Jaquar Amtolea Povu Zito Harmonize

Msanii Jaquar kutoka  Kenya ameibuka na kumtolea Povu Zito msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize Baada ya kushindwa kupiga shoo nchini humo.

Wikiendi iliyopita Harmonize alitakiwa kufanya shoo mjini El Doret nchini Kenya lakini alihairisha kufanya shoo hiyo Baada promota kushindwa kumlipa pesa waliyohaidiana.

Kitendo cha Harmonize kushindwa kupiga shoo kiliwauzi mashabiki wengi ikiwemo Mbunge wa jimbo la Starehe Jaquar ambaye kwenye mahojiano na Kipindi cha Mambo mseto alifunguka:

“Ni tukio la kuhuzunisha lakini mimi NAMSHTUMU sana Harmonize….wakenya wamemsupport sana, wamesupport wasanii wa nje sana. Wengine wanatumia pesa zao kupiga simu, kurequest nyimbo zao. Mimi mwenyewe siwezi nikakosa kupanda stage sababu ya balance ambayo promoter amebakisha na ni kitu nilikuwa nafanya. Kwanza nadeal na mafans wangu.

Kama Mimi ningekuwa Harmonize Saturday ningeenda kwa stage niambie watu samahani nimechelewa lakini kwa sababu mumenifikisha mahali nimefika saa hii mimi nitaperform lakini promoter hajanilipa…vitu zingine nitadeal nazo baadaye sababu bila nyinyi nisingekuwa Harmonize pale niko. Unapata kuna fans wametoka mbali hadi Eldoret kwa sababu yake. Sometimes unafaa kuanglia mafans Kwanza”.

 

Babu Tale-Tumeshaanza Kuwasiliana na Uongozi Wa Ali Kiba

Meneja wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi mipango yao ya kumpata msanii wa Bongo fleva Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Siku ya Jana kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz aliweka wazi mipango yao  ya kumpata Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye shoo yao.

Lakini sasa Meneja wa Diamond Babu Tale anafunguka kuhusu jitihada zao za kuwasiliana na Kiba ambapo amekiri kuwa hana mawasiliano na Kiba lakini anaelewana sana na meneja wake anayeitwa Seven.

Siongeagi na Alikiba kivile, mimi naongeaga na meneja wake maana alishawahi kunisaidia sana, lakini kuhusu inshu ya Wasafi Festival Sallam ameshaanza kuwasiliana na uongozi wa Alikiba”.

Baby Tale ameweka wazi kuwa siku ya uzinduzi wa Wasafi festival pamoja na wasafi fm mbali ya kuwepo kwa mipango ya kumpata Ali Kiba lakini pjs atakuwepo msanii Konki konki konki master Dudu baya katika tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Wasafi media.

Mwarabu Fighter Afunguka na Kueleza Alivyoteseka Kufanya Kazi Kwa Diamond

Bodyguard aliyejizolea umaarufu Bongo baada ya kufanya kazi kwa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter amefunguka na kuanika magumu aliyopitia kufanya kazi kwa Diamond.

Katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa Bongo 5, Mwarabu Fighter amefunguka na kuanika mazingira magumu aliyopitia wakati anafanya kazi kwa staa huyo:

Nilikuwa nakatwa mshahara nikichelewa kwenye tukio siku unaenda kupokea mshahara unakuta hata laki na nusu hakuna halafu unakutana na kijikaratasi kikieleza na kukupa ufafanuzi kuwa siku fulani ulichelewa pia unakumbuka siku fulani?”.

Lakini pia Mwarabu Fighter ameweka wazi kuwa kuna baadhi ya siku za mapumziko alizokuwa anatakiwa apumzike nyumbani alikuwa anapigiwa simu aende kazini na kupewa dakika  kumi au kumi na tano.

Mwarabu Fighter ameweka wazi kuwa wakati anafanya kazi kwa Diamond aliishia kupata ajali ya pikipiki mara nne katika harakati za kuwahi kazini.

Babu Tale Aweka Wazi Hali Ya Hawa Baada Ya Upasuaji Wa Moyo

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale ambaye yupo nchini India kwa ajili ya kusimamia matibabu ya Msanii wa Hawa Said ameweka wazi kua anaendelea vyema baada ya upasuaji.

Hawa amefanyiwa upasuaji wa moyo chini ya madaktaru bingwa watano na sasa Babu Tale anasema Mrembo huyo amepata fahamu baada ya kufanyiwa upasuaji huo mkubwa.

Baada ya opersheni hiyo kufanyika Babu Tale ameandika:

 

Babu Tale Afungukia Matibabu Ya Hawa Nchini India na Ugonjwa Unaomsumbua

Meneja wa Msanii mkubwa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kutaja ugonjwa unaomsumbua Msama Hawa na kudai sio ini kama ilivyoaminika hapo Mwanzoni.

Wiki iliyopita Babu Tale aliondoka na Hawa kwa ajili ya kwenda kufanyiwa matibabu nchini India baada ya Diamond kujitolea msaada wa zaidi ya Milioni 450 kwa ajili ya matibabu yake.

Babu Tale ametoa taarifa kuwa  Hawa atafanyiwa upasuaji wa moyo jioni ya leo Lakini pia Wataalamu wameangalia kila kitu na hawajaona tatizo kwenye Ini kama iliyokuwa inaripotiwa awali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale ameandika:

Asante Mungu tumefika salama India na tumefanya vipimo vyote upya salama na jibu lililotoka kwa wataalamu kwa asilimia 95% awajaona tatizo linalohusiana na ini kwa mgonjwa ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini ivyo basi kutaitajika kufanyika upasuaji mkubwa ambao utakua na uangalizi mkubwa wa wataamu then wametuakikishia baada ya hapo mgonjwa atapata nafuu na inawezekana izo 5% zilizobaki itakua poa na tatizo la ini alitokuwepo kikubwa tunaomba mtuombee dua na msiache kumuombea pia @diamondplatnumz apatenguvu ya kuendela kumsaidia kwa maana kutoa ni moyo. Kikubwa sana naomba tumuombee Hawa coz anaingia kwenye upasuaji mkubwa na hii ni atua ya yeye kua salama. Mungu tusimamie”.

 

Mavoko- Sina Tatizo na WCB, Niko Tayari Kupiga Nao Kazi

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Richard Martini maarufu kama Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo kabisa na uongozi wake wa zamani WCB.

Miezi michache iliyopita Rich Mavoko alitangaza Rasmi kujiengua Kwenye Label ya WCB alipokuwepo kwa miaka kadhaa kutokana na matatizo ya Kimkataba.

Leo hii Rich Mavoko yupo chini ya uongozi mpya ambao hajauweka wazi Lakini pia ameachia nyimbo zake kadhaa kama Ndegele, Hongera, Naogopa na Navumilia.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kuondoka WCB lakini hana tatizo nao:

Unajua watu wengi wanashindwa kuelewa, sikuondoka WCB kwa ugomvi kule hata kidogo ni mambo tu ya kawaida ya kimuziki lakini sina tatizo na yeyote yule”.

