Lulu Atangaza Rasmi Kuwa Yeye ni Simba

Mwanadada Lulu michael ametangaza rasmi katika vyombo vya habari kuwa yeye ni shabiki m,kubwa wa simba , ushabiki ambao aliupata kutoka kwa mama yake kwa sababu mama yake ni shabiki wa simba.

Lulu anasema alianza kuipenda simba kutokana na watu waliokuwa wakimzunguka hasa mama yake mzazi,.

Hata hivyo , Lulu aliyaongea hayo alipokuwa katika ziara yake katika kampuni ya habari ya mwananchi kabla ya mechi  ya simba na al ahly na kusema kuwa anawatakia kheri simba kufanya vizuri katika mechi hiyo huku akiwataka kutulia na kutokukata tamaa ya kufungwa magoli ,engi nyuma kuwafanye waumie na kushindwa kufanya vizuri.

Siwezi Tangaza Harusi Yangu Kwenye Mitandao :-Lulu

Mwanadada Lulu michael ambae kwa fununu zilizokuwepo hapo awali ni kwamba mwanadada hiuyo alienda kufungia ndoa yake nchini China amefunguka na kusema kuwa hakutaka na wala hatotaka ndoa yake itangazwe katika mitandao ya kijamii kwa sababu hilo ni swala ambalo sio lazima kila mtu kulijua hilo.

Lulu ameyasema hayo alipokuwa aktika tour yake kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwa ajili ya misaada atakayo itoa katika msimu huu wa valetine kwa watu wenye uhitaji katika jamii.

Lulu ambae pia aliwahi kusemwa kuwa mwanaume ambae anafunga nae ndoa amekuwa akimpiga na kumtesa sana kwa sababu ya pesa alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa maisha yakeya nyumbani yatabaki kuwa hivyo na wala hana haja ya kusema katika mitandao.

Lulu anasema kuwa tetesi zoozte hazina ukweli kuhusu ndoa yake na michakato ya harusi bado inaendelea.

 

Lulu Afungukia Tetesi Za Kuwa na Mimba

Msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuweka wazi kuwa sio mjamzito na hata alipotoka gerezani hakuwa mjamzito.

Lulu alitoka gerezani mwaka jana Baada ya kutumikia kifungo kwa miezi kadhaa lakini Baada ya kutoka kuna tetesi zilisambaa kuwa ametoka mapema kutokana na ujauzito na pia alikuwa ameongezeka kwa kiasi kikubwa.

Lakini siku ya Leo kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm, Lulu ameweka wazi kuwa hajawahi kuwa mjmzito kabisa bali alinenepa alipokuwa jela na kuongezeka karibia kilo 20.

Lulu amesema taarifa zilizowahi kusambaa kuwa alikuwa mjamzito hazily was za kweli bali alivyotoka jela alikuwa ameongezeka kilo 20 hivyo kupelekea mwili Wake kuwa mkubwa sana.

Lakini pia amefungukia tetesi za kugombana na Mpenzi Wake Majizzo ambapo amesema kuwa hawezi kuongea chochote kuhusu maisha yake binafsi:

Watu wanatengeneza vitu vyao ili wapate jambo kutoka kwako, watu wanatengeneza mambo yao, Mimi kuwa maarufu haimaanishi kila kitu katika miasha yangu lazima kiwe maarufu, hata mahusiano yangu yawe maarufu.

Juu ya hilo la kuvua pete Siwezi kukubali wala kukataa wacha waamini wanavyoamini”.

 

Dr. Cheni Baba Yangu Wa Sanaa- Lulu

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuongelea uhusiano wake  na muigizaji mkongwe wa Bongo movie Dr. Cheni.

Kwa miaka mingi sasa Lulu ameonekana kuwa karibu sana na Dr. Cheni na sasa anafunguka na kuweka wazi kuwa ni mtu wa muhimu kwenye maisha yake.

Katika mahojiano aliyofanya na Kituo cha Times Fm, Lulu amefunguka na kusema kuwa watu wengi hawajui uhusiano Wake na Dr. Cheni Lakini yeye amemtaja kama baba yake katika Sanaa.

Watu wengi hawajui Lakini Dr. Cheni ni baba yangu wa Sanaa, tangu alipogundua kipaji changu Nikiwa na miaka mitano, amezidi kuwa mtu wa muhimu kwangu katika kuikuza na kuiendeleza Sanaa yangu”.

Lakini pia Dr. Cheni ameonekana na Lulu katika wakati ambao alikuwa anapitia kipindi kigumu ikiwemo wakati ambao aliwahi kupelekwa jela.

Lulu Michael Akataa Kuongelea Swala la Kupigwa na Majjizo

Kumekuwa na tetesi zilizosambaa katika mitandao kuhusu mwanadada Lulu Michael kupigwa na mwanaume ambae amemtolea mahali na kumvisha pete ya uchumba huku ndoa ikisemwa kunukia siku yoyote.

Mwanadada Lulu Michael amekataa kuzungumzia swala hilo huku akisema kuwa wengi wanaozungumzia na kusambaza taarifa  hawataki kuona anapiga hatua katika yale anayoyafanya kwa sasa lakini hawzi kuzngumzia swala hilo kwa sasa kwa sababu yuko na kampeni kubwa na yenye manufaa kwa jamii kuliko kitu chochote kwa sasa.

Kama umeshawahi kuona filamu za mapigano , mwisho wa siku utakuja kuona jinsi adui anavyojaribu kumuadaha sterling,  na hivyo ndivyo ninavyoyachukulia maneno haya.

Tetesi hizo zlianza hivi karibuni baada ya mwanadada huyo kuonekana hana pete ya uchumba aliyovishwa hivi karibuni na mume wake huyo mtarajiwa.

 

 

Actress Lulu Michael now selling all her clothes months after completing her two years jail term 

Months after being released from her two-year jail term, Bong actress Elizabeth Lulu Michael has now settled back after making a fresh start.

The actress was in jail after killing her ex-love after an argument.

Since coming out, she has been maintaining a low profile and has avoided the media almost completely. Lulu is also planning to get married soon and settle down with media mogul Majizzo.

This Valentines, the actress plans to spend the day not with Majizzo however, but with the less fortunate. She has been selling her cloths to raise enough to donate to them during her visit.

 “Wakati Wengine Tumepata Fursa Ya Kuwa Na Furaha Kwa Vile Tulivyonavyo Kuna Baadhi Ya Wenzetu Wamekosa Nafasi Hiyo….. Na HUU NI MPANGO WA MUNGU. Kuelekea Siku Ya Wapendanao Februari 14,Nimeamua Kuuza Sehemu Ya Nguo Zangu Ambazo Yawezekana Umeshawahi Kuziona au Haujaziona. Na Pesa Yote Itakayopatikana Kupitia Mauzo Haya Itaenda Kusaidia Vitu/Watu Wenye Uhitaji Katika Jamii. Please Join me to Save My Valentine.#Savemyvalentine,” reads Lulu Michael’s post.

Wedding

On October 1st 2018, Majizzo proposed to Lulu during a home party he had organized to celebrate his three sons. The two later held a small, but lavish traditional wedding to pay bride price ahead of their planned white wedding.

