka Nigeria inayofanya vizuri sana katika stesheni nyingi za redio nchini.

Ebitoke: Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani

Siku chache zilizopita, Ben Pol alisema kuwa hataki aulizwe kuhusu mahusiano yake na mchekeshaji Ebitoke. Msanii huyo alieleza kuwa anajiusisha na mambo ya muziki kwa sasa na hangependa kuongelea mambo yake binafsi.

Ebitoke amedhibitisha kuwa yeye na Ben Pol bado ni wapenzi ila hawataki tu kuweka mapenzi yao hadharani. Akiongea na Times FM, Ebitoke alisema mipango walionayo kwa sasa ndio inapelekea kutoonekana pamoja kwa sasa na kupostiana kwenye mitandao ya kijamii.

Ben Pol na Ebitoke

“Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani, hatutaki tuviweke hadharani. Hamna siyo vya unyago na siwezi kumuongelea vibaya Bentoke labda watu wanaona haniposti mimi kila siku lakini si hivyo. Tunamipango mingi, kwanza kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika jambo lolote na ameniaidi lazima ahakikishe natimiza malengo yangu na ameona mimi bado ni mdogo ananifundisha kila kitu jinsi gani nikue kwenye hii tasnia na the way hii mitandao ya kijamii ilivyo na maneno ya watu yalivyo,” alisema Ebitoke.

 

Mchekeshaji Ebitoke afunguka kuhusu Ben Pol kushindwa kumuondoa ubikira

Mchekeshaji wa kike Ebitoke alipata umaarufu sana miezi michache zilizopita alipolia kwenye mahojiano kwa TV huku akitaka msanii Ben Pol afunge naye ndoa.

Ebitoke alisema anampenda sana Ben Pol na hata alitaka mwimbaji huyo amuondolee ubikira wake. Alisema alikua tayari kufanya lolote ili Ben Pol ampende.

Soma pia: Ben Pol amjibu mchekeshaji aliyelia na kumwomba amuoe

Ben Pol na Ebitoke hatimaye walikutana na kwa sasa inasemekana kuwa wawili hao ni wapenzi. Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) ya EATV, Ebitoke alisema kuwa Ben Pol hajafanikiwa ‘kufungua mlango wake’.

Ben Pol na Ebitoke

Mchekeshaji huyo alieleza kuwa bado hajawahi kulala na mwanaume yoyote yule katika maisha yake na alitaka Ben Pol ndo awe mwanaume wa kwanza kulala naye.

Hata hivyo kuna wale wanaodai kuwa Ben Pol na Ebitoke wanafanya tu utani ilhali wanazidi tu kujitangaza na kuzidi kupata kiki katika kazi zao.

 

Ebitoke: Sijampenda Ben Pol kisa nimpe ubikira yangu

Mchekeshaji wa kike Ebitoke aligonga vichwa vya habari kwa kusema kuwa anampenda sana Ben Pol na anataka mwimbaji huyo amoe.

Ebitoke alifungua roho katika mahojiano na Sasa TV na kueleza jinsi anavyompenda Ben Pol, machozi yalimchuruzika usoni mchekeshaji huyo akieleza jinsi anavyompenda Ben Pol.

Soma Pia: Ben Pol amjibu mchekeshaji aliyelia na kumwomba amuoe

Ebitoke

Katika mahojiano na Juma3tata, Ebitoke alifunguka kuhusu kumpea Ben Pol ubikira wake. Alisema kuwa lazima mwimbaji huyo amoe kwanza ndo ampe ubikira wake.

“Napenda watu waelewe kitu kimoja, mimi sijampenda Ben Pol kisa nimpe bikira yangu, kwa mfano akikataa kunioa basi nitamwacha aendelee na familia yake, kwa sababu watu wanaongea kinoma, lakini kuhusu hilo nitaendelea kujituza mpaka mwanaume wa kweli atokee kwenye maisha yangu ndiyo nitampa bikira yangu,” Ebitoke alisema.

Ben Pol amjibu mchekeshaji aliyelia na kumwomba amuoe

Mchekeshaji wa kike Ebitoke anampenda Pel Pol kwa dhati, alilia akifanya mahojiano huku akimwomba Ben Pol amuoe.

Ebitoke alifungua roho katika mahojiano na Sasa TV na kueleza jinsi anavyompenda Ben Pol, alisema ishu ya Ben Pol kuwa na mtoto ilimuuma sana kwasababu alikua anadhani ako na bibi.

https://www.youtube.com/watch?v=h_cKUc2TVgQ

Ben Pol amemjibu Ebitoke, anataka kukutane naye uso kwa uso ili kudhibitisha kama mchekeshaji huyo anamaanisha anachosema ama ni utani tu.

“Kwanza niseme tuu naheshimu hisia za kila mtu yeye ni binadamu na ameonesha hisia zake soo naziheshimu sana. Kweli nimeziona habari mitandaoni tuu tangia jana watu wakiposti lakini sikuamini siunajua habari za mitandao bro! ila leo pia nimeona video yake akisisitiza ombi lake lakini bado siamini na nitaamini na nitafurahi kama tukionana uso kwa uso,” alisema Ben Pol.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.