Lakini pia Mavoko ameweka wazi kuwa kama itatokea WCB watakuwa tayari kufanya naye kazi hivi sasa basi yeye hana tatizo:

Sina tatizo kabisa, tutakaa chini na kuzungumza si ni biashara tu?”.

 

Aikah Afunguka Kuhamia WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Kutoka katika kundi la Navy Kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuongolea taarifa za kuhamia WCB.

Baada ya kutoa hit single ambayo inaendelea kufanya vyema mpaka sasa ‘Katika’ waliomshirikisha Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuliibuka tetesi kuwa Nahreel na Aika wamehamia chini ya WCB.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers , Aika  amesema kuwa, amekuwa akisikia kwa watu wengi juu ya kuhamia WCB mara baada ya kuachia wimbo wao  na Diamond jambo ambalo halina ukweli.

Yaani watu wengi wanasema nimehamia WCB lakini ukweli ni kwamba tuna meneja anayetokea huko anaitwa Sallam na amekuwa akitusimamia sasa sijui hayo mengine yanatokea wapi.

Nilikaa na mwenzangu tukatunga Wimbo wa Katika tukaona ni vizuri tukamshirikisha Diamond ndiyo ikawa hivyo sasa nashangaa hao wanaoungaunga maneno”.

Tetesi hizo za Kuhamia WCB zilipamba moto mara baada ya Msanii kutoka WCB Harmonize kusema wazi kuwa wasanii hao wanahamia Kwenye Label yao taarifa ambazo Navykenzo walidai ulikuwa ni utani.

Diamond Amkabidhi Mpiga Picha Wake Gari Jipyaa

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemfanyia bonge la surprise mpiga picha wake anayejulikana kama Lukamba baada ya kumkabudhi gari jipya.

Diamond amempa gari aina ya Toyota Alteza Lukamba siku ya Ijumaa iliyopita alipoenda kutoa msaada Tandale, ambapo Diamond alifunguka:

Lukamba anakaa Bunju, kuna kipindi alikabwa na kuchukuliwa hadi laptop sasa leo nampatia gari,”

Baada ya kukabidhiwa gari hilo, Lukamba alimuandikia Diamond ujumbe huu Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Hadi Sasa Nimekosa Maneno Ya Kuandika Yatakayoweza Kubeba Hisia Zangu Za Furaha Niliyonayo,Nimekuwa Nikiandika Na Kufuta Kila Neno Ninaloandika Naona Halijitoshelezi Nahisi Halina Uzito Kuelezea Kilichopo Moyoni Mwangu….. Bro @diamondplatnumz umekuwa msaada sana kwa Sisi vijana maskini wenzako, Mungu azidi kukupa moyo wa kidogo unachopata kugawana na wenzako, pia nishkuru uongozi wa @wcb_wasafikwa kudhamini kidogo changu hii imenipa moyo sana wa kuzidi kujituma zaidi na zaidi
God bless you simbaaa ????????????@diamondplatnumz”.

 

Rich Mavoko Afungukia Bifu Lake na WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake na Label yake ya zamani ya WCB.

Rich Mavoko ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba ameondoka katika Label hiyo lakini hana tatizo lolote na CEO wa Label hiyo Diamond Platnumz.

Kwenye Interview aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Rich amesema kuwa kilichotokea mpaka akaondoka Kwenye Label hiyo sio ugomvi bali muda wa kufanya Biashara ulifikia kikomo hivyo sasa wapo vizuri.

Lakini pia Rich Mavoko amemtaka meneja wa WCB Sallam SK kuwa na busara na heshima ni baada ya Meneja huyo kusema Mavoko hajarudisha hata robo ya pesa waliyowekeza kwake na kumtengeneza kama Brand:

Unajua Kwenye masuala ya kumzungumzia Rich Mavoko unazungumzia Brand ambayo ilikuwepo kwaiyo uliichukua kwa nia ya kufanya nayo biashara sasa umesema hajarudisha sasa na huyo mwenye talent atakuwa amepata?”.

Mavoko aliendelea kutiririka na kumwaga povu zito:

Mimi sitaki kuongelea sana hivi vitu kwa undani kila mtu anatakiwa kuheshimu kitu cha mwenzake ndio tuanze kuongeleana na kuongeleana vitu vibaya ni kutafuta mtu kujitetea”.

Diamond Athibitisha Nafasi ya Mavoko Kupata Mrithi.

Ikiwa ni baada ya kupelekana BASATA, ndipo mkataba wa msanii Rich mavoko ulipofutwa katika lebel ya wasafi, msanii wa lebel hiyo ambae pia ni bosi katika kundi hilo Diamond Platinumz amethibitisha kuwa  kuna mpnago wa kusajiri msanii mwingine katika lebo hiyo ili kuziba pengo aliloliacha Rich mavoko.

Rich mavoko ambae alikuwa msanii katika kundi hilo ameondoka katika kundi  hilo huku akitoa tuhuma nzito kuhusu lebo hiyo kuwa wamekuwa wakinyonya wasanii na kwamba hakuna haki katika lebo hiyo na hata mikataba yao imkuwa ya unyonyaji.

Mbali na maneno ya Rich wasanii wnegine kutoka katika lebo hiyo walikataa skendo hiyo na hata ukiangalia wasanii wengi nje ya wasafi wamekuwa waktamani kuingia katikalebo hiyo kutokana na masiha wanayoishi wasanii hao katika umoja huo.

Wasanii Wanaofanya Vizuri Tanzania Wanatoka WCB- Babu Tale

Meneja wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa wasanii wote wanaofanya vizuri Kwenye gemu kwa sasa wanatoka WCB.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Babu Tale amedai hata watu wanune au waumie lakini ni ukweli usiopingika kuwa WCB ndio Label yenye wasanii wakali kwa sasa:

Wasanii wetu wote wanafanya vizuri,” alisema Babu Tale. “Wasanii wanaofanya vizuri nchini Tanzania kwa kipindi hichi wanatoka Wasafi iko wazi ukinuna ukiumia wasanii wanaofanya vizuri kwa kipindi hiki Wanatoka Wasafi”.

Babu Tale amepingana na vikali na baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakisemwa kuhusu mikataba ya WCB ambapo mapema wiki hii Mkurugenzi wa vipindi EFM, Sebo aliishauri kampuni hiyo kupitia upya mikataba ya wasanii wao kwani kitu ambacho kimetoka kwa msanii Rich Mavoko kwenda kulalamika BASATA hakikuleta picha nzuri kwa taasisi kubwa kama WCB.

