Timmy Tdat enlists G Nako and Dogo Janja for ‘I Don’t Care’ (Video)

Highly-acclaimed Kenyan musician Timothy Owuor, better known as Timmy Tdat, has released a new jam alongside  Tanzania’s G Nako and Dogo Janja and it’s getting a lot of love from their fans.

Also read: It’s official, Timmy Tdat is back to his winning ways!

The song titled I Don’t Care, which is off Timmy Tdat’s forthcoming EP dubbed Bonke, has been ruling the airwaves since it came out  few hours ago.

G Nako

To be honest, the first time I listen to this jam I didn’t really like it but with time I came to love it and now I can’t stop playing it. I guess it’s one of those songs that grow on you with time.

I’ll be the first to say that this collaboration was long overdue because it’s so infectious. There is just something about Timmy Tdat’s style and how it blends well Swahili rap that I can’t get enough of.

G Nako killed his verse. He has a natural flow and you just want to keep listening to him as he does his thing. To add to that, he also delivered an impeccable hook on this jam.

Dogo Janja

Dogo Janja also brought his A-game on this jam. Apart from his unique voice, this lad also has a some rare wordplay skills that will leave you with you with one finger stuck on the replay button.

As expected, our very own Timmy Tdat lived to the hype. If you are a huge fan of his, like myself, then I am sure you know that he is one of the best lyricists that we have in Kenya and he proved that yet again in this track.

To be honest, I was not really impressed by the beat. It is so basic. Maybe I find it different because it was made by a Tanzanian producer by the name Mr T Touch.

I absolutely love the video. Other than its crisp quality, I was also impressed by the lighting, styling, the sexy vixens, props, locations, lighting and the flawless scene transitioning.

Watch I Don’t Care below and tell us what you think.

“Nakupenda Sana, Kula Ushibe Halafu Kaza Chaga”-Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja ameibuka na kumtumia ujumbe Mpenzi wake  Mpya anayejulikana kwa jina la Linah.

Dogo Janja alitangaza kuchana na aliyekuwa mke Wake Msanii Irene Uwoya mapema mwaka jana Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miezi kadhaa.

Dogo Janja Hivi sasa yupo kwenye mahusiano na Mrembo ambaye ni Mfanyabiashara kutoka Arusha ambaye anasemekana kuwa na pesa ndefu kutokana na Familia yake kuwa kwenye biashara za madini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dogo Janja amemtumia ujumbe wa birthday mrembo huyo ambaye alizaliwa siku ya jana:

Hakuna neno linaloweza kutosha kuielezea furaha niliyonayo kwenye kufurahia siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu…..mengine nitakueleza chumbani…..kula ushibe kisha kaza chaga….nakupenda sana”.

https://www.instagram.com/p/BtlyFosFIt9/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1tdljljimtqu5

Dogo Janja- Mbali Ya Muziki Nafanya Biashara

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa mbali na kufanya muziki Lakini pia ni mfanyabiashara.

Dogo Janja ambaye anafanya vyema kwenye tasnia ya muziki nchini ameweka wazi kuwa pamoja na kuupenda muziki Lakini anaamini ni vyema Kuwa na kitu kingine cha kufanya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Dogo Janja amesema kuwa amekuwa akifanya biashara zake nje ya muziki wake ambazo zimekuwa zikimwingizia kipato kizuri na kujivunia kuifanya kwa moyo mmoja.

Nafurahi nafanya biashara ambazo zinanilipa nje ya muziki wangu, nafurahia kile ninachokifanya kwa kuwa biashara zangu zimekuwa na manufaa makubwa kwenye maisha yangu”.

 

Dogo Janja Amuanika Hadharani Mpenzi Wake Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja ameonekana kuendelea na maisha yake Baada ya kuachana na aliyekuwa mke Wake Irene Uwoya.

Dogo ameonekana akijiachia live na mwanamke mwingine anayetambulika kama Lina kwenye Mitandao ya kijamii ambapo walionekana wakiwa wanakumbatiana bila uwoga.

Wikiendi iliyopita Dogo Janja na mama yake mzazi walionekana kwenye party ya rafiki wa karibu wa Lina ambapo Dogo alikuwa anatumbuiza Lakini mara akaonekana akiwa anakumbatiana na Linah na mahaba hadharani.

Pamoja na taarifa za Dogo Janja kuwa kwenye mahusiano na linah Lakini Mpaka sasa hajathibitisha taarifa hizo.

Dogo Janja Aikana Familia ya Uwoya.

Msanii Dogo Janja ameonekana kuikana familia ya msanii Irene Uwoya ambae aliwahi kuwa mke wake na kuachana hivi karibuni huku akisema kuwa hajui kitu kuhusu familia hiyo na wala hana habari nayo hata kidogo.

Alipokuwa akifanya mahojiano na moja ya waandishi anasema kuwa kwa upande wa familia yake wanandekea vizrui akimaanisha familia yake iliyopo Arusha ambako amekuwepo huko kwa mud mrefu sana lakini kuhusu familia ya msanii Irene huyo hajui chochote hivyo anaombwa hasiulizwe kitu.

Ikumbukwe kuwa Dogo Janja na Irene wamekuwa katika ndoa kwa muda mfupi sana , ndoa iliyofungwa mwanzoni mwa mwak 2018 na kuachana mwaka 2018 , huku sababu kubwa ni kushindwana kwa tabia kati ya wawili hao.

 

Dogo Janja Amponda Bilnass na Style Yake ya Nywele.

Msanii kutoka Arusha Dogo Janja amemtupia msanii mwenzake Billnass,  Dongo baada ya msanii huyo kuonekana akiwa na style mpya ya nywele akiwa ametengeneza dread, style ambayo wasanii weng ka sasa wamekuwa wakiweka kichwani.

Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa style hiyo haijampndeza kabisa msanii mwenzake huyo na kumwambia kuwa  hata waliupokutana katika After school bash wikiend iliyopita hakumtambua mara moja kwa sababu ya  upya huo.

Dogo janja amefunguka na kumwambia kuwa msanii mwenzake huyo hajapendeza kabisa na kuamua kubadili style hiyo.

Wasanii hasa wa kiume kwa sasa wengi wamekuwa wakivutiwa na kutengeneza nywele style ya nywele ndefu yaan dread , ingawa wengi hupendelea kusuka lakini  sio kichwa kizima, vado haijafahamika kama dogo janja alikuwa akitania kuhusu swala hili au lakwa sababu wawili hao ni marafiki pia.

 

Lynn Akiri Kuvutiwa na Rayvanny na Dogo Janja

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Irene Godfrey Louis maarufu kama Lynn ameibuka na kuweka wazi kuwa wasanii waliomvutia kwenye Sanaa ni Mastaa wa Bongo fleva Rayvanny na Dogo Janja.

Wiki mbili ziizopita Lynn aliingia rasmi kwenye tasnia ya Bongo Fleva kwa kutambulisha wimbo Wake Mpya ‘Chafu’.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Lynn alisema kwa kipindi kirefu alikuwa na nia ila alikosa mtu wa kumshauri, lakini baada ya kuwasikilizisha nyimbo zake, Rayvanny na Dogo Janja walimtia moyo kuwa anaweza.

Muziki ni moja ya malengo yaliyokuwa ndani yangu, lakini ndoto zangu niliona kama zinakufa kutokana na baadhi ya watu kunikatisha tamaa. Lakini ilikuwa tofauti kwa Rayvanny na Dogo Janja ambao walinipa moyo kuwa naweza ndipo nikatoa wimbo wangu haraka”.