Lulu Atoa ofa ya Nguo kwa Mashabiki.

Mwanadada Lulu michael ameamua kutoa ofa kwa mashabiki wake kwa kutaka kugawa nguo zake nyingi zilizopo katbabtini huku akiwataka watu mbalimbali kumtumia picha ya nguo waliowahi kumuona nayo akiwa amevaa na kupendeza kisha yeye kuipenda ili aweze kugawa nguo hizo.

Mwanadada huyo ambae kwa sasa amekuwa nje ya mitadao amekuwa akitumia sana mtabada wake wa snap kwa ajili ya kupost kutokana pia na population ndogo iliyopo huko.

Akiandika katika ukurasa wak wa snap, lulu alisema kuwa ” kuna nguo yoyote uliwahi kuipenda  na ukatamani kuwa nanyo…oaky 2019 nitaanza kusafisha kabati langu ..who si ready ”

 

Makonda Athibitisha Lulu na Majjizo Kufungia Ndoa China

Mkuu wa moa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda amefunguka wakati akimpa pongeza za kuamua kuchukua jiko kwa mc pilipili huku akijikuta akifunguka engi kuhusuwatru wake wa karibu anaowajua ambao pia wao katika kiwanda cha burudani.

Kama itakumbukwa , Mh huyo ndio alikuwa master mind wa  harusi ya msanii lulu michael na mpenzi wake majizo ambapo tunaambiwa kuwa wawili hao waliamua kwenda kufumga ndoa yao nchini china ambapo watrakuja huku kwa ajili ya kufanya sherehe tu.

Mwanadada Lulu Michael na majizo wamekuwa nje ya nchi kwa muda sasa huku taaarifa za wali zilidai kuwa walienda kwa ajili ya matembezi lakini mkuu wa mkoa katoboa siri.

Mh makonda aliamshauri Mc Pilipili kumshauri diamond kuacha kuhairisha ndoa kama alivyofanya kwa sasa kati yake na tanasha huku akisema kuwa swala lake la kumvisha msichana pete limewaumiza wengi aliwahi kuwa nao katika mahusiano.

 

Lulu Adaiwa Kuwekewa Ulinzi Mzito.

Tangu ametoka gerezani na hata kukitumikia kifungo chake cha nje na hata sasa amekimaliza na kuanza process za harusi, mwanadada Lulu Michael amekuwa aonekani sana kama zamnai alivyokuwa kila kona ya mtandao unamkuta yeye.

Mwanadada huyo kwa sasa anadaiwa kutembea na ulizni mkali wa bodyguard anaetembea nae kila mahali anapokwenda kwa ajli yaulizni na usalama wake.

Haijulikana sababu kubwa ya mwanadada huyo kutembea na mlizni lakini almekuwa akionekana katika baadhi ya matukio hayo makubwa ya harusi yake akiwa na mtu anaetembea nyuma yake kuhakikisha ulinzi wake.

Wakisimulia wale walioshuhudia siku ya kutolewa kwa posa yake. Lulu alionekana akija ukumbuni huku nyumba yake kukiwa na mtu wa ulizni aliekuwa akimuelekeza kila kitu cha kufanya hata kuwa nae karibu muda wote.

Hata hivyo mashabiki wake wanasema kuwa swala la kuwa na mlinzi ni kwa ajili ya ulinzi wake lakini kwa mashabiki ina wanyima uhuru kwa sababu hapo mwanzo walikuwa kila wakikutana nae wanaweza hata kupiga nae picha na kumkimbilia lakini tangu amekuwa na walzini imekuwa vigumu kwake kuwa karibu na mashabiki.

 

Lulu Adaiwa Kuwekewa Bodyguard Baada Ya Kuvishwa Pete

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amedaiwa kuwekewa ulinzi mzito na mume wake mtarajiwa Majizzo Baada ya kumvalisha pete.

Gazeti pendwa la Amani linaripoti kuwa tangu Lulu avalishwe pete ya uchumba na kuwa mke mtarajiwa, aliwekewa ulinzi huo binafsi hivyo kila anapokuwa lazima awe na bodigadi.

Nafikiri jamaa wake kaona ni vizuri kwa vile Lulu ni staa na kumtengenezea muonekano wa kistaa, ni vizuri akawa na mlinzi binafsi, sasa hivi ana bodigadi anaitwa Livingstone“.

Gazeti hilo lilithibitisha taarifa hizo wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho kwenye jengo la LAPF baada ya kumnasa msanii huyo akiwa na bodigadi huyo mwenye ‘miraba minne’ alipokuwa amehudhuria kwenye harusi ya jamaa anayefahamika kwa jina la Renatus Nyakai na mkewe Glorian Jarimo.

Mmoja wa shabiki wa Lulu aliyejitambulisha kwa jina la Lucy Mnyate aliyeshuhudia jinsi Lulu alivyokuwa akilindwa, alipongeza na kusema anastahili kwani ni staa mkubwa.

Unajuwa Lulu ni kipenzi cha watu sana na zamani hatukuwa tumezoea hivyo ilikuwa kila akionekana watu tunajifotolesha mapicha lakini kwa sasa haya nafikiri ni mabadiliko mazuri kwani ni staa mkubwa“.

Tangu ametoka gerezani miezi Michache iliyopita Lulu amekuwa na upepo wa bahati nzuri kwani amechumbiwa na Mpenzi Wake wa muda mrefu Majizzo na kumaliza kifungo chake rasmi.

Lulu Athibitisha Kukutana na Mungu Live

Mwanadada Lulu Michael amefunguka na kutangaza kuwa alikutana na mungu live hasa baaada ya kukutana na matatizo makubwa katika maisha yake katika umri wake mdogo.

Akijibu moja ya pongezi alizokuwa akipewa na ke wa Mh Paul Makonda hasa baada ya kufanikisha zoezi kubwa katika maisha yake wikiendi iliyopita ambapo mpenzi wake alikwenda nyumbani kutoa mahali.

Mwanadada huyo amekuwa katika wakati mgumu mara nyingi hasa kutokana na makubwa aliywah kutapitia ikiwemo ya kufungwa gerezani akiwa na umri mdogo na hata kuwa na historia ya kuwa na kesi ya mauaji .

Lulu anasema kuwa kwa jinsi ambayo amekuwa akikutana na Mungu live katika maisha yake anaamini kuwa hakuna kinachoweza kumshinda katika maisha haya ya kawaida.

Lulu Michael Atolewa Mahali na Mchumba Wake.

Mwanadada Lulu Michael ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu kutoana na kuwa na kesi ya kuua bila kukusudia, wiki iliyoisha alianza kuonekana katika mitandao ya kijamii hasa baaada ya kuweka moja ya post zake kaika mitandao ya kijamii .

Lakini moja ya habari kubwa  ya kufurahisha ni kwamba mwanadada huyo kwa sasa anatarajia kufunga ndoa siku yoyote hasa baada ya matukio ya kuhararsiha ndoa hiyo yakifuata moja baada ya jingine.

