Harmonize receives shocking message from Ex girlfriend leaving fans talking!

Jackline Wolper a popular actress from Tanzania recently left many talking after sharing an emotional post dedicated to her former lover, Harmonize.

Through her Instagram page the lady who broke up with the singer about two years ago; went on to pour out her heart in a lengthy birthday message dedicated to Harmonize.

Wolper and Harmonize

From the post we can tell that this was not just a birthday post but also a way to celebrate the singer for launching his first album. Through her Instagram page Wolper wrote;

Nachukua Nafasi yakukuwish Mema kwenye launch yako ya leo New album.
Nakumbuka ilikua Ni Dream yako na atimaye umekamilisha,Tumetoka Mbali Tumepitia Mengi Tumegombanishwa sana yote Ni sababu ya kiburi changu. But all in all ukweli aujifichi kwakua siwezi acha kufurahia unachofanya naunavyopambana..

Still hurting on the inside!

Wolper with ex boyfriend, Harmonize

Since their breakup was filled with social media drama, Wolper and Harmonize rarely talk nor see eye to eye! So far the two have not talked for about 2 years and according to Wolper’s post; seems that she regrets some of the wrong things she did when dating Harmonize. She went on to add;

Hakuna mahusiano kati ya me na wewe lakin imani yangu inanituma kwakua nakujua Na me najijua Najua kla mmojaanaumia kwa nafasi yake kutokuongea Na mwenzie .
Nathubutu kusema maumivu yapo na ayajifichi ata Nizuge vipi ukweli unaujua wewe Rajabu Na Mimi Khadija ????

Fans react

Being a celebrity from Bongo, Wolper is now used to being insulted by fans; and after he post about Harmonize the lass was convinced that fans would insult her.

However Wolper made it clear that this would not bother her since her feelings always came first!

Huku insta watanitukaana kwa haya niliyoandika kama wolper na kama harmonies ila nikirudi gizani Me kama khadija naumia mwenyewe na akuna wakunisaidia ????????

Miss Wolper went on to conclude saying;

Katika huu ujumbe sina maana yoyote mbaya ya kuaribu mahusiano yako wala yangu ila nimekua huru kuongea hili nililotaka kuongea live mbele yako ila Tuu kutokana na Sababu za usafri leo nikakwama . Go kill it Tonight
Goodluck Raaaaj  @harmonize_tz

Tofauti na Ushonaji , Wolper Pia ana Kipaji Hiki.

Mwanadada Jackiline Wolper ameweka wazi katika ukurasa wake wa instagram kuwa pamoja na kwamba amekuwa na kipaji cha kushona na ndicho anachofanyia kazi kwa sasa lakini kipaji chake kikubwa ni  upambanaji na yuko njiani kufanya jambo kuhusu swala hilo.

Jacky ambae kwa sasa amekuwa akifanya vizuri ndani na nje y nchi kupitia kazi yke ya ushonaji, amekuwa moja ya wasanii wa kugwa kutokana na kazi hiyo huku akisem kuwa ana mpango wa kuwaonyesha watu kuwa ushonaji sio kipaji kikubwa kama ilivyo kupamba.

wapendwa msiojua kipati changu kikubwa zaidi ya kile cha fashooon na uiguizaji, niwajulishe leo kuwa nina derco yangu , yaaani ninafanya derco mpaka najishangaa, wakati naangaika na maisha nilishapigaga sana kazi ya upambani na nilichokuwa naambulia ni misifa na nauli ya kurudia nyumbani…

Hakithibitisha hilo katika ukurasa wake wa instagram, wolper alisema kuwa  ipo siku ana amini kuwa atauaja kupamba ikulu wa rais.

..siku zinazokuja hii dream lazima  nije kuifanya wala sio ombi ninachomuomba Baba ni uzima tu na afy njema…nitapamba kumbi zote hata ile ya rais atakapokuwa na shughuli, nakuamuru shetani fungua njia nipite katika ndoto yangu,

Wolper Atangaza Kuokoka , Wasanii wa Injili Wampongeza.

Mwanadada mjasiriamali nchini Jackline Wolper ametangaza kuwa kwa sasa hivi yeye ameokoka na anampenda sana yesu ingawa watu wamekuwa wakimshambulia kuwa kwanini habadilishi mavazi yake kama kweli yeye ameokoka.

Hata hivyo Jack anatetea maamuzi yake ya kuingia kwenye uokovu huku akisema kuwa swala la kuokoka aliangalii wapi unaenda au nini unafanya au ni unavaa kwa sababu swala la uokovu ni vile wewe mwenyewe unakuwa na imani ngapi kwa Mungu .

Jack anatolea mfano na kusema kuwa mashabiki wao wamekuwa wakiwaandaman sana watu kama hao kama walivyokuwa wakimuandana Muna kipindi ameokoka kutokana na uwepo wa tatoo nyingi mwilini mwake huku wakisema kuwa Muna sio mlokole kabisa.

Jack anasema kuwa watu wengi hasa vihjana wamekuwa wakitamani sana kuokoka lakini wamekuwa wakingalia jisi wanavyoandamwa pale wanapoanza kuslya huku wakiwa wametangaza kuwa wameokoka na kuona kama itakuwa ngumu kwao kuokoka lakini wapo wengi ambao wanak=mionekano ya kimjinimjini na wanataka kuokoka.

Hata hivyo Jack anawashauri watu wengine kukoka huku akiomba kuwa na disco la yesu ambalo wale walitoka katika mambo ya kidunia wasikose kuwa wakifurahia uokovu.

 

Sababu ya Wolper Kutolewa Kuwa Jaji Miss Tanzania.