Babu Tale amesisitiza kuwa Mikataba ya WCB ipo vizuri na wasanii wake wanaridhika na wanafanya kazi nzuri na ndio maaana wanatoa wasanii wakali na kazi zenye ubora:

Hatuna mpango wa kupitia mikataba wa wasanii wa WCB, mikataba ya wasanii wetu wote haina matatizo, kama unavyoona wasanii wetu wote wanafanya vizuri“.

 

Sallam SK Adokeza Ujio Wa Kolabo Ya Diamond na Rihanna

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Sallam SK amedokeza uwezekano wa Kolabo kati ya Diamond na staa wa RnB kutoka Marekani,  Rihanna.

Kwenye mahojiano na Kituo kimoja cha habari, Sallam SK alijibu maswali katika kipengele cha YES/NO au NDIO/HAPANA kwenye …swali la endapo kuna collaboration kati ya Diamond na Rihanna, Meneja alijibu YES.

Siku za nyuma kumsema wahi kuwa na tetesi kuwa Diamond ana mpango wa kufanya kolabo na Rihanna ingawa uongozi wa Diamond haujaongelea kiundani zaidi kuhusu kolabo hiyo.

Diamond tayari ameshafanya Kolabo na wasanii wakubwa Marekani kama vile Neyo katika wimbo wake wa ‘Marry me’ na Rick Ross wimbo wa ‘Waka waka’.

WCB Watoa Tamko La Rich Mavoko Kwenda Kujisajili BASATA Kwa Mara Ya Pili

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameamua kujitoa rasmi katika Label yake iliyokuwa ikimsimamia ya WCB kwa ajili ya mgogoro wa mkataba aliopewa.

Baada ya kutoka WCB, Mavoko alionekana akienda kushtaki katika Baraza la Sanaa Tanzania ambapo pia alidaiwa kwenda BASATA kwa ajili ya kujisajili upya pamoja na kwamba alishasajiliwa chini ya WCB.

WCB wameibuka na kudai taarifa za Msanii huyo kwenda kujisajili BASATA sio sawa kwani tayari ameshasajiliwa chini ya Label hiyo mapema mwaka huu.

Kwenye mahojiano na GPL, Meneja kutokea WCB, Sallam SK amesema hayo alipokuwa akieleza ushirikiano uliyipo kati ya WCB na Baraza hilo kwa sasa.

Suala la kusema hatushirikiani na BASATA hilo litakuwa si la kweli na sisi tunashirikiana nao sana kuna vitu vinatokea bahati mbaya. Lakini ukiangalia wasanii wetu wote wamesajiliwa BASATA na hamna yeyote ambaye hajawahi kujisajili. Hata juzi kati hapa ilisemekana kuwa Rich Mavoko ndio alienda BASATA akajisajili, hapana!, kashasajili kupitia WCB, actually mwezi wa saba mwaka huu”.

 

Diamond ni Mtu Mwenye Damu ya Kipekee:-Ricardo Momo

Meneja wa msani Harmonizie kutoka katika kundi la wasafi anaejulikana kama Ricadro momo amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsema na kumfikiria diamond vibaya bila kujua undani wake, kwa upande wake anasema kuwa wao wanaoishi na Diamond wanajua ukweli wa diamond ni mtu wa aina gani.

Momo anasema kuwa anaweza kumuelezea Diamond kama mtu wa kipekee sana mwenye kuogopa sana Mungu  na anaamini kuwa Diamond ataiona Pepo.

Diamond ni mtu mwenye damu ya kipekee sana, ana imani sanaa,sijui kama mwenyezi mungu ataweza kumnyima pepo kweli sijui.

Akiongelea kuhusu post yoyote anayoweka katika ukurasa wake wa instagram , Ricardo momo anasema kuwa anapoweka kitu katika ukurasa wake hamlengi mtu yoyote zaidi ya wale wanaomfollow tu.

kwa upande wangu huwa siandiki kitu kwa ajili ya kumu-atack mtu kwaio hata kama nimepost sijamwambia mavoko.linakuwa linamuhusu mtu yoyote anayenifollow mimi katika instagram.

WCB Wadai Mamilioni Waliyowekeza Kwa Mavoko Hayajarudi Hata Robo

Msemaji wa Label ya WCB ambaye pia ni mmoja wa meneja wa Diamond Platnumz, Sallam Sk amemfungukia sakata hilo na kudai pesa ambazo Label hiyo zimewekeza kwa Rich Mavoko hazijrudi.

Wiki iliyopita msanii Rich Mavoko ambaye alikuwa chini ya Label hiyo kwa muda kidogo alitinga BASATA na kwenda kuwashitaki kwa mkataba wao wa kinyonyaji.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Sallam Sk ameweka wazi kuwa mpaka hivi sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB kimkataba zaidi.

Lakini pia ameweka wazi Kuwa mpaka sasa pesa ambayo wamewekeza kwa muimbaji huyo katika project zilizotoka haijarudi hata robo.

Mpaka sasa sielewi malalamiko ya Mavoko ni yapi kwa sababu ukisema sisi tunamnyonya mtu hicho kitu hakiwezekani alafu isitoshe Pesa ambayo tumewekeza kwa Rich Mavoko haijarudi hata robo”.

 

Diamond Atinga BASATA Kwa Ajili Ya Kesi Ya Mavoko

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi amefika katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya madai ya aliyekuwa msanii wake Rich Mavoko.

Rich Mavoko alimburuza Diamond na Label nzima ya WCB mbele ya BASATA kwa madai ya mkataba wa kinyonyaji waliompa wakati amesainiwa chini ya Label ya WCB.

Diamond aliongozana na Mameneja wake wawili, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Sallam Sharraf katika ofisi hizo mapema leo ili kuitikia wito.

Kwenye mahojiano na Global Publishers mmoja wa meneja wa Diamond, Sallam, amesema waliitwa na Basata na sasa wapo katika mazungumzo ya kutatua jambo hilo na kufikia mwafaka.

Sallam amesema ni vyema watu wakasubiria yatakayoamuliwa huko, ambapo wanaamini Basata itauambia umma nini kilichoafikiwa badala ya wao  kuwa wasemaji.

 

Mbosso Awakingia Kifua WCB Adai Sio Wanyonyaji Kama Madai Ya Mavoko

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Maromboso amefunguka na kuwakingia kifua WCB dhidi ya tuhuma za unyonyaji walizotupiwa na msanii Rich Mavoko.

Wiki iliyopita RIch Mavoko aliwaburuza WCB katika Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) na kuwatuhumu kwa unyonyaji kutoka na mkataba waliompa.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari Mbosso amefunguka na kudai yeye binafsi hajaona unyonyaji wowote WCB  hasa kwa upande wa mkataba wake Tena anaamini wamempa zaidi anachostahili.

Kiukweli kwa upande wangu tangu naingia WCB mpaka leo sijafikisha pesa ambayo wao wali invest kwangu kwaiyo nikiambiwa nanyonywa binafsi nitapinga kwa sababu mimi ndio naona nawanyonya kwa sababu mpaka leo hela waliyowekeza kwangu haijarusi na kuna wasanii wapo WCB mpaka leo pia hawajarudiasha hata nusu ya pesa kwaiyo ukiniambia WCB wananyonya wasanii nakuwa sikuamini labda uje na vigezo”.