Mwezi uliopita mwanadada huyo alivalisha pete ya uchumba na mpenzi wake wa siku nyingi majizo na sasa wiki iliyopita mwanadada uyoa ametolewa mahali na mwanaume huyo kuashiria kuwa siku yoyote wawili hao wanatarajia kufunga ndoa.

Mwanadada huyo ambae mashabii wake wamekuwa wakimsubiri kwa hamu sana kumuona akiwa katika mitandao na kufanya yale aliyokuwa aktafanya hapo nyuma amekuwa kimya sana tangu ametoka gerezani na inawezekana baada ya hayo ameona ni bora kubadilisha maisha yake kabisa.

Lulu Avunja Ukimya Baada Ya Kumaliza Kifungo Chake

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu hatimaye amevunja ukimya tangu alipomaliza kifungo chake na kutoa shukrani zake za dhati kwa watu wote.

Mwaka jana Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka mieili jela Baada ya kukutwa na hayo a ya kumuua Bila kikusudia aliyekuwa Mpenzi Wake marehemu Steven Kanumba.

Lakini Baada ya kutumikia kifungo chake kwa miezi kadhaa Lulu alipata  msamaha wa kipunguziwa kifungo na kupewa kifungo cha nje ambacho ametumikia na kumaliza Wiki hii.

Baada ya ukimya mrefu kwenye mitandao ya kijamii hatimaye Lulu amefunguka na kuandika haya katika ukurasa wake wa Instagram:

https://www.instagram.com/p/BqO4xVJHf3d/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=fuqi471bjk50

Msemaji wa Magereza Akanusha Uhuru wa Lulu Michael

Huku taarifa za habari za furaha zikianza kusambaa katika vyombo mbalimbali kuhusu msanii Lulu Michael kuwa huru baada ya kusemekana kuwa kifungo chake kuisha lakinimsemaji wa magereza amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa lulu bado ni mfungwa kama wafungwa wengine na kifungo chake kitakapoisha atakuwa hurulakini si sasa.

Msemaji huyo anasema kuwa kwa kawaid ahaweiz kuwa huru kama hajafata utaratibu wa magerezawa kuachi wa huu hata kama hakuwa akiishi gerezani kwa kipindi cha muda mrefu kutokana na kutumikia kifungo chake cha nje.

Msemaji wa magereza anayasema hayo baada ya kuona kuwa taarifa za kuwa huru kwa mwanadada huyo zimesambaa sana katika mitandao ya kijamii, “taratibu nadhani anazifahamu kwa sababu lazima kuna utaratibu wa kufuatwa kabla ya kuwa huru,  na hata kama yuko kifungo cha jje kuna utaratibu anafuata pia kama wafungwa wengine tu hata kama ni mtu maarufu , kile ambacho lulu anafanyiwa ni kama anaweza kufanyiwa mfungwa mwingine yoyote yule...”

Msemaji huyo anasema kuwa kama ilivyo kwa wafungwa wengine kuwa hawakutangazwa kipindi anawekwa ndani na ndivyo itakavyo kuwa akiwa anatoka, na hata kama alikuwa na kifungo cha nje haimaanishai kuwa anatakiwa kuondokea huko huko uraiani bali anapaswa kurudi magereza na kufuata taratibu za kumaliza kifungo na ndipo atakapokuwa hur na maisha yake ya nje..

Lulu Amaliza Rasmi Kifungo Chake

Mwanadada Elizabeth Michael amemaliza rasmi kifungo chake alichokuwa akitumikia kwa muda saa akiwa nje na November 12 ndio ilitakiwa kuwa huru kwa kukimaliza kifungo hicho.

Mwanadada Lulu ambae alikuwa nje akitumia kifungo cha nje huku akipangi wa kufanya kazi mbalimbali za kijamii amekuwa huru kuanzia sasa na kwamba hata zile kazi alizokuwa akifanya za kijamii itakuwa zimefika kikomoe kuanzia sasa.

Lulu alihukumiwa kifungo cha jela baada ya kukitwa na kesi ya kuua bila kukusudia kwa mwanamaigizo mwenzake Steven Kanumba mabae alikuwa ni mpenzi wake pia walipokuwa wakikorofisha  na kumsukuma kwa bahati mbaya na kuuumia sehemu za kichwa.

Mwanadada Lulu anaingia uraia tena akiwa tayari amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa siku nyingi Majizo ambao walitangaza ndoa hiv karibuni.

Majizzo Atangaza ujio mpya wa Lulu

Mchumba wa mwanadada Lulu michael amefunguka na kuweka bayana ujio mpya wa mpenzi wake huyo kwa kuweka kipande kidogo cha picha inayoonekna kuwepo jikoni kwa sasa  .

Huku ikiwa ni zaidi ya mwaka sasa tangu mwanadada Lulu Michael awe kimya katika mitandao ya kijamii na pia katika televisheni tangu alipokumbwa na hukumu ya kesi ya kuua bila kukusudia, mwanadada lulu michael amekuwa akisubiriwa kwa hamu na kila shabiki yake.

katika ukurasa wake wa instagram Majizo aliandika”back to bussiness “

Mwanadada Lulu michael anarudi katika tsnia akiwa tayari amesubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki zake.

Kifungo cha Lulu Chabakiza Siku 40.

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael ’Lulu’, amebakiza siku 40 kumaliza kifungo chake huku akielezwa kuwa mtiifu kipindi chote.

Lulu alikuwa akitumikia kifungo cha miaka miwili jela, baada ya Novemba 13, mwaka jana kuhukumiwa na mahakama kuu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa gwiji wa filamu, Steven Kanumba.

Hata hivyo, Aprili 26 mwaka huu, msanii huyo aliye kwenye orodha ya wadada wanaojua kuvaa  hapa Bongo alibadilishiwa adhabu hiyo na kuwa ya kifungo cha nje.Kutokana na hilo, alipangiwa kazi ya kufanya usafi katika Wizara ya Mambo ya Ndani iliyopo maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam aliyoianza tangu Machi 14 mwaka huu.

Katika siku za mwanzo gazeti la Mwananchi lilipata picha akiwa ameanza kutumikia kifungo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa Probesheni na Huduma za Jamii, Charles Nsanze, amesema katika kipindi chote hicho Lulu amekuwa akitekeleza majukumu yake bila kukosa. “Amekuwa mmoja wa wafungwa wenye nidhamu ya hali ya juu na hakuna siku aliyokosa kuja na kufanya kazi kama alivyopangiwa,” amesema Nsanze alipoulizwa kuhusu utumikiaji adhabu wa msanii huo ulipofikia hadi sasa.

Kifungo cha Lulu kilipaswa kuisha Machi mwakani endapo asingebailishiwa adhabu ya kifungo gerezani na kuwa kifungo cha nje baada ya kupata msamaha wa Rais.Magereza ilifafanua kwamba ina utaratibu wa kutoa msamaha wa theluthi moja ya kifungo na msanii huyo alinufaika baada ya kuonyesha tabia njema.

Elizabeth Lulu Micheal engaged to Hamisa Mobetto’s baby daddy!