Lyyn ambaye ameachia ngoma inayokwenda kwa jina la Chafu na kusifia mapokezi kuwa ni mazuri kuliko alivyotegemea hivyo amepanga kuachia mwingine fasta.

 

 

Dogo janja Akumbuka Zamani

Msanii Dogo Janja Amerudi na kukumbuka kule alikotoka baada ya kuikabidhi shule aliyosomea darasa la kwanza mpaka la saba kwa kuwapa ndoo za rangi 20  pamoja na kuamua kukarabati shule hiyo kwa kuweka mabati.

Dogo janja mabae laisoma shule ya ungalimitied arusha, ameamua kurudisha fadhila na kukarabati mazingira hayo ili kuwasaidia wanafunzi waliopo sasa kusoma katika mazingira sala na safi.

Huu ni wakati mabao Dogo janja amekuwa akijitolea kwa jamii yake  kwa sababu tangu amekuwa Arusha ambao ndiko aliozaliwa , ameamua kujirudi kwa jamii yake na hata kujenga nyumba kwa ajili ya mama yak mzazi.

katika ukurasa wake wa instagra  Madee aliandika ; leo mapema @dogojanjatz alirudi kwenye shule #Ungalimited alisomalakwanza mpaka ka saba na kutoa ahadi ya kupiga rangi shule nzima na bila kuchelewa akapiga simu kiwandani na kuletwa ndoo kama zote … pia atapiga bati shule nzima

 

Dogo Janja Amjengea Mjengo Mama Yake Baada Ya Baba Yake Kufariki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chende maarufu kama Dogo Janja ameuanika mjengo ambao amemjengea Mama yake mzazi miaka miwili baada ya baba yake kufariki.

Siku ya jana December 4, 2018 Dogo Janja, amefanya dua ya kumuombea Baba yake ambapo pia ametuonyesha nyumba aliyomjengea Mama yake Mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha Mama yake anaishi sehemu nzuri.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Dogo Janja ameandika mjengo huo na kufunguka mengi:

Sisi tumekulia katika nyumba ya kupanga, Mimi na Kaka yangu tulikuwa tunalala sebuleni baada ya Baba kufariki Mimi nimebaki kama Baba wa familia, Mama angu anahitaji sana faraja, najitahidi sana kumpa faraja sababu siwezi badilishana na Mtu mama”.

Lakini pia Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dogo Janja amefunguka muhimu wa yeye Kama Mtoto wa kiume kumjengea Nyumba hiyo Mama yake:

Mimi ni Mfanyabiashara Sitakiwa Kuchagua Upande Kati Ya Wasafi Au Clouds-Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Abdul Chande Maarufu Kama Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye ni mfanyabiashara hivyo hawezi kufungamana na upende wowote.

Mgawanyiko huo kati ya wasanii ulitokea mapema Wiki iliyopita Baada ya sakata la Wasafi Festival na Fiesta lilopelekea wasanii waliokuwa wanaperfom kwenye Fiesta kushindwa kufanya hivyo na kuaababisha kukosa shoo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Sam Misago TV, Dogo Janja ameweka wazi kuwa hawezi kujiweka katika upande wowote ule kwa sababu yeye ni mfanyabiashara hivyo kokote atakapoitwa kupiga pesa yeye ataona sawa tu.

Mimi matabaka sioni ninachoamini Mimi mfanyabiashara hivyo sitakiwa kufungamana na upande wowote ilimradi naenda huku napiga naenda kule napiga hela basi hicho cha maana kwangu”.

Dogo Janja alikuwa mmoja wa wasanii ambao walitakiwa kupiga shoo ya Fiesta jumamosi iliyopita lakini walishindwa Baada ya shoo hiyo kuhairishwa Baada ya serikali kuizuia kufanyika katika viwanja vya Leaders.

Maneno ya Dogo Janja Kuhusu kifo Chake

Msanii wa bongo flea Dogo Janja amefunguka  na kuwataka watu kuwa na upendo  na watu pale wanapkuwa hai na sio kusbiri mpak pale watakapokufa ndo waanze kulia na kusema kuwa walikuwa ni wapendwa wao.

katika kurasa wake Dogo Janja aliandika “siku nikifa utataoa machozi lakini mimi sitayaona,utaleta maua lakini mimi sitayapokea, utanisifai asna lakini mimi sitakusikia utanisamehe makosa yangu lakini mimi sitayajua , utanimisi sana lakini sitafahamu na utauzinika sana lakini sitakuona.

Dogo janja ametaka watu kuwa wakweli wa  wale wanaowapenda kabla hawajakufa na sio kujifanya mnafiki kuonyesha kuwa unampenda mtu akiwa tayari hajuia wala haoni kile unachokifanya.

Jibu la Dogo Janja Kuhusu Sababu ya Kumsaliti Irene Lina Utata.

Msanii Dogo Janja amejikuta akimjibu kwa kumtolea povu moja ya mashabiki zake walimuuliza kwa nii aliamua kumsaliti mke wake wa ndoa irene uwoya na kwenda kutembea na mwanamke mwingie.

Ikumbukwe kuwa siku za hapo karibuni kulizuka tetesi za msanii Dogo Janja kutoka kimapenzi na mwana dada wema sepet na kusababisha ndoa yao kuvunjika, ndoa ambayo ilikuwa aikizungumziwa sana midomoni mwa watu katika mitandao ya kijamii.

Moja ya mashabiki zake walimuuliza  sababu kubwa ya  kumsaliti mke wake ilikuwa ni nini lakini kitu cha ajabu dogo janja alijibu jibu ambalo kama vule kosa hilo alikuwa amesingiziwa hakuna na hatia yoyote

Shabiki aliuliza, Dogo janja why didi you cheat on your wife,  Dogo janja nae aliwajibu kwa kusema ‘”stress ya ukweli ni pale unapokutana na mama wa demu wako alafu anakwambia wewe ndio uwaga kila siku unakuja na gari usiku kumchukua  mwanangu , wakati wewe hata mkokoteni tu hauna.”

 

 

Dogo Janja Atangaza Zawadi ya Mjukuu kwa Mama Yake

Msanii Dogo Janja katika hali isiyo ya kuhaminika kwa mashabiki wake aliweka picha ya mama yake mzazi huku akisema kuwa ni muda muafaka sasa wa yeye kumletea mama yake mzazi mjukuu kwa sasa kwa sababu mama yake anaanza kuzeeka.

Dogo janja anasema hivyo ikiwa imepita siku chache tu tangu kuvunjika kwa ndoa yake na mwanadada Irene uwoya hivyo hii inazua gumzo kwa mashabiki wake kwa sababu kutangaza uwepo wa mjukuuu ni ishara ya kujiamini na jambo hilo huku ikitaka kujulikana mwanamke anamletea mama yake mzazi Dogo janja mjukuu.

Msanii huyo ambae tang kumekuwa na skendo za kuachan na mke wake amekuwa akionekna yupo karibu na nyumbani kwao Arusha huku ikisemwa kuwa nyumba aliyokuwa akikaa na me wake inaoneknana kwa sasa haina mtu.

 

Maneno ya Mashabiki Baada ya Dogo Janja Kukitana na Jenipher Kanumba

Wikiend hii wasani walipokuwa katika ziara ya shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro, msanii Dogo janja alikutana na msanii wa bongo movies Jenipher kanumba  na kupiga nae picha ya pamoja.

Kata hivyo wawili hao wote ni wasanii lakini kwa maelezo ya dogo janja anasema kuwa hakuwahi kukutana na msanii mwenzake huyo na ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa siku hiyo.