 

Rich Mavoko Afunguka Baada Ya Kuwaburuza WCB BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko amefunguka kwa mara ya kwanza na kuongelea sakata lake na uongozi wake wa zamani WCB.

Siku ya jana taarifa zilisambaa kuwa Rich Mavoko amepeleka kesi yake mbele ya Baraza la Sanaa (BASATA) baada ya Tetesi za wiki kadhaa kuwa ameamua kujitoa WCB.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rich Mavoko amesema kuwa anashukuru kukutana na BASATA na kupata elimu ya kutosha huku akiwamwagia sifa kuwa hao ndio maana halisi ya walezi wa sanaa yetu nchini Tanzania.

https://www.instagram.com/p/BmRCQzVAj05/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=133n0dixilgpb

Siku ya jana Rich Mavoko alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ambapo amepeleka mkataba wake na WCB ambapo ameomba uangaliwe upya na kudai ni wa unyonyaji.

Wasanii kadhaa na wafanyakazi wanaojitoa WCB wamekuwa wakilalamikia suala la mikataba mibovu kutoka katika kampuni hiyo na wengine kudai walikuwa hawalipwi.

Mpaka sasa uongozi wa WCB hawajajibu tuhuma hizo na madai hayo ya Rich Mavoko.

Rich Mavoko Ashinda Kesi Dhidi Ya WCB BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameripotiwa kushinda kesi dhidi ya Label yake ya zamani WCB na kufanikiwa kuvunja mkataba na kutoka.

Rich Mavoko ambaye alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kwa vibao vyake vikali  alisainiwa na kujiunga na WCB siku za nyuma kidogo na kutoa nyimbo kadhaa zilizomrudisha Kwenye chati.

Lakini mapema mwaka huu kulikuwa na tetesi nyingi Baada ya Rich MAvoko kutoonekana Kwenye shughuli mbali mbali za WCB na hata kutoonekana kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Rich Mavoko pamoja na uongozi wake WCB wamekuwa kimya juu ya Tetesi za Rich Mavoko kuondoka WCB Mpaka sasa ambapo kuna taarifa kuwa Mavoko kajitoa rasmi.

Kituo cha Televisheni cha TV E  wanaripoti kuwa siku ya leo Mavoko amefanikiwa kushinda kesi dhidi ya WCB rasmi na inasemekana amejitoa Kwenye Label hiyo Lakini pia mkataba alikuwa nao umevunjwa.

Mpaka hivi sasa Rich Mavoko hajatoa tamko lolote kuhusu  nini kinachoendelea Mpaka sasa Uongozi wa WCB haujatoa tamko juu ya tuhuma hizo.

WCB Watoa Zawadi ya Gari kwa Wasanii Hawa.

wasanii wawili kutoka wcb, mbosso na lavalva siku ya 8-8 wamekabidhiwa zawadi ya gari na uongozi wa wcb ikiwa kama ishara ya kazi nzuri wanayoifanya katika lebel hiyo.Hii sio mara ya kwanza kwa uongozi wa wcnb kuwa wakitoa magari kwa wasanii wao hasa pale inapoonekana kuwa na juhudi katika kazi zao za muziki na katika kuitangaza lebel hiyo .

Hata baada ya kupewa zawdi hizo za magari,wasanii hawa waili walioneka akuwa na furaha na hata kusikika lavalava akisema ‘ eeeh bwana  kama unavyoona , mambo yamefana.tukutane sheli ,mwabie na mwenzio , mr mbosso waambie wasikie kuwa aiefanya kazi na asile.”

Wasanii hawa waili wamepewa magari aina ya Toyota Harrier , huku moja ikiwa nyeusi na moja ikiwa ni rangi ya maziwa.

Jux na Vanessa Wamewapa Changamoto Diamond na Wasafi Festival

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux na Mpenzi wake Vanessa Mdee wamewapa changamoto kubwa Diamond na timu nzima ya WCB.

Jux na Vanessa ambao wamemaliza tour yao ya ‘In Love and Money’ ambayo imesemwa kufanya vizuri sana kuliko ilivyotegemewa wameonekana kuwapa changamoto WCB ambao nao wametangaza kuja na Tour yao ya Wasafi Festival.

Babu Tale ambaye ni Meneja wa Diamond na mratibu wa Wasafi Festival ameiambia Bongo 5, kwamba mafanikio makubwa na tamasha hilo ni changamoto kwa tamasha la Wasafi Festival ambayo litaanza kutimua vumbi miezi michache ijayo.

Hii ni ishara ya muziki unakuwa, nchi zilizoendelea kila mwisho wa wiki unajua kuna show kubwa, kwahiyo hii ni ishara nzuri ukiangalia Vanessa amejaza viwanja kibao. Mimi nikiwa kama kiongozi au mratibu wa Wasafi Festival inanipa changamoto naanza mkoa gani? sisi tunafanya show zaidi ya mikoa 12 na tunapiga na Dar es salaam inakuwa histori“.

Kutokana na mafanikio makubwa ya Tour ya Vanessa na Jux wasanii hao wametangaza kwenda nchini Rwanda, Burundi na Congo.

Diamond Ataja Siku Wasafi Fm Itaanza Kurusha Matangazo Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amefunguka na kutaja tarehe ambayo Wasafi Fm, itaanza kurusha matangazo yake rasmi.

Mwaka jana mwishoni Diamond Platnumz ambaye sio msanii tu bali Mfanyabiashara pia alitangaza kuwa anaingia Kwenye ulimwengu wa Media kwa kufungua radio station na television station ambazo ni Wasafi Tv na Radio.

Diamond Platnumz amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ni lini kituo chake cha radio cha Wasafi FM kitaanza kurusha matangazo kama ilivyo kwa kituo chake cha Runinga cha Wasafi TV.

Kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha Mayotte la 1ère cha kisiwani Mayotte ambapo yupo anafanya shoo Diamond alifunguka:

Nimefungua Tv inaitwa Wasafi TV na inafanya vizuri sana na tupo katika mikakati ya kuhakikisha inapatikana bara zima la Afrika na ulimwenguni kote. Lakini pia mwezi wa kwanza au mwishoni mwa mwaka huu tunafungua pia Wasafi FM itakuwa hewani”.

Wasafi Tv imekuwa hewani kwa kama Miezi miwili hivi na tayari imepata mafanikio makubwa sana ingawa haijaanza hata kurusha vipindi Rasmi na hata matangazo ya wadhamini lakini kwa maangalizo ya awali inaonekana Wasafi Tv inapita katika njia sahihi.