Mkurugenzi mkuu wa The Look ambao ndio waandaaji wakuu wa mashindano ya miss tanznaia nhini kwa mwaka huu yanayotarajiwa kufanyikaSeptemba 8 amefunguka na kujibu maswali ya wadau waliokuwa wakiuliza kwanini jackline wolpre hayupo katika majaji watakaofanya kazi hiyo siku ya miss tanzania.

Basila anasema “katika ngazi ya kanda  majaji ni kamati ya miss Tanzania  au watu ambao kamati itawapendekeza, na Jackline Hakuwa kamati ya Miss Tanzania.

Lakini pia majaji wanapewa semina, wolpr alichelewa kufika katika semina hivyo ataingiaje katika majaji wakati hajaongozwa, sio kuwa super star u basi  uje kujaji , hapana kuna miongozo maarumu ambayo alitakiwa kupata endapoa ngehudhuria kama wale majaji wengine walivyopewa , lakini yeye kafika semeina ieshaisha.

 

Jackline Wolper Alizwa na Wezi, Aonyesha Masikitiko Yake.

Mwanadada Jackline Wolper ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha watu wanaofanya kazi ya kuiba navyorudisha nyuma maendeleo na kumvunja mtu moyo katika kitu kikubwa alichotaka kuwekeza au kukifanya kwa wakati huo.

Pamoja na kwamna mwanadada huyo hajasema moja kwa moja ni kitu gani amekumbana nacho au ameibiwa nini na ni wapi kati ya nyumbani kwake ao ufisini lakini katika ukurasa wke wa instagram , ameandika caption iliyofanya ielewekek kuwa hivi karibuni Jackline alilizwa na wezi.

Jackline aliandika ‘I cant , Mungu nipe nguvu” huku akiweka picha hii katika ukurasa wake

 

Sitoi Penzi Langu kwa Mwanaume Asiye wa Nchi Yangu;- Wolper

Mwanadada msanii na mjasiriamali Jackline Wolper amefunguka na kusema kuwa wala hata siku moja hajafikiria kutoka kimapezni na watu watu wa nje ya nchi yake pamoja na kwamba amekuwa akifanya kazi nyingi zinazompelekea kutoka nje ya nchi lakini hiyo haiwezi kuwa sababu.

Wolper anasema kuwa yeye anaamini kuwa mpezni bora atampata huku huku Tanzania na wala sio nchi nyingie ngawa kipindi yupo nchini Kenya kuna watu walianza kumsema kuwa alikuwa akitembea na raia wa nchi hiyo lakini hayo sio kweli.

sifikirii kabisa kutoa pezni langu kwa mwanaume ambae sio raia wa nchi yangu kwa sasa kwa sababu huko nyuma nilishapitia huko  lakini kwa sasa wala sihitaji, kama nimeamua kupendana basi atakuwa mwanaume kutoka nchini kwangu-Alijibu wolper ambae hapo mwanza aliwahi kutoka na mwanaume Mkongo.

Wolper Kuonekana Katika Cover la Jarida Maarufu Afrika Mashariki

Mwanadada Jackline Wolper ameonekna katika cover ya jarida moja la Afrika Mashariki linaloongekea maswala ya mafanikio ya wanawake upande wa afrika.

Hii inaonyesha ukubwa na mafanikio ya jcakline wolper kiasi kwamba anaweza kuwa mhasasishaji wa wanawake wengine kupitia kazi zake anazofanya katika jamii.

Tofauti na wasanii na wanawake wengine, wolper amekuwa moja ya wanwake wenye kuigwa kutokana na kuwa jasiri na kutokuogopa kujaribu kila njia ya kupata mafanikio na kukuza jina lake kupitia sana na sasa hivi upande wa fashion ambapo ndio anakofanya vizuri zaidi.

Jacky Atoboa Siri ya Mwanaume Aliyewahi Kumpa Raha Kuliko Wote.

Mwanadada Jackline Wolper hakusita kufunguka na kusema yaliyo moyoni mwake kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi aliyowahi kuyapitia hapo awali mpka asasa.

Katika mahusiano kuna mtu mmoja ambae utaona kuwa anaweza kuwa bora kuliko wote au m hata kama utapata anaekupedna sana lakini bado inawezekana huwezi kumsahau mtu fulani amabe alikufanya kuwa na amani katika mahusiano yak, na hii uweza kutokea kwa kila mtu.

Mwanadada Jackline Wolper amesema kuwa Alikiba ndi mwanaume aliyewahi kuwa nae katika mapezni na anaedelea kumkumbuka mpaka sasa” katika mahusiano yangu yote niliyowahi kuwa nayo alikiba ndio alikuwa the best kuliko wote”

Kauli hii sio mara ya kwanza kwa abaadhi ya wanawake waliowahi kutoka kimapenzi na Alikiba, hata Gigy moey hapo nyuma aliwahi kusema kuwa Alikiba ni mwanaume aliyewahi kuwa nae katika mahusiano na amekuwa akimuona kama ndio the best of all men aliyowahi kuwa nao.

 

Kunani Kati ya Wolper na Mr .Nice.

Kuna video imekuwa ikisambaa katika mitandao ikimuonyesha msanii mkongwe nchini aliyewahi kusumbua sana katika tasnia ya sanaa kwa style yake ya  takeu iliyovuma afrika mashariki na kati pamoja na mwanadada wa bongo movies wolper Jackiline wakiwa club na wakiwa na ukaribu usioelezeka huku wakionekana ku-enjoy sana mazingira waliokuwepo.

Swali linakuja je wawili hao kuna nini kinachoendelea mpaka kufika hatu ya kuwa karibu na kutoka wote kwenda sehmu kama hizo au walikutana tu katika mazingira hayo.