Katika picha hiyo Dogo janja alisema kuwa hiyo iliwahi kuwa moja ya ndoto yake ya kutaka kukutana na msanii huyo na anashukuru ndoto hiyo imekamilika.

Kama kawaida kwa maneno ya mshabiki walianza kumpingeza huku wengine wakimwambia kuwa wasichana kama jenipher ndio saizi yake na sio kukimbilia wanamwake wakubwa wakubwa ambao  wamezidi umri kama uwoya.

Baadhi za commentsa za wadau zinaonekna azikisema hivi ”

Wema Afunguka Tetesi Za Kufaidi Penzi la Dogo Janja

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amefunguka na kuongelea skendo nzito inayomuandama hivi sasa ya kufaidi Penzi la Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja.

Siku ya jana Mange Kimambi alidai kuwa  Wema  na Dogo Janja walikutana mkoani Arusha ambapo walikuwa nyumbani kwa rafiki yao lakini mambo yaliwazidi na kujikuta wanafanya yao.

Wema ameibuka kukataa tetesi hizo na kumtuhumu Mange kwa kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli wowote.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika maneno haya:

Wema amekana tetesi hizo na kumuanika mwanaume mwingine ambaye amedai atakuwa mume wake mtarajiwa.

Popular Bongo actress ends her marriage after Wema Sepetu sleeps with her husband

Wema Sepetu has been the new topic on Instagram after unveiling her new man. With good news spreading like wild fire; some bad news also happened to emerge thanks to Mange Kimambi.

Well, word has it that the Tanzanian sweetheart is the reason why actress Irene Uwoya walked out on her marriage with rapper Dogo Janja. According to Mange Kimambi who shared the details on her Instagram page; apparently Wema slept with Dogo Janja knowing well he is married to a colleague.

Irene Uwoya

This happened a few weeks ago after the two bumped into each other at a mutual friends house and after a few sessions of smoking weed; Wema and Dogo decided to enjoy each other’s company.

Dogo confirms the rumors

Just to make sure the stories were true, Mange Kimambi sent Dogo a few messages and judging from their conversation seems that the young rapper feared the story leaking.

But unfortunately Wema Sepetu ended up rubbing Mange Kimambi the wrong way and now everybody knows that she allegedly slept with Uwoya’s now ex husband.

Bill Nas Akana Bifu na Dogo Janja Baada Ya Kumwagiana Povu Zito

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana William Lymo maarufu kama Bill Nas amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na msanii mwenzake Dogo Janja hawana bifu lolote.

Tetesi za Bill Nas na Dogo Janja kusemekana kuwa na bifu zilianza mara baada ya wawili hao kurushiana maneno ya kejeli Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Dogo Janja alimtania Bill Nas kwa kuachwa na mwanamke wake kwa sababu ya mdomo  na Bill Nas alimchana kuwa ameolewa na Uwoya ili acheze na mtoto wake.

Global Publishers lilimtafuta Billnass ili azungumzie ishu hiyo ambapo alisema hana bifu na Dogo Janja bali maneno hayo yalikuwa ni utani tu.

Sina bifu na Dogo Janja, hayo maneno tuliyokuwa tunaandikiana yalikuwa ni utani tu, sisi tumeshazoea kutaniana kwa hiyo nawaomba mashabiki zangu wasichukulie kwamba tuna tofauti”.

 

Dogo Janja Akimbilia Kwa Mwanasaikolojia.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja ameanza kuonekana akitafuta msaada kwa kile kilichodaiwa kuwa anahitaji  msaada wa kisaikolojia kutoka na matatizo ya msongo wa mawazo unaomkumba hasa baada ya kushindwa kukubaliana na hali halisa ya mahusianoa yake.

Mwanamuziki huyo ambae aliweka picha yake akiwa na mwanasaikolojia Chris Mauki, imesemekana kuwa hali yake kwa sasa haiko sawa hivyo imembidi kutafuta msaada zaidi.

Kama utakumbuka basi wiki chache zilizopita, mwanamuziki huyo aliwahi kuripotiwa kuwa mgonjwa hospitali huku sababu kubwa ikisemekana kuwa ni msongo wa mawazo wa kusindwa kukubaliana na hali halisi ya mfarakano wake na  mkewe.

Hata hivyo Uwoya mwenyewe amekuwa akikanusha taarifa hizo ilhali kumekuwa hakua zile rapsha rapsha  za mapenzi kama ilivyokuwa hapo awali kati yao.

Kauli ya Dogo Janja Yawashtua Mashabiki.

Katika ukurasa wake wa twitter msanii Dogo janja amewashtua mashabiki zake baada ya kuweka ujumbe ambao kidogo umeashiria kama mtu aliyekataa tama kabisa na maisha hivyo kujikuta akiongea vitu vinavyoashiria kutaka kupoteza uhai.

Msanii huyo ambae hapa karibuni lizivuma tetesi kuwa alilazwa huku sababu kubwa ikiwa ni presha na mshtuko alioupata baada ya kugomabana na mke Irene uwoya ambae wamefunga ndoa mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo Dogo janja alipoulizwa kuhusu maneno hayo alikri kuyaandika huku akisema kuwa hiyo ni baadhi ya mistari katika nyimbo yake mpya huku akikataa kuongelea swala la yeye na mkewe.

Dogo Janja Atoa Sababu ya Kutobadili Jina Lake.

Msanii dogo janja amefumguka na kusema kwa pamoja na kwamba kwa sasa ameshakuwa na watu wamkuwa wakisema kuwa jina hilo halistahilitena kutokana na ukweli kuwa umri wake umeshakuwa , yeye anakataa na kusema kuwa hawezi kubadili jina hilo kwa sababu tayari hiyo ni brand na hawezi kuipoteza kwa sababu ameifanyia kazi kwa muda mrefu sana.

kama tukiangalia kwa nchi nyingi  duniani , wasanii wanakuwa na viunganishi vya majina ambavyo baada ya umri flani kuviondoa kwa sababu vinakuwa tayari havipaswi kutumika kutokana na umri wake na ndivyo inawezekana ilitakiwa kwa dogo janja kutokana na neno DOGO haliendani tena na umri wake sasa.

Dogo janja anasema ‘mimi ni forever young, dogo janja ni brand ambayo ilitengenezwa kwa miaka 9 sasa kwaio kwangu ni biashara ukiachana na udogo au ukubwa wangu.kwaio hiyo ni biashara ambayo inajitegemea.

 

Dogo Janja Asema Hana Bifu na Young Killer Wala Young Dee.

msanii wa bongo fleva dogo janja amefunguka na kukanusha tetesi zinazosambaa kuwa yeye na wasanii wenzanke young dee na young killer wamekuwa na kutokuwa na maelwano ya muda mrefu kitu ambacho sio cha kweli hata kidogo.

Dogo janja ameyaongea hayo alipokuwa katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa na EATV.

Sijawahi kuwa na ugomvi na msanii yoyote hapa nchi kwa sababu mimi ninapita katika njia yangu na wao sio njia ya mtu mwingine yoyote.kwaio watu wanaamua kufanya hivyo  na kuweka ule u-young lakini hakuna ukweli owowte kuhus sisi kuwa na ugomvi.

Upande wetu siis nje ya muziki tunayo maisha yet tofauti kabisa,kwaio huwa tunakutana na tunafanya tunayoyafanya kwa  amani tunakutana sana na huwa tunataniana sana na hawaniwezi mimi kwa matani na wao wanajua hilo.