Bongo actress Elizabeth Michael who is popularly known as Lulu is about to become someone’s wife.

This was confirmed by a viral video that is currently making rounds on social media. Well, surprisingly her long term boyfriend Majizzo decided to propose to the young lady at a private party he had held for his three kids.

In the clip, Majizzo’s sons take turn to appreciate Lulu before the youngest son pops the question on behalf of his daddy.

She said yes!

Judging from her reaction on the video, it’s clear to see that she had no idea that Majizzo was going to propose.

Anyway as for now it has been confirmed that Lulu Micheal will be getting married to Hamisa Mobetto’s baby daddy.

https://www.instagram.com/p/BoXNEMchpOl/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1iamde3gizpia

 

Mashabiki Wamtolea Povu Lulu kwa Kutomzika Patrick

Ikiwa ni siku kadhaa tu zimepita tangu maziko ya mtoto Patrick yamepita ambapo maiti ya mtoto huyo iliagwa katika uwanja wa Leaders na kuacha simanzi kwa watu wengi sana. Maombeloezo hayo yaliyohudhuriwa na watu mbalimbali huku wimbi kubwa likiwa ni wasanii walifurika katika viwanja hivyo.

Lakini kesi imekuja baada ya mashabiki kuanza kuhoji kwamba kwanini mtu muhimu na wa karibu na Muna Love , Lulu Michael hakuhudhuria katika kuagwa  kwa mwili huo katika viwanja hivyo ilhgali kuna video zilivuja zikimuonyesha lulu akiwa nyumbani kwa muna akiwa anaandaa sehemu kwa ajili ya wageni wanaokuja katika msiba.

Wengine wamesiitishwa hasa wanaojua maisha ya nyuma ya lulu na uhusiano aliokuwa nao na baba mzazi wa marehemu( Peter) ambae aliangaika sana na Muna kipindi cha kesi yake ya mauaji iliyokuwa imemsumbua sana msanii huyo.

Watu waliokuwa msibani , baada ya kuona video ile walitegemea kuwa lulu atakuwa karibu sana na Muna kutokana na pia Muna alivyokuwa akijitoa sana katika matatizo ya Lulu hata kipindi mtoto wake akiwa mgonjwa hospital.

Baadhi ya watu waliokuja msiba waliongea sana kuhusu hilo huku wengine wakisema kuwa kwa sasa  lulu hakuwa amepanga kutokea hadharani kwa watu na ndio sababu inamuwia vigumu kutokea kwa ghafla ukizingatia hajamaliza kifungo chake.

Wanaokuombea Mema Wako Wachache-Ujumbe Wa Makonda kwa Lulu.

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salam Paul Makonda amemuandikia ujumbe mzito msanii lulu michael katika siku ya kumbukumbu wa kuzaliwa amabyo kwa upande wak hatoweza kuisherekea kutokana na kuwepo gerezani akitumikia kifungo chale cha miaka miwili baada ya kukutwa na hukumua ya kuua bila kukusudia.

Katika siku hii ambayo ndugu wa lulu waliamua kusherekea siku hiyo  wakitoa zawadi na misaada katika hospitali ya Muhimbili kama moja ya kumuombea msanii huyo , Paul Makonda aliamua kutuma ujumbe huo hata kama hatoweza kuuona kwa sasa ila unaweza kumfikia.

kumbe wanaokuombea mema wako wachache ila wenye nyusoza huzuni wako wengi sana   japo hawamaanishi.kwa  kuwa mungu ametenda watakuja tena na nyuso zao za furaha  japo hazina uhusiano na mioyo yao.kwa kifupi hii ndio dunia ambayo mungu amkuongezea mwaka mwingine wa kuishi.Happy birthday mwanangu @elizabethlulumichael

Lulu alifungwa baaada ya kukutwa na hatia ya kusababisha kifo cha marehemu Kanumba ambae alikuwa ni mpenzi wake.

Profesa Jay Kumtembela Lulu Gerezani

Mwanamuziki mkongwe wa bongo hip -hop ProfesaJay anasema kuwa siku yoyote kuanzia sasa yuko mbioni kwenda  kumtembelea msanii wa bongo movie lulu michael ambae ayupo gerezani akitumikia kifungo chake cha miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.

                                                 

Profesa Jay anasema kuwa anaamini kabisa kuwa lulu ana mengi ya kuongea hivyo anatamani sana kuongea nae ili aweze kumwambia yalitopo moyon mwake na pia kumfariji kwa kila analopitia kwa sasa.

Ninatamani sana kuonana na lulu niweze kuzungumza nae,ninafahamu ana mengi ya kuzungumza na hivyo ninajipanga  na muda pia  na ikiwa tayari nitawafamisha ni lini ninakwenda kumuona.-  Alisema Profesa Jay ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake kipya cha Pagamisa alichomshirikisha Mr.T-Touch

 

Majizo Amtakia Lulu Kheri kwa Siku ya Wanawake Duniani.

Inaweza kutika huzuni kidogo unapoona mtu amemkumbuka mtu anaempenda lakini hawezi kuwa nae  karibu kwa muda huo kwa sababu mbalimbali.Hii imetokea katika siku ya wanawake Duniani ambapo Dj maarufu bongo na meneja wa Efm Majjizo alipoamua kumtakia mpenzi wake  Elizabeth Lulu  Michael kheri kwa siku ya kusherekea siku ya wanawake Duniani akiamini kuwa siku moja atakuja kusoma ujumbe huo.

Majizo na Lulu ambao walikuwa wapenzi kwa kipindi kirefu, mpaka Lulu anapata kifungo chake cha kutumikia jela kwa muda wa miaka miwili ameomyesha hisia zake za kumtakia kheri lakini pia kumuonyesha ni jinsi gani ambavyo amekuwa akijua mchango wake kama mwanamke jasiri aliyewahi kutokea katika maisha yake.

katika ukurasa wake wa instagram , Majizo aliandika“in life all people may probably be necessary Vvery useful if everything goes right or wrong.You are very important because you can be strong in all situation.Happy women’s day#utakujakuisomaoneday.

Lulu alihukumiwa mwaka uliopita kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.

Diana Apanga Safari ya Maombi Gerezani kwa Lulu

Msanii wa maigizo bongo movies Diana Kimari ambae amewahi kufanya filamu nyingi na mwanadada Lulu Michael na filamu hizo zimekuwa zikiwavutia mashabiki kutokana na wasichan hoa kuonekana kuendana tabia na hata umri hivyo kuendelea kunogesha filamu hizo.Diana Kmario  amefunguka na kuelezea nia yake ya kwenda kumtembelea rafiki yake huyo gerezani na kumpelekea wadada wa kufanya nao maombezi na kumpa neno la Mungu ambalo anaamini  litakuwa likimfariji mpendwa wake.

Diana anasema kuwa kwa muda mrefu zaidi ya mara tatu  amekuwa akitaka kwenda kumuona rafiki yake huyo gerezani  lakini anakosa muda kutokana na mambo kuwa mengi na kuingiliana lakini alishapanga kuwa atapeleka kikundi cha maombi  ambacho huwa kinatoa neno kwa wafungwa na kuwafariji  kwa ajili ya kufanya maombi na Lulu Michael na anaamini kuwa tafurahi sana na kufarijika kwa hilo.