Hapo nyuma Wolper alikuwa mpenzi wa Harmonize lakini pia Mr .Nice alishawahi kufanua kazi na wasafi na kuwa karibu na watu wa lebel hiyo, je ukaribu wa Mr. Nice na Jacky hautaaribu ukaribu wa mr  nic na harmonize na team nzima ya wasafi. hayo ni baadhi ya maswali ambayo wamekuwa wakijiuliza mashabiki wao , lakini mwsho wa siku ukweli wanaujua wao wenyewe.

 

 

Wolper :- Dear Sarah, Namuogopa Mume Wako Kama Ukoma

Mwanadada Jackline Wolper amemtumia barua Sarah wa Harmonize na kumwambia kuwa hata siku moja asije akafikilia kuwa yeye ataweza kurudiana na Harmonize kwa sababu anamuogopa kama ukoma, katika ukurasa wake wa snap chat Wolper ametuma ujumbe huo kwa sarah na kumwambia kuwa yeye hakae tu na amani kwa sababu hana mpango wa kurudiana na harmonize.

Wolper anamwamba Sarah kuwa hata kama mume wake hatakuja na billion 1 alizowahi kumuonga bado hawezi kurudaina nae na kwamba yeye awe na amani na maisha yake tu.

dear Sarah sikuchukii popote ulipo,simfwatilii bwana wako kwa sababu sina hata muda nae,namuogoa kama ukoma na hata iweje hata anipe billions alizochuma kwako ili nirudi siwezi kurudi hata siku moja  na wale siwezi kuwa na amani tena maana ningesharudi tangu kipindi kile natuma watu turudiane kwa siri

Haya yote  yanakuja baada ya kuwepo kwa mgongano wa mud a mrefu kuhusu kuwepo kwa tetesi kuwa wolper anampenda bado harmonize na amekuwa akimtumia sms ili warudiane ,  lakini harmonize hataki kwa sababu ameshaamua kuwa na sarah,

Sarah amekuwa akimtuhumu sana wolper kuwa anamtumia sms nyingi mwanaume wake ili arudiane nae lakini wolper siku zote amekuwa akikataa swala hilo na kusema kuwa maneno hayo ni uongo na hayana ukweli ndani yake.

Ikumbukwe kuwa Wolper na Harmonize walikuwa wapenzi siku za nyumba na kufikia hatua ya kuimbiana nyimbo lakini walikuja kugombana huku chanzo kikubwa Wolper akisem akuwa ni baada ya harmonize kumpata sarah ambae amekuwa akimpa ela nyingi  hivyo kumuona kuwa yeye sio wa maana.

kilichobaki kwa sasa ni ugomvi  baina ya wanawake hawa wawili , na hivi karibuni Harmonize alitoa list ya wanaume ambao Jackline Wolper aliwahi kutembea nao huku akitaka kumuacha mzungu wake kwa madai kuwa hawezi kulingana nae.

Wolper Bado Ateswa na Penzi la Harmonize

Mwanadada mjasiriamali na msanii wa bongo movies Wolper Jackline anaonkana bado kuandamwa na muzimu wa penzi la msanii wa bongo fleva Harmonize kutokana na ukweli kwamba amekuwa akirusha madogo katika mitandao ya kijamii kama vile anarusha madongo hewani na kwamba hawezi kurudiana na harmonize ilhali harmonize mwenyewe hana mpango na maneno yake.

katika ukurasa wake wa instagram , aliandika “taking you back is like trying to put a piece of shit back into my asshole#ebunipumzishenijamani…#nimeshakutoaukurututulia.

Maneno haya yanaonekana kumlenga harmonize kwa sababu kwa sikuza hivi karibuni mpenzi wa harmonize ndie aliekuwa akimtuhumu jack kuwa amekuwa akimtumia meseji za mapenzi harmonize na kwamba anaonekana kutaka kumrudia mwanaume huyo wakati mwenzake ameshaamua ku-move on.

 

Wolper Akacha Kumsapoti Harmonize Kikazi ili Kulinda Mahusiano yake na Sarah

Muigizaji na mjasiriamali Jackline Wolper amefunguka na kusema kuwa ili kulinda mahusiano yamsanii huyo basi ameamua kuacha kumsapoti Harmonize katika kazi zake za kimuziki kwa sababu inaoneana kama bado ana mapenzi na msanii huyo wakati yeye ni kama shabiki tu.

Wolper ambae hakuwahi kuonekana mwenye roho mbaya kila unapotoka wimbo mzuri wa Harmonize amekuwa akionekana kuimba na kucheza, amesema kuwa anapofanya hivyo inakuwa inaonekana kama vile bado ana hisia za kimapenzi na mwanamuziki huyo wakati yeye akishaacha amaecha.

Haya yote yanatokea pale wiki iliyopita ambapo Sarah mpenzi wa Harmonize alipomtuhumu  wolper kuwa amekuwa akimtumia  sms mwanaume wake na kuwa anaona kama Wolper anamsumbua na kumtaka mpezni wake ambapo Jacky alikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa inawezekana kuna watu wanatumiwa na mwanamke huyo ili kumchafua.

Akiongea na sam misago, wolper anasema “mimi sio mswahili na wala sina uswahili tulianza mapenzi kwa mimi kuwa nasapoti kazi zake,lakini sasa hivi naona nisikukwaze  na nisiharibu mahusiano yako naona bora niache sababu yule mwanamke wake  anahitaji sana kuhurumiwa.’

Wolper alisema pia kuwa pamoja na kwamba ameacha kusapoti kazi lakini pia ameona kuwa ni bora kuwablock wote wawili ili kupeusha shari na watu hawa.