Hata hivyo Dogo janja amefunguka na kusema kuwa hakuna changamoto anayoipata katika swala la muziki kwa sababu wenzake wamekuwa waki-ra na yeye akiimba hivyo hakuna changamoto.

Matumizi ya Kinga Yamzuia Dogo Janja Kupata Mtoto.

Msanii wa bongo fleva anetamba sana kwa sasa na wimbo wake wa Banana dogo janja ambae pia ni mume wa msanii wa filamu nchini irene uwoya , amefunguka na kusema kuwa  kabla hajaoa ilikuwa ni vigumu sana kwake kupata mtoto kutokana na wosia aliwahi kuachiwa na baba yake.

Akijibu swali aliloulizwa na mashabiki kuhusu  idadi ya watoto alionao mpka sasa , Dogo Janja anasema kuwa hana mtoto na wala hajwahi kusingiziwa mtoto katika maisha yake ya ujana .

sijawahi kusingiziwa mtoto maisha yangu yote ,kwa sababu mimi napenda sana kutumia kinga,alafu na marehemu baba yangu aliwahi kuniambia kuwa nisipate mtoto nje ya ndoa.kwa sasa nimeona kwaio siwezi kuendelea kutumia kinga na panapo majaliwa basi tutapata mtoto soon.

Dogo Janja Ataja Ngoma Ambayo Haikubali Kutoka Kwa Madee

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kuanika jina la ngoma kutoka kwa Msanii mwenzake Madee Ali.

Dogo Janja ameitaja ngoma ya Madee ‘Hip Hop haiuzi’ kama moja ya nyimbo za Msanii huyo ambazo hajawahi kuzikubali kabisa.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kwetu Flavor cha Magic Fm Dogo Janja ametaja ngoma ya Madee ‘Hip Hop Haiuzi’ kama wimbo ambao hakupendezwa nao kabisa pindi ulipotoka.

Kipindi hiyo unatoka nipo chuga, nachana sana na masela. Nikaona huyo vipi, masela wanasema huyu waki labda hasije chuga, tutamfanyia kitu mbaya”.

’Hip Hop haiuzi’ ni nyimbo ya Madee ambayo ilizua gumzo sana miaka ya nyuma ambapo wasanii wenzake ambao wanafanya muziki wa Hop Hop walimjia juu MAdee baada ya kuuponda muziki wao wa hip hop.

 

Belle 9- Dogo Janja Ndio Anatakiwa Kuchapwa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Belle 9 ameibuka na kudai kama kuchapwa anatakiwa kuchapwa Dogo Janja sio yeye.

Wiki iliyopita Dogo janja Kwenye Interview yake alisema Belle 9 anahitaji kuchapwa viboko 70 baada ya kusema Hamuelewi na hata nyimbo zake anzoimba huwa hazielewi.

Kwenye mahojiano na Enews ya EATV, Belle 9 amemjibu Dogo na kusema inabidi achapwe yeye kwani nyimbo yake mpya ya ‘Banana’ ni ngoma ya kihuni na hajaielewa:

Nilivyosema msanii ambaye simuelewi ni Madee sikuwa na maana mbaya na samahani kama wamekasirika lakini niliongea kwa uzuri maana ni msanii ambaye huwa namuangalia.

Kusema ukweli nilivyosikia anasema nichapwe viboko nilicheka sana na huenda tunatofautiana kufikiria na labda kwa mazingira aliyokulia yeye anaona kuchapwa viboko kunaweza kumbadilisha mtu ila sio pointi sana maana mambo yamebadilika.

Halafu kama ni viboko anatakiwa achapwe yeye kwa nyimbo anazoimba zenye  utata kwani nyimbo iliyopita alivaa kama mwanamke na nyimbo yake mpya ya Banana anaimba sijui your my Banana na wote tunajua Banana ina maana gani”.

 

Tip Top Haijafa Ila Majukumu Ndio Mengi- Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Dogo Janja ameibuka na kuongelea suala la kundi la Tip Top Connection kuvunjika ambapo amedai halijavunjika bali kila msanii ana majukumu mengine.

Kundi kwa Tip Top Connection liliwahi kuvuma sana na kufanya vyema sana miaka ya nyuma na liliundwa na wasanii kama Madee, Kassim Mganga, Keysha, Dogo Janja na wengineo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Dogo Janja amesema kuwa sio kweli kuwa kundi hilo limekufa kutokana na kwamba hawatoi wimbo wa pamoja bali majukumu mengine na muda vimewatenganisha.

Tip Top ipo pale pale, umri na majukumu sio watu tena wa kukusanyana masikani tena ndio kitu ambacho watu wanakuwa wanapishana sana lakini Tip Top ipo na inafanya.

Watu wanazungumza kwa sababu hakuna wimbo wa kundi nahisi ndio chanzo cha watu kuzungumza hivyo”.

Wasanii ambao walikuwa wanaunda kundi hilo wamesambaratika huku kila msanii akiwa anafanya muziki wake ingawa wamekuwa wakionekana pamoja Kwenye matukio mbali mbali pamoja kama Kwenye Harusi ya Dogo Janja.

Dogo Janja- Belle 9 Amemkosea Sana Madee

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Dogo Janja anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Banana’ amedai kuwa Msanii mwenzake Belle 9 amemkosea sana Madee hivyo anahitaji kuadhibiwa.

Wiki chache zilizopita Kwenye mahojiano na Jembe FM ya jijini Mwanza Belle 9, alimtaja Madee kama rapa wa Tanzania ambaye haelewi nyimbo zake kabisa anaona kama mzugaji kwani anaona ni msanii ambaye anatoa ‘beat’ tu na sio wimbo.

Katika interview na Enews ya East Africa Tv, Dogo Janja amemjia juu Belle 9 kwa kumwambia kuwa amekosea sana kumbeza msanii mkongwe kama Madee ambaye ameshawahi kutoa ngoma kali nyingi hata kabla ya Belle 9 kujulikana kwenye muziki.

Kitu cha kwanza hata yeye Belle 9 kuna vitu anafanya kuna watu huwa hawamuelewe, hata mimi mwenyewe kuna wanangu kibao huwa wananiambia bora Nuruely. Alichokifanya Made kwenye muziki, Belle 9 hata robo hajafikia.. Respect a legend, waheshimu wakongwe, waheshimu wazee sio busara kutukana wakongwe.

Kakosea amemkosea mzee, anatakiwa apigwe 70 bomani (wamasai hapo wamenielewa) ukivunja sheria au ukimkosea mkubwa au mzee unatakiwa uchapwe fimbo 70 mbele ya wanabomani wote.. Madee mpole sana ndio maana wanamuonea. ni mkongwe anayezeeka na heshima zake”.

 

Rayvanny Amwagia Povu Zito Dogo Janja

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Rayvanny amemwagia povu zito msanii mwenzake Dogo Janja na kumtaka ampe heshima yake.

Siku chache zilizopita Dogo Janja alimtaja Rayvanny kama msanii ambaye hajui kuvaa Kwenye Interview yake na Wasafi Tv na kujitolea kumvalisha.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Rayvanny amejibu tuhuma hizo na kusema kuwa Dogo Janja anakosea kusema hivyo kuni kuna tofauti kati ya mtu kujua kuvaa na mtu kupendeza.

Kuna tofauti kati ya kuvaa na kupendeza, mtu akikuambia hujui kuvaa, anakosea, labda akuambie hujui kupendeza.

