Playing With Fire? KTN’s Mohammed Ali’s Daring Message to Nkaissery after He Was Warned of Dire Consequences
Mohammed Ali, has guts, I will give him that.
After Nkaissery ordered Journalists Mohammed Ali and Yassin Juma to apologize to Kenyans for apparently spreading false information in regards to the Mandera graves, Mohammed Ali kept his silence.
He has come out and has said he will not apologize anytime soon because he does not know what he is apologizing for. Adding that Nkaissery should be the one issuing the apology for associating them with terrorism and also picking them out from all the other journalists, yet they had also reported the news on the Mandera Mass Graves.
He then went on to ask why they were singled out. Was it because they are Muslims or because they do not agree with the government. Read the rest of the statement below which was ominously titled ‘Nikifa Kesho’:
NIKIFA KESHO’
Shikamoo Meja mstaafu Joseph Nkaissery . Natumai u buheri wa afya popote ulipo chini ya ulinzi mkali unaotokana na ushuru wangu na wakenya wenzangu. Wiki iliyopita nilipokuwa nikitazama sherehe za Jamuhuri ya Kenya twasira yako ilinijia na kutaka kujua ni kwa nini tuwe katika hali ya utumwa tukisheherekea miaka 52 ya Uhuru wa taifa hili. Wiki hio hiyo nikiwa futi kadhaa angani kutoka Mandera niliarifiwa ulinitaja jina sio mara moja bali mara kadhaa na kuonekana kujaribu kuhusisha jina langu na wanamgambo wa Alshabab eti nilikuwa nikipasisha ujumbe wao na kutokuwa mzalendo mpenda taifa. Naarifiwa pia ulitutaka sijui kama ni mimi na Yassin Juma tuombe msamaha kwa kutoa taarifa za kutatanisha. Naomba kwa heshima nikuweke sawa mzee wangu. Kwanza kabisa siombi msamaha maana sijui kosa langu ni lipi. Pili wa kuomba msamaha ni wewe kwa kutuhusisha sisi wawili na ugaidi ukitumia wadhifa wako kutupaka tope huku ukilegeza kamba kwa kuchagua wanahabari wawili kati ya wote walioripoti tukio hilo. Je, ulituchagua kwa sababau sisi ni waisilamu? Je, ulituchagua kwa sababu sisi hatukubaliani na kauli ya serikali? Je, ulituchagua kutokana na msukumo wa wale maskauti wa propaganda 36 wa serikali? Nauliza unijibu. Taarifa hizo zilisemwa na wengi lakini ikija kwangu sijui ni dini, kazi yangu murwa, jina langu au msimamo wangu. Ningelipenda kukukumbusha kuwa kuna msemo unaosema mti mwenye matunda ndio upigwao mawe. Naona serikali imenichagua kuwa mti huo kwa sasa. Tuyaache hayo la muhimu ni kwamba naapa na kurudia tena ya kwamba sitaomba msamaha kwa kusema baadhi ya viongozi serikalini ni wafisadi, sitaomba msamaha kwa kusema tangu na uhuru wa taifa hili kuna mauaji ya kiholela kenya, sitaomba msamaha kwa kusema bunge letu limejaa mafisadi, sitaomba msamaha kwa kusema serikali iliyo mamlakani imetufeli kwa kutotimiza ahadi zetu, ahadi ilizotuahidi wakati wa kampeni zake, sitaomba msamaha kwa kuuliza ni nani aliyejaribu kupora ardhi ya shule ya msingi ya langata, sitaomba msamaha kwa kuuliza ni nani anayeua vijana na kutupa miili yao sio tu Garissa, Wajir, Mombasa, Mandera bali pia Nairobi, Muranga, Nyeri na maeneo mengine humu nchini kwa mujibu wa mashirika ya kutetea