Wolper:-Sitaki Kabisa Hela za Kuongwa

Mwanadada msanii wa bongo movies na mjasirimali wolper jackline amefunguka na kusema kuwa kwa maisha ya sasa hivi wanawake wasitegemee sana swala la kuongwa na wanaume kwa sababu hawata kaa kufankiwa kwa sababu maisha yamebadilika na wanaume wamekuwa wagumu sana kutoa hela zao.

Wolper  amewataka wanawake wote kuanza kufanya kazi na kujituma kama alivyoamua yeye kwa sababu hela ya kuongwa na wanaume haitawapeleka kokote.

Wolper anasema kuwa sasa hivi wanaume wameshtukia swala la wanawake kuwa wanawategemea wao hivyo hawatoi hela kama zamani givyo ni bora kuwa na kazi yao inayokuingizia kipata hata kama ni kidogo.

Mambo ya kusubiri hela ya kuongwa nilishafutaga katika akili yangu kwa sasa,ndipo nilipoamua kufanya kazi kwa nguvu zangu mwenyewe maana hela ya kuongwa siitaki kabisa.- Alifunguka Jacky.

Jacky ambae kwa sasa ameamua kuwa mjasiliamal kwa kuanza kufanya biashara ya ushonaji na kujipatia wateja wengi na hata kupata pesa anasema kuwa kamwe hana muda ya kusubiria hela ya kupewa.

 

Wolper Atoboa Siri za Wakongo

Msanii wa kike bongo Jackline Wolper ambae kwa sasa pia amejikita katika ujasirimali wa mavazi amefunguka na kusema kuwa kwa kipindi hiki cha kukaa na wanaume tofauti tofauti ameweza kujifunza na kuwaelewa sana wanaume kiasi kwamba ameshajua hawezi kukaa akiwategemea katika maisha endelevu ya kila siku kwa sababu wengi wamekuwa niwaongo lakini jinsi wanavyoishi na wewe huwezi jua kuwa ni waongo.

Jackline Wolper ambae kwa muda mfupi amekuwa na kesi za mara kwa mara za kutoka na wanaume tofauti tofauti na kuachana nao anaoenaka amepata funzo kuoitia kwao kwa sababu amekuwa akishindwana nao kwa sababu ya uongo wa wanaume hao.Jackline ansema kuwa tangu ajifunza hayo ameona ni bora ajikite katika kazi na bishara zake zaidi za ubunifu.

Kuna wanaume jamani wanajua kusifu tena hasa ukimpa mwanaume wa kikongo,unajina na kuhisi kuwa dunia hii yote ni yako lakini kumbe  hakuna lolote la maana ngoma subiri sasa yeye akuchoke  unajishtukia amekumaliza kwa kila kitu na bado anakukimbia.-Alisema Jacky

Kwa maneno hayo Jack anayoogea anakuwa na uzoefu nayo kutokana na kwamba alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume wa kikongo ambae alifikai hatua mpaka ya kumavalisha pete ya uchumba lakini mwanaume huyo alikuja kujulikana kuwa huko alipokuwa alikuwa na familia

Jacky anasema kuwa pamoja na kwamba anendelea na kazi ya usanii lakini anajikita zaidi katika kazi za ubunifu wa mavazi , na hii yote amekuwa akiifanya kwa sababu ana ndoto za kuwa na lebo kubwa ya mavazi itakayomfanya ajulikane mbali zaidi kwa kazi zake na kuziuza hata nje ya bongo.

Jacky anasema kuwa amekuwa akiwapenda sana wadada wenye mahusiano na wanaume wa kikongo kwa sababu wanajua kusigia ingawa ni wagumu kutoa ela ila yeye ananufaika kwa sababu anavyosifiwa na mwaaume huyo anakuwa tayari kununua kitu kutoka kwake.

Hata hivyo kwa sasa hivi Jacky hajatangaza kuwa na mahusiano ya kimapezni na mwanaume yoyote tangu alipoachana na Brown.

Husna Sajent Na Wolper Mambo Safi.

Wanadada wawili waliokuwa mahasimu wakubwa kutokana na kutembea na bwana mmoja kwa sasa wameamua kuweka mambo yao sawa na kuwa marafiki kama zamani kwa sababu yule aliyekuwa akiwafanya wagombane hayupo tena.

Kitendo hichi kimejidhihirisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwanadada Jackline Wolper ambapo alimuhalika mwanadada huyo na alihudhuria .Husna Sajenti na Jackline Wolper walikuwa kuwa maadui wakubwa baada ya Husna Sajent kutoka kiapenzi na aliyekuwa mpenzi wake na Jackline ambapo wawili hao waligombana kwa ajili ya mwanaume huyo.

Msanii  jackline wolper

mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la  Mwami Radjabu  inaesemekana ni mkongo alifikia hatua ya kumvalisha pete husna sajent lakini hawakubahatika kufunga ndoa na mwanadada huyo.

Hata hivyo moja ya watu wa karibu wa Husna Sajenti alisema kuwa wawili hao waliamua kuacha kugombana kwa sabau husna tayari alishaachana na mwanaume huyo na wameona kuwa hakuna haja ya wao kugombana ukizingatia wao wote ni wanawake.

Tulishamaliza tofauti zetu,sian tofauti  wala bifu na  Jackline, maana aliyekuwa anatugombanisha ni mwanaume na hayupo tena na sisi ni wanawake  na tujifunze kuwa wanaume ni watu wa kupita. Aliongea Husna Sajent

Hii itakuwa funzo pia kwa wasanii wngine hasa wa kike ambao wamekuwa wakiingia katika mabifu hovyo hovyo kwa sababu ya wanaume bila kujali maslahi ya urafiki wao kwanza.wasani wengi wa kike wamekuwa wakiingia katika migogoro kwa sababu ya kuibiana wanaume.