Cheni yake ambayo anaivaa sasa hivi, aliivaa Dully Sykes kwenye wimbo wa Sugar Mami. Kwa hiyo ukija kusema eti una uwezo wa kumvalisha Rayvanny hajui kuvaa, no!, unanikosea heshima kwa sababu mimi nimeenda sehemu nyingi nimeona watu wanavaa vitu tofauti”.

Dogo Janja ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Banana’ ambayo imeendelea kushika namba moja Kwenye mtandao wa YouTube.

Dogo Janja Aponda Mavazi Ya Rayvanny

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Banana’ Dogo Janja amedai msanii kutoka label ya WCB Rayvanny anamuangusha sana Kwenye suala la mavazi.

Siku za nyuma Dogo Janja ameshawahi kuachia ngoma maalumu kwa ajili kuvaa na kupendeza Inayoitwa ‘Ukivaaje unapendeza”.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kama  akipata fursa ya kumvalisha Rayvanny atafanya hivyo.

Nikiambiwa msanii ambaye niwe namvalisha namchagulia mavazi, nitamchagua Rayvanny huwa ananiangusha sana sometimes.

Kuna muda huwa anapatia halafu kuna muda unaweza ukatema mate kule, anaweza akala njano juu mpaka chini”.

Dogo Janja yupo katika Media Tour kwa ajili ya kutangaza rasmi Single yake mpya ‘Banana’ inayoendelea kufanya vizuri Kwenye chati mbali mbali.

Babu Tale Bado Anatusimamia Tip Top Pamoja na Kuwa Bize WCB- Dogo Janja

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kukiri kuwa Babu Tale bado anawasimamia wasanii wa Tip Top pamoja na kuonekana sana WCB.

Babu Tale ambaye kwa sasa ni Meneja wa staaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, lakini ni mmoja kati ya waanziloshi wa label ya kitambo ya Tip Top yenye wasanii nguli kama Madee, Dogo Janja, Kassim Mganga na wengineo.

Lakini tangu Babu Tale apate mafanikio katika label ya WCB Kumekuwa na tetesi kuwa amewatelekeza wasanii wote wa Tip Top baada ya kuonekana sana WCB tetesi ambazo Dogo Janja amezikana.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa hilo halina ukweli wowote kwani wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mengi.

Hapana sio kweli, Babu Tale anasimamia kazi zangu sana sana ila kwamba huku Tip Top sisi hatuko bize kama Wasafi ndio maana unaoa muda wote yupo kule, hatuna matukio.

Lakini nikiachia wimbo utaona redioni nitaenda na Babu Tale, so mimi sina matukio mengi ndio maana kwenye kazi zangu anakuwa mara chache sana pale ninapomuhitaji”.

Dogo Janja hivi sasa chini ya Label ya MMB (Manzese Music Baby) ambayo iko chini ya msanii mkongwe Madee Ali.

Dogo Janja Atoa Darasa kwa Wanawake Wasidanganyike.

Msanii Dogo Janja amewataka wadada kutodanganyika na wanaume na kuwa nao makini kwa sababu wanaume wengi wamekuwa wakitumia uongo kuwanasa wanawake na wakishawapata baadae wanawake wanaanza kujutia maamuzi yao.

dogo janja anasema kuwa wanaume wengi so wakweli kama ambavyo wanawake wanavyozani lakini wanapokuja huja na njia nyimgi zinazowafanya wadada waamini kuwa mwanaume anamtaka anaongea ukweli,dogo janja ameyaongea hayo alipokuwa akizungumza na kipndi cha DADAZ kinachorushwa na  EATV.

Unajua vijana wegi ni waongo sana tena hasa wanaume ni waongo sana,ogopa sana mwanaum anaekufata na gari , heshimu anaekufata na mguu maana anakuwa yuko real.anakueleza kuwa anakupenda na maisha yangu yako hivi na hivi , ninaweza kuatafuta nikapata au nikakosa kuliko anaekufata na kukupeleka huku mara kule mara akununulie wigi la laki 8,mwishowe ananza kukopa na kukuongopea.

Dogo janja ameamua kujitolea mfano yeye mwenyewe na kusema kuwa wakati anamfata Irene alimwambia ukweli kuwa hana kitu kikubwa na kwamba uwezo wake ni wa kawaida tu.

Alichojifunza Dogo Janja Kupitia Video ya Nandy na Bilnass Kuvuja.

Msanii Dogo Janja amefunguka na kusema kuw kutokana na kitendo alichokutana nacho Nandy amejifunza kuwa wasanii wengi hawana ushirikianao katika kupatwa kwa matatizo kwa wasanii wenzao zaidi ya kuwa wanashuapalia mambo.

Kupitia matukio mawili makubwa ambayo  ya roma kutekwa na nandy kuvujisha video inamfundisha tabia za wasaniiwengine huku akisema kuwa kwa tukio la nandy wasanii wengine wamefurahishwa na tukio ilo na walikuwa wakiomba sana Nandy aweze kufungiwa kama adhabu ili iwe faida kwao kwa kupata show.

Nahisi ninaweza kumaindiwa leo na wasanii wenzangu lakini ni lazima mtu aanze ndio hili donda ndugu litapona.wasanii sis ni masinchi sana na baada ya hii ishu ya nandy ndo nimepata uhakika , kipindi cha isu ya roma nilikuwa nikiona baadhi ya watu kwenye makundi walikuwa wakisema atakoma eeh amezoea huyo , lakini pia jana na juzi nimekaa nabaaadh ya wasanii wakubwa wanasema bora hili limetokea kwa nandy maana na spidi ya show zitapungua , bora baraza wamfungie kidogo hata miezi 6 ili apotee kidogo.walikuwa wanapiga stori kama utani lakini moyoni nimefikiria sana.

wasanii tuache roho mbaya wote sisi ni maskini tu na wote tunahangaikia ugali, tukipata ajali kazini tusiombeane mabaya.vita iwe kwenye kazi tu.

 

Dogo Janja Kuwa Video Queen Kwenye Video ya Niki Mbishi

Baada ya kushambuliwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu nymbo yake ya wayu wayu ambayo imekuwa gumzo baada ya yeye mwenyewe kutokea kama video queen, msanii Dogo Janja ajibu kwa kashfa  maneno ya msani mwenzake Niki Mbishi kuwa hata kama yeye atamwajiri kutokea katika video yake kama video queen kwake ni sawa na hana shida na hilo.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Nikki mbishi aliandika “dogo janja ni video queen’ na ndipo dogo janja hakutaka kuwa nyuma kujibu kwa kusema kuwa ni kweli yeye ni video queen na hata akitaka atokee katika nyimbo yake pia anaweza kutokea.

Chupa lako ukitaka niktokee wewe onana na manejiment yangu tu gharama zangu wala sio ghali,-  Alijibu dogo janja na kutasfiriwa kuwa yupo tayari kufanya hata hivyo katika video ya Nikki wa pili.

Tangu kutokea kwa video hiyo, Dogo Janja amekuwa katika wakati mgumu wa kukutana na maneno ya kshafa sana ilhali muziki ni sanaa ambayo imekuwa na uhuru wa kuwa wabunifi kila siku.

Dogo Janja Awatolea Povu Zito Wanaoiponda Ndoa Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja amewajia juu watu wote ambao bado wanaiponda ndoa yake na Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya.

Ndoa hii imezidi kutengeneza headlines kila kukicha pamoja na kwamba ilifungwa mwaka jana mwishoni na ndio ilikuwa stori ya kufungia mwaka lakini bado mpaka leo hii Ndoa hiyo imebaki kuwa gumzo.