Sio kwamba nipo kimya simkumbuki llulu , hapana.mwisho wa mwezi huu itaenda kumuona lulu kuna wadada ambao huwa wanaenda kutoa neno kila mwisho wa mwezi kwa wafungwa  gerezani kwaio nitaenda nao na ninajua tafurahi sana.-Alifunguka mwanadada huyo.

                                                      

            moja ya picha waliowahi kuwa pamoja Diana na Lulu.

Lulu Elizabeth Michael yuko gerezani akitumikia kifungo chake cha miaka miwili jela ikiwa ni  hukumu aliyoipokea mwaka 2017 mwishoni baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusidia na kusababisha kifo cha aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba miaka takribani minne iliyopita.

Mpaka sasa ni wasanii wachache waliofunguka kuwa wamekuwa wakimtembelea Lulu gere zani, wanaokwenda huko mara nyingi ni watu wa familia yake ,ingawa pia msanii Mwijaku alikwenda na kurudi na ujumbe mzito kutoka kwa Lulu.

Moja ya filamu pendwa ambayo Lulu Michael na diana kimari walishawahi kuicheza ni ile ya foolish age na ile ya Family Disaster ambayo wamecheza na Ray Kigosi

Hali ya Lulu Gerezani Yatajwa Kuwa shwari,Sio Kama Wengi Wanavyodhani.

Hali ya msanii wa maigizo ya bongo movies  Lulu Michael ambea alipata kifungo chake mwaka jana Novemba baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusuida msanii mwenzie ambae alikuwa mpenzi wake steven kanumba  yatajwa kuwa ni nzuri tofauti na vile watu wengi walivyokuwa wakidhani kwa sababu watu wengi walikuwa wakimuonea huruma kutokana na maisha mazuri aliokuwa akiishi alipokuwa uraiani.

Mwandishi wa magezeti katika kampuni ya GPL,alikwenda katika gerza aliliopo Lulu kwa ajili ya kutaka kumjulia hali na kuhojiana nae ili kujua hali yake kwa wakati huu tangu amezna kutumikia kifungi chake ambapo bahati mbaya maafisa wa gerza hilo walikataa kumruhusu kutokana na kwamba kwa utaratibu wa gerezani watu wanaopaswa kumuona mfungwa ni wale wa karibu nae na ambao wanakuwa wameandikwa katika vitabu vya kumbukumbu.

hata baada ya kushindwa kuingia ndani wa ajili ya kumuona lulu michael, mwandishi alianza kupiga stori na moja ya watu waliokuwa mlangoni hapo ambao wapo kwa ajili ya kufanya kazi zinazowahusu gerezani hapo abae alianza kwa kusema kuwa lulu kwa sasa hali yake ni shwari sio kama mwanzo kwa sababu muda wote amekuwa ni mtu mwenye tabasamu na ameanza kunawiri kutokana na kuyazoea maisha ya huko.

yaani amenenepa sana sasa hivi, tofauti na vile mwanzo alivyokuwa amekuja,anaendelea vizuri na hajwahi kuugua ugonjwa wowote tangu amekuja.

Afisa huyo anaendelea kusema kuwa mara nyingi lulu amekuwa akiwashangaza ndugu na  jamaa zake kwa sababu wengi wanakuja wakimuonea huruma lakini yeye mwenyewe anakuwa na sura  ya kujiamini na kujifariji muda wote.

anawashangaza kwakweli ndugu zake wanaokuja kila wiki kumuona,anawafariji na kuwapa moyo utafikiri yeye ndie yupo sehemu nzuri kuliko wenzake.huyu binti anasali sana na mara nyingi utasiki akiwaambia wenzie kuwa wasihuzunike kabisa,wachukulie tu kama yupo shule ya boarding atatoka tu.-Alisema afisa huyo.

Muna Love ambae ni rafiki na ndugu wa karibu wa familia ya msanii huyo ambae muda wote alikuwa bega kwa bega nae , alikiri kuwa ni kweli lulu amekuwa mtu wa kuwatia moyo sana ndugu zake wanapokwenda kumuona na hata hali yake kiafya sio kama vie walivyodhani itakuwa ya kunyongonea siku zote.

ni kweli anatushangaza hata sisi kwanza amenenpa sana, mara nyingine tunapokwenda kumuon  sisi tunakuwa na simanzi lakini  yeye anakuwa ndie mfariji wetu na kutuambia kuwa atatoka tu

 

Mama Lulu Afungukia Hali Yake Baada Ya Hukumu Ya Mwanae.

Ni wiki sasa imepita tangu Lulu Micheal ahukumiwe kwa kesi yake ya kuua bila kukusudia.Mama mzazi wa msanii huyo amefunguka na kuonglea hali yake aliyonayo tangu alipokea kifungo hicho.Mama wa msanii huyo hakuwahi kuongea kitu chochote tangu mtoto wake apelekwe jela pamoja na kwamba kulikuwa na maneno ya kumtuhumu mama na baba wa Lulu kuwa hawakuwahi kumpa Lulu malezi bora yaliyompelekea kufanya vitu vya ajabu.

Ijumaa wikienda, liliamua kumtafuta mama yake mzazi na Lulu  Michael, na kumuuliza hali yake na jinsi gani aliweza kupokea hukumu ya mwanae.Hata hivyo mama huyo alisema kuwa kwa sasa hawezi kuongea kitu chochote kwa sababu hata yeye hajisikii vizuri na hali yake hata kiafya haijatengema kwa sababu kama mzazi hawezi kuwa sawa hata siku moja.

Nafikiri kwa kipindi hiki nahitaji zaidi kupumzika zaid kuliko kuwa naongeaongea, sipendi kuzungumza hovyohovyo na  kwakweli siko vizuri kabisa tangu mwanangu afungwe.

Najua watu wamekuwa wakinishangaa kwanini nimekuwa kimya kwa muda mrefu lakini ukweli ni kwamba hata hali yangu haiko vizuri kabisa,na sidhani kama kuna mtu au mzazi yoyote ambae hataweza kuwa sawa kutokana na hali ya matezo anayokutana nayo  mtoto wake anapokuwa kule tena ni matso ambayo alishawahi kuyapitia, kwakweli ninaumia sana sana.

Lakini pia waandishi wa habari hawakuishia hapo waliamua kuwatafuta baadhi ya madaktri ili kuweza kuzungumzia ni kitu gani kinaweza kumpata mtu anaekutana na mateso  na hali ngumu ya maisha  ukizingatia Lulu ni msichana mdogo ambae alishayapia hayo na anakutana nayo tena kwa sasa.

Moja ya wataalamu wa afya anasema kuwa uwezekana wa Lulu kuugua ni mkubwa kwa sababu ya kuwa na msongo wa mawazo  ambao pia usababisha kwa kiasi kikubwa  mpangilio mbovu wa homoni  a hata kusababisha mtu kuchanganyikiwa kwa sababu ya kuwa na upweke muda mrefu na kuwa na mgandamizo wa hisia (depression).