Wolper Athibitisha Kuwa Single,Ni Baada Ya Brown Kukacha Kwenye Party Yake.

Msanii wa filamu nchini ambae pia ni mjasiriamali jackline wolper  amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yupo single na hata mahusiano.jackline ambae kipindi cha nyuma alikuwa akionekana na mpenzi  wake aliyejulikana kwa jina la Brown walikuwa wakionekana kuwa katika mapenzi mazito huku Jacky akisema kuwa hawataachana hata kitokee nini.

akiongea na kipindi cha Shilawadu cha Clouds Tv, na Soudy Brown, Jackline Wolper ambae aliulizwa kwanini mpenzi wake huyo hayupo na hajatokea katika party yake, Jacky alisema kuwa hajui kwanini kakak huyo hajatokea kwenye party yake,alipoendelea kuulizwa kuhusu mahusiano yake na Brown,  Jacky alisema kuwa hayuko tayari kuongelea mahusiano hayo kwa sababu ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa kwaio hasingependa kuongelea kitu ambacho kingemfanya apoteze amani yake.

Hata hivyo  baada ya mahojiano ya muda mrefu na kuanza kumchimba kwa undani, Jackline Wolper aliamua kusema kuwa kwa sasa yupo single hana mtu katika mahusiano yoyote.

Hata hivyo kabla ya party hiyo kulikuwa na tetesi kuwa wawili hao walikuwa katika mgogoro wa kimapenzi ambapo walikuwa wakikanusha habari hizo katika vyombo mbalimbali vya habari ambapo pia Jacky alitangaza kuwa siku yake ya kuzaliwa kutakuwa na party kubwa itakayounganishwa na kuvalishwa pete kwa ke na mpenzi wake huyo.

Kutokuwepo kwa Brown katika party hiyo kulifanya watu wengi kuhoji maswali juu ya mahusiano ya wawili hao.Hata  hivyo tetesi zinasema kuwa inawezekana kutokuwepo kwa Brown ni baada ya Jacky kumkaribisha ex wake katika party hiyo ambae aliachana nae miezi kadhaa iliyopita.

 

Matukio Ya Birthday Party ya Jackline Wolper

Juzi ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya mrembo na mjasiriamali na pia malkia wa bongo movies anaetamba sana katika mitandao kwa sasa jackline wolper ambapo jana aliamua kufanya birthday party yake na kualika watu mbalimbali katika party hiyo na ilifanikiwa kusherekewa na wasanii na watu wake wa karibu wengi kama inavyoonekana katika matukio.

Muonekano wa Jacky kwa usiku wa jana

Amber Lulu katika red carpet

Baadhi ya wasanii akiwemo Diamond Platinumz katika kumsapoti Jacky

Steve Nyerere akiwa na Aunty Ezekiel

 

Kulia ni Diamond na aliyekuwa mke wa Barnaba(Mama Steve) , kushoto ni Barnaba na Jacky

Wasanii wenzake na Jacky wakiwa katika party hiyo

Picha Za Brown Wa Wolper Akiwa Na Mwanamke Mwingine Zavuja

Imekuwa kama mtindo sasa kwa baadhi ya wasanii nchini na watu maarufu kuvujisha picha za utupa au wakiwa faragha na wapenzi wao.Picha zimevuja katika mtandao wa kijamii wa Instagam zikionyesha mwanaume ambae yupo katika mahusiano na msanii wa bongo movies na mjasiriamali maarufu Wolper  Jackline anaejulikana kama Brown zikimuonyesha akiwa na mpenzi mwingine tofauti na Jackline.

Picha hizo zimeleta gumzo kwa sababu wawili hao wanaonekana wapo faragha ilhali mashabki wa Wolper na mwanamitino huyo wanajua kuwa brown ana mahusiano na jackline na sio mtu mwingine yoyote.

Hata hivy wawili hao kuna kipindi cha nyuma ilisemekana kuwa walikuwa wamegombana kutokana na wawili hao kutokupostiana katika mitandao ya kijamii lakini walikuja wakakanusha na kusema kuwa hawajaachana, sasa swali linakuja kuwa je picha hizi zinaweza kuwa ni uthibitisho kuwa sasa hawapo pamoja tena?

Wolper akiwa na mpenzi wake Brown

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wasanii wa bongo kuwa wanaachia picha chafu katika mitandao ya kijamii bila kujali ni nani anaangalia picha hizo.Hata hivyo hakuna aliyefunguka  kitu chochote tangu picha hizo kuvuja katika mitandao ingawa mashabiki wao wanaonekana kukerwa na tabia hizo.

 

 

Wolper:Sio Kila Msanii Atapenda Ukifanya Biashara

Wasanii wengi bongo wamekuwa wakijiingiza katika biashara hasa ya mavazi na urembo kwa ujumla, Jackline Wolper nae ni mmoja wapo ambapo amekuwa akiuza nguo na urembo kwa watu mbalimbali lakini kitu anacholalamika Wolper ni kwamba wasanii wamekuwa sio watu wanaokuja sana katika duka lake kwa ajili ya kupata huduma anazotoa wakati alikuwa akitemegea kuwa wasanii ni moja ya watu wake wa karibu ambao walitakiwa kuwa  wateja wake wakubwa katika biashara hiyo.

Jackiline anasema kuwa wasanii ni watu wenye wivu sana ni bora wakanunue kitu kwa gharama kubwa zaidi kuliko kwenda kwa wasanii wenzao wakati wakijua kabisa kuwa wanakuwa wanawafaidisha wasanii hao, na anachokisema Jacky ni kuwa wengi wao wanakuwa wanawakomoa.