Dogo Janja amedai kuwa amechoshwa na watu wote wanaomsema vibaya kuhusu ndoa yake na Kwenye mahojiano na Enews Dogo Janja amesema nyimbo yake ya Wayu Wayu ni ujumbe kwa wale watu wote wanaomsema vibaya kwa kufunga ndoa na Uwoya.

Walitokea watu walikuwa na kejeli na nini mimi naonekana kidagaa sina chapaa wananitukana nini lakini mwisho wa siku nawakanyaga kama soksi zangu ilikuwa kama sehemu ya kufikisha maudhui kwa watu waendelee kuheshimu mahusiano ya mtu wasiangalie utofauti wowote kwenye mahusiano kinachotakiwa sana ni upendo kama watu mnapendana mnaheshimiana hivi vitu vingine ni vitu vya kawaida”.

Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Dogo Janja alimtolea povu zito Rapa Young Tusso aliyemwambia ameidhalilisha Arusha kwa kuvaa kama mwanamke kwenye video yake ya Wayu Wayu, Dogo Janja amesema hamfahamu Young Tusso na itakuwa vizuri kama ataendelea kuwa shabiki wake.

Nimemzidi Dogo Janja Kila Kitu Labda Yeye Kanizidi Dhambi:- Uwoya

Msanii wa bongo movie nchi irene uwoy amefunguka na kusema kuwa wala hajali watu wanaosema kuwa amemzdi mwanaume aliyemuoa miaka mingapi kwa sababu yeye anachojali zaidi ni mapenzi na wala sio kitu kingine.

Irene Uwoya ameyasema hayo leo alipokuwa katika mahojiano na kipindi cha Leo tena  cha Clouds Radio  alipokwenda yeye na mumewe huyo.Irene anasema kuwa kwake umri ni namba tu kwa sababu  hata kwa hao wanaume wenye kulingana nao umri hawakuweza kumpa kile alichokuwa anakitaka.

Ni kweli nimemzidi  umri na sio umri peke yake hata vitu vingine nimemzidi labda yeye kanizidi dhambi(Akiongea kiutani), Kwangu umri ni namba maana nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na watu ambao wamenizidi umri au tupo sawa lakini sikupata nilichokuwa nakitaka lakini kwa mume wangu nimekipata, 
Toka nimeolewa watu wengi wamekuwa wakisumbua japo hapo mwanzoni walikuwepo lakini kwasasa kuna aina ya watu ndiyo wamekuwa wakisumbua kwa kuhisi sababu Abdul kanioa basi hata wao wanaweza kupata nafasi hiyo

Irene anakiri kuwa katika mahusiano yake yote aliyowahi kuwa nayo, dogo janja ndio mwanaume aliyeweza kumpa kitu ambacho hajawahi kupata kwa mwanaume yoyote na wala sio ela bali ni mapenzi ya dhati.

Sijaolewa na dogo janja kwa sababu ya pesa,kuna vitu vingi ambavyo nimevutiwa kutoka kwake .Kwanza nilipenda mara ya kwanza alivyokuja na kuni-approch.Dogo Janja amenipa kitu ambacho wanaume wote niliokuwa nao walishindwa kunipa.

 

 

 

Dogo Janja Amekuwa James Delicious-Young Tusso

Msanii wa hip-hop nchi Young Tusso amefunguka na kumtaka Dogo Janja kuwaomba radhi watu wa Arusha kwa kitendo chake cha kuwadharirisha watu hao kutokana ka kuvaa nguo za kike katika wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni unaojulikana kwa jina la WAYUWAYU.

pamoja na kupendwa kwa wimbo huo lakini young tuso amesema kuwa ni lazima dogo janja awaombe radhi watu  wake kwa sababu hiyo ni tabia ya kike kuvaa nguo za hivyo kulingana na jinsia yake , maneno hayo aliyaongea alipokuwa akiongea na enews katika kituo cha televisheni cha EATV.

Nilishtuka sana kuona instagrma picha za dogo janja akiwa amevaa nguo za kike wakati katika huo wimbo wala hakukuwa na ulazima wa yeye kuvaa nguo za kike,kwaio mimi nimemtazma kama mtoto wa kiislamu kwaio ni lazima awaombe radhi watu wake wa Arusha.

Mimi nadhani nipo tofauti kidogo na watu wengine sikubaliana kabisa na hilo swala la yeye kuwa ni video queen,unajua kumuona msanii kama dogo janja tena wa hip-hop  ambae anatokea Arusha tena  tena kwenye asili ya ugumu  alafu mwisho wa siku anakuwa kama James Delicious inanipa tabu sana kuona hivyo.

 

 

Dogo Janja Awaombe Msamaha Mashabiki Zake Arusha -Young Tusso

Rapa anayefanya vizuri Bongo Young Tusso amedai Dogo Janja lazima akawaombe msamaha watu wake wa Arusha kwa sababu amewakosena sana kwa video yake ya wimbo wa ‘Wayuwayu’.

Dogo Janja alizua gumzo wikiendi iliyopita baada ya kuachia video yake ya wimbo wa Wayuwayu ambayo ilileta utata mkubwa sana kwani kwenye video hiyo ana one kama kuvaa kama mwanamke kuvaa kigodoro, kapaka make up na kuvaa wigi.

Kama unavyojua Dogo Janja anatokea Arusha Ngarenaro hivyo baada ya video hiyo kutoka watu wa Arusha walidai wamekasirika sana na kusema amewadhalilisha machalii wote wa Arusha.

Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Young Tusso amedai anaungana  na Wana wa Arusha na kumtaka Dogo Janja akaombe msamaha kwani hakutakiwa kufanya vile kwani yeye ni mwana hip hop alafu ni mume wa mtu na mtoto wa Kiislamu.

Kwa msanii kama Dogo Janja kitendo alichifanya hakupata sawa nimeona msanii wa Hip hop alafu anafanya hivi? huyu jamaa anatoka Arusha tunatarajia Arusha itoe wagumu maana wanasemega Hip hop inatoka Arusha sasa inakuaje anafanya hivyo alafu isitoshe yule mume wa mtu na pia ni mtoto wa kiislamu kwa kweli nimeshangazwa kumuona Dogo Janja kawa bibie”.

Young Tusso amesisitiza kuwa amem-diss Dogo Janja kwa sababu hajakubaliana na yeye kuvaa kama mwanamke kwa sababu anaidhaliliishia hip hop lakini pia anakudhalilisha Arusha hivyo amemtaka akawaombe msamaha mashabiki zake wa Arusha.

Dogo Janja Atoa Siri ya Kile Alichokifanya Kwenye Wimbo Wake Mpya.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja amefunguka na kuzungumzia swala lake la kutoa video mpya hivi karibuni  huku yeye mwenyewe akiwa amevaa uhusika  kila tukio. lakini uhusika uliozua mjadala mkubwa ni baada ya kutoka na muonekano wa kike ambao umewashangaza mashabiki wngi huku wengine wakisema kuwa amejidharirisha.

Akiongea na Planet Bongo ya Eatv, Dogo Janja anasema kuwa  alichoamua kukifanya katika video yake ya wayu wayu ni ubunifu na sio vinginevyo kwa sababu baada ya hapo maisha yake yanaendelea kama kawaida.

Nilivaa hadi kigodoro lakini ndo hivyo mwisho wa siku heshima yako inabaki palepale,sio unaigiza hivyo alafu baada ya hapo unaenda kuwa na maisha ya miyeyusho tena , hiyo inakuwa sio, swala ni umeigiza umemaliza na umerudi kulekule kwenye uanaume.