Almas Mzambele Afunguka na Kudai Babu Tale Ataiua WCB

Almas Mzambele ambaye alikuwa mfanyakazi wa WCB kwa miaka mingi kabla hajaonekana amefunguka na kudai mtu pekee ambaye ataiua WCB ni Meneja Babu Tale.

Almasi Mzambele alikuwa mtu ambaye alikuwa anashughulikia mambo ya mitandao ya kijamii WCB amefunguka kwa mara ya kwanza tangu ameondoka kwenye Label hiyo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Almas amefunguka mazito juu ya uongozi wa kampuni hiyo ambao ndio amedai una matatizo zaidi na unaweza kuua Label hiyo.

Tatizo pale lipo  kwenye uongozi wa WCB ambapo mwenye matatizo zaidi ni Babu Tale anayejiita meneja namba moja yaani anavuruga watu mpaka wanaacha kazi sio mchezo.

Babu Tale ndio mtu anayepelekea kuiua WCB kuna vitu vingi anakuwa anavifanya nyuma ya pazia ambavyo kama watu wangevifahamu sidhani kama wangetamani kumuona yeye anaendelea kuwa na Diamond kwa sababu naamini huko mbeleni sidhani kama tutaendelea kumuona Diamond huyu tunayemuona sasahivi”.

Lakini pia Almas aliendelea kutaja maovu ya Babu Tale:

Yaani kifupi tu Babu Tale ni mbinafsi na ni mmwinyi anapenda yeye ndio aonekane msemaji wa mwisho k a sababu ndio ametangulia kufahamiana na Diamond kwaiyo mkitofautiana mtazamo tu basi yeye anaanza kuleta visa vyake”.

Rayvanny Asitisha Ushindani Wa Kimavazi na Wasanii Wenzake

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka. WCB Rayvanny anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Chombo’ ameibuka na kutangaza Kumaliza ushindani wake wa kimavazi na wasanii wenzake huku akitaoa yeye ndio mshindi.

Sakata hili lilianza baada ya Dogo Janja kumtaja Rayvanny kama mmoja wa wasanii ambao haelewi anavaaga nini kwani hajui kujipangilia na kupendeza kitendo kilichomkera Rayvanny.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Rayvanny amesema kuwa anaamini ushindani upande wa mavazi anabaki kuwa yeye ni mwenye ujuzi na yuko katika viwango vya kuvaa vitu vya gharama zaidi hivyo hahitaji tena kushindana.

Akizungumzia hatua ya kutotaka tena kujihusisha na ushindani wa mavazi, Rayvanny aliongeza kuwa kwa sasa ana mambo mengi ya maana ya kufanya ikiwemo kujikuza zaidi kimuziki na kuandaa maisha mazuri ya mwanae JayDan kwa sasa na siku za Usoni.

Rayvanny ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chombo’ ambapo ametangaza ujio wa video siku yoyote kuanzia hivi sasa.

 

Babu Tale Aanika Ukweli Kuhusu Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Meneja wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Babu Tale amefungukia kwa mara ya kwanza tetesi zinazoendelea kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rich Mavoko katimuliwa.

Tetesi hizi zilianza wiki chache zilizopita baada ya Mavoko kutoonekana Kwenye tangazo jipya la Trailer ya Wasafi reality show lililowaonyesha wasanii wote wa WCB na familia ya Diamond.

Kwenye mahojiano  na Ijumaa kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa Marekani, Babu Tale alisema kwamba tetesi hizo siyo za kweli na Mavoko bado yupo WCB ila kipindi ambacho walikuwa wanachukua video ya Reality Show aliyoiposti Diamond ambayo ndiyo iliyozua maneno mwanamuziki huyo hakuwepo alikuwa kwao Mahenge, Morogoro kwenye msiba kwani alifiwa na dada yake.

Wakati tunarekodi hiyo video ya Reality Show, Mavoko alikuwa Mahenge kwao, alifiwa na dada yake kwa hiyo alikuwa kwenye msiba, lakini hizi siku zote yupo bize anashuti wimbo wake mpya na zamu inayokuja ni yake kuachia wimbo kwani sisi huwa tunaachiana muda wa kutoa nyimbo kwa hiyo sioni haja ya kuongopa kwamba hayupo WCB, kwa sababu hata asipokuwepo lazima itajulikana tu”.

Baada ya habari kuanza kusambaa Mavoko alimtafuta ili kuthibitisha taarifa hizo lakini alikataa kabisa kuongea na kutaka uongozi wake utoe majibu ya maswali hayo.

Mwarabu Fighter Athibitisha Bado Yupo WCB Hajafukuzwa Kazi

Bodyguard wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter ameibuka na kuweka wazi kuwa taarifa zilizosambaa kuwa amefukuzwa kazi sio za kweli.

Wiki chache zilizopita kuna taarifa zilisambaa kuwa Mwarabu Fighter amefukuzwa kazi na kudaiwa kuwa aliambiwa na Diamond akae nyumbani mpaka pale atakapopata taarifa.

Kwenye Interview na Global Publishers, Mwarabu amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa bado yupo WCB na anaendelea kufanya kazi na Diamond kama kawaida, kutokumuona naye ni kwa sababu ya taratibu za kiofisi ambazo hawezi kuziweka wazi ila siku yoyote tutamuona naye.

Taarifa za Mwarabu kufukuzwa ziliaminika kwa sababu aliokuwa anaonekana yuko Tanzania Wakati Diamond yupo na timu yake nchini Marekani kwa ajili ya Tour yake ya ‘A Boy from Tandale’.

 

Rayvanny Afungukia Suala la Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Rayvanny amefunguka kuhusu Tetesi za Msanii mwenzake Rich Mavoko kutimuliwa kutoka katika label hiyo.

Tetesi za Mavoko kutimuliwa WCB zilianza kusambaa mwezi uliopita baada ya kutoonekana Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na WCB ambao ulijumuisha wasanii wote wa label Lakini pia Mavoko hajaonekana Kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Rayvanny amesema hawezi kuliongelea sana suala hilo kwa sababu sio msemaji lakini amesema Rich Mavoko bado yupo na huwa wanawasiliana naye mara kwa mara:

Ujue sisi tunachekiwa kwenye group, leo kuna tukio hili na hili, so ukiona huyo kakosa ni masuala ya uongozi sana labda angekuwepo Diamond au Babu Tale angeweza kuongea sana lakini Mavoko yupo Wasafi kila siku.

Anakuja, anajiunga kwenye vitu lakini yeye kutokuja siku ile sijui sababu, kama kuna vitu vinavyoendelea ni yeye na uongozi. Mimi siwezi kuongea sana kwa sababu Mavoko ni mwanangu tunaongea tunachati, tunarekodi ngoma zetu“.

Lakini Hata hiyo Babu Tale alieleza kuwa siku hiyo Rich Mavoko alikuwa aki-shoot video ya wimbo wake mpya na kushindwa kuhudhuria.