Wolper aliendelea kwa kusema kuwa tangu ameanza kuwa na biashara hiyo ni wasanii watatu au wanne tu ndo wamekuwa wakienda kwake kwa ajili ya kuhudmiwa , ilhali biashara kama yake haifanywi na wasanii wengi .

Unapofanya jambo lolote la maendeleo kwa sisi mastaa sio kwamba kila mtu atakuwa anapenda au anafurahi unavyofanikia.Wengi wananuna na kwaio ndio maana hawaji kukusapoti. Alifunguka Jacky

 

Brown Aongelea Mahusiano Yake Na Wolper

Kulitokea tetesi nyingi hivi karibuni kuhusu mahusiano ya msanii wa bongo movies Jackline Wolper na mpenzi wake Brown ambae alifuta picha za Jacky zote baada ya kusemekana kuwa alichukizwa na kitendo cha Jacky kwenda katika birthday party ya Diamond Platinumz na kukutana na mpenz wake wa zamani Harmonize.

Akiongea na Friday Nite Live ya EATV, Brown ambae ni video model  anafunguka na kuongelea mahusiano yake na msanii huyo wa kike wa bongo movies na kusema kuwa Jacky ni mwanamke pekee ambae alishawahi kumpenda na bado ataendelea kumpenda daima na wala hana mpango wa kumuacha.Brown akisema kuwa Jacky ni mwanamke ambae amepitia mambo mengi tangu ameingia katika sanaa na tangu ameanza kuwa maarufu hivyo, maswala madogo madogo ambayo mpaka sasa yanaendelea katika mitandao na maneno anayozushiwa ni ya kawaida kwa sababu alishawahi kukutana na makubwa zaidi ya hayo.

Hata hivyo Brown alisema kuwa meseji zilizovuja hivi karibuni zikimuonyesha Jacky anachat na mpenzi mpya wa Harmonize sio za ukweli hata kidogo kwasababu hata yeye alipoangalia meseji zile alijua kuwa ile haikuwa charting ya mpenzi wake. ‘Zile meseji si zake, sio Jacky kabisa mimi najua mwandiko wa mwanamke wangu,yaani hata kama mtu akichukua simu ya Jacky akachart na mimi ninakuwa najua kabisa huyu sio Jacky’

Brown alifunguka na kusema kuwa kati ya wanawake kumi alikuwa nao tangu aanze mahusiano ,Jacky bado anampa namba moja na kutaja baadhi ya mambo ambayo yanamfanya amuweke Jacky katika nafasi iyo aliyataja pia kuwa ni “Nampenda sana Jacky nae ananipenda sana, kwanza ana heshima ni tofauti  na wanawake wengine ukimwambia kitu atakujibu weweeeee..,pili Jacky ni mcha mungu sana , familia yake ni ya dini na familia yangu ni ya dini pia.

Akiendelea kuongea, Brown alikana tetesi za watu kusema kuwa pamoja na kuwa Jacky yupo na yeye lakini yupo mwanaume mwingine mwenye fedha anaemuhudumia Jacky kifedha na kusema kuwa wao wamependana hivyo wanachojari ni mapenzi na wala sio kingine”kama alikuwa anafanya hivyo ni  kwa wanaume waliopita lakini sio kwangu maana ye mwenyewe anajua nini ninampa

Jackline Wolper Ampa Shavu Harmonize

Kwa jinsi ambavyo Wolper na Harmonize walivyokuwa wakitupiaa maneno katika mitandao ya kijamii inakuwa ni vigumu kuamini kuwa leo hii Wolper anaweza kumsapoti Harmonize kwa kitu chochote, lakini hali imekuwa tofauti kwa mwanadada huo ambae ni msanii mkubwa wa tasnia ya filamu nchini lakini pia kwa sasa amekuwa akijihusisha na ujasiriamali wa nguo  jijini bongo.

Katika ukurasa wake wa instagram jana oktoba 17, Wolper ameshangaza mashabaiki wake wengi na kuwaacha na butwaa  baada ya kuposti video zaidi ya tatu ambazo zinamuonyesha akiimba na kucheza wimbo mpya wa mpenzi wake huyo wa zamani Harmonize wimbo ambao unaitwa Shulala, aliomshirikisha Koredo Bello msanii kutoka Nigeria huku chini akiandika caption ya kumsifia msanii huyo kuwa kibao icho ni kizuri,

haka kanyimbo kazuri sana  na video ndo usiseme!!Raaaj bhana umejua kunyoosha, kama bado ujaangalia video ya haka kawimbo pita  kwenye bio ya @harmonize _tz. #uliyemchokozakaja #shulala #naukinibipuTuNakupigia.” aliandika Jackline Wolper

Kitu cha kuhoji na kinachowashangaza wengi ni kwamba juzi tu zilivuja meseji zikionyesha Wolper akimwambia Sarah ambae ndie mpenzi mpya wa msanii huyo kuwa kama amemshindwa Harmonize  basi amuache yeye amrudie kwaio mashabiki wengi wameanza kutoa majawabu kuwa inawezekana Wolper kaamua kufanya kweli na kumrudia Harmonize.

Jackline Wolper na Harmonize ni moja ya couple iliyo-trend sana mjini kipindi cha nyuma na kuwaaacha watu wengi midomo wazi wa sababu Harmonize alikuwa na umri mdogo kuliko Jacky, lakini kutokana na mapezi waliosema kuwa nayo hawakuona tofauti yeyote,baadae Jackline na  Harmonize walikuja kutengana na kusababisha wawili hao kutupiana maneno ya matusi mitandaoni.,huku sababu ya kuachana kwa wawili hao ikitajwa kuwa ni baada ya Harmonize kupata mwanamke mwingine wa kizungu ambae alikuwa akimpa ela nyingi Harmonize.