Lulu alipokea na kuanza hukumu yake mara tu alipoipokea kutoka mahakamani hapo tarehe 13 Novemba mwaka huu , baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kwa msanii mwenzie Steven Kanumba ambae alikuwa ni mpenzi wake.

Dr.Cheni Awashangaa Wanaosema Hukumu Ya Lulu Haitoshi

Msanii mkonwe wa filamu za bongo ambae pia kwa muda wote amekuwa mlezi wa msanii lulu michael na amekuwa bega kwa bega  na lulu pamoja na familia yake katika kufatilia kesi ya msanii huyo Dr.Cheni amefunguka na kuwashangaa wanaosema kuwa hukuma aliyopewa   lulu ilikuwa haitoshi na  haikulingana na kile alichokifanya.

Dr.Cheni amefunguka hayo baada ya kuona watu wamekuwa wakiongea katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa hukumu ya msanii huyo haiendani na mauaji aliyoyafanya  na wengine wakifikia hadi hatua ya kupendekeza kuwa ilitakiwa apewe kifungo cha kuanzia miaka mitano, sita na kuendelea.Hata hivy o mmoja wa watuwaliotoa maoni ya hukumu ya lulu alikuwa   baba mzazi wa Kanumba ambae alisema kuwa adhabu aliyopewa msanii huyo ni kama adhabu ya kuua kuku tu.

Dr. Cheni amesema kuwa watu hao wamekuwa hawamtakii mema lulu na kusema kuwa jambo baya lolote linaweza kumpata mtu yeyote  maana hakuna anaejua kesho yake, lakini pia amewashukuru wale wote waliomia na kutuma ujumbe wa pole kwa lulu pamoja na familia yake kwa ujumla.

Katika ukurasa wake wa instagram Dr.Cheni aliandika kuwa

Linapokukuta jambo wapo watakao kuonea huruma  na wapo watakaokuwa na furaha ila  niwakumbushe  jambo hakuana anaejua kesho yake kubwa kila mapito mwambie mungu  asante.watanzania tulio wengi  wanakuombea yaliyo meme na tunakuhaidi tupo nyuma yako  kukushika mkono  kwa kila hatua  maombi yao mungu atayasikia  hata kama hukumu imepita  tupo na wewe  na mungu yuko na wewe.-aliandika Dr.Cheni

Lulu alipata hukuma yake tarehe 13 november mwaka huu baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia , maujia yalitokea April 2012 baada ya kugombana na mpenzi wake ambae pia alikuwa msanii wa bongo movie Steven Kanumba.

Pamoja na kwamba watu wengi wameonekana kuumia na hukumu hiyo lakini wapo walikuwa wakilalamika na kusema kuwa hukumu hiyo haiendani na maujia hayo.Baada ya hukumu ya lulu mengi yamesemwa kuhusu msanii huyo.

Maoni ya Dr.Cheni katika ukurasa wake wa Instagram

 

Alichofanya Hamisa Ni Zaidi Ya Ubinadamu

Ni wengi tunaonekana kuwa na furaha tena hasa pale ambapo unaoona kama  mtu uliyekuwa haulewani nae au upo nae katika ugomvi kwa muda mrefu anapata matatizo na kuumia.Pengine miaka miwili ni mingi sana kwa Lulu kuona haya ambayo wasanii wenzie wameyaandika juu yake lakini pia Mungu ndie anaepanga kila kitu inawezekana pia ikawa ni bahati na akaweza kuyaona majonzi ya watu walikuwa wakimlilia hivi karibuni.

Hamisa alikuwa ni moja ya watu ambao hawakuwa katika maelewano mazuri na Lulu  kwa muda mrefu kidogo kama miaka miwili hivi, kwanza kabisa ni kutokana na msanii Lulu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba mzazi wa mtoto wa kwanza wa kike wa Hamisa, lakini pia hivi karibuni lilipotokea sakata la Hamisa na Diamond kuhusu mtoto wake wa pili ,Lulu  alionekana kwa kiasi fulani kuwa upande wa Zari.

Lakini yote hayo hayakumfanya Hamisa jana kuonyesha hisia zake za kuumia baada ya Lulu kupata hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela.Pamoja na yote bado Hamisa alitambua mchango mkubwa aliokuwa nao Lulu kwa mtoto wake Fantancy ambae alizoea kumwita aunty kutokana na uhusiano wa karibu wa Lulu na baba wa mtoto huyo,

Ukiachana na post aliyoweka instagram, lakini pia Hamisa alifanya interview jana na televisheni ya Clouds plus, na hakusita kuelezea maumivu yake kwa kile kilichomkuta Lulu. Na kusema kuwa bado hakuwahi kumuona Lulu kama mtu mbaya kwa sababu alikuwa ni mama mzuri kwa mwanae.

Namjua Lulu, naujua upande wa mama Kanumba na upande wa Lulu pia, lakini ukirudisha  nyuma two years ago mimi na Lulu tulikuwa na mambo fulani, everybody knows sio mpaka niyaseme,na inapofika kwenye jambo ambalo ni tatizo its not good, na unajua watanzania  hata ukifanya kitu kwa nia nzuri, as much as i would love to kwa sababu mwisho wa siku  she is not a bad person kwangu especially kwa mwanangu , she has been a very good aunty, ni mtu ambae nilikuwa naweza kumuamini kwamba akiwa na mwanagu yuko safe ingawa nilikuwa najua ni mwanamke mwingine wa baba yake lakini nilikuwa najua yuko stable.-   Alifunguka Hamisa Mobeto.

Lulu alikiuwa na uhusiano wa kimapenzi na mzazi mwenzie na hmaisa mobeto na hata mara nyingine mtoto huyo alikuwa akikaa kwa lulu kama kwa mama na alikuwa akimtunza vizuri kwa mujibu wa Hamisa mwenyewe.

Hamisa akiwa na mwanae  Fantancy, mtoto aliezoea kumwita Lulu aunty

Lulu akiwa  Majizzzo ambae pia ni  mzazi mwenzie na Hamisa Mobeto.

 

Baba Kanumba Hakuridhika Na Hukumu Ya Lulu

Wakati watu wengine wakilalamika na wazazi wa msanii Lulu Michael hata kuzimia na kushindwa kutembea kutokana na hukumu aliopewa msanii Lulu Michael ya kutumikia kifungo kwa miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua marehemu Steven Kanumba bila kukusudia , baba mzazi wa marehemu Kanumba amefunguka na kusema kuwa hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama ni sawa na mtu alieua kuku tu.

Akiongea kwa njia ya simu moja kwa moja kutoka mkoani Shinyanga anapoishi mzee huyo na mwandishi wa Global publisher, baba Kanumba aliulizwa anasemaje maoni yake kuhusu hukumu aliyopewa Lulu baaada ya kukutwa na hatia ya kumuua mwanae bila kukusudia na alijibu kuwa

Kwa upande wangu kwanini  hukumu hii imekuwa  ndogo sana, na haijanifurahisha hata kidogo, hata kama mtu aliua kwa kutokukusudia  lakini mahakama imetoa kifungo cha miaka miwili kweli kama mtu kaua kuku.-Alifunguka mzazi huyo

Hata hivyo alipoulizwa kama angefurahi ni miaka mingapi ambayo alitegemea Lulu angepewa mzazi huyo alisema kuwa,

nilitegemea kuwa mahakama ingetoa hata kuanzia miaka mitano,sita,saba na kuendelea.