Mwarabu Fighter Afunguka Baada Ya Kupata Ajali

Bodyguard wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter amefunguka kwa mara ya kwanza tangu apate ajali ya gari mapema wiki iliyopita.

Mlinzi wa Diamond Aliripotiwa kupata ajali hiyo mbaya wiki iliyopita ambayo kwa kiasi kikubwa ilimpa majeraha maeneo ya uso.

Baada ya kulazwa hospitalini kwa muda wa siku kadhaa Mwarabu Fighter ameonekana kupata ahueni na kusema kuwa kama si mipango ya Mungu basi angekuwa ameshafariki dunia kutokana na ajali hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mwarabu Fighter aliandika ujumbe huu:

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuiona siku ya leo maana kama sio mapenzi yake inawezekana kabisa leo hii nisinge kuwepo kutokana anajali mbaya sana nilio nusurika…?”.

Harmonize Afungukia Ushindani Uliopo WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize amefunguka na kuelezea ugumu uliopo katika kufanya kazi kama msanii wa label ya WCB kutokana na ushindani.

Harmonize amefunguka na kuweka wazi kuwa ushindani ndani ya Label hiyo kati ya wasanii ambao wapo ndani ya Label ndio ugumu ambao upo humo.

Kwenye mahojiano na Planet Fm, Harmonize amesema ugumu uliopo WCB ni kila msanii ana uwezo mkubwa, hivyo kila mmoja anahakikisha anafanya kazi nzuri.

Ugumu ni pale ambapo unafanya kazi na wasanii wote ambao ni talented, so way competion katika kurekodi ngoma kila mtu anataka kutoa ngoma yake kali kumshinda mwenzake, so ugumu unaanzia hapo“.

WCB ni Label kubwa kabisa Tanzania na inabeba wasanii wanaofanya vizuri sana, wasanii hao kama vile Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize, Rich Mavoko, Mbosso na wengineo.

 

Mbosso- Ujana Ulinipelekea Kupata Watoto Katika Umri Mdogo

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Maromboso au maarufu kama Mbosso amekiri kuwa na watoto wawili katika umri mdogo ni matokeo ya balehe.

Mbosso ambaye kwa hivi sasa anaendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya “Nadekezwa” ni Baba wa watoto wawili ambao watoto wote wana umri sawa lakini ni mama tofauti.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mbosso amekiri kuwa pamoja na kila mmoja kuwa na mama yake lakini hana uhusiano na kama zao kwa sasa kila mmoja ameshaolewa.

Sipendi kuwa muongo na sitakuwa na dhambi ya uongo, huwa inatokea katika ukuaji (balehe) hususani sisi watoto wa kiume, kuna vitu utajizuia navyo lakini hutashindwa tu.

Kwa hiyo sitaki kuwa muongo, ilitokea ikawa hivyo nimekuwa baba nina watoto wangu wawili, tunaishi vizuri“.

Mbosso alianza muziki katika umri mdogo baada ya kujiunga Kwenye kundi la muziki la Yamoto Band miaka kadhaa iliyopita.

Mbosso- Nyimbo Zangu Hazipigwi Redioni

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Maromboso au maarufu kama Mbosso ameongelea Kitendo Cha nyimbo zake kutopigwa na baadhi ya media.

Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz amekuwa kwenye mgogoro na baadhi ya vyombo vya habari hadi kupelekea nyimbo zake kufungiwa na vituo hivyo.

Wasanii wote ambao wako chini ya WCB wamekuwa wakibaniwa nyimbo zao kupigwa Kwenye Media hizo na Mbosso akiwa mmoja kati ya wasanii hao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mbosso ameweka wazi kuwa ingawa  nyimbo zake hazipigwi na baadhi ya media lakini anashukuru zinadai kila vyema kwa mashabiki zake.

Ukizungumzia moja ya wasanii ambao hawakupata bahati ya kupata nafasi kubwa kwenye radio station, mimi pia naweza kusema nipo.

Sikupata bahati kabisa nyimbo kupigwa kwenye radio station lakini wananchi wamenipokea, wamesema Mbosso tunakusapoti, wamenisapoti nashuru leo nimefika nilipofika”.

Baada ya media zaidi ya nne kugoma kupiga nyimbo za Diamond na wasanii wote wa WCB, Diamond alifikia uwaumuzi wa kufungua Stesheni yao ya Wasafi Tv.

Bodyguard wa Diamond Apata Ajali na Kupasuka Kichwani.

Body guard wa msanii mkubwa bongo mwarabu fighter amepata ajali katika maeneo ya Mbezi Afrikana alfajiri ya leo na kuumia  maeneo ya kichwa na kuwahishwa haraka  hospitali ya Lugalo ii kupatiwa huduma ya kwanza ambapo baada ya hapo mgonjwa huyo aliwahishwa na  gari la wagonjwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.

Hata hivyo Mwarabu anasema kwa sasa anaendelea vizuri na anawashukuru watu wote waliojitokeza kumsaidia katika kpind alichokuwa amepata ajali hiyo,akiongea na waandishi wa habari akiwa hospitalini hapo Mwarabu Fighter anasema

namshukuru mungu sana mpaka hapa sasa hivi maana madaktari wamenipigania sana m ilikuwa alfajiri mida ya saa kumi na moja nilipoata ajali lakininalitokea msamaria mwema akanikimbiza  lugalo na kukutana na daktari alienipigania sana na mpka kuwekwa katika ambulance na kufikishwa hapa na kama mnavyoona hapa kumekuwa na huduma nzuri sana tangu nimefika”

 

Mbosso Awalaumu Mashabiki Kwa Video Yake Chafu

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Maromboso au maarufu kama Mbosso ameelekeza lawama kwa mashabiki baada ya video yake kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Siku chache zilizopita video ilisambaa mtandaoni iliyomuonyesha Mbosso akiiwa stejini akitumbuiza kwenye shoo ya Kusi night huku akimbambia msichana mmoja katika staili za kimahaba.

Video hiyo ilisababisha mashabiki kumjia juu Mbosso huku wakiwarushia lawama WCB na kudai wamembadilisha Msanii huyo na kumfundisha tabia mbaya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Mbosso amefunguka hay kuhusu video ile:

Unajua watu wengi wanaamini mimi nimebadilika lakini hakuna kuna baadhi ya vitu vinachangia hasa kwenye shoo inakulazimu ufanye vitu fulani ili watu wafurahi kwaiyo unajikuta unafanya vitu fulani ili shoo ipendeze na watu wafurahi na mashabiki wawe na shangwe na wewe ndio inabidi uwape burudani mashabiki  zako”.

Lakini pia Mbosso amesisitiza kuwa yeye binafsi hakupenda kufanya vile ila kutokana na msukumo wa mashabiki waliokuwa wanampa ukumbini pale akajikuta akifanya vile.