Ugomvi wa Harmonize na Wolper ulisababisha mpaka Harmonize kuingia studio na kumtungi Jacky wimbo ambao uliongea mambo mengi yaliyohusu mahusiano yao yaliyopita, ukiachia hapo Sarah ambae ni mwanamke wa Harmonize pia alikuwa akigombana sana na Jacky kwa sababu ya Harmonize.Hata hivyo Jacky ndo kashaamua kumpa shavu Harmonize , hatujui kama ni kiki au anataka tu kumuumiza roho mwanamke mwenzie.

 

Penzi La Jacky Na Brown Matatani Tena

Msanii wa Bongo Movie Jackline Wolper na mpenzi wake Brown wamejikuta wakiaanza kuongelewa tena katika mitandao kuhusu mahusiano yao ambayo yana dalili za kuonekana kuvunjika, wawili hao ambao walikuwa wakiandamwa kwa muda mrefu katika mitandao huku baadhi ya mashabiki wakimtukana Jacky kuhusu umri mdogo wa mwanaume aliyenae.Hata hivyo kwa muda sasa Jacky amekuwa akimkingia kifua mpenzi wake huyo na kujibu tuhuma zote zinazomuhusu ikiwa hata kutukana mashabiki zake ilimradi tu kumuweka mpenzi wake huyo katika hali ya usalama.

Wikiendi iliyopita kulikuwa na shamrashamra nyingi kutokana na mfululizo wa sherehe za msanii mkubwa Diamond Platinumz kutimiza kadhaa, sherehe ambazo zilihudhuliwa na baadhi ya watu maarufu nchini.Hata hivyo katika kilele cha sherehe hizo zilizzofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Jackline Wolper alikuwa ni mmoja wa wasanii walioalikwa katika party hiyo ,lakini swali  ni kwanini Jacky hakutokea katika shughuli iyo na mpenzi wake huyo mpya.

Hata hivyo kuna picha zilizosambaaa mitandaoni , zinazomuonyesha msanii huyo wa kike wakisalimiana kwa kupeana mikono na mpenzi wake  wa zamani Harmonizee, inasemekana kuwa baada ya picha hizo kusambaa mpenzi mpya wa Jacky(Brown) alifuta picha zote za Jacky katika kurasa zake  za instagram.Swali linakuja je, kuna nini kinaendelea kati ya wawili hao, je ni kweli wameachana kutokana na wivu wa picha ya Jacky na Harmonize?Au ugomvi wao ulikuwa kabla ya hapo?

Akijibu tuhuma hizo, kupitia U Head ya XXL  ya Clouds Tv, Jackiline Wolper alipoulizwa kuhusu kufutwa kwa picha zake katika instagram ya mpenzi wake alijibu kuwa yeye hajui chochote taarifa hizo ndo anazipata muda huo,'”Kumbe kafuta, mimi sijaingia instagram,mi sijaona soudy huwezi ukaamini, izo taarifa ndio unanipa wewe” aliongea Jacky katika simu

Hata hivyo Jacky alipoulizwa sababu za mpenzi wake huyo kutokuudhulia katika party hiyo alisema kuwa , mpenzi wake huyo sio mtu wa kuudhuria katika party , huwa hapendi sana na mpenzi wake huyo ni siku ya tano sasa anaumwa kichwa pamoja na malaria , na hata hivyo yeye kutokea katika ile party ni kwa sababu ya heshima ya Diamond na sio vinginevyo.

kuhusu kufuta picha Jacky alisema kama amefuta ni kwa sababu maneno ya watu wamemfanya mpenzi wake huyo kupanick tu, lakini hawana ugomvi wowote.Lakini hata hivyo mpaka sasa Jackline Wolper amefuta picha zote za bff wake huyo na bff nae amemuacha kumfuata Jacky katika ukurasa wa instagram (unfollow)

Wolper na Harmonize ndani ya Bifu Zito

Mwigizaji wa Bongo movies Jackline Wolper na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki kutoka WCB, Harmonize wamejikuta katika bifu zito baada ya kuingia katika vita ya kurushiana maneno mtandaoni.  Wolper na Harmonize waliachana miezi michache iliyopta kwa kile alichokidai Wolper kuwa Harmonize alimsaliti na kutembea na msichana mwingine anayejulikana kwa jina la Sarah, katika mahojiano aliyoyafanya Wolper hivi karibuni alielezea machungu aliyoyapata baada ya kugundua kuwa Harmonize anatembea na msichana huyo mwingine kwa ajili ya tamaa ya pesa.

Baada ya kukaa kimya bila kutoa maelezo yoyote siku ya leo Harmonize ameachia wimbo wake mpya unaojulikana kama “Nimechoka” wimbo aliomuimbia mpenzi wake wa zamani Wolper wimbo ambao alituma kwenye ukurasa wake wa instagram na ujumbe usomao:

“Naomba nikupe jukumu la kumtumia #EX wako ambae kila kukicha anakuzumgumzia tena kwa ubaya na kutengenezea mazingira ya chuki katika jamii na umwambie nimechoka”, “Tena mwambie asijekuwa anajidanganya eti unamuwaza…!!! Ni kwasababu umeumbwa na stara hunaga uropo ropo wa kuongea vya ndani pia unaweza kung’oa mkali zaidi yake”.