Hata hiVyo kuhusu yeye kutokuwa anaonekana mahakamani, baba mzazi wa Kanumba alisema kuwa alishindwa kuja ili kukwepa gharama na ndio maana alimuachia mama yake aweze kufatilia swala hilo hata hivyo anaona ingekuwa ni upotevu wa pesa maana hata hiyo hukumu yenyewe sio ya msingi sana.

Sikuja huku nilimwachia mke wangu aendelee na kesi  hiyo kutokana na kupunguza  sizizo na msing na ndo hivyo hukumu yenyewe  ni miaka miwili tu kama mtu kaua kuku.si ningepoteza muda wangu tu hapo na hukumu yenyewe haikunifurahisha  kulingana na mazingira ya kifo cha mtoto wangu .-Aliongezea Baba Kanumba

Lulu Michael alimuua Kanumba bila kukusudia miaka kama mitano iliyopita na baada ya kesi yake kushughulikiwa kwa muda mrefu ameweza kuukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kitu ambacho kiliibua pia hisia za watu wengi wanaompenda Lulu na  watu wengi kuonekana na majonzi kutokana na hukumu hiyo huku kila mmoja akiibua lake.

Baada Ya Hukumu ya Lulu Kutolewa , Mama Kanumba Amwaga Chozi

Ikiwa ni dakika chache tu baada ya hukumu kutolewa leo Novemba 13 juu ya kesi iliyokuwa ikimkabili mwanadada Lulu Michael kuhusu kuua bila kukusudia ambapo msanii huyo amehukumiwa miaka miwili jela kwa kukutwa na hatia hiyo.

Mama wa marehemu Steven Kanumba ambae ndie alikuwa mpenzi wa eElizabeth Lulu Michael ameonekana nje ya mahakanma akilia kwa sauti hukua akisema kuwa anaishujkuru sana mahakama na serikali yake wa ujumla juu ya maamuzi waliotoa kuhusu kesi hiyo,mama huyo huku akilia amesema kuwa akitoka mahakamani hapo ataelekea makaburini alipolazwa Kanumba ili kwenda kumpumzisha kwa amani sasa tangu alipokuwa amezikwa .

mimi sina la kusem kwa sasa hivi ila la kwanza namshukuru mwenyezi mungu sana,pili ninaishukuru mahakama kwa kutenda haki na pia naishukuru sana seriakli yangu na hata nikitoka hapa nitaenda makaburini naamini  sasa naenda kumzika  na akapumzike kwa amani.-aliongea Mama Kanumba huku akilia kwa sauti

Kesi ya Lulu ambayo ilisikilizwa ushahidi wote mwezi uliopita ilikuwa imebaki kusikilizwa hukumu tu ambapo leo ndio ilikuwa mwisho wa kesi hiyo , hata hivyo leo tangu kumekucha kume kuwa na tension kubwa ya watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wakimuombea mwandada huyo kheri katika hukumu yake huku wengne wakiomba hasihukumuiwe kwa chochote,

Hata baada ya kutolewa wa hukumu hiyo watu wengi wameonyeshwa kuumizwa na hukumu iyo akiwepo Wema Sepetu ambao kwake ilikuwa ni habari mbaya tena ya kushtukiza sana.lulu atatumikia kifungio hicho cha kuua bila kukusudua kwa muda wa miaka miwili gerezani.

Lulu alikutwa na kesi hiyo mwaka 2012, ambapo alimuua Kanumba aliyekuwa mpenzi wake bila kukusudia kutokana na ugomvi wa mapenzi waliokuwa nao wawili hao ambapo katika purukushani hizo Kanumba alidondoakana kuanguka chini na ndipo mauti yalipomkuta.Hata hivyo baada ya kusikilizwa kwa ushaihidi kutoka kwa watu wa pande zote mbili  mahakama imeamuru lulu kutumikia kifungo hicho baada ya kuona kuwa katika ushahidi wake mwandada huyo alishindwa kuongea vitu vyote vilivyokuwa vimetokea siku ya tukio.

Lulu Michael Mahakamani Tena Kwa Kesi Ya Mauaji Ya Kanumba

Malkia wa bongo movie Elizabeth Lulu Michael  atatakiwa kupanda mahakamani tena Oktoba 19 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza tena kesi ya mauaji inayomkabili.Lulu ambae anakabiliwa na kesi ya mauji ya bila kukusudia ya msanii mwenzie Steven Kanumba yaliyotokea mwaka 2012,April 7.

Nyota huyo wa bongo movie alifanya mauaji hayo ya bila kukusudia kwa msanii mwenzie ambae pia alikuwa nae katika mahusiano ya kimapenzi walipokuwa pamoja.Mauaji hayo yalitokea baada ya wawili hao   kutokuelewana kwao.Hata hivyo miaka mitano iliyopita ambapo Lulu aliapoanza kukabiliwa na kesi iyo alikubali kumuua Kanumba  bila kukusudia walikuwa nyumbnai kwa marehemu Sinza Vatican.

Elizabeth Lulu Michael alikamatwa na polisi  kwa kosa la kumuua Kanumba bila kukusudia mnamo April 2012,na kupelekwa katika kituo cha Osterbay.Baada ya kukamatwa na kuwekwa ndani  alikuja kupandishwa kizimbani katika mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar Es Salaam  ambapo hakutakiwa kujibu kitu chochote, na baadae kesi iyo ilikuwa kuwamishiwa mahakama kuu ili kusikilizwa tena.

Lulu alikuja akaachiwa kwa dhamana mwaka  2013, January  baada ya hati ya kesi iyo kubadishwa kutoka katika mauaji ya bila kukusudiana , hati ambayo ilimfanya apate nafasi ya kupata dhamana hiyo.

Steven Kanumba na Elizabeth Lulu Michael wote walikuwa na wasanii wa movie za bongo , Kanumba alikuwa moja ya wasanii wakubwa walisaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza kazi za movie nchini tanzania, katika kujibu tuhuma za kesi hiyo miaka minne iliyopita, Lulu Michael alikiri kuwa na mahusiano na msanii huyo na kuwa ni kweli aliua bila kukusudia.