WCB Wagoma Nyimbo Zao Kupigwa na Habari Zao Kuripotiwa na Baadhi Ya Media

Label au kundi linalofanya vizuri hivi sasa nchini WCB linaloongozwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz limetoa tamko rasmi la kuwataka baadhi ya media wasipige nyimbo zao.

Meneja wa label hiyo Babu Tale ametoa tamko hilo jana wakati akichonga na waandishi wa habari Kwenye uzinduzi wa Wasafi Tv Kwenye king’amuzi cha Startimes.

Babu Tale amevitaka vyombo vilivyokataa kupiga nyimbo zao Mwanzoni viendelee hivyo hivyo na hata visijaribu kuripoti taarifa zao.

Tunaendelea kuwaomba waendelee kushinikiza wafanyakazi wao wasipige nyimbo zetu.

Hatutaki kuona wanapiga nyimbo zetu wala kutoa habari zetu kwa sababu wao walitukataa mwanzo, tunawakataa kwa sababu wao walitukataa“.

Diamond amekuwa katika mgogoro mzito na Media mbali mbali ambazo zimekuwa hazipigi kabisa nyimbo zake ambazo ni Clouds Media na hata East Africa Radio na Tv.

 

Zari Sio Chanzo Cha Diamond Kukonda, Babu Tale Ataja Sababu Hizi

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye pia ni CEO wa WCB amekuwa kwenye headlines sana na moja kati ya vitu vinavyo trend ni mwili wake kuisha.

Baada ya Diamond kuonekana anapungua mwili kwa kasi habari zilisambaa Mtandaoni kuwa kisa ni Zari ambapo ilidaiwa baada ya kumwagwa na Zari Diamond alipata mawazo sana na hata kudaiwa eti sahivi hapati matunzo aliyokuwa anapata wakati yupo na Zari.

Lakini Meneja wa Diamond, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa sababu za Diamond kupungua mwili kwa muda mfupi kuwa ni kukosa muda wa kulala kutokana na jukumu zito la ujio wa Wasafi TV.

Kuna baadhi ya watu wanasema msanii wangu anapungua mimi na nenepa navimba, Kama hamjui Media sio kitu kidogo, wakati tunaanza tulijua ni kazi ndogo, kwa miezi sita non stop msanii wangu analala masaa mawili tu, kwa sababu ya kuandaa hiki mnachokiona machoni mwenu.. Wiki mbili za mwanzo tukawa tunakasirika kwa nini anafanya kazi ngumu, ilipofika mwezi tukawa tunaona  ana-loose weight (kupungua uzito) na bado kazi zinaendelea tukawa tunashangaa ana nia gani huyu”.

Lakini pia mwana Familia wa Diamond mwenyewe,ambaye ni dada yake Esma aliwahi kunukuliwa akisema kaka yake kapungua kwa kumiss penzi la Zari.

Uzinduzi wa Wasafi Tv Kwenye Startimes (+picha)

Msanii wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ametangaza rasmi kuingia ubia na king’amuzi cha Startimes ambacho kitarusha matangazo ya Wasafi Tv.

Siku ya jana Diamond Kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kuwa atakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Slipway siku ya leo saa tano asubuhi.

Diamond amezindua rasmi Wasafi Tv ndani ya Startimes Tanzania Bara na visiwani ambayo itakuwa inaruka Live Kupitia chaneli namba 444 katika king’amuzi hiko.

Wasafi Tv tayari inapatikana katika king’ Cha Azam na sasa unaweza kuipata kupitia king’amuzi cha Startimes.

Hizi ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri ukumbini hapo:

 

 

Huddah Afungukia Mahusiano Yake na WCB

Socialite maarufu kutoka Kenya mrembo Huddah Monroe maarufu kama Huddah The Bosschick amefungukia uhusiano wake na Label maarufu nchini WCB.

Huddah alitua nchini Tanzania mwishoni mwa wiki hii na mara moja alionekana akiwa katika ofisi za WCB na CEO wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi The Playlist ya Times FM, Huddah amesema kuwa ukiachilia mbali sababu za kibiashara, amekuwa akivutiwa na uchapakazi wa timu nzima ya WCB.

The vibe is, WCB napenda sana ni watu wanajima, watu wana njaa ya maisha , so for me WCB have the some kind of vibe the i have. Wanapenda maisha mazuri, so they very work hard hawalalai saa 24 wapo kwenye kazi, so that I like that”.

Huddah ambaye ni Mfanyabiashara anayemiliki make up line yake inayoitwa Huddah Cosmetics ambayo imekuwa ikifanya vizuri.

Huddah Monroe alikuja nchini Tanzania kwa ajiili ya ku-host show ya Harmonize iliyofanyika siku ya leo June 16, 2018.

Nandy Alikuwa Msanii wa WCB Kabla ya Kutoka:Lizer

Mtayatrisha ji wa nyimbo nyingi kutokaWCB Lizer amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake elimu yake aliyoishia ni darasa la saba na alifaulu vizuri lakini alikataa shule na kusababisha kufukuzwa nyumbani ndipo alipoamua kukimbilia Burundi alipotokea nyumbani kwao kigoma na ndipo alipoenda kujifunzia muziki.

Lizer anasema kuwa alijifunza kuimba na baadae kuwa producer ndipo moja ya wasanii nchini Burundi alipomtambulisha kwa Diamond lakini Diamond alimuomba kufanya nae kazi na alikataa lakini kutokana na hali ya amani kutokuwa shwari nchini Burundi aliona bora arudi Tanzania ambapo baaada ya muda aliona maisha yanabadilika na kumtafuta Diamond na kukuta nafasi yake bado ipo na ndipo alipoanza kufanya kazi na Diamond.

Hata hivyo alipoendelea kuongea lizer alitoboa siri na kusema kuwa nandy pia alikuwa msani kutoka WCB lakini alipoona amekaa muda mrefu bila kutoa ndipo alipoamua kuanza kufanya kazi zake .

Hata hivyo Lizer anasema kuwa tangu ameanza kufanya kazi na wcb, ndoto zake imewea kutimia kwa 70% na kwamba kuhusu kufanana kwa nyimbo zake katika beats , hiyo ni identity yake ambayo anaitengeneza.

Rosa Ree Afunguka Kuhusu Kujiunga WCB

Msanii wa Bongo fleva Rosary Robert ‘Rosa Ree’ aliyejizolea umaarufu kutokana na  miondoko yake ya kuchana amefunguka juu ya mipango ya kusaini na Label maarufu nchini WCB.

Rosa Ree ambaye amekuwa akiulizwa mara kwa mara kama ana mpango wa kujiunga na label hiyo ameweka wazi kuwa hajwahi kufikiria kujiunga WCB.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Rosa Ree ambaye awali kabisa alikuwa katika label ya The Industry amesema  kuwa hawajawahi kuzungumza hilo ila ni watu ambao wamekuwa bega kwa bega na yeye katika muziki wake.