Video hiyo ya Wayuwayu ya dogo janja kwa sasa imeshika nafasi nzuri katika mtandao wa you tube.

Ndoa Ya Dogo Janja Na Uwoya Ni Kiki

Ikiwa bado kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusu ndoa ya msanii wa muziki Dogo Janja na mwana bongo movie Irene Uwoya, ebu tuangalie jinsi wasanii hawa ambavyo wanataka kuchanganya akili za mashabiki na watu wanaowapenda lakini wanashindwa kufunguka na kusema ukweli wa mambo yao yote.

Baadhi ya vyombo vya habari vilianza kuwatafuta wasanii hawa mara tu baada ya picha za msanii Irene Uwoya kusambaa zikionyesha amevaa gaunu la harusi.alipopatikana dodgo janja alijibu tu kwa mkato na kusema yeye hajui chochote.Jitihada zilipoendelea irene uwoya alipatikana na moja ya waandishi wa gazeti pendwa nchini, katika simu irene alijibu” mimi ni wa kuolewa, na ntaolewa na nani?” hata hivyo mwanadada huyo aliongezea na kusema kuwa hiyo ilikuwa ni movie tu inachezwa.

Madee akiwa kama mtu wa karibu kabisa na Dogo Janja alikuwa ni moja ya watu waliokwepa kwa muda mrefu kutoa taarifa zozote kuhusu ndoa ya Dogo Janja lakini baadae katika ukurasa wake wa instagram Madee aliposti picha yenye kuashiria kujua kiundani tukio ilo

Ndoa ni jambo la kheri, itakuwa ni tatizo kama inakuwa vigumu kwa msanii huyo kuweka wazi swala lake la ndoa hasa mwanaume wake anaeenda kukaa nae katika ndoa hiyo.Leo tarehe 30 Oktoba, Irene Uwoya aliposti picha yake nyingine na kusema kuwa ameolewa na mwanaume anaempenda huku akimshukuru na kumtag dogo janja kuwa ndie mwanaume wa ndoto zake.

Kwa kumbukumbu zinazoonyesha,katika akaunti ya instagram ya mwandada Irene Uwoya zipo baadhi ya picha zinazohusiana na ndoa iyo, moja ya picha hizo zilionyesha kadi za harusi hiyo, je ni kweli tunashindwa kuhoji mbona jina lililopo katika kadi ni tofauti na jina la mtu tunaeambiwa kuwa ndie aliefunga nae ndoa.Nani amegundua hili

Hii ni kadi ya harusi  ya Irene Uwoya , ambae inavyoonyesha na kwa jinsi ilivyosemekana ni kuwa alibadil jina na kuitwa Sheila baada ya kuabdili dini na kuamia upande wa mwanaume anaemuoa.

Nadhani kuna kitu hapa wasanii hawa wanataka kutuchezea,kuwa wazi ni vizuri zaidi ingawa italeta gumzo sana kutokana na umri wa Dogo Janja na irene uwoya ,lakini pia wawili hawa walishasikika mara nyingi wakikanusha tetesi za kuwa wapenzi.je nini kinaendelea?, kwanini Irene hataki kumuweka wazi mwana harusi?, au wanatengeneza kiki kutokana na mitandao inavyowapa muda mwingi kuwazungumzia.

Dogo Janja Amtuhumu Uwoya Kumgombanisha Na Mpenzi Wake

Kwa muda mrefu sana kumekuwa na tetesi za msanii wa muziki wa Bongo fleva  Abdulazizi Chende maarufu kama Dogo Janja anaefanya vizuri kwa sasa na kibao chake cha Ngarenaro  kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Bongo movie Irene Uwoya. Pamoja na kukutana na mahojiano ya mara kwa mara na waandishi wa habari tofauti wawili hao hawajawahi kukubali hata kidogo kuwa wapo katika mahusiano ingawa pia wapo wanaosema kuwaona pamoja baadhi ya sehemu.

Katika wimbo wa Ngarenaro ambao Dogo Janja alitaja jina la Irene Uwoya , ilifanya watu wazidi kusema kuwa wawili hao wapo katika mahusuiano, lakini wao wenyewe wamekuwa wakikataa kabisa huku kwa uhalisia Dogo Janja anaonekana kuwa mdogo sana kwa Irene Uwoya kiumri, inawezekana hiyo pia inaweza kuwa ni sababu ya wawili ho kutotaka kuweka mahusiano yao wazi  ingawa kwa sasa hivi wasanii wengi  wa kike kutoka na wanaume wanaowazidi umri imekuwa ni kitu cha kawaida kabisa.

Hivyo Dogo Janja amefunguka na kusema tena kuwa hana mahusiano yoyote na msanii huyo wa bongo movie na tetesi za yeye kutembea na Irene Uwoya zimemletea mgogoro mkubwa sana kati yake na mpenzi wake  aliyenae huku akudhani kuwa maneno hayo yanayosambaa katika mitandao  yana ukweli ndani yake.

Sina mahusiano yoyote ya kimapenzi na irene uwoya, kwanza hii ishu imenileta ugomvi sana na mamlai wangu (mpenzi wake), ni stori ninzikia lakini sio ukweli,uwoya ni mshikaji wangu tu  na tunawasiliana mara chache sana, lakini mapenzi nae sina.” alifunguka kwa undani Dogo Janja huku akitupia tuhuma izo kwa watu wanaozusha kuwa yeye naIrene  uwoya wako katika mahusiano wanaharibu mahusiano na mwanamke aliyenae kwenye mahusiano kwa sasa.

Hitmaker huyo wa Ngarenalo kwa sasa amekuwa katika headline za vyombo vya habari kutokana na habari za mahusiano yake na msanii huyo wa kike lakini pia kutokana na bifu la chinichini lianloendelea kati yake na Young Dee ambapo  wenyewe kwa wenyewe wamekuwa wakibishana kuhusu nani kuwa makli kuliko mwenzie  na hakuna anaetaka kufananishwa na mwenzie.

Bifu La Young Dee Na Dogo Janja,Chanzo ni Muna

Kwa muda sasa kumekuwa na chokochoko kati ya wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva yaani Young Dee na Dogo Janja ambapo katika kufatilia sababu inaonekana ni yale maneno ambayo Young Dee aliyaongea yaliyokuwa yanamuhusu Dogo Janja na Young Killer Msodoki kuwa yeye (Young Dee) ni mkubwa kimuziki hivyo hataki kabisa kusikia watu wakimfanisha na wasanii hao wawili ambao kwake anawaona bado wachanga hawajamfikia kiwango chake. Young Killer alinyamzaza na hajaonekana kuongea chochote kuhusu ili lakini Dogo Janja hakuweza kuvumilia na kuamua kujibu maneno ya Young Dee na kumwambia kuwa hata yeye hawezi kulinganishawa  msanii kama yeye ambae anavuta unga, kabisa hawezi kuongea na ‘mteja’.

Bifu limeendelea na kuwa kubwa mpaka baadhi ya wasanii waliamua kuingia nakuwashauri kuyamaliza mambo hayo, kati ya wasanii hao ni pamoja na Nikki wa Pili.Lakini jana msanii wa muziki wa singeli Sholo Mwamba nae aliamua kufunguka kuhusu bifu ilo huku akiamua kumwaga ubuyu hadharani kuhusu sababu ya wasanii hao kugombana ni mwanamke.