Wolper naye kwa kupitia ukurasa wake pia alimjia juu Harmonize na kumrushia maneno:

“…Tusilazimishane kuongea nimeshaachana na wewe kiusalama ongelea vilivyopo kwako saivi sio mimi, Nilishatokaga huko kirahisi unaweza ukadeal na style yako ya mziki bila kunihusisha maana unampa hofu pia BFF anahisi labda kuna kitu kumbe hakuna, usiniharibie mahusiano yangu mapya , BFF wangu ni bora kuliko wewe ni adimu na sitaki kumpoteza kwa ajili ya watu kama wewe…Mimi ni Jackie Wolper ambae siwezi kuacha kuongea ukinianza namaliza kwa wale wanaosema bora kunyamaza subirini yawakute alafu mjipe huo ushauri”.

Harmonize na Wolper tangu wameachana kila mtu ameendeelea na maisha yake kwani Wolper ana mpenzi mpya anayejulikana kama Brown na Harmonize yupo na mpenzi wake mpya Sarah lakini tangu wameachana wawili  hao wamekuwa wakirushiana vijembe vya hapa na pale huku kila mtu akimtuhumu mwezie kwa kutokuwa mwaminifu kwenye mapenzi yao.

Baada Ya Kimya Kirefu, Wolper Afunguka Chanzo Cha Kuachana Na Harmonize

Ikiwa ni zaidi ya miezi mitatu kupita tangu penzi la msanii wa bongo movie na mjasiriamli jackline wolper na msanii wa bongo fleva harmonize kuvunjika, wolper aamua kufunguka kuhusu chanzo cha wao kuachana,wolper anasema kwa muda mrefu alikuwa kimya huku watu mitandaoni kila mmoja akisema lake kuhusu wawili hao.Ikumbukwe kuwa ni muda mfupi tu tangu kuachana kwao ,wawili hao kila mmoja alianza kujirusha na mpenzi mpya bila kujali mahusiano yao yaliyopita huku wolper akikiri kabisa kuwa mahusiano yake na harmonize ndio mahusiano yaliyovunjika na kumuuma sana kuliko yote, ikiwa ni mahusiano yake ya nne.

Akiongea katika mahojiano na mwanahabari millard ayo ,wolper anasema sakata lilianza siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa ambapo yeye alikuwa  Burundi kikazi  na mpenzi wake huyo wa zamani alipost picha yake katika ukurasa wake wa instagram na kumsifia sana lakini cha kushangaza baada ya siku mbili picha ile ilifutwa na alipouliza aliambiwa wanatafuta kiki ya wimbo mpya, wimbo ambao unakwenda kwa jina la  “happybirthday” ulioimbwa na harmonize kwa ajili yake”nimefuta baby nataka tutengeneze kiki ,unajua kuna wimbo mpya nimekuimbia” wolper asimulia.

Hata hivyo wolper anasema kuwa kipindi icho chote harmonize alikuwa tayari ameshaanza mahusiano na mwanamke mwingine anaejulikana kwa jina la sarah, mwanamke ambae alikuwa anamkataza harmonize kupost kabisa picha za jacky mitandaoni, mwanamke yule alpoona wolper anazidi kumpost harmonize mtandaoni alijua kuwa bado hawajaachana ivyo sarah aliamua kumtafuta wolper”mwanamke alikuwa hataki kudanganywa ,alichofanya akanitafuta,alichukua namba yangu ya ofisi instagram”  asimulia wolper. Kipindi icho mwanamke yule alikuwa ameshawatafuta na kuwatumia picha baadhi ya watu wangu wa karibu ikiwepo mdogo wangu, na hata alipomfikia wolpre mwenyewe alimwambia aachane na harmonize maana tayari yuko na mwanamke mwingine”unajua wewe ni kama unajichoresha,endelea na maisha yako,harmonize ana mwanamke na wanategemea kuzaa”  jacky aendelea kusimulia

Hata hivyo Jacky anasema kuwa pamoja na kwamba yeye kingereza  kinampiga chenga lakini cha Sarah kilikuwa kina kona sana,akimaanisha mwanamke mpya wa harmonize hakuwa na kingereza kilichoonyooka.

Wolper aeleza kinachomfanya kunona sana

Watu wengi wanadai kuwa kula kwingi ndiyo kinacho sababisha Jackline Wolper kuongeza uzito. Kuna ata wale ambao wanasema mwigizaji huyo wa filamu za Bongo havutii tena.

Nini haswa kinasababisha mwili wake Wolper kuwa mnene? Wolper mwenyewe amekiri kuwa pombe ndiyo inayomsababishia unene.

“Unajua sikuwa mnywaji na nilikuwa nikiichukia pombe sababu nikinywa ndio napata hamu zaidi ya kula chakula kingi, hivyo kwa sasa nimeanza harakati za kurudisha mwili wangu wa mwanzo uliokuwa ukinionyesha vizuri kwa mashabiki wangu na pia nipo kwenye harakati za kuachana na unywaji wa pombe,” Wolper alieleza.

 

 

 

Msanii kutoka Wasafi Harmonize azungumza mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na Wolper

Msanii Harmonize juzi alikuwa kwenye Clouds fM na alizungumzia mambo mengi kuhusu wimbo wake na sana sana kuhusu uhusiano wake na Wolper.

Harmonize aliulizwa na Mami baby kama ilikuwa kiki au nini baada ya kudaiwa kuachana na Wolper na ukaribu wao kurejea leo wakati anaachia wimbo wake mpya.

Harmonize

“kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi ila sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na Mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki nilianza naye nikiwa sina hata gari”  Harmonize alieleza.

Alihakikisha lakini hawakuwa pamoja;

“Ukiona mtu anatumia nafasi yako kuvuma ni jambo la kumshukuru Mungu, sikatai yupo kwenye miahangaiko atatoka, Mungu amjalie najua wote tunatoka kwenye familia za kimaskini ni wakati wake sasa kuonyesha alichojaliwa” Alimtakia Wolper kila la heri.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.