Hapana ilikuwa hamna, ndiyo timu mzima ya WCB wamekuwa wakinisapoti katika muziki wangu. Nafurahia hilo ila hatukuwahi kufikia hatua hiyo”.

Rosa Ree aliondoka The Industry, record label inayomilikiwa na Nahreel na Aikah wa Navy Kenzo mwaka jana oktoba na amekaa bila management kwa miezi kadhaa mpaka aliposainiwa mapema mwezi huu.

Queen Darleen Athibitisha Kurudi kwa Zari Mjengoni, Amtupia Hamisa Dongo

Mwana dada pekee kutoka katika lebel ya wcb leo amethibitisha kurudi kwa  zari katika mjengo wa WCB  baada ya kuondoka na kugombana kaka yao muda mrefu lakini kumetokea usuluhihso na kurudi.

mwanadada huyo aliweka picha ya kaka na wifi yake huyo huku akiandika kwa kuwapa taarifa watu  amabo kwa namna moja ama nyingine inawza kusemekana kuwa ni hamisa amabe alikuwa katika penzi zito na daimond hivi karibuni.

 

Zamaradi Athibitisha Show ya WCB Itapamba Moto.

Zamaradi mketem akiwa kama moja ya viongozi wa  Wasafi Tv amethibitisha kuwa kuna show itakayo kuwa inaonyeshwa katika televisheni iyo ambayo itakuwa habari ya mjini itakapo anza.katika ukurasa wake wa instagram zamaradi aliandika,

Kuna vingi vikubwa vinakuja kutoka Wasafi Tv, ila niwe mkweli moja kati ya vitu vikubwa MNO ambavyo hata mimi binafsi i cant wait ni this BIG REALITY SHOW.. kumeshafanyika kadhaa Bongo, ila hii nakuhakikishia HAIJAWAHI KUTOKEA TANZANIA, na sio kwasababu ya watu walio mbele tu, ila pia TIMU KUBWA ILIYOJIPANGA nyuma ya reality show hiyo, bila kusahau exclusivity ambazo hata Dunia ya Social Medias haijawahi kuzishuhudia zitakazowekwa kwenye creativity ya ya hali ya juu, na hata uwazi mkubwa wa characters waliopo and how real watakuwa, Its time to watch OUR STARS and be proud of production ya vipindi vyetu.
Hao ni BAADHI tu ila kuna wengi (wahusika) utawaona humo and I swear hautachange channel kwa vyovyote on that Day’
The real life of WCB 
And BTW, Lifestyle ya Nani unayotamani kuiona kwa karibu zaidi kutoka Wasafi!!!???? Ama Nyumba ya nani utakayotamani kuiona zaidi kuliko nyingine!!? 

Abdu Kiba- Ninaweza Kufanya Kolabo na WCB Lakini Inategemea na Wimbo

Msanii wa Bongo fleva Abdul Kiba ambaye pia ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kudai kuwa yupo tayari kufanya Kolabo na mahsimu wao wakubwa WCB.

Sio siri kuwa Diamond na Ali Kiba hawapikiki chungu kimoja pamoja na kwamba wameshasema hawana bifu lolote lakini ni wazi kuwa Kumekuwa na tensions fulani baina ya makundi hayo mawili.

Lakini Abdu Kiba ameibuka na kudai kuwa kama ikitokea kuwa kuna wimbo ambao utakuwa na uhitaji wa msaniii kutoka WCB ndio ukae sawa hataona shida kumtafuta ili wafanye kazi.

Abdu Kiba amefunguka hayo Kwenye mahojiano na EFM Radio Lakini amejitetea Kuwa Mpaka sasa hajapata wimbo unaohitaji sauti kutoka kwa msanii yeyote wa WCB:

Kufanya kolabo na msanii yeyote kutoka WCB inategemeana na muziki gani ambao nimeimba, naamini kila muziki una sura ambayo inaonyesha ni nani unaweza kuimba naye, ikitokea kuna muziki ambao naona kuna haja ya msanii kutoka WCB nitafanya naye na kama sina tutabaki hivi hivi WCB na Team Kiba”.

 

Queen Darleen asema Diamond Atasubiri Yeye Aolewe Ndio na Yeye Aoe

Mwanadada pekee kutoka kundi la wcb  Queen Darleen,amefunguka na kusema kuwa wakati wake wa kuolewa ukifika lazima na yeye ataaolewa tu kwa sababu hata yeye ni binadamu na pia ni mwanamke kwaio hawezi kuacha kuolewa.

Watu wengi wamekuwa wakitilia mashaka sana mahusiano ya kimapenzi ya Queen Darleen kutokana na ukweli kwamba mwanadada huyo hajawahi kuonekana sana akiwa na mwanaume yoyote  na pia ni kutokana na muonekano wake ambao mara nyingi  anaonekana ni wa kiume.

Mimi sina shida , ndoa ni majariwa na kama mungu atanijalia basi na mimi  nitaolewa  na mimi ni binadamu na nina hisia vile vile  kwaio nikipata mwanaume na mungu akinijalia basi nitaolewa tu.

Hata hivyo queen darleen anasema kuwa pamoja na kwamba yeye bado hajajua muda wa kuolewa lakini yeye ni mkubwa sana kwa diamond kwaio lazima diamond atasubiri sana kuoa mpaka yeye aolewe kwanza.

Mameneja Wa Diamond Wadaiwa Kuhusika na Kusambaza Video Ya Ngono Ya Nandy

Kama utakumbuka mwezi uliopita jiji zima lilizizima baada ya video ya ngono iliyomuhusisha msanii wa Bongo fleva Nandy na Billnas kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha skendo kubwa kwa wasanii hao.

Chanzo cha video hiyo hakikujulikana kwa sababu Nandy na Billnas wote walikataa kuhusika na kusambazwa kwa video hiyo lakini aliyeiweka video hiyo Mtandaoni ni kurasa ya Udaku inayojulikana kama UdakuTz.

Sasa tangu wikiendi iliyopita kuna taarifa zilizodai kuwa mmiliki wa kurasa hiyo ya udaku ametekwa na watu wasiojulikana kwani familia yake haijui alipo, mpaka jana ambapo ilidaiwa alichukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano juu ya kuvuja wa  video ile ya Nandy na Billnas.

Lakini taarifa iliyotolewa jana na mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown ni kuwa mmiliki wa kurasa hiyo yupo kituo cha polisi na Kwenye mahojiano hayo amewataja watu waliompa video hiyo avujishe ambao walikuwa ni mameneja wa Diamond ambao mi Salaam SK na Babu Tale.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Soudy Brown aliweka posti hii:

Mpaka sasa haijajulikana kama Watajwa hapo juu  ambao wote ni mameneja wa Diamond wameshatiwa mbaroni au bado.

Lakini pia haijawekwa wazi ni vipi Msanii Diamond anahusika vipi katika hilo lakini yote hii inarudi katika bifu la Diamond na Clouds Media.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.