Katika kujibu mashitaka yake, Lulu michael alieleza kuwa siku ya tukio alikwenda kwa marehemu Steven Kanumba  maeneo ya Sinza Vatican ambapo  walikuwa na ugomvi, hata hivyo hakusema bayana kitu kilichosababisha ugomvi huo.Lulu aliongezea na kusema kuwa katika purukushani na mpenzi wake huyo walivutana na alifanikiwa kutoka nje ya mlango lakini huko ndani kwa marehemu ambae alijigonga na kuanguka mambo hayakuwa shwari.Kila la kheri kwa malkia ya Bongo movie

 

LuLu Michael Akiri Kunyooshwa Na Zari

Haikuwa matarajio ya wengi kuwa Zari The Bossy akifika Tanzania ataweza kupokelewa kwa shangwe kama ilivyokuwa mwanzao.Hii yote ni kutokana na mambo mengi mengi yaliyotokea hapo katikati,  baada ya marumbano na scandal nyingi zilizokuwa zikiiumba familia ya Diamond na mama mzazi  wa watoto wake (Zari) , watu wengi katika mitandao walikuwa wakionyesha kuwa na chuki na Zari The Bossy malkia kutoka Uganda.

Lakini weekend hii Zari The Bossy alikuaja Tanzania kwa ajili ya kufanya uzinduzi wa duka lingine kubwa la Mlimani City mali ya Gsm,akiwa kama balozi Zari alitakiwa kuonekana kwenye uzinduzi wa duka ilo ivyo ilibidi yeye kuja Tanzania.Kitu cha kushangaza au cha kufurahisha ni jinsi ambavyo Mama Tee alivyopokelewa kuanzia uwanja wa taifa mpaka katika shughuli hiyo, watanzania walikuwa mstari wa mbele kumshangilia sana .

Kutoka kwa malkia wa bongo movie, Elizabeth Michael nae hakusita kuonyesha hisia zake kwa tukio ilo la watanzania kujaza umati katika viwanja vya Mlimani City katika uzinduzi huo ambao Zari pia alikuwepo, na inawezekana kabisa umati huo ulijazwa na uwepo wa Zari katika uwanjan huo.kitu ambacho ni mara chache kutokea kwa wasanii wa Bongo wenyewe.

Katika ukurasa wake instagram, Lulu Michael aliandika”Ule umati wa Mlimani City leo wa kumuona Mama Tee….Dada ametunyoosha nyumbani kwetu wenyewe.TUMPENDE Tu..HATUNA NAMNA” aliandika Lulu

Inaweza kuwa ni kama fundisho kwa wasanii wengine wakaubwa Tanzania kuwa Zari The Bossy , amekuwa ni mwanamke aliyeweza kujizolea mashabiki kibao kiasi kwamba wanatokea kumsapoti kuliko hata ambavyo  wanavyokuwa wanasapotiwa wasanii wenyeji, swali la kujiuliza ni kuwa je Zari ana nini na watanzania, Zari amewafanyia nini watu hawa mpaka kufikia hatua ya kumsapoti kiasi icho.Nadhani mashabiki wanasapoti pale ambapo wanaona mtu yuko makini na kile anachokifanya.

Zari ni mwanamke wa msanii mkubwa Tanzania , kumekuwa na mambo mengi na ugomvi hapo katikati, watanzania walidhaniwa kuwa ndo watu wa kwanza kumchukia mwanamama huyu lakini nadhani kutokana pia na jinsi Zari amekuwa aki-handle matatizo ya familia yake vizuri  na kujitahidi kuwa-keep mashabiki wake ndicho kitu kinachowafanya watu wazidi kumkubali zaidi.hivyo wasanii waache kusema huyu wa huku au kule wanapaswa kuiga kitu kutoka kwa Zari , ambae nadhani yupo makini sana na kazi, biashara na mashabiki wake wanaomfanya aendelee kufanya vizuri katika kazi zake.

Picha 10 Zitakazokuonyesha Kuwa Lulu Michael ni Mkali wa Fashion

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ anasifika kwa uzuri wake pia muonekano wake mda wote kwani huwa anapendeza anavutia. Kwenye kila event, red carpet atakayokanyaga utamuona jinsi alivyopendeza pia aina yake ya uvaaji hubadilika kwani sio tu anapendeza kwenye red carpet bali hata akitoka mchana kwenda beach au location kufanya muvi utamuona jinsi anavyovutia.

Zifuatazo ni picha 10 zitakazokuaminisha kuwa Lulu ni moja kati ya mastaa wa bongo anayeva vizuri mwenyewe hujiita ‘Fashion Icon’;

1. Lulu amependeza ndani ya gauni jekundu na heels nyekundu akimechisha na clutch ya floral.
2. Lulu akiwai amevaa gauni jeupe lenye maua ya pinki na clutch ya pink.
3. Lulu akiwa ndani ya ‘Denim on denim’ jeans amevaa na heels nyekundu na wallet nyekundu.
4. Lulu amependeza kwa kuvalia sketi fupi na shati ya mikono mirefu na heels.
5. Lulu amependeza very simple ndani ya little black dress na silver heels.
6. Lulu amependeza kwa kitenge dress na heels za pink
7. Lulu alipendeza ndani ya Gauni refu jekundu na white na huo umeremeto.
8. Lulu kavaa elegant pink dress na clutch ya silver.
9. Lulu kavaa jumpsuit nyeupe na heels nyeupe #chic
10. Lulu amependeza na short denim jeans jumpsuit na long sleeve shirt na oversize bag

“Ndoa yangu ipo karibu” Lulu Michael

Lulu Michael amefunguka na kusema ya kwamba ndoa yake na mpenzi wake Dj Majay ipo karibu.

Amefunguka kuwakosoa mahaters ambao walidhani uhusiano wake na Majay ambaye ni bosi wa EFM na TVE hautaishi na watakuja kuachana.

“Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni,” ameliambia gazeti la Mtanzania.

Lulu ameongeza kuwa anatamani kuwa mke bora kwenye ndoa yake kama alivyokuwa sasa kwenye mahusiano yake.

Mwanamuziki wa Kenya Bahati aelezea masaibu aliyopitia chini Lulu Michael

Mwanamuziki wa Kenya Bahati wakati huu ako Tanzania kwenye tour yake ya wimbo wake na Ray Vanny ambao uliachiliwa juzi na ambao unapatikana wasafi.com.

Katika pilka pilka hizo alijipata kwenye Magic FM ambapo alizungumzia mambo mbali mbali ikiwemo Lulu Michael na vile alipomhangaisha.

Kwa wote wanaojua msanii huyo, amekuwa akizunguliwa na Lulu Michael kwa muda mrefu na kwa hio alitaka akue kwenye video yake ya Maria.

Alikuja hadi Dar kumfata Lulu lakini hakufanikiwa.

Hii ni siri ambayo nadhani hata Wakenya hawakujua, AY peke yake ndiye alijua. Nilitoka Nairobi kuja hapa [Dar es Salaam] natafuta connection na Lulu kwasababu nataka awe kwenye ile video [Maria] ambayo nimemweka Jokate. Nimekaa kwa hotel Lulu amekataa kushika simu mpaka ikafika mahali nikamwambia ukija kuniona Mungu atakubariki, siku ya pili akakataa kabisa nikamwambia mshikaji AY acha tu nirudi nyumbani. Nikarudi hivyo,” Alieleza.

Bahati ameongeza kuwa sababu ya kufanya kazi na Ray Vanny katika wimbo wao mpya ‘Nikumbushe’ ilikuwa ni mipango yake ya muda mrefu ili muziki wake uweze kupata tobo hapa nchini.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.