Akiongea na eNews ,Sholo Mwamba ambae alikuwa chini ya menejiment ya Muna Entertainment alifunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye na Muna hawafanyi kazi pamoja na sababu sio kwamba yeye alichokwa na Muna bali yeye alimchoka Muna, alipoulizwa sababau ya yeye kumchoka meneja wake alijibu “Kitu ambacho mimi kiliniuzi na nilikichoka kwa Muda ni kitendo cha sisi wanaume kufanya kazi na kutafuta ela  afu tukienda pale  kwa muna tunakuta madogo wengune wamekaa kwenye makochi wamejiachia, sisi wahuni tunaenda kuimba visingeli vijijini tunaleta mpunga kwa bosi alafu bosi anatumia na wajinga”aliongea Sholo Mwamba

hapo wote vingasti tu, tunawakuta pale kwa bimkubwa wanajiachia achia tu, Dogo Janja, Young Dee, wanagombana wanagombania demu, ila sisi tunakuja kwa bosi tunawakuta hayo mambo ya kugombana ni miyeyusho tu” aliongezea Sholo Mwamba

Hata hivyo Sholo pia anaonekana ana wivu wa mapenzi kwa Muna Love na kufikia hatua ya kusema ” namshangaa bosi si angenipa hata mimi, akinipa sisemi, tunakula kimyakimya”

Dogo Janja Amwita Young Dee Teja

Ikiwa ni siku kadha zimepita na ugomvi kati ya wasanii wa Bongo Fleva Young Dee na Dogo Janja unazidi kuwa mzito huku kila mmoja akitaika kuwa juu zaidi ya mwenzie, ugomvi huu ambao ulianza kwa Young Dee kukataa kabisa kufananisha na wasanii wengine ambao hawapo kabisa katika level zake, kwa mujibu wa Young Dee anasema wasanii kama Dogo Janja  wa Arusha na Young Killer wa Mwanza ni wadodgo sana katika swala la muziki na yeye ndie kaka yao hivyo kwanza wanapaswa kumheshimu lakini pia vyombo vya habari havipaswi kumfananisha wa wasanii hao.

Hata hivyo Dogo Janja ameamua kumjibu rapper huyo  na kusema kuwa yeye hawezi kubishana na Young Dee kwa sababu Young Dee ni teja.Dogo Janja anasema kuwa ni sawa kabisa kwa Young Dee kukataa kufananishwa na yeye kwa sababau hata yeye pia hayuko tayari kabisa kufananishwa na Young Dee kwa sababu rapper huyo anatumia madawa ya kulevya na muda mwingi anaongea akiwa tayari ameshatumia madawa  , na kutokana na matumizi ya madawa hayo ndio maana anaongea mambo ya ajabu ajabu”Young Dee ni mteja,na hawezi kufanana na mim.Mtu mwenye akili timamu hawezi kutukana kwenye Media matusi makubwa kama alivyofanya Young Dee, akiacha unga ndo ninaweza kuzungumza,siwezi jua kama saivi ntakuwa nazungumza  au nabishana  na yeye au na mteja.Mtu mwenye akili timamau unamsamehe  tu maana inawezekana kashavuta mambo yake na yupo kwenye dunia yake nyingine” alifunguka Dogo Janja

Hata hivyo Dogo Janja anasema kuwa yeye hakatai kufananishwa na mtu lakini anaangalia mtu wa kufananishwa nae”mimi pia sipendi kufananishwa  japo pia sikatai kufananishwa, Young Killer nilishawahi kuwa Role model wake kwaiyo kufananishwa nae si kitu kibaya lakini kufananishwa na mla unga ni kukosea.. Young Dee akiacha kula unga tutakaa mezani tuzungumze  lakini kfananishwa nae kwa sasa hivi sitaki”

Baada ya Dogo Janja kuongea hivyo Young Dee  alimjibu tena msanii huyo na kusema kuwa wao kama wasanii wadogo wanatakiwa wamfate yeye kaka yao ili wajue sababu ya yeye  kusema hataki mkufananishwa nao,hata hivo Young Dee anasisitiza kuwa bila yeye wasanii wengine wadogo wasingekuwa hapo kimziki maana wote wamefunguliwa njia na yeye.

Dogo Janja amkana Muna Love baada ya tetesi kuwa wawili hao ni wapenzi

Dogo Janja amefunguka kuhusu uhusiano wake na muigizaji wa filamu Muna Love. Akizungumza kwenye interview hivi karibuni Dogo Janja alisema kuwa yeye na mrembo huyo hawana uhusiano wowote wa kimapenzi Kama wengi wanavyodhania.

Muna Love

Msanii huyo wa Bongo alidai kuwa tetesi hizi ni za uongo. Aliendelea kwa kusema kuwa uvumi huu umemuumiza na pia familia yake. Dogo alisema,

“Hakuna kitu kibaya kama utandawazi, yaani kila mtu ana simu na bando lake kwa hiyo akiamka asubuhi anajisikia kufanya chochote au kutunga vitu kama hivyo lakini siyo kitu kizuri, maana yananiumiza mimi na familia yangu, Uongozi wangu lakini pia vinamuumiza mpenzi wangu kwa sababu tuna malengo makubwa hivyo haya yanapoendelea yanazidi kumuumiza au kumchanganya”,

Aliendelea kwamba,

“Mimi siyo mtu wa kuonesha maisha yangu binafsi kwenye mitandao ndio maana hata mpenzi wangu sijawahi kumuweka mitandaoni, maisha yangu binafsi ni ya kwangu na siyo ya kila mtu hata huyo dada wa watu anaumizwa na hili na anafamilia pia kwa hioyo hizi habari zinazidi kumuweka pabaya.

Magari ya kifahali na mavazi ya kuvutia zatawala video mpya ya Dogo Janja – Ukivaaje Unapendeza?

Dogo Janja ameachia wimbo wake mpya – Ukivaaje Unapendeza? Msanii huyo wa Tip Top Connection inayomilikiwa na Babu Tale, ameonyesha umahiri wake wa kung’ara kimavazi kwenye video yake mpya.

Janja pia alitumia magari ya kifahali kwenye video yake. Kwa ujumla wimbo wake msanii huyo unadhibitisha ukomavu wa nyimbo za hip hop Tanzania. Tazama video hio hapo chini:

Maoni ya Dogo Janja kuhusu uhusiano wa Jacqueline Wolper na Harmonize

Dogo Janja ametoa maoni yake kuhusu uhusiano wa Jacqueline Wolper na Harmonize kufuati matukio ya hivi karubuni.

Kuliibuka uvumi kuwa wawili hao (Harmonize na Wolper) waliachana lakini baadae Harmonize alikuja kuthibitisha ukweli wa mambo.

Dogo Janja alikuwa na mengi ya kusema kuhusu uhusiano wa Wolper na Harmonize; akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, msanii huyo wa Tip Top Connection inayomilikiwa na Babu Tale, alisema kuwa maisha ya watu mashuuri ni filamu.

Jacqueline Wolper na Harmonize

Dogo alisema kuwa mapenzi ya Harmonize na Wolper ulikuwa kama drama ulipokua unaanza lakini mwishowe ukawa ‘serious’.

“Ukishakuwa na mpenzi staa hiyo ni flamu tayari, maisha yenu ni filamu watu wanafuatilia. Kingine mapenzi yao yalivyokuwa yananza watu walikuwa wanachukulia kama Drama lakini mwisho wa siku unakuja kuona kama wapo serious, kwa hiyo ni vitu kama hivyo.

“Mimi kama mimi siko interested nao sana, ni verse tu zile, siko interest nao kwa vile na mimi nina mapenzi yangu , kila mtu ana mitikasi yake” amesema Dogo Janja.

Dogo Janja

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.